KIAPO CHA MASIKINI (65)

SEHEMU YA 65

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA NNE: Tayari Emma alikuwa amesha kunywa soda ya baridi, kupunguza kilevi, ambayo alimwambia Sada akanunue, na Sada alinunua kwa fedha aliyokuwa amebakiwa nayo jana, alitumia mia tano na kubakia na mia tatu, shilingi za kitanzania, akiamini kuwa Emma ata mwachia fedha ya kutosha, “sasa baby, uniachii ata ela ya chai” alikumbusha Sada, yani Queen, ………..Endelea…

baada ya kuona Emma akuwa na dalili ya kumwachia chochote, “sina ata mia hapa” alijibu Emma, bila ata kugeuka nyuma, zaidi alifungua mlango akatoka na kuufunga, hapo hapo Sada akaanza kuhisi njaa kali, ikimsokota tumboni mwake.***

Saa tatu na nusu iliwakutia mama na baba Sada wakiwa wanashuka toka kwenye basi pale stendi ya kusini, wakiwa wameshikilia mfuko chakavu wenye nguo chache, na hapo ndipo walipoona dalili ya ugumu ulipo mbele yao, maana awakujuwa wataingilia wapi, “lakini kwakuwa Sada ni tajiri, tukiulizia tu, lazima watu watakuwa wanamfahamu, alisema mzee Nyoni, huku wanatazama kushoto na kulia, kutazama ni mtu gani wanaweza kumwulizia awaelekeze juu ya mwana dada tajiri, mwenye kumiliki ghorofa pale mjini, anaeitwa Sada Nyoni.

Watu walikuwa wengi sana pale stendi, hivyo awakuangaika sana kumpata mmoja wa kumwuliza, “salama baba” alisalimia mzee Nyoni, huku akimtazama mtu mmoja ambae alikuwa anapita mbele yao, “salama shikamoo mzee lakini sina chochote” alijibu yule jamaa ambae ni kijana mdogo tu, alie zania kuwa, wazee awa ni omba omba, “jiheshimu kijana, sisi siyo ombaomba, sisi ni watu na heshima zetu, sisi ni wazazi wa Sada Nyoni, yule mwanamke tajiri mwenye ghorofa” alisema mama Sada kwa sauti ya ukali, na kumfanya yule kijana ashangae kidogo, “hoooo! samahani, sikujuwa kama ….. lakini jinsi mlivyo mtu awezi kuamini” alijitetea yule kijana, na kuwafanya wakina mzee Nyoni na mke wake aminikuwa, kijana yule alishamfahamu Sada ndie ndani.

Na hapo wakina mama Sada wakaona isiwe shida, “sawa tumekusamehe, sasa tunaomba utuelekeze kwa Sada” alisema mama Sada kwa sauti ya kujiamini, “kwakweli simfahamu huyo Sada, labda mkaulizie huko mjini” alisema kijana yule kwa sauti tulivu, iliyojaa nidhamu, huku anawaonyesha upande wa mjini, kisha akaondoka zake, “mh! kwani hapa siyo mjini” alisema mzee Nyoni, “ndiyo maana siyaoni maghorofa ebu twende basi mjini, tumpate Sada mapema, ili tupumzike, maana imeshoka” alisema mama Sada, huku wanaanza kutembea kuelekea upande walio onyeshwa na kijana yule.

Naam baada ya kutembea kama mita mia moja nje ya stend, huku wanayatazama majengo marefu yaliyotanda na kuota kama uyoga, wakijiuliza lipi kayake ni nyumba ya Sada, walimsimaisha mtu mwingine, na kumwuliza swali lile lile, “mh! Sada, mbona simjuwi, huyo mwanamke tajiri anaeiywa Sada, kwani amna namba yake?” aliuliza Dada flani walie mwuliza kuhusu Sada, “namba yasimu hatuna, wala simu yenyewe hatuna” alijibu mzee Nyoni, “aliwaambia anaishi mtaa gani” aliuliza yule mwanamke, “kwakweli hatujuwi” swali ilo lilimfanya yule mwanamke awatazame kwa macho ya mshangao, “inamaana nyie mme kuja kumtafuta mtu ambae amna namba yake ya simu, na wala hamjuwi anaishi mtaagani?” aliuliza kwa mshangao yule mwanamke.
hapo wakina mzee Nyoni wakakosa jibu, “sasa mimi nawashauri endeleeni kuulizia, au mumtafute mtu mmoja atakae kuwa anamfahamu” alisema yule dada na wao wakaelekea kati kati ya mji, huku wanaulizia kila wanapo ona pana faa kuulizia, lakini majibu yakawa ni yale yale atumjuwi.****

Yap! mita chache toka kwenye lango la kanisa la matogoro, lilionekana gari moja dogo aina ya Toyota noah, la rangi nyeusi, likiwa limeegeshwa kwa kutazama upande wa kanisa, ambalo leo lilikuwa limejaza watu wengi sana, ukiachilia waliokuwa ndani, pia wengine walikuwa wametapakaa nje ya kanisa ilo, upande pembezoni mwa wa barabara iliyopita mbele ya kanisa ilo, ndiyo barabara ya kuelekea mahilo mpaka nchi ya jilani ya #mbogo_land, wakinunua bidhaa mbali mbali, za mashambani, zinazotoka kwenye vijiji vya jilani, kama vile luhila kimoro, kwa mkwawa, na chem chem,

Ndani yake kulikuwa na vijana wawili, yani Dullah, na Seba, ambao macho yao, yalikuwa yameelekezwa kwenye mlango mkubwa wa kanisa, pamoja ile midogo ya ubavu wa kulia wa kanisa ili, ambapo licha ya kusubiri misa ikamilike, lakini pia walikuwa wanatazama kila anaeingia na kutoka, kama wangemwona RCO Mlashani akitoka pamoja na familia, yani mke wake na mtoto Jasmin, mjukuu wao mpendwa.

Upande wa kushoto wa kanisa ilo, yalionekana magari kadhaa yaliyoegeshwa, magari ambayo, ungezania kuwa yote yalikuwa tupu ndani yake, kwamba wenye magari walikuwa ndani ya kanisa, lakini aikuwa hivyo, kuna gari moja dogo aina ya Toyota IST rangi ya silver, lililokuwa miongoni mwa magari yaliyokuwepo pale kwenye maegesho, ambalo ndani yake kulikuwa navijana wawili, yani Emma, pengo ambae makovu yake usoni, asa sehemu ya mdomo, yalikuwa yameshakauka na kuacha alama nyeusi, yaliyosabashwa na magamba, pamoja na msaidizi wake Hussein au Janja kama wanavyo mwita wenzake, wakiwa wana litazama gari aina ya Toyota spacio rangi nyeusi, lililoegeshwa mita chache jilani yao, wakitenganishwa na gari moja dogo, aina ya Toyota Passo.

“ujuwe Queen simuelewi kabisa, nikweli alipata fedha toka kwa yule fala, alafu na yeye akaibiwa, au una kamchezo anajaribu kunichezea?” aliuliza Emma, ambae alikuwa amelaza seat ya pembeni kwa dereva, na yeye kujilaza juu yake, “inamaana kaka umwamini kabisa shem?” aliuliza Janja, ambae alikuwa amejilaza kwenye seat kama ilivyokuwa kwa Emma, “nimwamini kivipi, yani demu na mkuta bar alafu nimwamini kilahisi hivyo, ata kwao sipajuwi” alisema Emma kwa sauti iliyojaa dharau, “haaaa aja utani kaka, unaishi na demu miezi sita mizima, alafu unasema umwamini?” aliuliza Janja, akipinga kauri ya Emma, “tena bro, sasa hivi namwona kama mzigo, kuna wakati nikiitaji kuwa na demu mpaka niende guest au niazime ghetto” alisema Emma kwa sauti ya kulalamika.

“kwahiyo unataka kumtimua, itakuwa poa sana, maana sidhani kama utakuwa nasehemu ya kumpeleka endapo utampatia ujauzito” alisema Janja, akimshauri Emma, ambae alicheka kidogo, “mimba itaingiaje, unazani mimi ni mjinga hiyo?” uliza Emma kwa sauti iliyojivisha ushindi, “mh! kaka sijawai kukusikia ukizungumzia matumizi ya sox katika maisha yako, inamana Queen umwamini, kiasi cha kumvalia mpira?” aliuliza Jania huku anacheka kidogo, “zana wapi kaka, mimi uwa na malizia uwani” alisema Emma akimalizia kwa kicheko cha chini chini,
Kauri hiyo ilimshangaza sana Janja ambae kabla ajasea lolote, mala akasikia sauti za watu zikisikika kwa wingi, zikionyesha kuwa watu wanatoka kanisani, “hoya wanatoka hao” alisema Emma, huku anainua seat ya gari, akifwatiwa na Janja, ambae pia alifanya hivyo hivyo, huku anatoa simu mfukoni, “wacha niwaambie wakina dullah wawe makini” alisema Janja, huku ana bofya simu yake kumpigia Dullah,

Lakini kabla Dullah ajapokea simu, tayari wakamwona RCO Mlashani, akiwa ameongoza na mke wake na mjukuu wao, wakija kwenye gari lao, “haoooo wanakuja” alisema Emma, na wakati huo huo, simu nayo ikapokelewa, “hoya Dullah, huyu bwege anaingia kwenye gari, sasa kuweni makini mnapo mfwatilia, asije akajuwa kuwa mnamfwata” alisema Janja na kukata simu, huku wanashuhudia RCO na familia yake wanaingia ndani yagari nakuondoka zao, kuelekea upande wa mjini, nao wanamwachia dakika kadhaa kicha wanandoa gari, kumfwatilia, na wanapo fika usawa waliokuwa wakina Dullah, wanaliona gari lao wakina Dullah, wakiondoa gari, na kuanza kuwafawtilia wakina Mlashani.**

Tayari walikuwa wamesha maliza kunyanduana, na kupeana kile ambacho, mama yake Careen alisea wasubiri mpaka wafungee ndoa, walipeana utamu kiasi kwamba, ata saa walipokuwa mezani walishindwa kutazamana, ata macho yao yalipokutana kwa bahati mbaya walijikuta wakitazamana kwa sekunde chache, nakisha kukwepesha macho huku wakitabasamu kwa aibu, hali hiyo ilikuwa kubwa sana kwa Careen, “Peter mimi naenda ofisini, nitakuwa huko kwa muda mfupi, nyie mtapelekwa NPF kwenye viwanja vya watoto, nita wakuta hapo, nataka Michael akacheze kidogo” alisema Careen, ambae mpaka mida hiyo alikuwa amesha jiandaa tayari kuelekea ofisini, “kumbe mjini kuna sehemu za kucheza watoto?” aliuliza Peter kwa auti iliyojaa mshangao.

“ndiyo ni sehemu nzuri sana, utajionea mwenyewe” alisema Careen ambae uso wake ulionekana wenye furaha, tofauti na siku kadhaa nyuma, kabla aja kutana na Peter, “sawa tutaenda hapo, lakini sisi tutapajuwaje hapo NPF?” aliuliza Peter, ambae mpaka sasa, bado akuwa anaujuwa mji vizuri” “ata wapelaka Jasmin, na kuwaacha hapo, kisha mimi nita wakuta hapo” alisema Careen ambae baada ya kumaliza kula aliondoka kuelekea mjini, yani ofisini kwake pale mtaa wa Zanzibar.

Huku nyuma Peter akianza kujiandaa, kwaajili ya kwenda NPF na Michael, ambae tayari alikuwa ana andaliwa, kwaajili ya safari hiyo ya kwenda NPF, sehemu ambayo mke wa RCO na anataka kumpeleka mkuu wake.***

Sijuwi umasikini na njaa uwa vinapendana sana, kama ilivyokuwa kwa Sada, ambae kiukweli, mpaka mida hii ya saa nne, alikuwa anasikia njaa kali sana, kila alipo fikilia sehemu ya kwenda kuomba fedha akaona ni vigumu, ukiachilia kujishusha, endapo angeenda kwa Rose, kule bombambili, asa akifikilia kuwa alisha ondoka kule na wenzake wana chukulia kuwa anaishi maisha mazuri huko aliko.

Mtu pekee ambae angeweza kumsaidia, ni Kadara ambae yupo kijijini, sasa ataenda wapi, hakika alikuwa na njaa kari, na akuwa na uhakika wakula asubuhi, mchana wala, ata usiku kama Emma ata chelewa kurudi kama jana, “bora ata nisinge mnunulia soda kwa ela yangu” alisema Sada kwa sauti ya kujilahumu, ambae leo alijikuta anakumbuka ata ile fedha, aliyo mwibia Peter, na yeye kuibiwa, na watu asio wajuwa, “sijuwi nita fanya nini” aliwaza Sada huku anapepesa macho chumbani kwake, na asione chochote cha kumsaidia.

Lakini wakati anafikilia cha kufanya, mala akaliona begi lenye nguo za Peter na mwanae Michael, nilile alilo liiba siku ile kwa Peter kule hotelini, “yes kimfahacho mtu chake, hivi siwezi kupata ata elfu tano kweli” alijisemea Sada huku anainuka na kulifwata lile begi, ambalo alianza kulipekuwa pekuwa, kuona kama kunaamacho anaweza kuuza na kujipatia ela ya kula, kwa siku ile.

Bahati nzuri kwake, kila ngo na viatu alivyo vikuta mle ndani vilikuwa ni vipya kabisa, na avikuwai kuvaliwa ata mala moja, Sada akaachia tabsamu pana kweli kweli, “hapa nita jipatia ela ya kula” alisema Sada huku anarudisha vitu vile kwenye begi, na kujiandaa, tayari kuelekea mjini kuuza nguo alizo ziiba kwa mumewake wa zamani na mwanae wakumzaa….………..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata