KIBOKO YANGU (07)

KIBOKO YANGU 7

Sasa akaanza kuweka sharia, akawa hataki nitoke, nilikuwa namshangaa sana, kwa sababu yupo nyukmban kwangu kwanini ananipangia maisha kiasi kile, na alikuwa anataka niamke asubuhb nimuandalie chai, na nimuhudumie kama mume wangu, ila hata sikuwa nafanya hata kimoja anachokitaka nilitaka nione atanifanya nini, mwanzo alikuwa ananiagiza kisha anakaa kimya…
Siku hio nilikuwa najiandaa zangu niende kwenye miradi yangu nikashangaa linakuja gari la crdb, wakaweka mabango kwenye nyumba yangu kuwa nyumba inauzwa, nilishangaa sana kwa maana sikuwah kucxhukua mkopo hata mara moja huko crdb, sasa inawezekana vipi wauze nyumba yangu…
Niliwafata na kuwauliza, ila wakanambia kuna mkopo wa kama million nane umechukuliwa miezi saba iliopita, na kilichowekwa dhamana ni hati ya nyumba…
Nilikataa kata kata kuwa mimi sijawah kuchukua mkopo ila hata hawakunielewa, nikaomba basi wanipe muda nitawapa pesa zao, maana kutafuta million nane haikuwa ishu kubwa sana kwangu, ila napo hawakunisikiliza, ikabidi nimpigie simu mdogo wangu mmoja, maana yeye ndio nilimuachia hati zangu, na kumuuliza imekuwaje mpaka hati za nyumba yangu ziwe mikonon mwa crdb na sio kwake, akaanza kuniomba msamaha, nikajua lazima yeye ndio kaniharibia mambo, sikutaka hata kumsikiliza kwa maana nioliona kama atazidi kunivuruga tu, na hana kingine ambachpo anaweza kunambia…

Alinitumia sms inasema “ samahan sana dada, unaweza ukanipoa adhabu yoyote ile ambayon unataka ila ni shemeji yako alikuwa anataka pesa nyingi kwaajili ya kufungua biashara, nikaona nikamkopee na akaniahidi kwa miezi miwili atarudisha hio pesa yote, ila biashara haikwenda vzr ndio maana tukashindwa kulipa, naomba nisamehe sana dada, niliona kama ananivuruga tu kwa maana muda huo sikuwa nataka maelezo nilikuwa nataka million nane za watu ili nyumba yangu isiuzwe, Robert muda wote alikuwa kimya ananiangalia ninavyohangaika, nikaingia ndani kisha nikawa naangaika kuwaomba watu wanikopeshe, ila hakuna mtu hata mmpja ambae alikuwa tayar kunikopesha million nane, mara Robert akaniita, nikapuuza kwa maana nilihisi kama atazidi kuniongezea hasira..
Akaniita tena, wala sikumjal, ikabidi anifate kisha akaniuliza “ ni lini utaacha kiburi wewe mpuuzi…
“ siku ambayo utaondoka kwenye maisha yangu, nikajibu kwa nyodo…
“ kuondoka kwenye maisha yako sahau kabisa kuhusu hicho kitu kwa maana hakitakaa kiwezekane, labda wewe uanze kunipenda na kujifunza kuishi na mimi, akasema Robert
“ naomba usinichanganye, kwa maana wewe mwenyewe unaona nina matatizo na wewe unaniletea upuuzi wako, nikafoka…
“ sikuletei upuuzi wife ila nataka nikusaidie, akasema Robert
Nikacheka kwa dharau kisha nikasema “ wewe, yaan wewe ambae nakulisha na unachambia maji ambayo mimi ndio nalipia bill unasema kuwa utanisaidia, haya niambie utanisaidia vipi zaidi ya kuniletea upuuzi wako, haya nipe hio million nane sasa hivi niuone uanaume wako, nikasema kwa dharau…

Robert akatabasamu kisha akasema “ nitakupa ila kwan sharti..
“ sharti gani? Nikauliza
“ nikiss hapa, akasema Robert akiwa anashika lips zake..
“ hivi wewe unakichaa, yaan niache kuwaza namna ya kuikomboa nyumba yangu nianze kufanya kazi kichaa ya kukukiss wewe, embu acha ndoto zako za mchana, nikasema..

Robert hakutaka hata kusikiliza maelezo yangu, akanisogelea na kunikiss, ila huyu mwanaume alikuwa na lips tamu, na alikuwa anajua kukiss mno, sijui hata alijifunzia wapi, yaan aliumaliza ubishi wangu wote, nikajikuta na mimi nampa ushirikiano kwenye kiss, tumemaliza akaingiza mkono mfukoni kisha akatoa card yake kisha akasema “ twende tukachukue hela, ila hakikisha unakuwa mke bora kwangu na tutaandikishiana, na kama hautafanya kama ni9nachokitaka nitaiuza hii nyumba mimi na sio crdb tena, nilikubali ingawa sikuwa na iman kama Robert anaweza kuwa na pesa zote hizo, kwa maana alikuwa anaoenakana kama mwanaume wa kawaida tu…
Tumefika bank card ikamezwa, nilihisi kuvurugwa na tulipoingioan ndani kuuliza, wakanambia kuwa tunatakiwa kusubiri masaa 24, nilihisi kuvurugwa, akataka turudi nyumban, nilikuwa kama nimechanganyikiwa kwa maana hata sikuwa namuelewa alikuwa anaongea nini, alijua hilo, alinishika na kunipeleka kwenye gari kisha akanirudisha nyumban, ila tukiwa njian akanambia nisign karatasi za mimi kukiri kuwa nitakuwa naishi kama mume wake na sio kijakazi wake, nilikataa kwa maana sikuwa na uhakika, akalazimisha sana ila niligoma, akachukua kidole gumba change na kukichovyesha kwenye wino kisha akaweka kwenye lile karatasi, yaan ni kilazima…
Na wakat tunafika nyumban sikumuona mtu hata mmoja, kwa maana hata wale waliokuja kuuza nyumba yangu hawakuwepo kabisa, nilishangaa na robet akasema “ nimeshawalipa haya twende ukawe mke kwangu sasa…

Sikuamin macho yangu, nilijikuta namfata na kumkumbatia, kisha nikamshukuru sana na kumuambia nipo tayar kufanya kila anachokitaka, akaniangalia kisha akatabasamu na kusema “ sina ninachokitaka zaidi ya kuishi kama mke wangu na unitii kama mumeo, akasema Robert nikatabasamu na kusema kuwa niko tayar…

Ishi ikaja kuwa, nilikuwa nimezoea kufanyiwa kila kitu na wafanya kazi, yaan nina muda mrefu sana sijawah kufanya kazi yoyote ile zaidi ya kula na kutembea, ila Robert sasa akawa anataka akiamka asubuh akute nimeandaa chai na vitafunwa kwa mkono wangu, akute niumefanya usafi wa nyumba nzima, nilikuwa nakasirika sana, ila alikuwa ananiambia kuwa ananidai, kwa hio kama siwez kufanya anavyotaka basi nimlipe hio hela…
“basi naomba nipe mwezi mmoja na nitakulipa pesa yote unayoitaka, nikasema, nikashangaa Robert anacheka kisha akasema “ najua unawaza kudanga na wakat tayar wewe ni mke wewe ni mke wa mtu, haya nambie unataka kwenda kudanga na nani?…

“kwani wewe inakuhusu nini, niende kudanga au nisiende ni maisha yangu na hakuna mtu hata mmoja ambae kuna chochote kile kinachomuhusu, hivyo naomba uachane na mimi, na maisha yangu hayamuhusu mtu yoyiote Yule, nikasema
“ hayamuhusu mtu yoyote ila yanamuhusu mumeo au ujui kama umeolewa…
“ ndoa ganin unayozungumzia, ndoa ambayo mwanamke amelazimishwa kuwa mke, hakuna ndg wala rafiki hata mmoja anaejua kuwa nimeolewa alafu unakuja kunambia ety nimeolewa, hakuna anaeruhusiwa kunioa mimi zaidi ya pesa, naondoka kwenda kutafuta hizo pesa zako ili usije ukaninyanyasa tena, nikasema na Robert akaniangalia kisha akasema “ haya nenda…

Kweli wakat huo huo nikaingia chumban kwangu kisha nikaanza kuoga na kujiandaa, nikavaa kagauni change kafupi cheupe na viatu vyangu vya dark blue na pochi ya dark blue, na hivi nina kashepu cha kujambia mbali, utanitaka, nikatoka nikampita hata hakunisemehsa, nikampigia sugar dad wangu mmoja na kumuomba nionane nae, na huwa hakataagi kabisa, akakubali, basi tukapanga sehemu ya kukutana nae, huyu mzee kulala nae siku moja ni million moja kupanda, yaan ni kimwaga balaa, nikajua nikilala nae wiki tu tayar nitakuwa nimetajirika….

Sasa bibi mimi huyo mpaka sehemu ambayo tulipanga ukutana, nikaenda mpaka chumba alichonambia, nikaenda mpaka kwenye kile chumba nikafungua mlango, ile naingia ndani, nakutana na sura ya Robert akiwa amefunga taulo kana kwamba ametoka kuoga, na alikuwa anamimina shampein kwenye glass, akasema “ karibu wife wangu, samahan nimekusuprise ila naomba uje tufurahie honeymoon yetu….

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata