KIBOKO YANGU (15 na 16)

Sehemu ya 15 na 16

Yaan mim na Robert wote tukaanza kulia, maana kwa hali ambayo tulimkuta nayo, ni kweli] mungu alimuadhibu, basi tukiwa tunatoka pale nikashangaa namuona mama yake Robert na mama mwingine wakiwa wanakuja mbio mbio, na mama yake Robert akasema “ peace mwenyewe ndio huyo hapo aliemuuwa mwanao, yule mama akanivamia na kuanza kunipiga, ikabidi Robert aingilie, akaanza kunikinga na kusema kuwa peace hajaua, ila mwanao alikuwa anamtafuta kwa sababun nyingine ila Yule mama hakuwa anaonekana kuelewa kabisa, alikuwa na hasira sana na mimi…..

Basi mazishi yakapita na baada ya msiba ndio ikaja barua na hapo yule mama alituma watu waje waniue kama nilivyomuuwa mtoto wake, na kweli nikawa nashangaa nyumba yangu inachomwa moto, mara nashangaa muda huo huo moto unaanza kuzimwa kisha baada ya ule moto kuzimika ndio nashangaa namuona Yule mama, alikuwa amekuja , akaja na wapaka rangi na mafundi, wakaanza kurepair nyumba yangu nikawa nashangaa imekuwaje tena…

Baada ya kumaliza kukarabat yule mama akaingian ndani kisha akapiga magoti na kuanza kuniomba msamaha, na wakat ambao nyumba ikiwa inawaka moto obert hakuwepo kabisa, amekuja kupata taarifa baadae sana, na kwakuwa nyumba yangu haikupata maafa ya kueleweka , akakuta wakat ambao nilikuwa nasoma barua ilioachwa na jimmy, basi mama yake jimmy akatoa bahasha na kunipa bahasha ambayo ndani yake kulikuwa na karatasi ambayo ilikuwa imeandikwa “ najua wakat ambao mtakuwa mnasoma karatasi hii tayar nitakuwa nimeshakufa, na naomba mnisaidie kumtafuta peace na mumuombe sana msamaha kwa kumkosea, na huenda laan zake ndio zimenitafuna, nilitaka kumuona anapagawa, ila badala yake mungu akaamua kuniadhibu, lakin lawama zote ziende kwa shangazi zawad, mama yake na robet maana ndio alipanga mipango yote ile, alikuwa hataki kabisa kumuona peace akiwa na Robert na kuamua kumuharibu peace kisaikolojia, aliamua kutuma watu kipindi peace akiwa bint mdogo ila hata ikiwezekana wamuambukize maradhi au wamfanye apagawe, ila ,Mungu wetu ni wakila mtu, alisimama na peace, ingawa kwa tabu sana bint huyu alipata mali, na akaamin kwa kupata mali atapata amani, ila haikuwa hivyo kwa maana ndio nilitumwa mm, kwakuwa nilikuwa na muonekano mzuri ilikuwa ni rahis peace kunipenda, alinipenda sana, na kuna muda kama binaadamu nilikuwan najisikia vibaya kumfanyia ambayo shangazi alitaka nifanye, alitaka kumuona peace akichanganyikiwa, alikuwa anataka kumuona peace akifilisika, akanikodia nyumba kwa siku chache na kuwa ananipa pesa nyingi ambazo zitanitengenezea njia kwa peace na kweli peace alinipenda na kuniamin sana, ila nilichomlipa ni kumuachia deni na million mia na kuondoka na gari lake, ilikuwa ni pesa nyingi sana, nilikuwa nachukua huku naumia, na k mimi pamoja na shangazi tuliamin kwa hasara tuliompiga ni lazima atafilisika na nilazima atapagawa, ni kweli alipagawa, ila mungu hakutaka kumtesa kwa muda mrefu kwa maana aliamka tena na kupambana kutafuta pesa na kweli alizipata kwa njia ambayo aliijua yeye mwenyewe, naomba mumtafute peace na mumuambie kuwa, yeye hajaniadhibu ila mungu ameniadhibu kwa niaba yake kwa maana nimepata kansa ya damu ambayo nina uhakika itaniua, barua iliishia hapo….

Mama yake jimmy alikuwa analia sana kisha akawa anasema “ zawad kwann wewe ni mnyama kiasi hichi, na kwani9ni uliamua kumuingiza mwanangu kwenye dhambi zako, kwann usingefanya ujinga wako pekee yako, akawa anasema mama yake jimmy akiwa analia, na kuniomba sana nimsamehe mwanae, na sikuwa na hiyana, kwa maana hata mungu huwa anatusamehe makosa yetu, sasa kwanini mimi nisimsamehe kiumbe mwenzangu ambae huwa nakosea kama yeye, na baada ya mama yake jimmy kuona nimekiri kuwa nimemsamehe mwane basi akaamua kuondoka, muda wote Robert alikuwa anamlaan mama yake, na kuniomba msamaha kwa sababu ya mambo ambayo mama yake amenifanyia, sikuwa namuona kama anakosa, maana yote yaliotokea kwenye maisha yangu yeye hajasababisha chochote kile, kwa hivyo hapaswi kujilaumu na wala hapaswi kujiona anamakosa……

Basi bana maisha yangu na Robert yalikuwa yanaendelea ila kilichokuwa kinanishangaza ni kuwa hakuwa anataka hata kidogo kunigusa kipindi chote ambacho nilikuwa nae, na nikamueleza kuhusu mimba, akanambhia hio mimba ni yake na sio ya Yule mpuuzi ambae nilikuwa naishi nae, na hatak kusikia nikimuambia mtu yoyote Yule kuhusu mm kuwa na mimba ya mtu mwingine zaidi yake, nikakubali, maana niliona kama mungu ndio kaamua kuniletea mtetezi wangu hivyo napaswa kutulia….

Akawa ananipeleka clinic, akawa ananijal kama vile yeye ndio baba wa mtoto, ila hakuwa anataka tu kunipa haki ya ndoa, alikuwa anamfata mama yake mara kadhaa kumtaka aje kuniomba msamaha, ila mama yake hakuwa anataka kabisa kujuta kwa alichokifanya na akidai watu wote walikuwa wanamsingizia nay eye hata iweje hawez kufanya hayo mambo ambayo watu wanayasema, na kama mtu yoyote Yule anabisha basi aende na ushahidi wa kuwa yeye ndio anahusika kwa mateso yote ambayo yametoke kwenye maisha yangu….

Na kiukweli hakuna mtu hata mmoja ambae alikuwa na ushahidi hivyo ikabidi tutulie tu kama tumemwagiwa maji, basi Robert alikuwa bega kwa began a mimi, na alikuwa ananipenda mpaka nilikuwa naona kama anaelekea kupagawa, ila shida yake ni haki ya ndoa, siku moja nikamfata na kitumbo change nikaanza kumtega, nikawa nashangaa ananikwepa, kila nikimtega ananikwepa, ikabidi nimfate na kumuuliza shida nn…
“ wewe ni mjamzito kumbuka, na hio miumba mimi sio baba, unataka nikutese wakat unajifungua peace licha ya mm kukupenda sana, ila pia nakuonea huruma sana, naogopa sana kukuona unaumia au jambo baya lolote lile linakutokea, kwa maana nataman kukuona kila siku unafuraha nan ataman kila wakat nikuone ukiwa na aman, hivyo naomba tusubiri ujifungue, maana hata mm nina hamu sana na wewe kuliko unavyofikiria, ila ujauzito wako unanifanya nisubiri mpaka ujifungue, akasema, na kiukweli nilimuelewa maana hata mimi sikuwa na elimu ya kutosha kuhusu kulala na baba ambae sio baba aliekupa mimba inakuwaje…
Basi siku zikaenda, siku moja rpobert aliniaga kuwa kuna sehemu anaenda, ila mpaka saa tano usiku hakuwa amerudi kwa maana nilikuwa naishi nae nyumba moja, mara nikashangaa video zinaingia whatsap kutoka kwa namba mpya, na nilipozifungua nikamuona Robert wangu anafanya mapenzi na Yule Doreen, mwanamke ambae mama yake alikuwa anataka amuoe, nilihisi kupagawa, na sijui ni mshtuka nikaanza kutoka damu sehemu za siri na wakat muda wa kujifungua haukuwa umefika, pale nilipokuwa naishi kulikuwa na mlinzi nikamuita akanipeleka hospital, na tumefika madaktar wakawa wanahangaika na mimi mwisho nikaambiwa kuwa mimba imetoka…..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata