KIBOKO YANGU (11)

KIBOKO YANGU 11

Skiuamin kama nina ujauzito tena wa baba ambae sikuwa najua hata anaishi wapi, niliyachukia maisha yangu, niolijiona sina thaman kabisa kwenye maisha yangu, sikujua hata Yule Robert wa mchongo yuko wapi, nikiwa nimekaa nashangaa shangaa nikapigiwa simu na rafiki yangu mmoja akanambia kuwa siku hio anavalishwa pete ya uchumba anaomba nifike, nikaona bora hata nitoke kwa maana mawazo yataniuwa nisipokuwa makini….

Kweli jioni nikaenda kwenyen hio party ya shoga yangu, alikuwa ni mdangaji kuliko mimi, ila ndio hivyo anaolewa ama kweli kila mtu na bahat yake, ilikuwa ni shughuli ya maana, walikodi ukumni kwaajili ya kuvishana pete tu, nikaenda, nikiwa nimepodoka zangu hatar, kila mwanaume ambae aliniona alitaman kuja kukaa na mimi, ila sikutaka, nikaenda mpaka sehemu ambayo kulikuwa na vinywaji, nikachukua chupa ya whisk, nikapiga yote haraka haraka kama maji, nikachukua nyingine, nikagonga baada ya hapo nikatoka nje, maana niliona kama sauti za watu na ile miziki iliokuwa inapigwa pale kama wananipigia kelele, nikaondoka na kwenda kukaa kwenye swimiing pool ambayo ilikuwa eneo lile, maana kulikuwa kama hotel, na baada ya hapo nikaanza kulia, sijui ndio pombe nikaanza kulia, nlilia sana kwa takriban nusu saa, sijui ilikuwaje maana sikuwa nakumbuka chochote kile ……..

Sikujiuliza hata maana ni kama pombe bado hazikuwa zimeisha kichwani, nikaingia bafuni na kuoga, na hapo hata sikujiuliza ni nani ambae alikuwa amenileta nyumban, nimemaliza nikatoka na kwenda kuandaa supu maana nilkuwa na hangover hatar, lakin nikakuta supu ya kuku tayar imeshaandaliwa, hata sikujiuliza nani atakuwa ameandaa, nilikunywa pale kwa raha zangu mpakja nikashiba, nilipomaliza kula mara nikashangaa mlango unafunguliwa, nikashangaa Robert anaingia pamoja na mwanaume ambae alikuwa kama shombe shombe, alikuwa na karangi flani hivi, alikuwa anaonekana kama ni mtu wa pesa nyingi , nilipomuona alikuwa anaonekana kama mtu ninae mfahamu au mtu ambae nimeshawah kumuona, ila sikujua nilimuoena wapi….

Akamtaka Robert apige magoti kisha aniombe msamaha, kweli alipiga magoti kisha akasema “ peace naomba nisamehe sana kwa maana tamaa ziliniponza na nilitumwa nikuchunge usifanye ujinga ila nikajikuta nakutaman na kujifanya mm ndio Robert na haikuwa kweli, maana kuanzia siku yakwanza nilipokuona ulinivutia mno, nikajikuta nataman sana kuwa na wewe, akasema Robert

“ naitwa milla Jacob ni binamu yake na Robert, Robert alikuwa masomoni na alikuwa ananiamion sana ndio maana alinipa jukumu la kuja kukuchunga ila mimi ni binaadamu, na kukaa nyumba moja na mwanamke mrembo kama wewe ilikuwa ngumu sana kwangu, nilikuwa najikaza sana kuwa sawa ila mwisho wa siku nikashindwa na kujikuta nataman sana kuwa na wewe, nataman kuwa karibu yako nan ataman sana kuingia kwenye maisha yako, ndio maana nikafanya mambo tofauti na tulivyokubaliana na boss wangu, Robert pamoja na peace naomba mnisamehe sana, akasema Robert, aiseee huyo milla aliwekwa mangumi mfululizo kisha akaambiwa haya ni kwaajili ya kumuumiza tena my lollipop, kwanini lakin umemtaman shemeji yako, najuta sana kukuamin, akawa anasema Yule mwanaume mwingi,e, nilikuwa naona mauza uza tu na sikuwa naelewa kitu hata kimoja kati ya vitu ambavyo walikuwa wanavisema, Yule mwanaume mwingine aliekuja na Robert fake alikuwa ananisogelea na mimi nikawa nasogea nyuma kwa maana sikuwa na iman na yoyote kati yao, nikashangaa anavua shati lake na kunionesha kifuani kwake, alishwah kuandika jina langu na ule utomvu wa korosho, nilipoona hio alama nilikumbuka na mimi niliandikaga jina lake kwenye paja langu, nikajikutab naanza kulia, akaja akanikumbatia kisha akanambia “ nisamehe sana peace wangu, nisamehe kwa kuchelewa kuja kwenye maisha yako mpaka ukatokwa machozi, nisamehe kwa kumuamin mpumbavu mmoja nikijua atakufaya uwe sawa kumbe ndion anakuzidishia majeraha, akawa anasema Robert na mm sikuwa nasema chpchote kile zaidi ya kulia tu, kwa maana niliona kama naota…

Yule Robert fake aka milla, akaondoka zake nikabaki na Robert orginal, na ni kweli alikuwa Robert kwa maana hakuna mwanaume hata mmoja amabe alikuwa anajua kuwa nilikuwa napenda kukumbatiwa zaidi yake, yaan nilikuwa nikikumbatiwa natulia hata kama nilikuwa na hasira kiasi gani, nilikuwa napenda sana catoon ya cindella, nilikuwa naweza hata kuiangalia siku nzima, na kusema nataman na mimi niwe kama cindellela, basi rpobert akaiweka, nikajikuta naanza kulia, kwa maana alinikumbusha utoto wangu, alikaa na mimi pale, tukapika tukala kisha akanambia kesho kuna sehemu natakiwa kwenda nay eye naondoka, niliotaman asiondoke ila ndio hivyo sikuwa na uwezo wa kumzuia, akaondoka na kunambia kuna nguo chumban kwangu, niliingia chumban nikakutana nan gauni refu jekundu pamoja na hills nyeupe na pochi nyeupe, nilililala nikiwa nimezikumbatia….

Aiku hion ilipita na hatimae siku mpya ikaanza, nilishinda na subiri muda ambao Robert amesema anakuja kunichukua ufike…

Kwenye majira ya kama saa kumi na moja lilikuja gari jeupe mpaka ndani, kulikuwa na dereva tu akasema kuwa “ nimeagizwa na boss nije kukuchukua…
Nikaachia tabasamub kisha nikapanda kwenye gari kwa mbwembwe, nikashangaa tunaenda mpaka sehemu moja kuna hotel moja kabambe, ila kabla sijaingia ndani alikuja mdada akaanza kunifanyia makeup pale pale kwenye gari, kwa maana sikupaka chpchote, mpaka kagiza kakaanza kuingia, kisha ndio nikaingia ndani, na macho ya kila mtu aliekuwa pale yalikuwa kwangu, na mc akasema “ huyuu ndio mwanamke mrembo ambae ameutesa moyo wa kijana wetu kwa muda mrefu na nataka leo aje atulize mapigo ya moyo ya kijana wetu, kuangalia mbele namuona Robert alikuwa kapendeza mno na alikuwa anajua udhaifu wangu, yaan alinyoa ndevu namna flan hivi nikajikuta namuangalia muda wote, nimefika mpaka mbele nashangaa mwamba anapiga goti kisha akasema “ will you marry me…

Kiukweli sikuweza kukataa na wakat huo huo akanivisha peta na shangwe na nderemo zikawa zimetawala pale ukumbini, na muda wote Robert alikuwa ananiangalia kwa jicho tamu balaa, nilikuwa mpaka nataman kumkiss, na kila dakika alikuwa ananisifia kwa kunambia amebahatika kumpata mwanamke mrembo mno, akiwa anamaanisha ni mimi, na sikuwa na lakufanya zaidi ya kutabasamu…

Tukiwa kwenye furaha zetu, mara akaingia mmama wa makamo na bint ambae alikuwa kama marika yangu na kusema “ Robert huweza kuwa na mwanamke mwingine zaidi ya Doreen, kama mimi ni mama yako utamuoa doreen na kama sio mama yako utamuoa huyo chagudoa wako, mara nikashangaa taa za ukumbi mzima zimezimwa na baada ya hapo likawashwa projector yakaanza kuoneshwa matendo yangu, namna nilivyokuwa nawatesa wanaume na namna nilivyokuwa najiuza, nyie nilihisi kuishiwa nguvu nikajikuta nimedondoka chini na kujiona kama mwanamke mwenye mkosi kuliko wanawake wote duniani

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata