Sehemu ya 9
Tulipoishia,mimi hapo nalia sanaa machozi tena kwa nguvu sanaa kama nimepigwa mimi vile,dylan akanikumbatia kwa nguvu kwa nyuma,wanafunzi walikua wanatuangalia tu mm muda huo hata sielewi na nahisi hata dylan alikua haelewi kama kuna watu pale,mara john akaja akanishika mkono ndio d akastuka akaniachia, ticha John akasema twende ofisini santa nikaanza kumfata ticha,huku madam monica akasema na nyie wengine ebu tawanyikeni yn wenzenu wanagombana nyie mnafurahi pumbavu kabisa wangeuana hapa ingekuaje?wanafunzi walikimbia,madam akamshika vanessa hapo ameivaa vizuri sanaa ana alama zangu kama zote usoni na shingoni, nilibakiza meno tu nimng’ate shingoni nikamilishe kuwa vampire,basi tukapelekwa ofcn ticha d nae akaja,madam akasema ehee kwa nn mlikua mnapigana mtueleze,vanessa hapo analia akasema mi sijui nilikua na wenzangu mara nashangaa huyu amenivamia tu ananipiga,jibu lake lilinikera yani anadanganya tena? nikamrukia tena pale pale, nikaanza mpiga,ticha john akanishika akanidhibiti, madam akasema santa wewe nakuonaga mpole sana ila kumbe ww ni mtu hatari sana wala hata hutuogopi nikamwangalia tu, akausema haya sema kwa nn unampiga mwenzio kiasi hiki sikuweza kuongea wala nina hasira hadi kigugumizi kitu kimenikaa kooni hapa, madam akasema nakuskiliza santa sema,nikasema madam huyu kanichafulia sana jina langu kaniharibia sifa yangu nikakaa kimya tu siku zote, haya leo najipitia akaanza nitukana tena na wenzie wananicheka kwa vitu vya uongo alivotunga? nikashindwa kuvumilia nikaona nimpige madam mi sina maneno mengi kama yeye nilijibu huku nalia,madam akasema ni kuhusu nini mpaka mnapigana kiasi hiki? Kutukanana?nikamuangalia ticha d ambae muda huko alikua ananiangalia kwa makini, nikasema madam ni mambo ya kike madam siwezi ongea mbele ya kina ticha john,madam akasema hilo tu? Sawa akawaomba kina ticha watoke wakatoka, akasema ehee sema sasa nikaona kama mbwai mbwai, nikamsimulia kila kitu kilichotokea siku tumetoka lkn sikuongea ya ticha d na nilijua vanessa hawezi sema mana yeye pia anamtaka d na uzuri tuliomba ruhusa,madam alishangaa sana akasema vanessa ni kweli umemfanyia mwenzio hivo?vanessa akaniangalia na mm nikamkata jicho kali lile la ole wako udanganye akasema kweli madam ila naomba anisamehe ni shetani tu alinipitia naomba nisamehe madam ,madam akasema Vanessa mbona ww ni mtu mbaya sana?yani unamfanyia hivo mwenzio?ulitaka mwanaume amfanye nn wakati amelewa?we mtoto muuaji ww, lkn niliwapa ruhusa ya kwenda kufanya hao? Ila vanessa tabia zako hapana jmn hee,alishangaa madam, Vanessa akapiga magoti eti anaomba msamaha, madam akaongea mengi sana akamsema sana vanessa na kutusema wote na akasema kesho kikao cha nidham kitakaliwa kuamua hatma yenu sawa tukasema sawa,tukatoka nje nikamkuta ticha john na d wamekaa nje d hakunisemesha wala akawa kimya tu john akasema we mtoto una hasira ww haaa kumbe unaweza ngumi vike hahaha tutakupeleka ulingoni ukacheze na kina matumla, mi nilikua kimya tu akasema haya nenda kapumzike upunguze hasira, nikaanza kuondoka kumbe wanangu wako jirani hapo wakanikimbilia na kunikumbatia wakaniuliza kilichotokea nikawasimulia tukaenda room kwetu,wakaniambia mami ila umemdunda yule mshenzi afu hata nguvu halina linalia tu tukacheka,pat akasema ila mama ticha d alichanganyikiwa ujue alikukumbatia Pale wote tulishangaa yn ni kama aliumia kukuona unalia vile mm nikacheka nikasema hakuna alikua anaamlia tu ugomvi mi nina nguvu sana huoni madam hakuniweza,wakasema ila mnapendezana kama awe sii ticha awe ndo dady etu,nikacheka sana mwanangu mwingine anaitwa dayana akasema mm kiukweli nahisi ticha d ni dady yule,toka siku amempiga mamy wote wakacheka diana akasema kweli mana alikua ananiuliza sana maendeleo ya mamy na anauliza kama anakula na zile siku nakuletea chips na juic mamy sikuwa nanunua mm ni ticha d alikua anatoa nje kijijin kule, ila alisema nisiseme nikashangaa afu nikacheka wakaanza nitekenya wanasema mamy sema jmn mamy semaaa yule n dad ee?mm nasema hapana jmn ni ticha afu msiseme ivo watu wataskia bure ikawa kesi, wao wamekazana wanasema hapana leo sio kwa kumbato lile katuachia maswali mamy bana, mie nikacheka,nikasema hizo chips alinunua vile alinipiga akawa anajua tu nitachukua hatua mana alinipiga kipigo kikali kinyume na sheria ndo mana lkn sio dady enu bana, wakacheka basi tukapiga stor pale, pat alichukua simu yangu aliwasha mana ilibidi wajue tu wanangu kuwa nina simu, mara ikanza kuita nikaichukua kuchek n d,nikatoka nje karibu na fens kabisa kupokea waKati natoka wanangu wakawa wanasema atakua dady huyo kapiga nikacheka nikaenda zangu nje,d akasema mambo nikasema poa akasema unajiskiaje nikasema poa tu akasema uje nyumbn badae nikasema siji akasema kwa nn?nikasema nije kufanya nn?akasema mm si nakuita jmn?nikasema sioni sababu ya kuja mana tulishamalizana akasema iv unajua kosa lako la kupigana ni kubwa?nataka uje nikufundishe jinsi ya kusema nikasema siji napo, d na naomba usinitafute tena,mm ni malaya nitakuua kama ulivosema kuhusu kesi mimi si ndo muhusika? Nitapokea adhabu yoyote nikakata simu,d hakunitafuta tena nikaingia room nimekasirika,kesho yake tuliitwa cha ajabu d hakuwepo tukaskilizwa kesi niliongea kila kitu na vanessa akakili wakasema tutoke tusubiri maamuzi siku io hatukuingia hata darasan baada ya muda tuliitwa,vanessa alipewa adhabu ya fimbo sita mstalini na kwenda kwao siku 21 asiwepo shule,mm fimbo nne na visiki viwil kwa kosa la kupigana,na vanessa akirudi tu visiki vinne na mashimo mawili ya taka na fimbo sita tena wakasema hapo ni msamaha sababu ilibidi afukuzwe shule kaonewa huruma vile ni form six wanampa msamaha,basi kengele iligongwa vanessa akasomewa makosa yake na adhabu na mm nikasomewa yangu na niliadhibiwa kwa kosa la kuchukua sheria mikononi basi vanessa akafungasha mabeg na kuondolewa shule hapo d hayupo nilijiuliza alipo nilitaman askie kilichojili hadi nikaeleweka lkn hakuwepo niliumia kwa hilo,baada ya wik d akarud na gari zuri sana,inaonekana alienda nunua gar hapo sie tumebakisha miezi mitatu iv tumalize shule.
Siku nampiga vanessa mwanangu pat alivofata simu yangu kwa begi la vanessa alichukua na simu ya vanessa kumkomesha tu ivo nilikuwa nayo, siku io nikawasha simu ya vanney nikaanza pitia picha ktk simu ya vanessa mana sikuangaliaga natukio, nikakuta picha zangu nimepiga na Gerald zingine ananipiga denda mara nimemuegamia yn wakati nimelewa hata sikuwa nakumbuka hizo vitu zingine wala, nakumbuka tu gelard alikua ananifosi kumuegamia,zingine ni video vile Gerald anasema atanitia sana kuliko Dylan na anajisifia kuwa anamashine kubwa tam cha ajabu mm nilicheka tu ktk video akati nakumbuka nilisema hakuna wa kumzidi dylan,nikafungua upande wa kutuma nikaona vitu vyote katumiwa Dylan,nikachoka nikasema sasa dylan ataniamin nn kwa hizi video?nikadata kabisaa sikuwa na jinsi,basi ilipita wiki mbili mm na d hatuna stor nasoma tu sana yn hasira nilihamishia kwenye masomo,nikaanza tabia ya kusinzia sana mchana,kichefuchefu, nikawa sipendi kula,mara kila siku natapika nyongo nikasema hapa sijui nina homa mm mbona hiv,wanangu wakawa wanaona sina raha wakawa wanauliza nini shidaa lkn mi sikuwa na jibu pia, nikanza kukonda vile sili ngozi ikakosa nuru amani sina na sijielewi kabisa.
siku moja d akamuita diana(mwanangu mwingine) akamuliza santa ana matatizo gn mbna anakonda na anakua vile?diana akasema anahoma d akasema ameenda hospital diana akasema mbishi d akasema mlazimishe muende hospital akampa na hela kama kawaida akasema usimwambie nimekupa hela, diana akaja akanilazimisha kwenda hospital ikabidi nikubali tukaomba ruhusa kwa madam monica akaturuhusu tukaanza safari ya dispensary tukiwa tunatoka nje ya get mana hospital n mbali kidogo mara tukaona gari ya d nayo inatoka alivotukaribia akashusha kioo akauliza mnaenda wapi?diana akasema hospital mamy anaumwa d akasema poleni na mie naenda huko pandeni twendeni,mm nikasema hapana nafanya mazoezi pat akasema mamy hospital mbali bana twende, pat na diana wakapanda mi nikaona hakuna namna nitaonekana wa ajabu,nikapanda na mm wote tulikaa nyuma,ticha d akaendelea kuendesha akaanza maongezi akasema diana ivi baba enu ni nani?mana naona mna mama tu,diana na pat wakacheka, diana akasema mama hajatutambulisha pat akasema mm namjua dady etu,d akastuka akasema nani huyo na mimi nimjue mkwe, mm niko kimya tu, namjua pat mropokaji lkn hakusema kitu akacheka tu,d akasema pat mtaje baba enu nimjue na mm,pat akasema anaitwa mr d, mm nikastuka nikasema we pat wewe ebu acha mambo ya ajabu ,nilikasirika,pat akasema mamy nn jmn acha tumwambia dady kuwa yy ndo dady etu tunajua,jmn nilitetemeka nilitamani gari linitapike, d akacheka akasema uyo d ni mie Dylan au?pat akasema ndio ni ww dady etu na tunakupenda sana,ticha d cha ajabu akacheka tuu akasema hamna baba mwingine kweli mi nasingiziwa, pat akasema hatuma dady zaidi ako wewe dady d, d akasema haya wanangu,mm nililoa jasho mwili mzima, nilihisi fedhea, nikashangazwa na naman d alivochukulia hii ishu aiseee pat alikua kunitia presha,nikajiuliza huku nikishangaa huyu d nae kama teja anachekelea ujinga huu? analewa sifa tu,tukafika hospital nilishkukuru, nikienda kwa dokta hakuepo tulimkuta mkaka wa maabara tu, akauliza nikasema tu naumwa kichwa sana akasema ngoja nikupime malaria lzm itakua maleria, ajachukua dam akapima, nikakutwa sina wakasema labda homa tu,ngoja upewe dawa na nesi, wanangu wakasema labda uchovu pia mana anasoma sana huyu,basi nikapewa panado na midawa ya maleria na kuambiwa nipumzike na ninywe maji mengi,d akatuchukua hadi kibanda cha chips akampa pat hela akamwambia nunueni chakula na juic ya mgonjwa,pat tena na anavopenda kula akanunua kisha akaturudisha shule,midawa ya maleria nilitupa kule nikanywa panado tu, nilizidi kuwa mchovu mm na nikaanza kutapika zaidi na mate machungu hadi yanajaa mdomoni, nikajitafakari matiti yanauma na hata siku zangu sikuziona ,nikawa najiuliza mbona sijaenda brid toka mwezi ulee uliopita??sikupata majib nikaanza kuwa na wasiwasi rasmi kuwa nimenasa mie.
Niliamua kumtafuta da silvia baada ya salam tukaongea story mbili tatu nikiwa naogopa kumwambia kilichonifanya nimpigie simu, yeye akaniuliza hali yangu nikashukuru hapo sasa nikamsimulia hali halisi akasema mdogo angu kwa dalili hizo utakua na mimba,nikasema dada haiwezekani akasema nakwambia tena nikasema uwii nitafanyaje sasa mimi?akasema kanunue kipimo upime nikasema sijui nitanunuaje mana wataona mwanafunzi kule kijijini nanunua hapo si nitakua najisemea? na hata kupima sijui, da silvia akasema nitakufundisha na nitakununulia vipimo viwil nakutumia kwa gar panoja na pedi,katikati ya pedi nitaviweka,ukivipata nitakuelekeza sawa?nikasema sawa asante dadangu,,dada silvia alikua ananipenda tokea anasoma mana alikua akinituma kitu sikatai na vile napenda kusoma,kweli kesho yake akaniagizia pedi ndani kuna vipimo na ubuyu niliufurahia ubuyu mnoo,nikampigia usiku nikiwa chooni nikamshkuru akasema usijali kojoa kwenye kakopo kisha soma iko kipimo fata maelekezo afu upime ukiona mistar miwil ujue imoo ikiwa mmoja jua haimo afu utapima tena kesho asubuhi mkojo wa kwanza ukiona majibu ni Yale Yale basi, nikasema sawa dada asante. Muda huo napiga watu walikua prep nilitoka chooni nikatafuta kikopo nikakojoa nikapima aisee mstar wa kwanza wa chini fasta ukajichora mara wapili ivo ikakamilika mistar miwil mda huo niko chooni sikujali nikaishiwa nguvu nikakaa chini hapohapo, sikuamin yn mm ni mjamzito?bdo miez miwili na kidogo nimalize kidato cha sita jmn nafukuzwa mm,na baba mtoto ni ticha d sasa na zile picha nipo na wanaume atakubali kweli mimba hii?mbali na wanaume pia mm ni mwanafunzi atakubali si atafukuzwa kazi na kufungwa nikachanganyikiwa..santa mm nitamwmbia nn mama yangu tena m ndio wakwanza?wadogo zangu wataiga nn kwangu?santa mm nimekwisha, nikaanza kulia sielewii na shuleni kwetu mwezi mmoja kabla ya pepa tunapimwa mimba..kwisha habari yangu mm jmn …nini kitajili hapo?santa mie tyr yamenikuta kitumbo ndiii
USIKOSE
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU