
KIBOKO YANGU 19 mpk 20
Robert aliponiona akaanza kucheka, kisha akasimama maana alikuwa amekaa na kuja mpaka nilipo, kisha akanishika mkono na kusema “ msiwe na wasiwasi huyu ni mke wangu nay eye anamchango mkubwa sana kwenye hichi kikao…
Baada ya hapo akaendelea na kikao, na nikashangaa anajadili namna ya kumfilisi mama yake, basi wale watu wote pale wakakubaliana watoe share zao na kuzipeleka kwenye kampuni ya Robert na baada ya hapo wakaagana, kisha Robert akanigeukia na kuanza kucheka, kisha akasema “ wivu utakuuwa wewe mwanamke…
“ amna mm sijakufata wewe, nikasema kama kujitetea, “ najua … najua umejikuta tu unataka kufumania, akasema Robert huku anacheka…
Basi ikabidi na mm nicheke maana nilikuwa na wasiwasi kuliko kawaida, nilikuwa nahisi kama Robert ananisaliti, ila bana wasiwasi ndio akili siku zote..
Robert kuanzia hapo akawa anakuwa busy kuliko kawaida, siku moja akanifata na kunambia kuwa atahakikisha mama yake ananiomba msamaha kwa kila alichonifanyia, na anataka kupoteza jeuri ya pesa aliokuwa nayo..
Kweli nikaja kusikia mama yake Robert nyumba yake imeuzwa kwa sababu ya mikopo, alikuwa ameishiwa lakin akawa anataka kuishi yale yale maisha ambayo alikuwa nayo mwanzo, na tena akawa anasema kwa watu kuwa peace ndio kamloga mwanae mpaka amemfukuza, alikuwa anasema bado kwa watu kuwa mwanae anataka kuoa Malaya, yakle maneno yakikuwa yanamkera sana Robert kwa maana ali kuwa anataka mama yake ajutie mambo aliyoyafanya tu na aombe msamaha, ila kibvuri na jeuri yake kilikuwa kikubwa sana kuliko kawaida….
Siku moja nilikuwa nimetoka na robert tulikuwa sokoni, tukamuona mama yake amenunua viazi vitamu Robert alipomuona alimuonea huruma sana, maana hata kama ni muovu alikuwa ni mama yake tu, ikabidi tuanze kumfuatilia, alienda mpaka kwenye nyumba moja iliochoka sana kisha akaingia ndani na robhert akaniomba nibaki kwenye gari kisha akamfatilia, akamkuta mama yake anakula vle viuazi vitamu na maji, kwa maana hakuwa na hela hata ya kununua sukari apike chai, akatoka akiwa amemshika mama yake na kuja nae mpka karibu na lilipo gari kisha akasema, ‘ ni wakat wako wa kujutia matendo yako mama, naomba umfate peace na kumuomba msamaha na uhakikishe unampenda kama mkamwana wako, kwa maana hakuna mtu ambae ataweza kunitengenisha nae hata iweje, akasema Robert …
Mama yake chozi likamtoka, kisha akasema “ nitawezaje kwenda kumuomba msamaha, nitawezaje kwenda kumuambia nisamehe maana ninauhakika peace hawez kunisamehe kwa nilichomfanyia, kwa maana nimemtesa mno, na nimemliza mno kwa uchukia kwangu wanawake maskin, mwanangu naijua njaa, maana na mimi nimeshawah kuishi maisha ya dhiki sana, na mm nimeshawah kuishi maisha ya njaa mno, hivyo naelewa nini maana ya umaskin, na uchukia sana umaskin, maana sitaman hata kuufikiria ndio maana nilitaman mwanangu uoe mwanamke ambae ametoka amilia nzuri na sio huyo mwanamke wako, akawa anasema mama yake Robert na nikawa namsikia kabisa…..
“ kwenye maisha hakuna kosa lisilosamehewa hata moja, kwa maana aliekamilika ni mungu tu na hakuna binaadamu hata mmoja ambae ni mkamilifu, hivyo nakuomba sana mfate peace na umuombe msamaha, akasema robert na mama yake akaangalia chini akawa anajizuia kulia, nikaona nitoke kwenye gari, kwa maana nilikuwa na uhakika kuwa hakuwa ameniona, hivyo nikaona nijitokeze anione sasa, aliponiona nikashangaa anapiga pot na kusema “ naomba nisamehe mwanangu, najua sistahili kusamehewa kwa nilichokufanyia, na jua mim ni mty muovu sana, ila naomba usiniangalie kwa jicho hilo na unione kama mama yako tu, na makosa pamoja na mapungufu tumeumbiwa binaadamu akasema, nikamsogelea na kumnyanyua kisha nikamkumbatia kwa upendo na kumuambia kuwa nimekusamehe, kwa maana hata mm nimemkosea mungu wangu mambo mengi sana, maana hata mm ninastahili kusamehewa na alieniumba, hivyo usiwe na mashaka, na nipo tayar kukupokea na naomba na wewe unipokee kama kipenzi cha kijana wako, nikasema….
Nikashangaa Yule mama ananikumbatia vzr zaidi kisha nikahisi kitu kinapita kwenye tumbo langu, akawa kama amenichoma na kitu, kisha akasema “ usifikiri kama nafurahioa kuona umemloga mwanangu, tutakutana baadae, ndio maneno ya mwisho niliyoyasikia na nikapoteza fahamu….
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU