
KIBOKO YANGU 10
Nilianza kulia, na kuanza kujilaumu kwanini niliamua kumuamini Robert na wakat nilishaapa kuwa sitakaa nimuamin mwanaume hata siku moja kwenye maisha yangu, nilijilaumu sana na kiukweli sikujua ni nani huyo alikuwa amemlipam kwa sababu ya kunibadilisha mimi, roho ilikuwa inaniuma sana, nilikuwa nataman sana kupiga kelele kwa maumivu ambayo nilikuwa nayasikia, nililia kwa tani yangu kisha nikajifuta machozi na kutoka nje, nilianza kujipaka mafuta taratibu kisha nikavaa na kumtaka robert turudi nyumban, Nilishindwa kuwa mnafki na nilishindwa kujifanya nipo sawa na wakat sikuwa sawa kabisa.
nilishindwa kujifanya kuwa naendelea vzr na wakat nilikuwa kwenye maumivu makali mno, nilipofika nyumban nilijifungia ndani na kuanza kulia, nilishindwa kujizuia, kwa maana nilikuwa nimeshaanza kumpenda sana, nilikuwa nipo tayar kubadilika kwaajili yake, nilikuwa nipo tayar kuwa anavyotaka yeye, nilikuwa katika maumivu makali na kujiapiza kuwa wanaume wote ni mijibwa na sipaswi kuwa na moyo mwepesi kama niliokuwa nao kwa Robert kwa maana aliukuwa ametumwa kumbe na mwisho wa siku mpaka amenikula, kumbe sio kwa mapenzi yake, ila alikuwa anafata maagizo aliopewa tu, na sio kwa mapenzi yake, nilimuona kama yeye ndio kazidisha ukatili kuliko hao wanaume wengine ambao wameshawah kuniumiza..
“ acha niwe Malaya, huenda mungu ndio kaniandikia niwe hivi kwa maana haiwezekan kila mwanaume ambae anakuja kwenye maisha yangu ni lazima aniumize, nikjiambia….
Basi siku hio nilishinda ndani nalia, mwisho nikapata wazo kuwa, kwakuwa ananichezea na mimi ni mchezee, maana umalaya nauweza vzr sana, sasa ngoja tyuoneshane na tuone nani atake mchezea mwenzake zaidi……
Nikaingia kenye kabat langu, nikatoa zile pigo zangu za kichangu, nikapiga na vikuku vyangu, na baada ya hapo nikapiga vikuku vyangu na la kalipstic flan hivi katamu, kisha bada ya hapo nikatoka na kwenda kukaa ukumbini, alikuwa jikoni na alipotoka alishtuka sana kuniona nipo vile, jicho likamtoka, hata sikumjali, jikafungulia mziki kisha nikaanza kunengua, nikanengua pale, akawa anataka kunigusa ila nikamzuia, nimenengua mwisho nikapanda zangu ngazi na kwenda chumban kwangu, nikamuacha ametoa macho, nikakaa chumban kwangu mpaka nilipohisi nay eye ameingia chumban kwake, nikatoka na kwenda kumchyungulia, nikaona namna ambavyo alikuwa anateseka kihisia, na ndiocho nilichokuwan nakitaka, yaan anitese mimi kihisia alafu mimi nimuache hivi hivim “ wewe ulisikia wapi….
Nikakaa pale mlango kisha nikatoa mguno mmoja mkali, mpaka akakurupuka huko chumban kwake, na kuja kuangalia nimefanya nn, nikaanza kujiliza, huku namtazama usoni, yaan nikawa najiliza ile kimadeko, nikashangaa mwamba jasho linamtoka sio mchezo, kisha aksema “ mamaaa shida nini.. nikawa kimhya sisemi neon namuangalia tu, ile kimapozi, akawa anasogeza lips zake kwenye zangu, nikajitoa chap kisha nikasema “ nasikia usingizi sana naomba nikalale, akataka kunizuia ila niligoma kwa maana alikuwa anataka kwenda kulala na mimi, ila nilikataa kata kata, kwa sababu lengo langu nikumuona anateseka kihisia tu, kuna muda nilikuwa nahisi sio Yule Robert ambae alikuwa best yangu kwa maana Robert alikuwa anarangi kidogo ils huyu ni mweusi, ila nikawa najiambia maisha yana mambo mengi huenda amebadilika, maana hata sikuwa namkumbuka sura, kwa maana nimetoka na wanaume wengi sana, hata mim I sijui idadi yao ni ngapi, na sina ninae mkumbuka hata mmoja, sasa kumsahau david ilikuwa ni kitu cha kawaida tu….
Nikawa nazidisha mitego na kila akitaka kunigusa natoa udhuru mpaka akome, maana kumbe ametumwa kwaajili ya kunibadilisha, kumbe ametumwa na mtu na hafanyi kwa moyo wake, basi anatakiwa kuteseka kuliko alivyonifanya mimi nijisikie vibaya…
Mara simu yake ikaanza kuita, akatoka pemben kuongea na simu, sikutaka kupitwa nikataman kujua anaongea na nani na wanaongea nini, nikamuona ameshtuka sana kisha akasema ‘ unakuja! Kwa saut ya mshangao kabisa, nkaona ghafla kakosa raha na kusema “ sawa boss nitafanya kama unavyotaka…
Hapo ndipo nilipojihakikishia kuwa ametumwa na hakuwa anafanya jambo lolote lile kwa mapenzi yake, bali ni kwakua kulikuwa na malipo ambayo alikuwa anatakiwa kulipwa, kwa akili za haraka haraka nikajua ni wazaz wangu, kwa maana wamepiga kelele kwa muda mrefu, kuwa wanataman kuniona nimeolewa na wanataman mjukuu, ila mimi ndio sikuw naeleweka, nikahisi labda wanataka kuniozesha kwa nguvu ndio maana wakaamua kumtumia Robert kama chambo…..
Kuanzia amemaliza alikuwa anaonekana kama anawasiwasi sana, akaingia chumban kwake na kujiandaa haraka haraka kisha akaondoka zake, sasa na mimi nikjaingia kwenye chumba chake na kuanza kumchunguza kuwa Robert ni nani na amekuja kwenye maisha yangu kwa sababu gani, nikapekuwa vitu vyake vyote ila sikuona kitu chochote kile ambacho kingeweza kuyaondoa mashaka yangu, nikaangalia mpaka chini ya uvungu, ndio nikaona chini ya godoro kama kuna bahasha, nikatoa godoro na kuangalia hio bahasha inanini…
Nikakuta kuna kama mkataba, ambao umesainiwa na Robert Clinton pamoja na milla Jacob, sasa sikujua huyo millah jaco ni nani na Robert ni nani, nikaendelea kupekuwa ndipo nikaona picha yangu ya utoton pamoja na Yule best yangu Robert, ni kweli alikua mweupe, na alikuwa kama shombe shombe flan hivi, ni dhahiri kuwa huyu Robert ninae ishi nae sio Robert halisi…
Nikaona na barua imeandikwa kuwa “ nakupa jukumu la kwenda kumlinda mpenzi wangu kipenzi peace, mpe furaha hakikisha anaacha tabia zote za ajabu na nyumban kwake nimefunga cctv camera so chochote amvacho atakuwa amepanga nitakuambia ila hakikisha usilale nae kwa maana huyo ni shemeji yako,na miaka yote hii sijaoa kwa sababu nataka kumuoa peace, hivyo muheshimu na mfanye kama shemeji yako ajae, ni mimi wako Robert….
Hapo ndipo nikapata uthibitisho wa asilimia mia kuwa Yule ambae nilikuwa naishi nae hakuwa ni Robert, nilisunya na chuki yangu kwaken ikazidi kwa maana niliona kama amenichezea kwa mara nyingine, na kuanzia siku hio sijawah kumuona tena Robert, hata sikumtafuta kabisa, ila nilikuwa na hasira nae kwa maana alikuwa ameniumiza sana, na kuamua kuacha maisha yangu yaendelee, niliamua kutulia kwanza na kuyatafakari maisha yangu kwa maana nilishachoka kuwa katili, nilishachoka kuishi maisha ya udangaji, nilitaman sana kuwa na familia, nilitaman sana kuwa na mume na watoto sasa, mwezi ulipita bila kumuona Robert maishan mwangu, nikashangaa sioni siku zangu, nilihisi kupagawa na nilipoenda kupima nikakutwa na ujauzito wa mwezi mmoja
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU