
KIBOKO YANGU 12
Robert alikuja na kunishika kisha akanikumbatia kisha akasema “ usijal mke wangu hakuna mtu hata mmoja anaeweza kunitenganisha na wewe, waliweza mwanzo ila sio sasa wife, najua yote uliyopita, unaweza ukahisi ni makosa yako ila kuna mikononya watu ndani yake, Robert alimgeukia Yule mwanamama kisha akasema “ mama mimi kuachana na peace labda mniue, maana damu yangu na pumzi yangu bado inataja jina la peace, akasema Robert nikabaki nimetoa macho…
“ najua wewe ndio umetengeneza kila kitu mpaka peace wangu akawa hivi ambavyo alivyoleo, na sijawah kuamin kama peace anaweza kuwa chagudoa, kwa maana namjua alikuwa ni bint muoga na mwenye huruma sana, kwa nini abadilike ghafla, akawa anaendelea kusema Robert, kisha akatoa picha za baadhi ya watu ambao nilishawah kuwa nao, akanionesha mm na kumuonesha kila mtu ambae alikuwa pale kisha akasema “ nimewakuta wanaume wote wanalipwa na mama kila mwezi, embu ataambie, kwa namna anavyomchukia peace anawezaje kuwalipa wanaume wote ambao walikuwa ni maex wa mrembo wangu, sijui umepitia nini ila najua uliyoyapitia yamesababishwa na mtu na hujasababisha wewe kama unavyofikiria, mama yake Robert akamgeukia kijana wake, kisha akasema “ nitahakikisha anateseka zaidi ya hapo kisha akaondoka zake, nilijiskia vibaya sana , kwa maanan nilijiona kama sina bahat kumbe kuna mtu alikuwa anaharibu bahat yangu, kisa kijana wake alikuwa ananipenda na kuniongelea sana, na hapa ndipo nilipogudua kuwa usipende kuhukumu kitu ambacho hukijui kiundani…..
Robert aliwatuliza watu wote ambao walikuwa pale kisha akachukua mic na kuanza kusema “ huyu bint mnaemuona hapa mbele yenu alikuwa ndio first lover wangu, nilimpenda sana kuanzia namuona, alikuwa ni bint muelewa na alikuwa ananielewa sana kuliko hata wazaz wangu, wazaz wengi wenye uwezo wa pesa huwa wanaamin kuwa watoto wanatakiwa wraith biashara zao, na ikitokea mtoto hafanyi kama wanavyotaka wanamuona mkaidi, na kusahau kila mtu anandoto zake, namshukuru sana peace maana alikuwa ananisupport kwenye ndoto zangu, alikuwa ananambia kuwa siku moja nitakuwa ninavyotaka kuwa kama nikiwa na juhudi, yalikuwa ni maneno ya kawaida ila ndio maneno ambayo yalinipa sana moyo na kunifanya niwe huyu Robert wa leo, Robert ambae anabiashara na miradi yake ambayo anaisimamie, anabiashara na miradi yake ambayo inamuongoza, Robert ambae anaamini9 sana kwenye kutekeleza ahadi, na anaitekeleza ahadi aliompa peace ya kuja kumuoa siku moja na hio siku imefika, sitakubali mtu yoyote Yule aniletee maneno yoyote yale na sitakubali mtu yoyote Yule anitengenishe na peace wangu kwa namna yoyote ile, akawa anasema Robert, kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu mwanaume mmoja alinifanya nijisikie vzr na kuamin kuwa binadamu hawafanani, ila nilitaka kujua ilikuwaje mpaka mama yake Robert ahusike na maumivu yangu, nilitaman kujua sana, maana nilijiona mwenye mkosi sana kwenye swala zima la mahusiano kumbe kuna mtu alikuwa anasababisha maumivu yangu ya kila siku…….
“ nilikuwa nikimtaja peace kila siku, kweny vitabu vyangu na vitu vyangu vya kuchezea vyote niliweka jina peace my lollipop, kila mtu alitaman kujua huyu peace ni nani, huyu peace kwanini amenikaa akilini kwa kiasi chote hicho, huyu peace imekuwaje mpaka nikawa namtaja kila siku, nilipofika secondary nilikuwa najiita mume wa peace, watu hawakuwa wanamjua peace ila kila mtu alijua kuwa kuna mtu nampenda sana anaitwa peace, sisemi kuwa sijawah kuwa na mahusiano, mimi ni mwanaume tena rijal kabisa, ni ngumu sana kutokuwa na mwanamke kabisa kwenye maisha yangu, nimeshawah kuwa na wanawake kadhaa ila mar azote nilikuwa nawaambia kabisa kuwa siwez kuwaoa na nampenda peace, kuna ambao walinielewa na kuna ambao walikuwa wananing’ang’ania ila msimamo wangu ulikuwa pale pale…
nikamaliza elimu ya sekiondary na wazaz wangu wakanipeleka nje kusoma, huko nilikuwa mpweke sana, ila kila nikifikiria kuwa nilikuwa nasomea kitu cha ndoto zangu, nilipata moyo na kuamin kuwa siku moja nitakuja kukutana na mwanamke wa ndoto zangu ambae ni peace wangu, na hata hicho nilichkuwa nasomea wazaz wangu hawakutakja ila nilipambana mpaka nikaenda kukisomea…
basi nivyokuwa mwaka wa mwisho niakanza kutafuta habar za peace ndio nikasikia anajiuza, nilishangaa sana kwa maana ni bint ambae nilikuwa naamin alikuwa anamaadili sana, sasa imekuwaje mpka ajiuze? Nilikuwa najiuliza hilo swali kila siku bila kupata majibu yoyote yale….
nikaanza upelelezi wangu ndio nikagundua kuwa mama yangu alikuwa anatengeneza watu kwaajili ya kumuharibu kisaikolojia peace wangu, na kuanzia hapo lolote lile ambalo alikuwa analifan ya peace niliamin ni matokeo ya matendo ya mama yangu hivyo sikuwah kumuhukumu peace wangu kwa chochote kile, na leo mbele ya kila mtu naomba niseme kuwa, kijana wenu nimeshakuwa na nataka kuoa na ninaetaka kumuona ni mwanamke wa ndoto zangu bibie peace, akaendelea kusema erobert na watu wote waliokuwa pale wakaanza kupiga makofi na kutupongeza, na baada ya hapo tukala, kisha tukanywa na baada ya hapo Robert akataka twende hotel tukalale, sikuwa na nguvu za kukataa, nikakubali hao tukachukua chumba, ila hata haikuwa siku ya kujilia vyetu, ila robert alikuwa anataka kujua mambo yote ambayo nilikuwa nimeyapitia….
“ mama naomba nijue maisha yako yalivyokuwa mpaka ukawa hivi ulivyoleo, akasema Robert mara baada ya kumaliza kuoga….
“ ni story ndefu kidogo ila ni story ambayo inaniumizaga sana, kwa maana nimeteseka mno kwenye mahusiano, nimeteseka mno kwenye mapenzi , kiasi kwamba nikawa najihisi kama sina bahat kabisa kwenye huo upande, na mtu wa kwanza kuniumiza alikuwa ni leonard, nilimkuta akiwa anafanya mapenzi na rafikin yangu wa damu, sio siri sikuamin kabisa, nikawa nahisi kama naota na kuhisi kama haiwezekan, maana nilikuwa namuamin sana leonard na mar azote nilikuwa naweza kukaa na simu yake kwa muda mrefu bila kuona sms wala call ya mwanamke tofauti nan dg zake, nilitokea kumuamin sana, ila siku niliomfumaania ndio nikaona kwamba nilikuwa najidanganya kuhusu leoanard na waliponiona hata hawakujal wakawa wanaendelea zao na yao kama mimi sipo vile, nikasema huku nikiwa najizuia kulia….
“ lia mamaa, lia uchungu wako wote utoke, usipende kujifanya kama upo sawa, na ukipata nafasi ya kulia wewe lia mpaka mwisho wa uchungu wako, akasema robert na mm nikaanza kulia, maana kila nikifikiria kile kitendo nilikuwa naumia sana, na Robert hakuwa na kazi nyingine yuoyote ile zaidi ya kunibembeleza, alinibembeleza weee kisha akatoa picha ambayo kwa nyuma aliandika the first ex kisha akanionesha na kusema “ ndio huyu…
Nilishangaa sana kumuona na ile picha ila nikaitikia kwa kusema kuwa ndio yeye, akaniangalia kisha akasema “ tuishie hapa mpaka alipie maumivu aliokusababishia, kisha akanikumbatia kwa hisia sana na kunambia, tutafanya kila kitu siku ambayo kila aliekufanya ulie nay eye anateseka kuliko alivyokutesa wewe, akasema Robert kisha tukakumbatiana ila kwa tabu kwa maana kila mmoja alikuwa na hisia juu ya mwenzake kisha tukalala mpaka asubuh…
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU