Mahaba ya Dhati (26) 💞❤️

Sehemu ya 26

Tahiya akasema shogaa rodney kweli kidume khaaa hahahaaa,nikasema mwenzio naogopa,tahiya akasema we vip unaogopa nn sasa, nikasema hii mimba uwii labda hatapenda?akasema atakua mwehu akati mm naona anakupenda sana, nikasema tee huna unachokijua ebu twende nyumbn kuna kitu nikakusimulie,akasema sawa,tulitumia gari ya tahiya siku hio tukaenda hadi nyumbn kwake maana alisema anataka aniuguze mwenyewe nyumbn kwake,(nimekuana na tahiya mwaka na miezi kadhaa nimempima kwa vingi na akafuzu kuwa rafiki yangu,) basi tulivofika nikamsimulia stor nzima ya mm na Dylan na rodney lkn Tee akasema rodney ndio mme shoga angu sijui kwa nini hukuona tokea zamani, 

ebu mwambie una minba yake na sahau hayo yote ya nyuma dear, nikasema lakini siwezi mwambia kwenye simu bora niende iringa akasema poa napo vizuri sana ukifanya ivo, nikasema sawa akasema utapanda basi na hali hio hapana acha nikupeleke maana mm niko likizo si unajua nikasema asante dear wangu ,na mm nlikua na ka cheo lidogo ofcn hivo kuomba ruhusa nj rahisi,keshk yake nilienda ofcn nikaomba ruhusa kuwa naumwa naenda tibiwa nikakubaliwa nikarudi nyumbn kujiandaa na safari, baada ya siku mbili tukaanza safari ya iringa tena wala sikumwambia rodney kama naenda niliraka nikamstukize,tuliondoka mbeya mida ya saa moja asubuhi,saa tano tukawa iringa tyr,

tukaenda kwa aunt rose kwanza, akafurahi sana kuniona akanipokea vizuri japo alikua na hali ngumu ya kiuchumi wakati huko tuliongea mengi akanisimukia pia kuhusu kushuka kwake kiuchumi akasema ana madeni mengi sana,nikampa pole nikawaza kumfanyia kitu japo sikumuambia,nae akauliza maisha yangu nikamwambia namshkuru Mungu pia nimerudiana na rodney alifurahi sanaa hadi akaimba akasema yn wewe mtoto uliacha dhahabu aunt yangu lkn rodney anakupenda sana,nikasema najuta yote niliofanya, basi tulikaa pale hadi jioni nikaahidi kumpa aunt pesa kiasi za kununua vitu supermarket mana mtaji alikua hana ivo nikaajidi kumpa mtaji akashukuru sana na kusema nikimpa tu atafata vitu,baada ya maongezi nikasema ngoja niende kwa rodney mana nilikua nachat nae akasema amerudi nyumbn tayari tokea kazini asijue mimi nipo hapo iringa ,

Tahiya akasema aunt naomba nibaki hapa nikae hapa wakati huyu anaenda kwa mmewe, mm nikasema rodney ana nyumba kubwa twende wote, yeye akasema nimekuleta uwe huru na bby wako ivo usijali mm nitakuepo hapa kwa aunt tu,aunt hakuwa na hiana akasema kweli tahiya hawa waache wakaishi wenyewe huko kwanza sie tubaki hapa nikacheka basi wakanipeleka kwa rodney tulivofika tukagonga kengele rodney akaja kufungua akaona gari ya tahiya akaanza kucheka akafungua geti lote tukaingia tukashuka akamsalimia kwanza aunt rose akamsalimia tahiya kisha akanikumbatia mm akasema mke wangu umekuja kwako hatimae nikacheka nikasema ndio nimekuja kufumania, akasema ona sasa utajifumania mwnyewe,

tukacheka tukaingia ndani,sebleni aliwekaga picha zangu za zamani nikiwa nae nilishangaa sana bdo hazijatolewa,tulipiga stor rodney alipeleka begi langu chumbani akaja akasema sijapika mm naomba twende nje tukale hatukua na pingamizi tukatoka hadi hotel tukala na kunywa lkn mimi chakula kikawa kinanishinda kabisa naenda sana kutapika na rodney ndie alikua ananisindikiza akasema bby homa bado io nikasema naona bdo na najiskia vibaya naomba turudi tu nyumbn akasema sawa,tukarudi walipo kina tee na aunt, rodney akasema samahani jmn santa hayupo poa naomba nimrudishe nyumbn aunt akasema pole aunt yangu nyie nenden mm na tahiya tutakuepo bado rod akasema sawa akatoa hela akampa aunt akasema asante aunt,wakati nataka kuondoka aunt akaniita akaniambia kimimba kichanga ikoo kinasumbua nikachekaaaa sana aunt alishagundua nikamkumbatia tee nikamuaga tukaondoka,tukafika nyumbn mm ni natapika mtindo mmoja yn kama ndo sifa imeanza sasa, 

rodney alihangaika sana nikamwambia anitaftie malimao akaondoka usiku huo akahangaika huko akapata kaniletea nikaanza kuyalamba na chumvi ndio nikatulia,akasema pole bby wangu nikasema asante akasema kesho twende tena hospital nikasema bby haina haja mwanzoni huwa inakua hivi akasema mwanzoni?? Sijakuelewa bby,nikachukua mkono wake nikagusisha tumboni nikasema bby nina mimba unatarajia kuwa baba,rodney akacheka akasema bby unanitania nikasema hapana bby mm ni mjamzito na nimekuja kukuambia hilo akawa kama kapigwa butwaa hajaamini, akaanza kunipa mabusu huku amefurahi sana, akasema bby sijawahi ambiwa hivo tokea nazaliwa,yani mi naenda kuwa baba sasa,

nakupenda sana mama k wangu nitakulea na kukupa kila kitu utakacho,nikasema nakupenda pia baba k wangu akanikumbatia tukalala vile,asubuh aliwahi amka akapiga simu kazini kwake kuwa haendi kazi zote wamtumie kwenye email yake,alinipikia supu na malimao kibao ilikula vizuri tukaenda hospital kupima vipimo mbali mbali wote pia kupewa ushauri wa vyakula na jinsi ya kujitunza wakati wa mimba nikapimwa utra sound rodney alifurahi sana,kisha tukarudi nyumbn,rodney alisema anataka kunioa kabla ya kujifungua hataki mtoto wake azaliwe nje ya ndoa nikasema mmh utawezekana? akasema yah kwa nini isiwezekane? Wewe utawaambia byunbn kwenu nikaanza na mimi nitawaambia kwetu,

pia nakuja kukuhudumia mwenyew kazi zake atafanya kwa njia ya mtandao nikasema sawa bby baada ya wiki nikarudi mbeya na shoga angu nikamwambia mama lengo la rodney mama akasema yeye hana pingamizi ataongea na shangazi zangu na mama zangu wadogo baada ya wiki akanipa jibu kuwa waje walete mahari nikampa jibu rodney nae alikua ashaongea na kwao,walikuja wazazi wake wote na ndugu zake baadhi akiwemo mshenga wakatoa mahari tukala na kunywa rasmi nikavalishwa pete,huku kimimba kinakua na rodney akihudumia kwa hali na mali,ikaja majadiliano wapi tutaishi mm nikasema iringa akasema sawa atanifanyia mpango kazi pia nihamie iringa nikasema sawa,tuliandikisha ndoa iringa siku ikafika tukafunga ndoa yetu iliofana sana sikuamini nailewa na rodney sasa, 

baada ya ndoa honeymoon mtoto nikapelekwa south Africa mie nilikaa huko hadi nikajifungua cha ajabu nilijifungua mapacha akati utra sound ilionesha mtoto mmoja nikapata wakike na wakiume,furaha yetu ilizidi bada ya ,miezi miwili tukarudi bongo, nikifanyiwa mchakati wa uhamisho kazini nikafanikiwa kuhamia rasmi kwa mme, aunt nikimpa mtaji alifurahi na kushukuru sana. nyumba yangu mbeya wakahamia wadogo zangu niliwapa mashart wakiharibu nyumba watalipa na nitawahamisha vile nyumba nzuri wakasema wataitunza,maisha yangu yalikua mazuri sana kila nilichotaka nilipata watoto wadogo walishafunguliwa account yao bank,mapenzi niliokua nayapata kwa rodney sikuwahi hata ota kupendwa hivi,tulikua ni zaidi ya mme na mke tulikua marafiki wakubwa tupo kolikoli tulikua tunafanya vitu vingi vya kimaendeleo tulinunua maeneo tukajenga maduka ya kupangisha tukajenga hoteli ikaanza kazi watoto wakazidi kukua hadi wakatimiza miaka miwili,

mm pesa yangu ya mshahara rodney alikua hata haulizi wala hataki nitumie kwa mambo ya ndani wala mavazi ya watoto wala mm mwenyewe alisema yeye ni mme kila kitu atafanya ivo nikawa namtumia mama na nasomesha mwanangu Yule wa mbeya,siku moja tulikua nyumbn na mme wangu na watoto yeye alikua juu kipindi hiko tumehamia mjengoni kwetu kwingine ni nyumba alioanzaga kuijenga rodney kabla hajanioa ni nyumba kubwa ya ghorofa moja ya kisasa ina eneo kubwa sna,sasa mm nilikua sebleni na pacha wa kike mme wangu alikua na pacha wa kiume wanabadilishana nguo juu alikua amejisaidia,mara mlango uligongwa nikaenda kufungua nikakutana uso kwa uso na dylan akiwa na begi kubwa analivuta akastuka baada ya kuniona na kushangaa sana akasema santa?unafanya nn hapa we mwanamke?,,,,je nn kitaendelea

USIKOSEE

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!