KIBOKO YANGU (05)

KIBOKO YANGU 5

Nilishikwa na hasira sio siri nakuona kama Robert amezidi kunifanyia ujinga, nilienda chumban kwangu ila muda wote nilikuwa nawaza nifanye nini ambacho kitamkomoa Robert maana nilitaman aniheshimu na aniabudu kama wanavyofanya wanaume wenginewote ninao walipa….
Iloa kila nilichofanya kwa Robert kilikuwa mwisho wa siku kina nigeukia mimi na kunikera, nilikaa karibu masaa mawili nikiwaza nifanye nini, mwisho nikajan na wazo, nikavaa kijitaulo kisha nikachukua sabun na ma brush kisha nikatoka zangu ukumbini, na nilipofika nikaita “ Robert, akaitikia maana wakatv huo alikuwa ameshamaliza shughuli zake na alikuwa amepumzika kwenye stoo ambapo ndio chumba chake, baada ya dakika chache alifika, kisha akasema “ naam madam, kuna jambo lolote lile ambalon naweza kukusaidia…
“ ndio naomba unioshe kucha, nikasema na nikashangaa anaanza kucheka, kisha akasema “ kwa mara ya kwanzaq tangu nikujue umekuwa na heshima, embu sema tena, nikabaki nimetoa macho maana sikuona ni kitu gani cha heshima ambacho nilikuwa nimekisema pale…
“naomba useme tena boss, akasema robert
“usiniletee utan wako hapa, rmbu nioshe kucha haraka, nikafoka…
“ aahhh boss unaharibu sema tena kama ulivyosema mwanzo, yaan sema “ naomba unioshe kucha, yaan mpaka nilisikia raha, akasema Robert, nikajikuta nimetabasamu bila kutaka, akaona autumie upenyo huo huo kuanza kunisifia sasa, akaanza “ ona sasa hizo dimple zako, yaan ukitabasamu najiona kabisa namna unavyonipoteza, ila wewe mtoto ni mzuri jaman, akasema Robert, nikajifanya nakaza sura kwa maana sikutaka kuendeleza matani yake…
“ sitaki utani na ufanye ninavyotaka sasa hivi, nikafoka…
“nipo tayar kufanya kila unacxhokitaka, kwa maana nikikukatalia najiona kabisa kama nimefanya dhambi kubwa sana ambayo haistahili msamaha, akasema Robert
“ una nini lakin wewe, nikasema huku nikiwa nimekunja sura..
‘ siwez kuwa na jambo lolote zaidi ya kukupenda, maana ni ngumu sana kuishi na mwanamke mrembo kama wewe alafu nisikupende, nina uhakika hauta nihukumu kwa hilo, akasema Robert..
“ mimi ni boss wako, na unatakiwa uniheshimu kama boss wako nasio kapurwa mwezio, na nikuambie tu acha kujidanganya kuwa naweza kulala na mwanaume kama wewe mnuka njaa mmoja, nikasema kisha nikawa naondoka zangu kwa maana niliona kama ananizingua tu…

Nikashangaa kanishika mkono kisha akanivuta karibu yake kisha akawa ananiangalia machoni na akaanza kusema “ kama kujidanganya ni kosa acha niangamie, maana nimeshajidanganya sana kuanzia siku ya kwanza nakuona, na hauwez amin najisikia vzr nikifikiria kuwa kuna siku utakuwa wangu hata kama sio kweli, akasema Robert, kuanzia nimeanza kuwa kwenye mahusiano sijawah kuwa na mwanaume mwenye maneno matamu kama Robert,simulizi hii imeandikwa na simulizi za husqer baltazar, hakikisha unaisoma kwenye account ya husqer baltazar pekee, nilitaman kutabasamu ila niliona kama nitampa kichwa…
ila mpuuzi huyu ni kama alikuwa ananijua vzr akaanza kusema “ usifiche tabasamu lako ambalo linakufanya uwe kama ua machoni mwa mwanaume yoyote Yule rijal, tabasamu tu ili uupe nguvu urembo wako na kuondoan athar zozote zile za makunyazi na uzee, tabasamu hata kidogo ili uusisimue moyo wangu, tabasamu tu mamaa ili nizidi kuwa kichaa kwa ajili yako, akasema ribert kisha akanivuta na kunikumbatia, kisha akaninong’oneza na kunambia kuwa “ nitahakikisha unakuwa peace ambae nilimpenda siku ya kwanza nilipomuona,.
Maneno yake yalinisisimua sana, na nilijikuta nataman sana aendelee unisifia na kunikumbatia, nilitaman niendelee kuihisi pumzi yake, nilitaman niendelee kuhisi joto la mwili wake, ila badala yake ainiachia na kwenda jikon na baada ya dakika kabdaa alirudi na beseni pamoja na ndoo ambayo ilikuwa na maji ya moto…

Nilibaki nimeduwaa na namjuangalia muda wote ambao alikuwa jikon, na hata alipokuja kunikalisha nilitulian kama kazezeta flani hivi, akanikalisha chini kisha akachukua miguu yangu na kuiweka kwenye beseni, alianza kuimassage taratibu kitu ambacho kilikuwa kinanipa msisimko wa ajabu, na baada ya hapo alianza kuniosha miguu, sio siri nilijisikia vzr sana, na kutaman asimalize anachkifanya, ila baada ya muda flan alimaliza kila kitu, kisha akanikausha miguu yangu na kusimama kisha akanambia, “ kuna chochote ambacho naweza kukusaidia boss…

Nilitaman kumuambia anioshe mwili mzima ila niliona kama nitakuwa mdhaifu kwake, niliona kama ataniona nambababikia sana, nikasimama na kusema “ huduma yenyewe mbaya, najuata hata kuoshwa miguu na wewe…
Aliniangalia kisha akacheka na kusema “ hiloo akati mpaka ulikuwa unasinzia, usikute nimeshakufanya uharibu mambo ndio maana unaninifokea, naweza kukupa hata huduma zingine za kitandani ila sikupi ng’o, maana una dharau kama umeshawah kutengeneza hata sisimizi, kisha akaondoka zake, nikajikuta nimeshikwa na hasira kwa yale maneno ya Robert, nilikuwa nimeshika kakisu kadogo, si nikamrushia, sadsa alikuwa amegeuka kuniangalia, saa ngapi kisimpate cha shavu, na wakat huo huo damu zikaanza kumwagika, sio siri niliogopa sana, nikamuita mlinzi kisha tukamchukua na kumpeleka hospital, walikataa kumpokea bila pf3, ila nilihonga hela mpaka wakamchukua na kuanza kumuhudumia, alishonwa shavu, maana nilimchana sana, baada ya kutoka pale wale madaktar wakamshauri aende hospital na hata hakunisemesha akanyanyuka na kuondoka, nilikuwa na mashaka sana, na kweli alienda mpaka polisi, na baada ya kwenda akarudi nyumban, nilikuwa na mashaka nae sana, nilihisi amekuja kunichukua na kunipeleka ndani, alipoingia ndani akaachia tabasamu kisha akasema “ boss nina shart la kukupa kama utakubali sitakufungulian mashtaka ya kiunidhuru kwa kukusudia, akasema Robert

“ yaan unataka kumfunga boss wakpo, haya kanifunge tuone kama nitakaa ndani kama unavyofikiria, nikasema kwa nyodo, aliachia tabasamu kwa mara nyingine kisha akachukua simu na kubofya namba kadhaa na baada ya muda mchacxhe simu ikaanza kuita, nilisikia tu neon “ afande mnaweza kuingia sasa, na baada ya dakika chache waliingia maaskari watatu ambao walikuwa wamevaa maganda na mmoja alikuwa mwanaume na wanawake wawili, akasema “ ni huyu mnaweza kwenda nae sasa…
Sikutegemea kabisa kama mfanyakazi wangu mwenyewe anaweza kunipeleka ndani, kweli nilichukuliwa na kupelekwa cetral, kama masikhara nililala hapo usiku kucha, yaan sikuwah kutegemea kama naweza kulala ndani hata siku moja kwenye maisha yangu, sikuwah kutegemea kama kuna siku na mimi nitashtakiwa na wakat nilikuwa najiona kama nimeshajipata, sikuweza hata kumuambia mtu yoyote Yule kuwa npo ndani, ni lazima alieniweka ndio aje kunitoa, na asubuh ya saa moja Robert alikuja pale polisi, aliniletea chai ila sikutaka kabisa kunywa, nilikuwa na hasira nae sana, akacheka kisha akasema “ hiki kisiran chako kinaelekea kuisha muda si mrefu………………
Alinisogelea kisha akasema “ nimekuja kiukutoa ila kwa sharti…
“ sharti gani? nikauliza…
“ unatakiwa kusign hizi nyaraka sasa hivi na baada ya kusign ni lazima utoke humu, kwa kuwa nilikuwa nimeshayachoka maisha ya mule ndani,kwanza kulikuwa kunanuka mikojo mno,na kwa hadhi ambayo nilikuwa nayo sikupenda kuendelea kuishi maeneo kama yale…
Nilichukua hizo nyaraka na kusign na kwa akili zangu fupi zikawa zinanituma kuwa Robert alikuwa anataka pesa tu, maana nilimuona kama mtu asie na muelekeo wa maisha…
Nikasign kweli na baada ya muda mchache nikaachiwa na nilikuja kuchukuliwa na mlinzi wangu na nilipofika nyumban nikamkuta Robert mlangoni akiwa na liplasta lake usoni akinisumbiri, aliponiona tu alikuja kunikumbatia na kusema “ karibu nyumban mke wangu..
Nilimsukuma huko na kumuambia “ acha ndoto zako, nambie ulikuwa unataka shingapi nikulipe maana umekuja kuyavuruga maisha yangu, na sitaman tena kuendelea kuishi na wewe, akatoa zile nyaraka na kunionesha kumbe nilikuwa nimesign nyaraka za ndoa……..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata