
KIBOKO YANGU 21 na 22 MWISHO
Sikujua nililala hospital siku ngapi, maana nimekuja kupata fahamu na kumuona Robert amelala pemben yangu, alikuwa amedhohofu sio kawaida, aliponiona nimeamka, nikashangaa anapiga goti na kuanza kumshukuru mungu kwa sauti, mpka manurse wakaja na kumtaka atoke na kuangalia wanaweza kunisaidia vipi, wakaja kunihudumian pale ila nilikuwa naweza kusikia na kuona tu, ila sikuwa naweza hata kuongea neon hata moja…
Ndio nikaja kujua kuwa nimekaa hospital kwa miezi mitano nikiwa kwenye coma…
Nilianza kuendelea vzr taratibu ila kwa bahat mbaya ule upande ambao nilikuwa nimechomwa kisu, mguu wake haukuwa unafanya kazi, kwa maana niliparalyse, mguu mmoja kuanzia kwenye kiuno mpaka kwenye nyayo, ila upande mmoja…
Hiloa halikuwa tatizo kwa Robert kwa maana alifurah sana kunioana nipo hai kwa mara nyingine…
Hakutaka kuchelewa chelewa maana alihisi huenda anaweza kuja kukuta mwana sio wake bure, akaenda nyumba kwetu na kuwaambia ia yake wazazi wangu, na kwa namna ambavyo alikuwa ananipambania, hakuna mtu hata mmoja ambae angeweza kukataa Robert asinioe, na hata hawakutaka kumtajia ma mahari makubwa kwa maana alikuwa ameonesha ushujaa wa hali ya juu, kutaka kunioa na hali ya kuwa aliona tayar nilikuwa na mapungufu…
Basi ndoa ikapangwa na nikafunga ndoa nikiwa kwenye wheal chair, ila hilo halikuwa tatizo kabisa kwa Robert, kwa maana kitru pekee ambacho alikuwa anakitaka kwenye maisha yake ni kunioa na kunifanya mke wake, na hatimae nikawa mke halali wa kipenzi change Robert….
Tulifunga ndoa, na nilishangaa moyo wa huyu mwanaume, kwa maana hakutaka ndg wala rafiki kunihudumia, alikuwa ananihudumia yeye pekee yake, kwa maana alikuwa ananifanyia kila kitu, kisha nikawa naenda nae kazin, kuna wakat nilikuwa naona aibu, nilikuwa naona kama namdhalilsha vile, kwa maana alikuwa ni boss mkubwa, na wakat wote alikuwa anatembea na mke wake ambae yuko kwenye kiti, ambae hawez hata kutembea na nikimuambia aniache nyumban, maana ananihangaikia sana, akawa ananiambia kuwa anataka kuwaonesha watu kuwa wanaume wenye mapenzi ya dhati bado wapo, na sio wanaume wote ambao wanawaza kuwasaliti wake zao tu, na sio wanaume wote ambao hawajui thaman ya mwanamke kwenye haya maisha…..
Kila mtu alikuwa anatusifia na kutuona kama mfano bora sana, na hatimae Robert siku hioo akasikia kuwa kuna daktar wa mazoezi ya viungo anaweza kunisaidia nikawa sawa, basi akamuajiri Yule daktar akaanza kunifanyiasha mazoezi, yaikuwa yanauma sana, na kuna muda sikuwa ata nataka kuyafanya, ila sikutaka kumvunja moyo Robert, nikawa nafanya kwa moyo, ilichukua karibu miezi nane, nikawa wnaweza kupiga hatua kidogo, na karibu mwaka nikawa naweza kutembea ila mwendo mdogo, nilikuwa namshukuru sana Robert kwa kuja kwenye maisha yangu…
Kuna muda nikawa naamin kuwa “ hata kama unapitia magumu kiasi gani ila mungu hajawah kukuacha, iloa huenda anakujenga uwe bora zaidi, na nyakati ngumu hata zina muda mrefu kiasi gani la kuna siku zitapita na itabaki kama story tu…
Nikabeba ujauziro mume wangu alikuwa kama kachanganyikiwa maana akawa yeye ndio kama kaibeba hio mimba, kwa maana alikuwa anapenda sana kukaa na mimi, yaan naqweza nikaenda kazin kwake, akaacha kazi zake, akaanza kunikanda miguu, alafu ananiambia “ nataka mtoto wetu ajue kuwa nampenda sana kama ninavyompenda mama yake……
Kuhusu mama yake Robert nilikuja kusikia kuwa alipotea kusikojulikana, ila nilikuwa nahisi ni Robert alimpoteza mama yake, maana kwa alichonifanyia alitakiwa kwenda kufungwa hata kifungo cha maisha, ila Yule mama alitakiwa kuwa mchawi, kwa maana sio kwa roho mbaya ile aliyokuwa nayo…..
MWISHO
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU