
SEHEMU YA 63
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA MBILI: lakini licha ya kukuta duka lipo wazi, Sada alishangaa kuona pale dukani, kuna mwanadada mwingine kabisa, na siyo Kadara kama alivyo tegemea, “mambo” alisalimia Sada kwa sauti ya kirafiki, usingeweza kuhisi kama anauchovu uliochanganyika na njaa, “poa tu karibu” aliitikia yule dada alie kuwa dukani, na kumkaribisha, niwazi alizania kuwa ni mteja, “walaa mimi siyo mteja, nimekuja kumuulizia huyu mrembo” alisema Sada kwa swaga za kimjini na kisister du, “nani dada Kadara, ameondoka jioni ya leo kwenda kijijini, kuna vitu baba yake amemtumia fedha amnunulie, ndio amevipeleka kijijini kwao” alisema yule mwanamke ambae umri wake ni mdogo kwake. ………..Endelea…
Hapo Sada akaona kuwa, mambo ni magumu kwa upande wake, “jamani kwanini anaondoka bila kunijulisha, na mimi sininge mwagiza” alisema Sada ambae moyoni mwake alikuwa anajuwa fika kuwa, ata angejulishwa mwezi mmoja kabla asingekuwa na kitu cha kupeleka kwa wazazi wake, “amaletewa jana hivyo toka asubuhi alikuwa anafanya manunuzi ya vifaa hivyo vya nyumba yao” mpaka hapo Sada alionyesha kuchoka kabisa, tena alionyesha wazi wazi, “jamani simu yangu imeisha chaji si ninge mpigia” alisema Sada kwa sauti ya kinyonge, kisha akauliza, “kwani anarudi lini?” aliuliza Sada, kwa sauti ya kukata tamaa, “anarudi kesho kutwa juma tatu, na gari la asubuhi” alisema yule mwanamke, na hapo Sada aliona njaa inazidi kuongezeka, “jamani simu muhimu sana” alisema Sada kwa sauti iliyotia huruma, “kwani ulikuwa na shida nae kubwa sana, ninaweza kumpigia” hapo Sada aliona kuwa amepata bahati, maana alimini kuwa Kadar akipigiwa lazima ange toa msaada kwake, “itakuwa vizuri sana, maana hapa nipoteza pochi yangu sina ata Nauru ya kwendea nyumbani” alisema Sada na hapo nikama yule dada akaingia huruma, “kwahiyo unafahamiana nae vizuri tu” aliuiza tule dada huku anaviuta pochi yake na kuifungua, “siyo kufahamiana, yeye ni kama ndugu yangu, tumetoka kijiji kimoja kabisaa, tena majirani, wewe ukimwambia tu Queen alikuja, utamsikia” alisema Sada, huku akitoa ufafanuzi mrefu, “nazani akuna aja ya kumpigia simu, kama ni nauri chukuwa tu hii” alisema yule mschana, huku anampatia fedha tathrim tsh elfu mbili, “asante sana” alisema Sada, huku anapokea ile fedha na kisha akaaga mala moja na kuondoka zake huku anaifanyia bajeti ile elfu mbili, na katika bajeti yake akiweka kitu kinachoitwa nauri.***
Nikweli, saa mbili na nusu ndiyo mida ambayo bus aina ya layland old model yani mound wa zamani sana, lilikuwa linasimama eneo la magengeni, ambapo ndiyo kituo cha mwisho, cha bus, lakini kwakuwa Kadara alikuwa amekubariana na wasafirishaji hao wa bus ilo kongwe, ambalo ufanya safari zake songea mjini kwenda kijijini, Mwanamonga, kwamba wata mfikishia mzigo wake ambao uliwekwa kwenye carrie na mwingine kulazwa kwenye kolido, la gari ilo lenye urefu wa kutosha, kwamba watamfikishia mpaka nyumbani.
Basi Kadara alisubiri mpaka abiria wote waliposhuka na yeye kuendelea na safari mpaka nyumbani kwao, ambako, kiukweli siyo tu nyumbani kwao ambako akukuta watu, pia kijiji ni kama kilikuwa kime hama, hivyo baada ya kushusha mzigo na kuwekwa pale chini, akaanza kusaka wazazi wake na baadhi ya vijana waweze kumsaidia kuuingiza ndani, alitembea mitaa miwili mitatu, mpaka alipoibukia kwa mzee Jacob, ambapo kwa mbali aliona watu wengi sana, wakiwa wana milikwa na taa kila kona.
Naam ilimshangaza sana, aikuwa tofauti na umeme wa mjini, hapakuwa na kelele za music wala vikilio, sasa kulikuwa na nini, na alipoamua asogee akaulize ndipo alipo baini kuwa kulisikika sauti ya toka kwenye TV, siyo kwamba mzee Ndumbalo na mke wake ni washamba sana, lakini akajuwa kwa mazingira ya kijijini lazima watakuwepo pale, kitu kilicho mshangaza ni kwamba, aya mambo mzee Jacob ameyatoa wapi, maana akufikilia kama alienda mjini kununua vile, au Peter amekuja navyo, lakini ata kuja navyo vipi wakati alisikia kuwa alitapanya mali na makahaba.
Kadara akutaka kuhoji kwa mtu yoyote, akajuwa ni lazima akikutana na baba yake mzee Ndumbalo au mama yake ata msimulia kila kitu, na akuangaika sana kuwapata, aliwaeleza juu ya ujiowake na mizigo ambayo hipo pale nyumbani, hivyo alikuwa anaitaji watu wakwenda kumsaidia, ilifanyika mipango ya kupata watu na wakenda kumsaidia kwa makubariano ya malipo baada ya kazi.
“Kadara kumbe mjini kutamu hivyo, unazidi kunawili tu, nifanyie mpango sehemu ya kiufikia na mimi nije huko” alisema mmoja kati ya vijana, waliokuwa wanabeba vifaa kuingiza ndani, ambao wote walionekana wamelewa, “mh! nani amekuambia mjini, kupo kama unavyosema, we acha tu watu wanaangaika kama nini, naukiingia kichwa kichwa huko, unarudi na kilio” alisema Kadara, alie kuwa anawasimamia wale vijana, akiwamulikia kwa mwanga wa tochi ya simu yake, “wewe mtu ametoka juzi tu na leo amekua na nagari, na amependeza utazani amezaliwa huko huko” alisema mmoja akipingana na Kadara.
“nani huyo anae kudanganya?” aliuliza Kadara, akiitaji uthibitisho, “nani mwingine zaidi ya Peter, wewe siumeona pale kwao alipo pabadirisha” alisema mmoja kati ya wale vijana, akiwa na uhakika na alicho kisema, na kumfanya Kadara mwenyewe atoe macho kwa mshangao, “weeee usiniambie, Peter huyu baba Michael mume wa Sada?” aliuliza Kachiki kwa mshangao, “kwani kuna mwingine” alsema mmoja kwa namna flani ya kebehi, “jamani Peter ametoa wapi, mbona mke wake Sada amekuja pale amesema kuwa Peter, alienda bar, akakutana na wanawake wamemwibia kila kitu, na yeye alipojaribu kumshauri akampigaweeeee, ata mimi nimeona jinsi da Queen alivyo umia” alisema Kadara, na kuwavuruga kidogo wale vijana, ambao idadi yao walikuwa wanne,
“sisi tunamzungumzia Sada , kwani huyo Queen ndiyo nani?” aliuliza mmoja kati ya wale vijana, huku wanatoka nje kuchukuwa mzigo mingine, “”tatizo nyie washamba, kwani amjuwi kuwa sikuizi Sada anaitwa Queen” alisema Kadara, hapo wote wakasimama na kumtazama Kadara kwa mshangao, “eti Sada sijuwi Queen, we! unachekesha kweli, ungejuwa ata usingesema, tena huyo Sada ata sababisha vijana wakutoka kijijini wawakiumbie, huko mjini wakiwaona” alisema mmoja kati ya wale vijana, kisha wakaendelea kutmbea kutoka nje, “kutukimbia kivipi, wakati nyie wanaume ndio tuta wakimbia” alisema Kadara, na wale vijana wakacheka kwadharau ya kilevi, kiasi cha kumshangaza Kadara, ambae akaishi kunajambo ambalo, lilitokea kule mjini, kati ya Sada na Peter,
kwamza alikumbuka alicho ambiwa na Sada kuwa Peter aliibiwa kila kitu, na leo anambiwa Peter ndie alie wafanyia mambo yale wazazi wake, “sasa fedha amepata wapi” alijiuliza Kadara, ambae aliona kuwa sasa ndio muda sahihi wakupata ukweli, “jamani Peter amepata wapi, mke wake ameniambia kuwa ameibiwa kila kitu” alisisitiza Kadara, lakini kwa lengo la kuchokoza vijana walei wamsimulie kilichotokea, “yani usije ukamwita mke wake, Peter amekuja na mke bomba kinoma” alisema mmoja wao, na hapo Kadara akaona bi vyema kama akisubiri mama yake aje mwelezee kilochotokea, maana bado alikuwa na baba yake kule kwa mzee Jacob.**
Saa tatu za usiku ndio mida ambayo Careen Peter na Michael walikuwa wanaingia kulala, huku Michael akielekea chumbani kwake, na Peter na Careen wakielekea chumbani kwao, “yaya naomba kesho saa nne umwandae Michael kwaajili ya kumpeleka akacheze na watoto wenzake, pale kids cental, alafu mwambie Jasmin, kesho akanunue simu mbili nzuri, kwa ajili ya wakina baba kule kijijini” alisema Careen, wakati anaelekea chumbani akiwambia yaya Glory, alie kuwa anawasindikiza, kwamaana ya kupata maelekezo au ratiba ya kesho, “sawa Careen nawatakia usiku mwema” alisema yaya Glory, na kugeuka zake na yeye kwenda kutoa maagizo kwa wafanyakazi.
Nikweli ulikuwa usiku mzuri sana kwao, ukichanganya na furaha waliyo kuwa nayo, walipata glass kadhaa za wine, kabla ya kuingia kitandani, labda nikuambie kitu kimoja, ambacho unapaswa kukijuwa msomaji, Careen ni nywaji mzuri wa wine, na amejiwekeea utaratibu wake, wakwamba kila siku ni lazima apate grass japo mbili za wine ndipo alale, ni tabia ambayo aliianza miaka miwili, iliyopita, pale ambapo alishuhudia rafiki yake kipenzi wa utotoni, yani #king_Elvis wa #mbogo_land, akimchagua mwanamke mwingine kuwa mke wake, yani Malikia wa mbogo land.
Hiyo basi Careen licha ya kuja Tanzania kujaribu kubadiri mazingira na kumsahau Elvis, ambae siyo kwamba alikusudia kufanya hivyo, yeye alimini kuwa Careen asinge kuwa tayari kuwa mke wake, au pengine ange mchukuwa kwa ulazima tu, kwa kuwa ni mwana wa mfalme (kipindi hicho kabla aja kuwa mfalme) ndio maana akafunga safari kwenda Tanzania kutafuta mwanamke wa maisha yake,
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU