
KIAPO CHA MASIKINI (71)

SEHEMU YA 71
ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI : “kwanini Dulla, sema haraka kimetokea nini?” aliuliza Emma wakati huo Janja alikuwa anapunguza mwendo kwenye round about ya songea girls secondary, kisha akazunguka na kuingia upande wa kulia yani kuelekea mateka, “kaka yani nilisha mchukuwa mtoto, lakini kuna fala mmoja akaingilia mchongo, ameniotea ngumi kama mbili hivi, sasa watu wakaanza kuongezeka, ikabidi niingie kwenye gari tukimbie” alisema Dullah. Hapo Emma akahisi tumbo lina unguruma, maana kiukweli ili ni tukio la pili linashindikana…..………..Endelea…
sasa ata mwambia nini boss Kalonga “Dah! Dullah umearibu kila kitu, sasa nyie mpo wapi?” aliuliza Emma, huku anamwonyesha Janja ishala ya kupunguza mwendo, “tupo Manzese hapa kijiweni” alijibu Dullah na hapo Emma akashtuka, “acha ujinga wewe, ebu leteni gari haraka huku mateka, ujuwi kuwa polisi watakuwa wameshaanza msako, msisahau kubadiri namba za gari” alisema Emma kwa sauti ya ukali, na msisitizo, kisha akatulia kidogo gari likiendelea kushuka mtelemko wa daraja la mateka, huku Emma anawaza cha kumweleza boss wake, ili kuhusu kushindikana kwa mango wao wautekaji.***
Sada alitembea kwa haraka huku akiwaza juu ya mambo mawili aliyo ya shuhudia, moja kumwona Michael akiwa katika hali kama ile ya unadhifu wa kupitiliza, tofauti na week moja iliyopita, ambapo alionekana wazi kuwa ni mtoto alie lelewa kijijini, tofauti na leo ambao ameonekana kuwa ni mtoto alie lelewa katika familia ya kitajili, na kama aitoshi yupo na mfanyakazi, alie kuwa anamtazama, “yani yule yaya tu! anapendeza kuliko mimi mama yake” aliwaza Sada, huku anatembea kufwata barabara ya kwenda nyumbani kwao mahenge.
Sada aliendelea kujiuliza juu ya uweo wa Michael hapa mjini, tena katika mwonekano wa kitajiri, “inamaana Peter ajarudi kijijini, na kwamaana hiyo Peter alikuwa na fedha nyingine zaidi ya zile nilizo mwibia” alijiuliza Sada, huku anaanza kujutia kwa kumkataa Peter siku ile wamekutana pale mtini Pub, “bola ninge mkubari siku ile” aliwaza Sada, huku anaendelea kutembea, “na awa wazee sijuwi wamefwata nini?” alijiuliza Sada, ambae kwa hakiri yake anajiona alifanya vizuri kuwakataa, “yani wao wanahisi kuwa nina ghorofa, nani aliwaambia kuwa, watu wanapata maghorofa kiolela, wakati hiyo sehemu ya kulala yenye chumba kimoja” alijisemea Sada, huku anaendelea kutembea, “watarudi kama walivyokuja bwana, tena sitaki ata kusikia kilicho waleta” alijiesema Sada, huku kichwani mwake akipanga, cha kufanya, “nikifika nyumbani, niwashe ile simu alafu nimpigie mama Kachiki aniambie wakina mama wamefwata nini huku mjini, pia ata niambia kama Peter bado yupo huku au la” alisema Sada, huku anaendelea kuburuza sendo zake, kwenye njia za mkato za vumbi, huku njaa ikimchonyota tumboni mmwake.****
RCO Mlashani, akiwa njiani ndan ya gari lake binafsi na pamoja na mke wake na mjukuu wao, bado alikuwa na maswali mengi sana, juu ya mtu ambae alimpigia simu na kumweleza kuwa kuna kazi anajiandaa kumpatia, na kazi yenyewe ilikuwa ni hii ya kumkomboa mjukuu wake, “hii baba Sophy huyo mtu anaetaka kumteka Jasmin unamfahamu?” aliuliza mama Sophy, wakati safari inaendelea, “ndio najaribu kufikilia ni nani , lakini sipati jibu” alijibu mzee Mlashani, ambae alikuwa anaendesha gari, maana yule dereva wake alishaondoka na gari la serikali, “lazima watakuwa ni kati ya waharifu ambao unawachunguza au ambao umesha wakamata” alisema mama Sophy, aliekuwa amempakata Jasmin.
Naam hapo nikama mama Sophy alikuwa amemfungua hakili, mume wake, yani bwana Mlashani, “hoooo! sasa napata picha kamili, huyu atauwa ni Kalonga” alisema Malshani, huku anacheka kidogo, “ni mpuuzi sana huyu bwana mdogo, sasa nikifika nyumbani nita mchokoza, ili nione ata hamaki kiasi gani” alisema Mlashani, ambae sasa alikuwa anakaribia kukata kona ya kuingia nyumbani kwake.
Yap, baada ya Mlashani, kuingia nyumbani kwake wote wakashuka tka kwenye gari, na kuingia ndani, ndipo kamanda mlashani alipo chukuwa simu yake na kuanza kupiga kwa makanda mbali mbali wa idara, akiwajulisha akuwa amesha mpata mjukuu wake, na mwisho akawapigia makamanda wakuu, yani RPC na staff officer kuwajulisha juu ya tukio ilo, huku akipanga baada ya hapo, apige simu kwa OC CID, kuomba namba ya Kalonga.***
Naam mzee Nyoni, sasa aliweza kuona watu wengi wakiwa wamewazunguka, wakiwasangaa kwa jinsi mke wake alivyokuwa anapolomosha kilio, kilio cha mke wake kili kusanya mambo mengi, ikiwa ni hali waliyo mwona nayo Sada, ambae alionyesha wazi kuwa maisha yake ni magumu sana kule mjini, pili mama Sada, alilia kwa kukataliwa na binti yake mwenyewe, ambae amejifanya awajuwi kabisaaaa, tatu atarudi vipi kijijini, maana waliitaji elfu tano kwa wote wawili, ili waweze kufika japo namtumbo, ili wtembee kilomita zaidi ya nane kufika mwanamonga, achana na nauri, kulikuwa na deni linalowasubiri kule kijijini, deni la elfu tano, waliyo iazima kwaajili ya nauri, ilo siyo tatizo kubwa kama watajieleza vizuri, juu ya kile kilichotokea huku mjini, sasa inshu ni vipi wataanza kueleza kilicho watokea huku mjini, niaibu kiasi gani kita wakuta mala baada ya kueleza jambo ili.
Wote wawili wanapofikilia ilo, wanajikutana nwazidi kupatwa na machungu, na mama Sada anazidi kuangua kilio, “jamani sahamani naomba niwatambue awa ndugu, pengine nawafahamu” ilisikika sauti ambayo ilimfanya mama Sada akaache kulia, kisha yeye na mume wake wakatazama, kule ilikotokea sauti, ambako walimwona kijana mtanashati, alie kuwa anajipenyeza kwenye kundi la watu, kuja pale walipokuwepo wao.
Naam wote wawili walijikuta wanainamisha macho chini kwa aibu, ni mala baada ya kumwona Peter, kuwa ndie kijana aliekuwa anaitaji kuwaona, ili awatambue kama anawafahamu, “mama yangu tumeumbuka leo” aliwaza mzee Nyoni, huku mke wake akiendelea kulia kwa sauti ya chini, mzee Nyoni aliona ni bora wange kutwa na mtu mwingiene yoyote wa kijijini kwao, lakini siyo kijana huyu, ambae ndie alikuwa mume wa binti yao, kama hiyo aitoshi kijana huyu alisha zaa na binti yao, lakini walisha mfanyia mambo mengi sana, na pia kuna uwezekano wa kuwa, kijana huyu ambae alikuja mjini kwa nia njema ya kukutana na binti yao iliwarudiane, na yeye akamuibia, na kumroka baba huyo wa mtoto wake, hiyo siyo mzee Nyoni pekee ata mama Sada, aliona kijana huyu, asingeweza kuwasaidia kwa haya ambayo yalikuwa yametokea, siku za nyuma.
“mama, baba, nini kimetokea, mme kujalini huku mjini, Sada amepita sasa hivi je mme mwona?” aliuliza Peter, kwa sauti ya mshangao, aliuliza maswali kadhaa, lakini akupata jibu la swali ata moja, baada yake wazee wale wawili walikuwa wameinamisha vichwa chini, huku mama Sada akiendelea kulia, lakini safari hii ikiwa ni kwa sauti ya chini, “baba kuna nini kime tokea unaweza kunieleza tatizo nini ili tuweze kutatua” aliliza tena Peter, kwa sauti iliyojaa urafiki, “kaka unawafahamu awa wazee” aliuliza mmoja kati ya mashuhuda, waliokuwepo pale, “ndiyo ni wakwe zangu wa zamani, tumetoka kijiji kimoja” alijibu Peter, ambae alionekana kuumizwa na hali waliyokuwa nayo wale wazee wawili, “bro ni vyema kama utawachukuwa ukaongee nao mbele ya safari, hapa walikuwa wanaonge na mwanamke mmoja hivi, kabla huyu mama ajaanza kulia” alisema mtu mwingie kati ya mashuhuda, na wengine wakaunga mkono wazo lile.
Basi Peter akawachukuwa wazee wale wawili na kwenda nao kwenye gari, nao wakaingia kwenye gari, wakikaa seat ya nyuma kabisa, na hapo wakaweza kumwona yule mwanamke alikuja na Peter jana, kule kijijini, ambae aliwasalimia kwa sauti iliyojaa upendo, “pole sana jamani, kwani kimetokea nini?” aliuliza Careen, wakati huo gari bado lilikuwa lime simama pale pale, lakini linaunguruma. na hapo mzee Nyoni na mke wake wakaanza kueleza kilicho tokea, kuanzia siku Sada alipo wadanganya, kuwa ananyumba kubwa, nakwamba yeye Peter na Michael walifikia kwake.
Pia walieleza jinsi Sada alivyowaambia kwamba, kuna mizigo kwaajili yao, hipo njiani inaelekea kijijini, mzee Nyoni na mke wake wakaeleza wavyo amua kuchukuwa maamuzi ya kuja mjini kumwona binti yao, ambae licha ya kuangaika kumsaka, na kufanikiwa kumpata, lakini matokeo yake amewakataa kwamba hawajuwi, ilikuwa ni hadithi ya kusikitisha toka kwa wazee wale wawili, hadithi ambayo iliwaumiza wote mle ndani ya gari, kiasi cha Careen kupiga simu, ofisini kwake, kwamba aje dereva mmoja na gari, wata kuta kwenye maegesho ya chini ya pale NPF.
Nikweli Careen sogeza gari kwenye maegesho hayo na kuegesha gari wakisubiri gari jingine lije, na ndio wakati ambao, Peter nae alisimulia jinsi alivyopokelewa na Sada, ambae alimwibia na kumtelekeza hotelini, bila ata shilingi moja, na nguo zenyewe alizo iba ni hizi hapa, na bagi lililokuwa na fedha ni ili hapa” alisema Peter akionyesha begi ambalo lilikuwa kwenye seat waliyokuwa waamekaa wakina Michael na dada wakazi.
Michael akaeleza jinsi alivyokutana na Sada siku yapili, na akaeleza jinsi Sada alivyotoa kiao cha kuto kurudiana nae, na kile ambacho alikiomba kimkute, endapo ata rudiana na Peter, ata ile kauri ya kwamba akuwa na mtoto, na nisimtambue kama mama yake “inamaana amemkana mpaka mtoto?” aliuliza mama Sada, kwa mshangao mkubwa sana, “sasa unashangaa ninikama amekukataa wewe mama yake mzazi, ata shindwaje kufanya hivyo?” alisema mzee Nyoni, akionyesha kuitambua vyema tabia mpya ya binti yao****
Naam, ndani ya muda mfupi tayari habari za kunusurika kutekwa kwa mtoto wa RCO zilitambaa kwa watu wengi sana, kupitia mitandao ya kijamii, kati ya watu walio ipata taarifa hivyo ni RPC na staff officer, ikiwa ni muda mfupi toka wapigiwe simu na RCO mwenyewe, kuwaeleza juu ya tukio ilo, ukweli iliwashangaza sana ujasiri wa mtekaji, ambae nikweli aliigasimu kwa RCO, muda mfupi kabla ya jaribio.
Watu wengi, akiwepo RPC na staff officer, waliweza kuona video ya kijana alie kuwa anazungumziwa kuwa, ndie shujaa alie mwokoa mjukuu wa RCO, ambae pia alionekana video ile, ambayo ilikuwa inaendelea kusambaa kwa kasi sana, na kuwafikia watu wengi sana, “Mlashani, huyu kijana uliwai kumfahamu mwanzo, naona hapa Careen anamtamburisha kuwa ni mume wake, mbona sija waikusikia kuwa huyu mwanamke anamume, hapa mjini” aliuliza RPC, mala bada ya kumpigia simu RCO, kuzungumzia ile Video, “ata mimi mwanzo nilishangaa na kumtilia shaka huyu jamaa, lakini nilipomsikia Careen akisema vile, nikaondoa mashaka yote juu yake” alisema RCO Malashani.
Makamanda hao waliongea mengi ikiwa na kujadiri nani anaweza akawa nyuma ya jambo ili, “mpaka sasa afande, kuna mtu mmoja nina mfanyia uchunguzi kuwa anaweza kuwa nyuma ya ili” alijibu RCO Mlashani, ambae tayari kichwani mwake, alisha anza kutilia mashaka bwana Pitus Kalonga, mtu ambae jana alimwita kituoni, na kumwachia bila kumfanya lolote, ikiwa ni mpango wa kubaini kama, kuna mtu anae msaidia kupata taarifa za kijeshi na yeye kuweza kuficha ushaidi au kuwakwepa polisi, “sawa RCO, nazani kesho utanipa taarifa kamili” alisema RPC, kabla ya kukata simu.****
Naam bada ya maongezi ya muda mrefu ndani ya gari pale NPF, hakika wazazi wa Sada, yani mzee Nyoni na mke wake, walisikitishwa na kile alicho kifanya binti yao, kwa kijana Peter na mtoto wake Michael, sijuwi ni kwavile na wao liliwakuta, maana waliumia sana mioyo yao, kwa kitendo kile cha binti yao, kuiba fedha za Peter, na kuwakana mume wake na mtoto wake mwenyewe.
Gari dogo aina ya Toyota wish lilifika, na kuwachukuwa wakina mama Sada, huku dereva akikabidhiwa shilingi laki moja za kitanzania, kwamba ahakikishe wazee wale wanapitishwa madukani, kununua vitu vya kwenda navyo Mwanamonga, na kiasha awai saa nane kuwapeleka stendi, wakapande basi na kurudi kijijini, nao walishukuru sana, na kuomba msamaha kwa Peter juu ya kile kilicho tokea, kati yake na Sada, nao wali kili kuwa wamegundua kuwa walikuwa wanakosea kusimama uande wa binti yao, pasipo kum onya, kwa lolote, juu ya yale anayo ya fanya.
Ilikuwa hivyo, wakina mzee Nyoni, walitembezwa mjini, wakifanya manunuzi, yanguo chache, na vitu vidogo vidogo, ambavyo wangebeba kijijini, pamoja na kwenda sehemu na kupata chakula, kabla ya kupelekwa stendi kupanda gari, huku mioyoni mwao wakimshukuru sana Peter, ambae huku wakitambua na kukili kuwa binti yao, amepoteza mwanaume bora.**
Naam akiwa nyumbani kwake bwana Kalonga, akisubiri taarifa ya kufanikiwa kwa mpango wake wa kumteka mjukuu wa RCO, huku anapata glass ya pombe kali, na sigara yake kwa pembeni, hakauwa na wasi wasi wowote juu ya kubainika na RCO, kuwa yeye ndie alie fanya mchezo wa utekaji, maana simu alipiga kwa private number.
Wakati bwana Kalonga anaendelea kunywa Pombe yake, mala akasikia simu yake inaanza kuita, hapo Kalonga akatabasamu kwa kuona sasa anapewa taarifa za kupendeza, “yes mambo yame iva” alijisemea Kalonga uku anaichukuwa simu yake mezani na kuipokea, kisha akaiweka sikioni, “niambie Emma mpango unaendaje?” aliuliza Kalonga kwa sauti ambayo ilionyesha kuwa alikuwa anahamu ya kusikia matokeo, ya jaribio lake la utekaji, “bwana Kalonga vijana wameshindwa, nivyema ukabadiri mpango” ilisikika sauti tulivu iliyojaa upole na ustaarabu, toka upande wapili wa simu.
Hapo Kalonga akashtuka kidogo, maana akuitaji ufafanuzi toka kwa mtu yoyote, ili kuitambua ile sauti, ambayo alikuwa ametoka kuwasilina amida ya saa tano za asubuhi, na hapo ndipo alipo gundua kuwa, akuitazama namba ya mpigaji, kabla aja ipokea ile simu….. itaendelea

