Sehemu ya 10
Tulipoishia..santa mm nikaanza kulia sielewi na shule kwetu mwezi mmoja kabla ya pepa tunapimwa mimba…kwisha habari yangu mimi jmn kitumbo ndii.tunaendelea sasa,
nikawaza sana nikaona ninyanyuke tu, nikanyanyuka nikaoga nikampigia DA silvia akasema vip dogo nikamdanganya sina mimba dada nimeona mstari mmoja, mana nilijua nikasema atauliza habari za baba wa mtoto na sikutaka sema baba ni nani,akasema afadhari sasa soma kwa bidii nikasema sawa,nikawaza nimwambie ticha d?je atanielewa kweli?na mambo yote yale si atajua niliwahi kuwa na mwanaume mwengine yule gerald?nilijawa mawazo sana siku io nikaona liwalo na liwe ngoja niende kwa d nikarud rum nikavizia usiku kabisa watu wamerud kutoka prep wamelala nikatoka kama naenda darasani, nilivofika mitaa ya kwenye kamba kuna wanafunzi walikua wanaanika nguo huku wanaongea wanasema, jmn umemuona mwanamke wa ticha dyln?yn mzuri uyoo jamani, ndo mana ticha anaringa kumbe, mwengine akasema ndo Ivo yn dada mzuri mno anamshepu balaa,nilikosa nguvu niliskia maumivu kama mtu ananikata moyo na msumeno, nikajiuliza niende au nisiende nikaona wee hapana maneno ya kuskia acha nikajihakikishie,nikaenda kimya kimya naangalia huku na kule kama mwizi,hapo ni SAA sita hivi usiku, nilivofika mlangoni nikaskia d anaongea na mtu nikazunguka dirishani kuchungulia mara nikaona mdada kweli mrembo kavaa kigauni kifupi amekaa kwa sofa mi niliposimama naona sura yake vizuri wanaangalia muvi, yule dada akasema muvi inapanda na hii wine hatari pata picha mzuka wake,d akacheka afu akasema hatari mamangu hapo mzuka wa kushea hapo ndo mana nakupenda mnyamwezi wangu unaweza kukesha,wakacheka yule dada akasema kwa kudeka njoo unimasag shingo mana kama imekaza ivi, d akasema poa naja bby,akanyanyuka hapo yupo na kaptula tu na singlend alikua sofa lingine hapo akamfata mdada akajilaza akalalia tumbo jitako kubwa lipo juu, d akamkalia kwa juu sijuweza kuendelea kuangalia na sikua na cha kusema tumbo la kuharisha lilinibana majib nilishayapata nikaondoka zangu nikiwa sina raha machozi yananitoka tu,nafanyaje na hii mimba?nilijiona nimetengwa nje ya dunia nipo peke angu mdogo mdogo nikarudi bwenini,tokea siku io nikawa mtu wa kukosa raha nakonda sili vizuri lkn najitahidi kusoma sana mwezi ukaisha d alikua anauliza wanangu tu mbna mama yenu anakonda haonekani, wanangu wanasema anasoma sana siku zikaenda vanessa akarudi shule ila hatuna stor,nikaendelea na masomo mara kipindi cha graduation kikafika mama akaja na wadogo zangu,waliniletea keki na zawad pia nikapata zawad za shule za taaluma mana nilikua nafanya vizur sana na siku hio d hakuepo sikujua kaenda wap,mama alishangaa na kupungua kwangu nikawa na vipele sana usoni yani nimepoteza nuru nipo kama ganda la limao kabisa utafkiri nimepigwa chuping usoni vipele vimejaa,mama akauliza ww una matatizo gn mbona upo hivo? Nikasema masomo magumu akasema mmh masomo hadi vipele husoni nikasema mama jmn mabadiliko ya hali ya hewa haya afu nipo brid mama akasema ooh kumbe haya,dada silvia alikuja pia kwenye graduation akaniona sasa nilivo na kuna muda nikajiskia hovyo nikatoka kumbe ananifata sijaona akanikuta natapika akasema mdogo angu nn shida mbona hivyo? Ebu niambie nikusaidie, nikaona hakuna namna nikamwambia huku machozi yananitoka nikasema dada mm ni mjamzito akasema wee santa wewe kweli?nikasema ndio akasema pole miezi mingap nikamwambia mpaka sasa itakua miwili naelekea mitatu hiv akasema daaa baba wa mtoto yuko wapi sasa, nikasema mpaka sasa sijui alipo mana hapatkani kwenye simu,silvia akasema pole mdogo angu jmn pole sana sasa jikaze ufanye mtihani sawa nikasema sawa,akasema unapenda kula nn?nikasema napenda mishkaki tu na ubuyu,akasema sawa nitakua nakutumia hela uwe unakula kila siku ila jitahid bdo wik tatu muanze pepa ivi mmepimwa mimba? Nikasema hapana akasema mtapimwa muda wowote sasa sijui itakuaje?, nikasema itajulikana tu akasema sawa jitahid kujificha usikae karibu na kina madam nikasema sawa,basi tukarudi kwenye sherehe dada silvia alikua mwenyej mitaa ya shule akaagiza mishkaki mingi kijijini ikaletwa nikala sana baada ya sherehe kuisha wakaondoka kina mama na wakaenda kulala kwa dada silvia kesho yake mama safari ya mbeya ikaanza.
Baada ya siku nne walikuja manesi shule kutupima mimba nilivoskia tu nilianza kulia bwenini sijui nafanyaje nikapata wazo, nikabaki nimelala bwenini nilichukua bunda la pedi nikaweka kitandani nimezifungua hapo wanafunzi wote wameitwa nikachukua na wembe nikajikata kiganjani mkononi mkono wa kushoto nikaangusha dam chini zingine nikajipaka kwenye nguo niliovaa na shuka afu nikapaka chumvi mkononi kukata damu mana nakuaga na chumvi bwenini,nilikua walimu watakuja kuangalia wanafunzi waliobaki, ni kweli madam akawa anakuja nilivoskia sauti nje nilianza kugalagala hapo chozi linanitoka ujasiri wa kujikata sijui nilitoa wapi jmn, madam alivoniona akasema vipi wewe? Nikasema madam naumwa sana tumbo la brid yn naumwa sana huku nalia, madam akasema jmn ndo ujichafue hivo santa jmn ona hadi chini damu jmn? Mbona aibu hizi angekuja wa kiume je? Nilikua kimya najigeuza geuza tu akauliza limeanza lini nikasema jana usiku akasema umepata dawa nikasema sijapata, akasema ngoja nikakutaftie, hapo nalia mnoo, dasa jikaze ufute damu uloweke nguo na ilo shuka jmn santa, nikasema sawa, madam alitoka nikashkuru nikafuta damu na nikatoa nguo fasta na kubadiki shuka, baada ya muda akarudi na dicloper akanipa nikanywa, akasema pumzika jikaze ndo ukubwa litaacha kisha akatoka,nilifurahi na hio ndio nilikua pona yangu jmn mana hapo utulivu wangu wa uongo shule ulisaidia, DA silvia alinilea wiki zote tatu ananiagizia mishkak na ubuyu kwenye gar inaletwa nakula angalau nikawa na nguvu,d hakuwepo na sikujua yupo wapi nikapiga sana namba yake ya simu lkn hakuwa anapatkana basi sikuelewa kabisa,siku zikaenda ikafika kipindi cha mitihani nikafanya mitihani vizur tena ilinijia vizuri mengi niliyajua nilijikaza sana hadi nikamaliza salama,nikajaza fomu ya kukabidhi vitu na vitabu vya shule nikapewa living nikaondoka nikalala kwa DA Silvia kisha kesho yake nikaanza safari kurudi nyumbn mbeya nikiwa na ujauzito wangu,hakuna aliejua mm ni mjazito shuleni na mtu pekee aliejua mm n mjamzito ni dada silvia,nikafika mbeya mama alifurahi sana kuniona nikapokelewa vizuri, majirani walinijua na tabia zangu nzuri sana msikivu na nimetulia pia mtiifu nilikua wa mfano mtaani, nao walinipongeza kwa kumaliza salama na kumwambia mama yani unajua kulea mama santa binti yako n mfano wa kuigwa kwa watoto wetu yani anatabia nzuri sana kitu ambacho kiliniuma na kunichoma sana hawajui mm nina mimba na mbaya zaidi baba yake ni mwalimu wangu jmn nikawaza nifanyaje mana nitamtia mama yangu aibu mtaani wakijua nina mimba tena baba haeleweki nilijikaza nilikaa nyumbani mwezi nikijikaza kazi zote nafanya na kula najitahidi kila kitu nisijukikane, nikaongea na dada silvia kuhusu hilo DA Silvia akasema nakushauri uondoke hapo nyumbn labda ukajishkize mahali ujifungue, nikasema wapi na kwa nani sasa dada? Akasema popote tafuta kibarua labda, nikaomba yeye anitaftie kazi nifanye nijitegemee dada silvia akakubali akasema subir, baada ya wiki akaniunganishia na mtu iringa akanipa kazi ya kuuza supermarket sikutaka kuaga nyumban nilijua mama hatotaka niondoke ivo nikapanga nguo zangu kadhaa kubwa kubwa na kanga na vitenge vichache nguo nyingi nikaacha,nikaandika barua nikamwambia “mama nisamehe kwa maamuzi haya nilochukua bila kukushirikisha mamangu imenibidi nifanye hivi, mimi nimepata kaz ivo naenda kufanya nataka nijiandae kimaisha wakati nasubiri matokeo, sitaki kuwa mzigo kwako mama yangu ,nakupenda sana naomba nielewe usinikasirikie maana nitaishi kwa tabu sana na pia naweza ata kufa kwa kukasirika kwako mama yangu,nakuomba nibariki na niombee mama naondoka nikiwa na huzuni sana,sitaki kukutia aibu mama yangu naomba ujue mm nipo mahali salama natafuta pesa na wakati ukifika nitarudi mama,nakupenda sana ww na wadogo zangu,mimi santa” nikaweka kitandani nikatoroka nyumbn asubuh na mapema nikavunja na laini ya zamani huyoo hadi iringa mana bosi alinitumia nauli,nilivofika kule nilipokelewa na bosi wangu alikua n mama mtu mzima mnene na mremboo sana akasema karibu mwanangu,nikasema asante akasema twende nyumbn nikasema sawa mama akafungua gari yake nzur aina ya prado tukaingia tukaanza safari hadi kwake,tukaingia kwenye mjengo mzuri sana nikapewa chakula akasema leo utalala hapa lakin nimekupangia chumba na sebule karibu na duka utakua unaishi huko, nikasema sawa nashkuru,tukapiga sana stor akasema silvia ni mtoto wa mdogo ake,pia akauliza nimeambiwa una mimba nikasema ndio akasema ya mda gn nikasema miezi minne hivi sasa akauliza umeanza clinik nikasema bdo akasema kesho nitakupeleka nikasema sawa asante mama akasema niite aunt rose nikasema sawa aunt rose, nililala pale ile siku kesho yake mapema niliamka nikasaidiana usafi na msichana wa kazi lkn aunt rose alivoamka akasema sitaki ufanye kazi hizo bana mana huyo namlipa kwa kazi hizo nikasema sawa,tukajiandaa akanipeleka alikonipangia kwanza nikakuta chumbn kuna kitanda kizur na godoro kuna sofa mbil frij ndogo,jiko la gesi na vyombo vichache pia chumba kilikua na choo ndani ni pazur sana akasema hapa ndio utakaa nikamshkuru sana akasema twende tukatoka nje kulikua na flem kubwa sana imefungwa akasema hapa ndo supermarket sasa akafungua jmn vitu ni vingi mno akasema utakaa hapa hapa na ofisi hapa hapa sawa ili uwepo muda wote nikasema sawa akasema kazi yako usimamiz na kupokea pesa tu ww ndio bosi nikiwa sipo sawa mana kuna wafanyakaz wengine watatu,ww utakaa hapa akanionesha sehemu kuna meza nzur na kiti cha sponchi cha kuzunguka akasema kesho nitakuelekeza kila kitu nikasema sawa,akasema twende clinic tukaenda nikapimwa vipimo vyote nikawa sina shida wakanichoma sindano za TT na vidonge vya folic nikapewa,tukaondoka akasema ndani kwako huna chakula tununue kila kitu nikasema sawa,tukapita sokoni akaninunulia mchele debe,tambi,nyama,samaki hadi kuku na sosej,nyanya vitunguu hoho yn mazaga yote ya jikon nilishangaa sana nikashkuru mungu,tukaondoka hadi kwangu nikaweka vitu akasema sasa twende dukani nikakuelekeze kwanza wakati tunasubir chakula nikasema sawa,tukaenda akapiga simu akaagiza chakula akasema mama k wangu unataka kula nn nikasema nyama choma tu akasema sawa aliagiza kuku mzima choma na chips tukala akanielekeza kila kitu akasema mm ni mfanyabiashara wa nje ya nchi ivi nina wik naondoka ivo nakuachia ofc hii sababu namuamin silvia nikasema sawa akasema pesa weka kwenye acc manunuzi nitafanya mwenyew nikija au nitakuelekeza kama bidhaa zimeisha wapi ukafate nikasema sawa aunt,basi kesho yake nikaanza kazi rasmi mm nakaa tu na kuandika na kupokea hela,kazi mwanzo ikikua ngumu lkn nikaelewa nilimshkuru sana dada silvia sikuacha kuwasiliana nae,mshahara wangu alikua ananilipa laki mbili na nusu akasema kazi ikiwa nzur ataniongeza,kwangu mm hela ilikua nyingi sana hio,boss alisafir nikabaki mm nilianza kupendeza na kunenepa nikawa mzur zaidi najua kupaka mafuta na mimba yangu ikawa haichagui vyakula tena da silvia alikua ananifundisha kuweka akiba na kununua vifaa vya kujifungulia,nilivozidi kupendeza wanaume wengi wateja wateja walikua wananitaka na pesa ya soda nilikua naachiwa sana wanavolipia mana supermarket ilikua na wateja wengi sana wakishua,sikua na hamu ya wanaume mana najua yaliyonipata,nilimkumbuka sana bby wangu Dylan lkn sikujua kwa kumpata,niliendelea na maisha yangu nikawa natunza pesa bnk mana bosi alisema pesa ya kula natoa ofisini ivo zangu nikafungua acc nikawa naweka bnk tu najiandaa na uzazi na pia chuo mana nilijua nitafaulu,pesa ya wateja za ofa nilikua ndio nanunua nguo na matumizi madogo madogo madogo pia nikawa natuma nyumbn kwa mama kila siku elfu kumi bora nisile mimi najibana napiga dili cha juu pia natuma kupitia wakala sisemi m nani,kazi ilikua nzur bosi alinipenda sana nilikua naiba kwa akili nikiona mtu anaonekana bos nazidisha bei, bosi alisema alikua na mtu anasimamia akafilisi lkn mm anakuta faida kubwa hivo akawa akisafiri akirud ananiletea zawadi nguo,mara simu nk,nilikaa mimba ikafika miezi saba matokeo yametoka nimepata division three mbovu,sikufaulu vizur lkn at a ivo nilijua siwez soma nikiwa na mimba hivo nikatulia bosi hakuwepo,nilimwambia da silvia akasema utafanyaje nikasema nitazaa kwanza nilee mtoto akichangamka nitaanza hata mwakani kurisit au chuo diploma, mana sijafanya poa akasema sawa,nikasema natafuta hela sitaki nisome kwa shida mana nitajisomesha na kumuacha mwanangu ktk maizingira mazuri dada akasema sawa,pia bosi nilimpigia simu akasema sawa,nikaona nimpigie na mama kwa kutumia namba ya mtu,nilivojitambulisha tu mama alifurah sana akanipa pole akasema mwanangu rudi basi nyumbn tuangalie cha kufanya usiogope najua ni bahati mbaya nikasema mama mda bdo mamangu nitarudi lkm acha nitafute hela kwanza mwaka huu kisha mwakani nitaanza chuo mama akasema kweli nikasema niamin mama yngu,mama akasema sawa hii ni namba yako nikasema hapana nitakupa yangu,nilivoona mama amefurahi hana shida nikampa namba yangu,akashukuru akasema zile peda najua unanitumiaga wewe mwanangu nikasema kweli mama akashukuru sana, akasema anafanya biashara na amejiunga na vikundi sana iv mana anahela nikacheka tu,bosi wangu alirudi akaniletea zawad ya kitanda cha mtoto na nguo nyingi za mtoto mchanga zingine kubwa kipind hiko miezi nane tayar nipo napiga kazi tu na mshahara aliniongeza akawa ananipa lak 3 nanusu kwa mwezi bdo marupurupu na akijiskia ananipa tu hela mm naweka bank kwangu mana mm namuingizia mil kadhaa kwa siku.
siku moja alikuja kaka mmoja mtanashati sana akapak gari yake nzur nje akaja akanisalimia akaingia kutafuta vitu alinunua vinywaj vya bei mbaya pombe kali,akachukua na kuku na vitu vingine akaja kulipia,bili yake ilikua mil 2 na kidogo,alivolipa akasema na ww chagua kitu chochote unachotaka,nikasema jmn asante nitachagua badae akasema noo chagua sa iv nataka nikupe zawad ya huyo kijacho wetu yn kitumbo nilikua ndii kweli hakijifichi, nikacheka nikanyanyuka kulikua hakuna wateja wengi sana nikaenda kutafuta bby show nzur akasema chukua na kile pale akaonesha kile kibaskeli cha kusukumia mtoto kama mnatembea ni bei nilishangaa nikasema jmn asante akasema usijali akalipa cash,afu akasema naitwa rodney nikasema asante kaka rodney,akasema sawa mama k akaniwekea dola mia mezan akasema hio utakula jioni sawa nilistuka nusu nizimie mie santa mepewa dolali? nikasema jmn asante yeye huyo akaondoka zake,nikashangaa sana,kuna msichana mmoja nafanya nae kazi anaitwa lulu n rafik angu yy anawaelekeza wateja wanapotaka vitu na kuwasaidia kusukuma kitololi pia kupanga vitu supermarket akaja akasema mmh shoga angu una kismat yn na aliepo tumbon anakismat sana nae anapewa zawadi nikacheka tu akasema ila kaka mzuri huyo khaa na ww ulivo mtaendana sana,nikasema lulu mm mjamzito hawez nitaka mm na mimba hii basi tu kanionea imani tumbo kubwa nipo kazini tukachekaa lulu akasema na huo mshepu umevaa gauni pana lkn bdo mshepu umejichora ukitembea mtako unatikisika hatari niliaon anakuangalia ndo mana akasema ongeza na kile 😂😂nilicheka sana, nikasema ebu niache bna wateja hao kawapokee akaenda huku anacheka,kazi siliendelea yule kaka alikua anakuja kila siku na ananiachia pesa za kula eti na kijacho, mwishowe siku moja akaja na bosi wangu akiwepo wakasalimiana kama wanajuana akanunua vitu akaja kulipa afu akaniambia leo naomba tukale wote chakula cha usiku santa kama hutojali,nikastuka mana sikuwah mwambia jina,akasema nipe simu yako kwanza nikampa akaandika namba yake akajibip muda huo bosi yupo kwa ndani anapanga mizigo alioleta Rodney akasema badae pliz sawa nikasema sawa huku nikitabasamu (si ananipa dolali jmn nakataaje sasa?) kama kawaida akaniachia dola akaondoka,bos wangu akaja mbio mbio akasema santa huyu kaka ni tajiri mtoto hatar anahela nyingi sana ana makampuni na hana mke,kakupenda sana ameniambia ivo usilaze damu changamka,ushamba wa mbeya utowe sawa?nikasema lkn aunt mm ni mjamzito akasema kwani shida yako nn?we unafkir kipofu yule?tumbo lote hilo unafkir hajaona?tulia mama ule raha za dunia mimba mimba babake yuko wapi? Tulia na tajili wewe nikacheka akasema ehee kasemaje kasemajeee nikasema kasema jioni tukale wote chakula,bos akasema sasa nenda mama tena pendeza usimkatalie,nikajiwazia na mimba yangu jmn iv niende au nisiende? Kweli mtu anaeza penda mjamzito?au mchawi huyu kaka?au hazimo?
USIKOSEE
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU