
KIAPO CHA MASIKINI (70)

SEHEMU YA 70
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA TISA: Sasa basi ile Sada anageuka kutazama kule anakoelekea, akajikuta anamvamia, mtu aliekuwa mbele yake, nusu amwangushe, “unashangaa nini mjini hapa jiangalie wewe” alisema Sada, huku anamtazama kwa hasira yule mtu alie msukuma ambae alikuwa ni mama mtuzima, ambae sasa aliweza kumwona usoni, hakika Sada akatoa macho kwa mshangao wa kutoamini alie mwona mbele yake, huyu alikuwa ni mama yake, alie simama pembeni ya baba yake, wote wakimtazama kwa mshangao kama yeye alivyo watazama……..………..Endelea…
Siyo kwa sababu ya kuto kuonana muda mrefu, ila ukweli nikwamba, wakati Sada anashangaa kuwaona wazazi wake hapa mjini, wakiwa katika hali kama hii, wakati nijana tu aliongea nao kwenye simu, wazazi wake walishangaa kumwona binti yao akiwa kati hali ambayo aifanani na vile walivyokuwa wanajuwa wao, kutokana na maneno ya binti yao, kwamba Peter alilala kwake, na kutoroka siku ya pili, “samahani tumekufananisha na na binti yetu” alisema Mzee Nyoni, huku anamshika mkewake nakuanza kutembea, “we unakichaa, umemfananisha wapi, niyeye huyu Sada” alisema mama Sada huku anajipapatua mkono wake toka kwa mume wake, kisha akamtazama Sada, ambae bado alama za makovu usoni mwake, yalionekana wazi kabisa, akuwa tofauti na kibaka au mwizi alie kutana na dhahama siku chache zilizopita.
Wakati huo baadhi ya watu walikuwa wamesha gundua kuwa kunajambo silo la kawaida linaendelea pale, “we! Sada, wewe siulisema,….” alisema mama kwasa kwa sauti ya mshangao iliyojaa uchungu, lakini Sada katika hali ya kushangaza akumwacha amalize alicho taka kukisema, “Sada nani anaitwa Sada, mimi naitwa Queen, mtakuwa mme nifananisha” alisema Sada, bila kupepesa macho, japo akujuwa wazazi wake wapo pale mjini kwaajili gani, alicho jari yeye ni wakukakataa ili asije akazalilika, maana kama akikubari kuwa yeye ni Sada, inamaana wazazi wake itabidi wafikie kwake, ambapo aliwaambia kuwa ananyumba kubwa, waliyo fikia wakina Peter, wakati yeye akuwa ata na shilingi moja.
Hapo mama Sada akaoa mshangao mkubwa ulioambatana na sauti ya bata, “khaaaaaa!!! wewe hivi umechanganyikiwa, eti unaitwa nani, aya vyovyote vile, sasa ilo ghorofa liko wapi, tunataka kwenda kupumzika” alisema mama Sada kwa sauti ya ukali, huku watu wakianza kuwasogelea, wakitaka kujuwa kinachoendelea.
Ukweli hapo Sada akaona kuumbuka kunakuja mbele yake, lazima azidishe maigizo, ili kuepukana na wazazi wake, “khaaa! ghorofa, kwani nyie wakinani, na mnatokea wapi?” aliuliza Sada, huku akimtaazama mama yake toka chini, mpaka juu, na kufanya hivyo kwa baba yake pia, “mama Sada, nimekuambia huyu tume mfananisha, sio yeye” alisema mzee Nyoni huku anajaribu kumshika tena mkono mke wake, “Sada we Sada, Sada nimekuota mala tatu, unajifanya utujuwi, aya tupe nauri turudi na gari la jioni” alisema mama Sada huku ananyoosha mkono kuomba hiyo fedha, “nauri, niwape nauri toka wapi, mtafuteni binti yenu” alisema Sada huku anaanza kutembea kuelekea kule alikokuwa anaelekea, “we Sada sisi tutarudije kijiji, na kule tuna daiwa nauri ya watu” alisema mama Sad kwa kulalamika, lakini Sada akujibu lolote, akazidi kutokomea akilipita gari la Emma pasipo kujuwa kuwa ndilo lenyewe, akatokomea zake, huku akisindikizwa na macho ya watu wote waliokuwa eneo lile.
Na baada ya Sada kuondoka ndipo wakina Emma ambao muda wote licha ya kuwaona wakina Dullah, wakipita kwa mwendo mkali, wakihisi kuwa wamesha mteka mtoto, lakini walibakia pale wakitazama jinsi Sada au Queen kama wanavyo mfahamu, akiongea na wale wazee wawili ambao, waliwachoma na moto wa bangi, japo awakusikia walichokuwa naongea, lakini waliweza kuona malumbano, na sasa vijana awa wanaofanya kazi kwa Kalonga wakaondoa gari, kuelekea kule walikoelekea wakina Dullah, huku Emma anapiga simu kwa Dullah, ili kujuwa kama wamefanikiwa, kumteka Mjukuu wa RCO.
Hakika Mama Sada akuamini kilicho tokea, alishikwa na uchungu mkubwa sana moyoni mwake, akahisi miguu inakosa nguvu, akakaa chini, huku anaangua kilio kikubwa sana, “jamani yoyooooo!! mwanangu mieeee, sijuwi amkutwa na nini jamanieeeeeeee” mzee Nyoni ambae alishikwa na uchuku kama mke wake, ambae tunaweza kusema kuwa, alikaukiwa na machozi, alijaribu kumbembeleza mke wake, ambae kilio chake kilizidi kuwasogeza watu, katika eneo lile.****
Naam kila alie shuhudia Peter akimwokoa Jasmin, alimsifu sana kijana huyu, kwa jinsi alivyo jitolea na kufanikiwa kumwokoa, mtoto yule mdogo wakike, maana watu wote walikuwa wanashangaa kinachotokea, “asante sana mwanangu, awa watu sijuwi wanataka nini kwetu” alisema Sophia, huku anachukuwa Jasmin toka kwa Peter, “niwatu wabaya sana, sijuwi kwanini mjini, watu wanawinda watu wenzao” alisema Peter, wakati huo Careen aliekuwa amemshika mkono Michael akimsogelea Peter taratibu, huku uso wake, ukiwa umechangamka kwa tabasamu, wakati huo kiba baadhi ya watu walikuwa wanachukuwa video kwa kutumia simu zao za mikononi.
“yani inashangaza sana, nime pigiwa simu sasa hivi, kwamba niondoke hapa, na wao ndio wanataka kumchukuwa mtoto” alisema mama Sophia yani mke wa RCO, huku watu wote wakiliona gari moja jeupe lenye namba za kiraia, likiingia kasi na kusimama mita kama kimu na tano pembeni ya eneo lile ambalo watu walikuwa wamejikusanya, kisha akashuka RCO, mlashani, na kuja mbio mbio, “vipi mama Sophy, mpo salama” aliuliza RCO, mala baada ya kumfikia mke wake, “walitaka kumteka Jasmin, huyu kijana ndie alisaidia” alisema mama, Sophia huku anamwonyesha Peter kama ndie kijana alie saidia.
RCO alikamtazama Peter, kwa macho ya kumshuku, “habari yako kijana” alisalimia RCO, huku anamtazama Peter ambae sasa alikuwa amesimama na Careen na Michael, “safu tu mzee shikamoo” aliitikia Peter, huku akitabasamu, “marabaha kijana, natakujuwa kama ulikuwa unafahamu juu ya ili tukio, hapo mwanzo?” aliuliza RCO, swali ambalo lilimshangaza kila mmoja alie kuwepo pale, akiwepo mke wake, “huyu ni mume wangu, tumeleta mtoto hapa” alijibu Careen, akionyesha kushangazwa na swali la mzee Mlashani.
Siyo yeye peke yake wala mke wake, ni kila mmoja maali pale alishangaa, kusikia eti, Peter ni mume wa Careen, “hoooo! kumbe asante sana kijana, sijuwi unaitwa nani?” aliuliza RCO, akionekana kuondoa shuku yake, juu ya Peter, naitwa Peter, huyu ni mke wangu anaitwa Careen, na huyu ni mtoto wangu anaitwa itwa Michael” alitambulisha Peter, kwa sauti iliyojaa urafiki mkubwa, “nimefurahi kukufahamu, pia nasema tena asante, nazani wewe ni mgeni kidogo hapa mjini siyo” aliuliza RCO, na swali ilo lilijibiwa na Careen, “yes! anaweek sasa”
Hapo Mlashani akakubari kwa kichwa, “kwahiyo ametokea #Mbogo_land kama wewe?” aliuliza RCO, kwa maana ya kwamba lilikuwa ni swali la mtego, maana rafudhi ya Peter, ilikuwa na chembe chembe za kabira lao, “hapana mimi nimwenyeji wa Mwanamonga, huko namtumbo” alijibu Peter, na hapo RCO akaitikia tea kwa kichwa, “ok! naitwa Cletus Mlashani, nazani umeshawai kunisikia” alisema Mlashani, lakini aikuwa kama anavyo fikiri, “hapana ndio na kuona kwa mala ya kwanza” alijibu Peter, jibu ambalo alikumshangaza Mlashani, “ok! kwakifupi mimi nikamanda wa upelelezi wa makosa ya jinai, mkoa wa Ruvuma, vipi lakini uliweza kuwaona vizuri hao jamaa na kuwa tambua kama ulisha wai kuwaona sehemu?” aliuliza RCO, “hapana kwanza alivaa kofia kubwa sana, alafu nilipo mtandika akakimbilia kwenye gari” alisema Peter
Hapo waliongea mengi, ikiwa na jinsi ilivyokuwa, ata dada wakazi akasimulia jinsi walivyo kutana na Sada, ambae aliawaachia nguo na viatu, baada ya Michael kumng’amua, na wao kuamua kutoka nje, huku wakifwatiliwa na mtu ambae, hapo mwanzo awakumtilia mashaka yoyote.
Baada ya hapo RCO na Peter wakapeana namba za simu, kisha wakaagana, huku wakipanga kuwasiliana kwaajili kushiriki chakula cha jioni week end ijayo “sawa bwana Peter, basi endapo utawaona tena, unaweza kunipa taarifa, pia kama unalolote unaweza kunipigia muda wowote” alisema RCO, kabla ajachukuwa kile kisu ambacho Dullah alikidondosha, kisha yeye na familia yake, kuingia kwenye gari na kuondoka zao, huku wakina Peter nao wakiingia kwenye gari na kuondoka zao, kuelekea upande wa mjini, wakikatiza kwenye vibanda vya mama ntilie, huku wanazungumzia matukio yaliyotokea kwa ghafla muda ule mfupi.
Lakini wakati wanakaribia kumaliza eneo ilo, wakashangaa kuona watu wamejaa kiasi cha kuzuwia barabara yenyewe, wakiwazunguka watu wawili, sambamba na sauti ya kilio, “jamani yoyo mtoto huyu, ameniweza mie” ilikuwa sauti ya kike, “Careen sauti hiyo ni kama ya mtu wakwetu” alisema Peter, huku akiendelea kumsikiliza yule mama alie kuwa analia, watu wa kwenu walitupokea vizuri sana jana, kamtazame kama niyeye kweli” alisema Careen alie kuwa amekaa kwenye seat ya dereva, huku anapiga honi, kuomba njia.
Bahati nzuri watu walikuwa wasikuvu, nao wakapisha na yeye akapitisha gari, nakwenda kuegesha gari ilo, pale lilipo kuwa limeegeshwa gari la wakina Emma, ambalo sasa lilikuwa limesha ondoka, “aya sasa nenda kamtazame, kama ni yeye ujuwe anashida gani, pengine anaitaji msaada” alisema Careen na hapo Peter akashuka toka kwenye gari na kuelekea pale kwenye mkusanyiko wa watu.****
Naam Emma na janja bado wapo ndani ya gariwana elekea mateka, huku Emma anapiga simu kwa Dullah, huku Janja akijaribu kutembea kwa mwendo wa kasi, kulifukuzia gari la wakina Dullah, ambalo walikuwa na uhakika kuwa limeelekea upande huo, simu ilichukuwa muda kidogo kisha ikapokelewa, “hoya Dullah, mbona unazingua, yani hupo kwenye mission alafu unachelewa kupokea simu?” aliuliza Emma kwa sauti ya ukali, “kaka ule mchongo siyo kabisa” alisikika Dullah akiongea kwa sauti ambayo ilikuwa ni utambulisho tosha kabisa kuwa Dullah aikuwa katika maumivu makali, “kwanini Dulla, sema haraka kimetokea nini?” aliuliza Emma wakati huo Janja alikuwa anapunguza mwendo kwenye round about ya songea girls secondary, kisha akazunguka na kuingia upande wa kulia yani kuelekea mateka, “kaka yani nilisha mchukuwa mtoto, lakini kuna fala mmoja akaingilia mchongo, ameniotea ngumi kama mbili hivi, sasa watu wakaanza kuongezeka, ikabidi niingie kwenye gari tukimbie” alisema Dullah. Hapo Emma akahisi tumbo lina unguruma, maana kiukweli ili ni tukio la pili linashindikana…..………..

