SEASON 01: CONNECTION YA BALTASAR (01)

SEHEMU YA 01

😂😂😂😂Em kwanza nicheke mieee  , hivi mnakumbuka zile issue za yule baba wa kule sijui  wapi wapii  mi hata sijui bwana anatokea wapiii yulee wa 400+ video 😜😜😜

   Siku enyewe nilikuwa saloon bwana nimeenda kuosha osha nywele hivi nisuke kilimanjaro yangu ya buku 🤗🤗🤗

  Wamama wa saloon hapo wakaanza kupiga story sijui kuna mbaba video zake zimevuja anafanya mapenzi na wanawake 400 heee🙄🙄 nikashtukaa aaweeh hii tena mbona mpyaa , Sikutaka kuchangia mada mana mie mpole mpolee  😅😅najifanya sina hatia ila nikawa nameza maneno na mie nirudi mtaani kuwahadithia shost zangu

Mana habari zilikuwa bado za motooooo😜😜😜wakawa wanasema kuna huyo baba sijui wa nchi gani huko, ni  kiongozi mkubwa tu serikalini , amekutwa na video 400+ za ngono kwenye Laptop yake akifanya mapenzi na wanawake  tofauti tofauti

Embu Imagine yaan wanawake 400 halafu hizo video zotee ni zake yeye ila wanawake ndio tofauti tofauti  wanafika 400 tena na kupita we huogopiii

Nakuuliza we huogopii??😅😅😅Mi niliogopaa mwili ukanisisimkaa,
Ndio maana mie sitaki  kuwa na bwana akaa bora nitunze kidude changu😜😜 tena nilichoka baada ya kusikia et ni mume wa mtu mmh🙄🙄mi sitaki kuolewa bwana😫😫😫, Umbea nikaumeza wotee .

Nilipo toka hapo sasa mimi ndio kinara mtaani story zote ninazo nawakarisha watu chumvi kama zoteee 😂😂😂

   Basi mie nina Tambo langu bwana , yaan nikisema tambo namaanisha lisiimu kubwaa la Tecno lakini mie ndio natambia nalo si langu

Hata siwekagi bundle  nikupigiwa tu nakupokea kwanza niweke bundle nina hela miee ya kuchezea😅😅😅

Sasa kwakua mie mtaani nishaonekana star mana kila mtu alikuwa ananifata kuniuliza  kama ni kweli , nikimuhadithia huyu nae anaenda  kuhadithia wenzie hukoo wakimuuliza alipotoa anasema kwangu nao wanakuja kuthibitisha  , 
  
  Ilibidi   nimuibie jero mama ili niweke bundle  la jero ili namie nipate habari kamili mana nilisikia wale wa mama wanasema huko mtandaoni kumechafuka kila sehemu ni habari za huyo baba tu na video zake zimesambaa kila kona

Nikaweka zangu ki bundle cha jero tu( 500Tsh) safari ya kwanza ni mjini  FACEBOOK 😅😅😅Niingie insta kufanya nini yaan mie insta jamani naonaga kumepoooza hata hakunogi sijui ndio mshamba  hata sijui  ila kule kwa mr Fb aloooo🙌🙌🙌 

Huko ndio naonaga umbea full full, sasa nikaingia ili niongeze materia  ya bwana mianne plus😅😅😅 ili niwaadithie vizuri  mtaani  nikiwa na ushahidi wa kuona mwenyewe

Nilikuwa napita kila page nasomaaaa tena kwa umakini hatarii , kila page kila page , kila taarifa inayo muhusu mr mianne plus nilikuwa siiachi inipiteee

  Sasa nikapita kwenye page moja hivi nikakutana na post inasema et bwana mianne plus mbona anapenda kushika chuchu hii inamaana gani??
  Nikazama kwenye Comments ili nipate data namie , nikikaa kusimulia nitoe udaku mzitoo😅😅😅😅
   Kuna Comments  zingine zinasema anatema tema mate mie ananikera mwengine anasema  hata mimi sipendi linavyotema mate basi tuuu

  Namie roho ya kutaka kuona video sasa si ndio ikanivamiaaa🙄🙄🙄

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

CHAGUO LA MOYO FULL

KIAPO CHA MASIKINI FULL

JOGGING MASTER FULL