
KIBOKO YANGU 9
Kipindi nilipokuwa bint mdogo wa kama miaka 12, niliwah kukutana na kijana mmoja ambae alikuwa kama anamiaka 14, alikuwa anaitwa Robert, alikuwa amehamishiwa kwa shangazi yake kwaajili ya masomo kwa maana alikuwa anawasumbua sana wazaz wake kuhusu kusoma, hivyo wakampeleka kwa shangazi yake ili walau amazlize darasa la saba tu, alikuwa kijana mtanashati sana na alikuwa anaonekana kama ametokea kwenye maisha kidogo mazuri, siku hio nilikuwa napiata, akanipiga na mpira bahat mbaya, kipindi hicho, nilikuewa kabint flani hivi kapole kasichokuwa na makuu, alinifata na kuniomba msamaha, ila nilimtoa hofu na kumuambia kuwa asijal kwa maana sikuwa nimeumia, ila aliniona nimevimba, akaniomba anifanyie huduma yan kwanza, alikuwa amelegea huyo, hata kushika plasta hakuwa anajua, nikaanza kumcheka, akanambia kuwa “ anaweza kwenda kuninunulia kitu ninachotaka kwa aajili ya kumsamehe, nikamwambia kuwa akaninunulie icecream, na urafiki wetu ukaanzia hapo, alikuwa ananipenda sana, na aliniahidi kuwa tukiwa wakubwa atakuja kunioa….
Nilikuwa nadhan ni utani, la wakat wote alikuwa ananihusia kuwa nijitulize na atakuja kunioa yeye, tulikuwa tunapendanan sana, ila alipomaliza darasa saba wazaz wake walikuja kumchukua, na kabla hajaondoka ndio akaniachia usemi unaosema kuwa “ friendship is sweet like lollipop, akanambia kuwa tutakapokutana ukubwan, ikiwa mmoja wapo atakuwa kamsahau mwenzake basi autumie huo msemo nan tutakumbukana, kiukweli sikuamin kama naweza kukutana na Robert na mbaya zaidi nimemfanyia mambo mengi ya kipuuzi kwa chuki zangu za kuchukia wanaume……
“nimekuja sasa kukuponya maradhi yote ya moyo uliokuwa nayo, nimekuja kukufanya ujisikie mwanamke wa pekee sana kwenye hii dunia, ila niahidin kuwa utaacha ujinga wote na kuamua kuishi na mimi kama mumeo na kama haujakubali ndoa yetu nitakuchumbia upya na kila mtu atajua ni kiasi gani nimekuwa nikikupenda miaka yote hio….
“ embu nambie umenipata pata vipi? Nikauliza…
“ haikuwa kazi ngumu sana kutokana na maisha ambayo ulikuwa unaishi, kwanza nilikuona siku moja kwenye hotel moja hivi ulikuwa na mbaba mwenye kama miaka hamsini naa, ulikuwa unajichetua chetua pale, nikahisi kuwa nimekufananisha, kwa maana nilikuwa namjua peace ambae alikuwa ni bint mwenye adabu na aibu sana, nilihisi nimemuona mwanamke aliefanana na wewe na sio, wewe ila nilipokuja kuuliza jna lako ndio nilichoka, ndio nikaambiwa kuwa unaitwa peace, mama ya mahaba, toa pesa nikupe utamu, huyo alienambia hio kauli nilitaman kumuweka kibao, kwa maana niliona kama ananiumiza, nikaanza kukuonea wivu upya na kuanza kufuatlia mienendo yako, akaendelea kusimulia Robert ….
“nikaja kugundua kuwa ulikuwa ukinunua wanaume kwenye maisha yako, na ukawa unawatumikisha kingono, na endapo ukiishiwa pesa ulikuwa unanunuliwa wewe, hizi kauli ziliniumiza sana, kwa maana nilijihisi kama nimechelewa kukufahamu au sikuwa nakujua vizuri, ila nilipokuja kufuatilia namna unavyowafanyia wanaume, ilikuwa ni wazi kuwa ulikuwa unalipiza kisasi, hivyo nikata kujua kuwa ulikuwa unalipiza kisasi kwa wanaume kwa sababu gani, yaan sikujua bint mdogo kama wewe unawezaje kuwa na chuki kubwa kiasi chote hicho na wanaume ambao hata hawajakukosea wao, nikaanza kufuatilia kila mwanaume unaemnunua na kuanzisha urafiki nae, walikuwa wanakusifia kwa kumwaga hela, ila walikuwa wanakusema sana, kwa kuwanyanyasa kingono, kwa namna walivyokuwa wanakuongelea ni kama umechanganyikiwa, kwa maana chuki yako ilikuwa inaonekana wazi kabisa kuwa ni kubwa sana kuliko hata utu na ubinaadamu wako, akawa anasema Robert ….
“ basi nikaanza kutafuta namna za kuingia kwenye maisha yako, ilikuwa ni ngumu sana, kwa maana sikuwa nataman kununuliwa kama unavyowanunua wanaume wengine na nilikuwa naona kama ni uzalililishaji, ila mbinu zote nilizokuwa naziwaza za kukuingia nilikuwa naona kama hazifanyio kazi, ndio nikaamua kujichetua ile siku niliokutana na wewe ukiwa na meshack, nambie yule jamaa alikupa penzi tamu eee, maana huwa anasifika kwa kuwaidhisha wanawake, na hio ndio kazi yake mjini, akaendelea kusema Robert …
“ wala hakunifanya chochote, kwanza hata hajui mapenzi, nikajitetea…
“ najua huwez kukubali, lakinkuanzia nimeanza kukufuatilia, nimeona kuwa meshack ndio mwanaume pekee ambae ulimleta na gari lako mpaka anapoishi tena ukamlipa mara mbili na wakat sio kawaida yako kabisa, akasema Robert ……
“ hamna kwanza ananuka jashon baya, nikasema, Robert akacheka kisha akasema “ ni sawa.. ni sawa…
“ basi ndio ikawa hivyo, nikawa nataka kupata nafasi ya kusihi na wewe, na kweli nilipata, na nikapambana kuzuia mwanaume yoyote asije karibu yako, na hata siku ambayo ulitaka kufanya yako na Yule kijana kwenye gari, nikwatuma wale wasela wangu waje wawape jamba jamba, na kuanzia hapo nikawa nafuatilia matendo yako yote, nikawa namzuia mwanaume yoyote yyule utakae muita, na hata huyu mzee ambae ulipanga kukutana nae leo mim I ndie niliemzuia asije, nilimfata na kumuambia kuwa wewe ni mke wangu na nakupenda sana, na yeye najua anamke, je atajisikia vzr akiona mke wake anatembea na mwanaume mwingine, alionekana kunielewa, na nikamuomba anielekeze chumbab ambacho mlipanga kukutana , akanielekeza pale, mwanzo alikuwa anasita sita, mpaka nilipomuoneha picha za mimi nawewe tukiwa nyumban pamoja na nilizipiga bila wewe mwenyewe kujua, ndio akaamin na kunisaidia kwenye kila kitu mpaka ukanikuta hapa, akaendelea kusimulia Robert….
“ kwa hio unaniahidi kuwa hautaniumiza? Nikauliza…
“ nakuahidi peace nakuahidi nitakufanya mwanamke mwenye bahat sana kwenye huu ulimwengu, nakuahidi nitakufanya kama malkia kwenye falme yangu, nakuahidi kukutuza na kukutuliza, akawa anasema rpbert, basi kwa shoo zake na care yake, nikawa najiambia kuwa nitatulia tu, kwa maana niliamua kumpa Robert nafasi ya mwisho kwenye maisha yangu, na kama atafanya hivyo anacyovisema nitaishi nae maisha yangun yote na nitatulia……
Basi nikamuambia Robert kuwa naenda kuoga na baada ya kutoka bafuni nakuja kumsimulia na mimi yalionikuta mpka nikaamua kuwa mshenzi na mwanamke ambae yuko tayar kufanya chochote kile ili kuhakikisha mwanaume anaumia au kudhalilika…..
Basi nikaingia bafuni, muda wote nilikuwa naoga huku nacheka na kuyafikiria maisha yangu mapya ambayo nitaishi na Robert, kufikiria ni namna gani nitaacha kuwa mdangaji na kuwa mke halali wa Robert, nikawa nafikiria ni namna gani nitaishi kama mke, na ni namna gani nitakuwa kipenzi cha Robert kwenye maisha yetu yote, basi nikaoga ila wakat natoka nilisikia maneno ambayo yalinivunja moyo sana, na kujikuta nataman kutoa chozi kwa maana tayar nilishatengeneza fikra tamu kwenye akili yangu, ila zilikatika ghafla, nilimsikia Robert anasema “ ameshaingia kingi, yaan ameniamin kupita maelezo usijal, wapi mimi nitampenda vipi demu mwenye sura mbovu kiasi chote hichi, mwanamke mwenyewe hajui hata kutembea, yaan umbo lake lenyewe halieleweki lipo kama kabati, yaan akienda kama anarudi na akirudi kama anaenda, yaan nikishapewa changu naachana nae, akawa anasema Robert na kwa akili za haraka haraka nilihisi ananiongelea mimi , nilihisi kuchoka, nikarudi kwanza bafuni na kuanza kulia……
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU