SEASON 2: BIKIRA YA BIBI HARUSI (23)

SEHEMU YA 23

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA 22: “ebu! mchukueni huyu mpuuzi, mka mchinjilie mbali, pumbavu jambo baya jambo mbaya jambo mabaya, sasa anaenda kufanyiwa huyu demu wako” alisema yule jamaa, na hapo wakainuka wale jamaa wote, waliobakia pale kwenye gogo, na kuanza kumfuata Edgar, pasipo kujuwa kuwa Edgar alikuwa na store ya silaha mwilini mwake. ENDELEA ……….
Hapo Monalisa akiwa anatetemeka, akamwona Edgar anajipapasa kiunoni, kama anajikuna hivi, “sina tena msamaha na nyie wapuuzi” alisema Edgar, akimweleza yule jamaa alie kuwa karibu yake, ambae alistuka kwa jinsi Edgar alivyo jiamini, akamtazama vizuri, akaona mkanda wa silaha begani kwake, na kutazama vizuri alikuwa na SMG, “mama yangu!” alistuka kwanguvu yule jamaa, na ile kutahamaki, tayari mkono wa Edgar ulikuwa umeibuka na bastora, toka kiunoni, na kuelekezwa kwa yule alie shikilia gobole, ikifwatiwa na ‘tyuuuu!’ hapo wakamwona kiachia lile gobole likianguka na kujishika bega, “mamaaaaa” alisikia yule jamaa wagobole, na hapo ukasikika mlipuko mkubwa wa risasi ya gobole lililo jifyetua, baada ya kujibamiza chini, wenzake wakashangaa na kumwona akitokwa na damu kwenye bega, lakini hapo hapo Edgar akamwongeza risasi ya mguu, na yule jamaa akaanguka chini akilivamia gogo nyuma yake, huku akijipigiza chini, hapo wale wengine wanne ukiachilia huy aliekuwa karibu yake, wakagutuka, na kutambua kuwa huyu kijana hakuwa wakawaida, wakataka kuanza kukimbia, lakini aikuwa bahati yao, maana kufumba na kufumbua, ikasikika ‘tyuuu! tyuuu! tyuuuu! tyuuu!’ wale wa nne pia wakala wakaonekana kila moja moja, akijishika kwenye mguu, karibu na paja, huku wakishindwa kukimbia, na kuanguka chini, huku wana angua vilio, “nazani ume elewa nilicho maanisha, na hivi ndivyo tunavyo tafuta heshima iwapo kuna mtu anatuvunjia heshima” alisema Edgar huku anageuka kumtazama yule jamaa, ambae alikuwa anatetemeka kama vile amefumaniwa na mke wa mwanajeshi, anae toka vitani, nikweli hakutegemea kabisa, tukio lile, hapo hapo Monalisa akaokota kibade cha kuni kwenye ule moto, na kumpiganacho kichwani yule jamaa, ambae alikata mto na kundoka chini, “shenzi we! ulitaka umfanye nani?” alisema Monalisa huku akiuvuta tena ule mti wa kuni, na kuushusha usoni kwa yule jamaa, ambae alikuwa ametulia pale chini, pasipo kuwa nafahamu.**
*
Hokololo alisimamisha gari, sambamba na magari mengine, yani la mbele la OCD na lile la nyuma yao, “nini hicho,?” aliuliza kamanda Kingarame, huku yeye na Hokololo wakishuka toka kwenye gari, kama wengine walivyo fanya, kwenye magari yote, “nazani kuna gari moja lime pata bust” alisema Hokololo, huku wakisaidiana kutazama gari la mbele na nyuma yao, lakini na wao wakawaona wenzao wana watazama wao, “afande huo mlio umetokea upande huu, tena inaonyesha ni mbali kidogo” alisema askari mmoja aliekuwa nyuma ya gari la Kingarame, “unaweza uwa mlio wa nini?” aliuliza Kingarame “hiyo ni bunduki, watakuwa wawindaji hao” alisema yule askari na wengine wakaunga mkono, na muda huo wakaliona gari jingine likitokea upande ambao wao wanaelekea.
Alikuwa ni sajent Kibabu na askari wake, wakifanya doria, na walisha yaona magari ambayo yalikuwa yana kuja upande wao, na walisha sikia uli mlipuko wa risasi toka msituni, nao wakahisi kuwa watauwa ni wawindaji wapo kazini,
Sajent Kibabu kwanza alifurahi sana kumwona mkuu wake wakazi, wakaitana pembeni na kupeana report kama zilivyo, huku Kingarame akimweleza uwezekano wa Kisona kuja huku Njombe, na uamuzi aliochukuwa wa kuyapoteza maisha ya kanali huyu Kijana, alie amua kuingilia mpango wao, “ila afande inaonyesha huyu bwana mdogo, ana ujuzi mkubwa sana katika mapambano, na matumizi ya silaha, asa katika pori, maana siyo wakawaida, na sizani kama ni kweli huyu dogo ni mwanafunzi” alieeza wasi wasi wake sajent Kibabu, “yote kwa yote nimeelezwa kuwa mpo wengi sana huku, na mimi nimekuja na askari wengine, lazima kesho mapama tu! tuakikishe ana lejea kwa muumba wake” alisema Kingarame, nawaliendelea kupanga mipango yao, ikiwa ni pamoja na mpango wa kumwangamiza Kisona, ambae walikuwa na uakika kuwa, lazima ataitaji kuja porini, kwa lengo la kuakikisha Edgar anakamatwa bila kuuwawa, “hivyo tuta kuwa makini kuangalia muda atakao toka mjini, na sisi tumtegee ambush, andaa askari na mabomu ya kutosha, tumgeuze jivu kabisa, ndani yagari, tufute ushaidi, kesi tuta mpa huyu mpuuzi, Edgar” alisema Kingarame akiamini kuwa ni jambo jepesi sana, kumwangamiza kanal Joseph Kisona, “wazo zuri afande, wacha nikachague askari wakuanda ambush” alisema Kibabu, ambae mambo aliyo yashuhudia huko porini ni siri yake.
Baada ya maongezi ya muda mfupi, Kingarame aliaga kwa kudai kuwa amechoka na safari, ya kutoka songea na kuaidi kuwa ata rudi kesho, huku wakisitiziana kumfwatilia kwa karibu sana bwana kisona kule atapo kuwepo na mawazo yao yalihisi kuwa atakuwa anampango wa kufikia makambako, kwenye kambi la jeshi la ulinzi, “kesho mapema, nita tuma askari, kwenda kuwa fwatilia Makambako” alisema Kingarame na kuelekea kwenye gari, na safari ya kurudi mjini Njombe ikaanza, na kama walivyo kuja, OCD aliongoza msafara. ***
kule kwenye kambi ya wawindaji haramu, alionekana yule jamaa alie jifanya kiongozi wa lile kundi la wawindaji haramu, akiwa amelala chini, damu zina mvuja usoni, huku amefungwa kamba mikononi na miguuni, lakini sasa alikuwa amesha zinduka, anawatazama awa vijana wawili wakike na wakiume, wakiwa wamekaa kwenye lile gogo pembeni ya moto, walio kuwa wana jikatia mapande ya nyama ya swala, iliyo kuwa imebanikwa, kwenye ule moto, na kuitafuna kwa fujo wakishushia na maji, akika walionekana kuwa wenye njaa kali sana, huku ndoo moja ya bati ikiwa kwenye moto ikionyesha walikuwa wanachemsha maji,
Na kama alivyo kuwa yeye, pia aliwaona wenzie wakiwa wame fungwa kamba kwa pamoja, kama vile fungu la mzigo wakiunganishwa kwa pamoja, wasiweze ata kujifungua kamba zile, na hawakuthubutu ata kumsemesha, Edgar, maana walihisi kwa jambo ambalo walitaka kumfwanyia mwanzo, ingekuwa lahisi kwake kuwaangamiza, kama wange mkela kwa maneno.
“nitamu hen! yani natamani tungeipata toka mchana” alisema Monalisa, alie kuwa amekaa pembeni kabisa ya Edgar, “kila kitu kinakuja kwa wakati, pengine usinge iona tamu, sababu usinge kuwa na njaa kama hii” alijibu Edgar alie kuwa ana geuza pande la mnofu, juu ya kichanja kwenye moto, “mh! mwenzio njaa ilianza kuniuma toka asubuhi” alisema Monalisa huku anaendelea kutafuna nyama ya mnyama huyu wa porini, Edgar akamtazama Monalisa, kwa sekunde kadhaa, bila kuweleza jambo, yani nikama alikuwa anatafakari jambo, kisha akasema “dah! pole sana, basi kesho nitahakikisha aupatwi na njaa tena” ilikuwa sauti tulivu ya Edgar, ambayo ilimletea kitu flani Monalisa, ambae aliinua usowake na kumtazama Edgar, na macho yao yaka kutana, hapo Monalisa akatabasamu kidogo, sambamba na Edgar, “kwani wewe ujajisikia njaa?” aliuliza Monalisa huku akimtazama Edgar, na kuendelea kutafuna nyama, “siuweza kuhisi njaa, wakati wewe ujala” alisema Edgar na kumshangaza Monalisa, “ebu lione kwanza, kwani mimi nani wako mpaka iwe hivyo?” alisema Monalisa kwa mshangao, huku akimgonga Edgar kwa kibega chake, “kwani wewe unahisi nini, hivi unazani mwanaume naweza kulalamika njaa kabla ya wanamke?” alisema Edgar akibadiri maana yay a manen yake ya mwanzo, kichwani kwa Momalisa, hapo Monalisa akaishia kuguna tu!, alafu akajaribu kuyagusa maji, kwenye ile ndoo ya chuma, “Eddy yamesha pata” alisema Monalisa, huku akichukuwa maji mangine kwenye kidole chake na kumgusisha Edgar, juu ya kinganja chake cha mkono, “poa basi wacha nikaoge” alisema Edgar, huku akitaka kuinuka, “wewe! situme kubaliana nikaanze mimi” alisema Monalisa huku ana mzuwia Edgar asisimame pale kwenye gogo, “sasa kwanini unaniambia mimi kuwa yamepatamoto, baada ya kuchukuwa ukaoge, na mimi nibandike yakwangu” alisema Edgar huku akimtazama Monalisa, kwa macho makavu, “alafu huyuuuu! sinimekuambia, ili unitolee kwenye mto” alisema Monalisa, kwa sauti flani hivi kana kwamba anamshangaa Edgar. **
Saa tatu hii ikiwa inaenda saa nne kasoro, gari aina ya Nissan Patrol lilionekana likikatiza maeneo ya Madaba, na kuupita mji huo mdogo ukiwa kimya kabisa, ukungu ulikuwa mwingi sana, na kumfanta dereva atembee taratibu sana, akiogopa kuliingiza gari kwenye makorongo, kwa kuto kuona bara bara, zenye kona miinuka na mabonde mengi sana, kiukweli dereva huyu alifanya kuwa na wakati mgumu sana, maana alikuwa peke yake, akisikia mikiromo ya kilevi, toka kwa abiria wake, ni baada ya wengine wote kuwa wamelala, kasoro mama Monalisa alie kuwa ana vuta kamasi na futa machozi, **
Huku nako mama Edgar alikuwa anagala gala, kwenye kitanda chake kikubwa, huku mala kwa mala akiitazama album ya picha za familia, akiitazama picha ya Edgar, “hapana jamani, baada ya kufurahi kuwa anamemaliza chuo, sasa anaingia kwenye matatizo” aliwaza mama Edgar, “naomba wale wanajeshi wamsaidie baba Eddy, kumpata mwanangu akiwa salama” alisema mama huyu ambae toka mume wake aondoke, alikuwa anatumia muda mwingi kusali juu ya mwanae. Njombe nako ndani ya chumba namba tatu cha hotel ya Serena, mzee Mbogo alikuwa ame jilaza kitandani, pasipo dalili ya usingizi machoni mwake, akiwaza juu ya mwanae wapekee, alie ingia kwenye matatizo ambayo, moja kwa moja ni kwamba alkuwa amesingiziwa. ***
Tukirudi tena porini, walikokuwa Edgar na Monalisa, sasa wote walikuwa wamesha maliza kuoga, kila mmoja kwa wakati wake, na sasa wawili hawa walikuwa wametulia pembeni ya mto, wakiongea hili na lile asa mpango wao wakesho, “nazani nimuimu kesho tukielekea mjini, ili tutsfute mawasiliano na wazazi wetu, pia na kamanda Kisona, pengine tunaweza kupata msaada” alisema Edgar ambae sasa alikuwa ana kata kata nyama zilizo iva, na kuzifunga vizuri, Monalisa aliinua usowake na kumtazama Edgar, nikama alikuwa amekumbuka jambo flani, “Edgar nashukuru sana kwa msaada wako” alisema Monalisa kwa sauti tulivu, iliyojaa chembe chembe za upendo, “msaada gani Mona?” aliuliza Edgar , huku akiendelea kukatakata nyama, “Edgar japo sikuzote tulizo wai kuwa marafiki, umenionyesha kuwa unajali, lakini toka jana nimegundua kuwa unanijali zaidi ya nilivyo kuwa na juwa” alisema Mona na kutulia kidogo akiutazama moto, “unasema nilikujari toka zamani?” aliuliza Edgar kwa mshangao, na Monalisa akastuka na kumtazama pia, “kwahiyo unataka kujifanya ujuwi?, kwani ukumbuki kuwa ulisha pigana mala kadhaa, kwaajili yangu” alisema Monalisa kwa kuhamaki, “inishangaza sana, kama ulikuwa unajuwa kuwa nakujali sasa kwanini, ulipeleka barua yangu kwa mama yako, si ungeniambia mwenye kama utaki” alisema Edgar kwa sauti iliyo ashilia utani, “lakini Eddy uwezi kusahahu mambo ya zamani?” alisema Monalisa, kwa sauti ya kubembeleza, huku akiupeleka mkono wake mgongoni kwa Edgar, na kufanya kama anampapasa kwa kumpooza flani hivi, nae akainua uso wake na kumtazama Monalisa alie kuwa ana mtazama, “siwezi kusahau, japo nilisha samehe” alisema Edgar, huku ana tabasamu, hapo Monalisa akagundua kambo, akautoa mkono wake mgongoni kwa Edgar, “umemsamehe, nani sasa?, ukamsamehe ulie mtuma barua” alisema Monalisa, na kama ungewasikia ungesema tukio hili lilitokea sikuchache zilizopita, Edgar alitulia kidogo na kumtazama Monalisa kwa mshanga, huku akiaacha kukata kata nyama, zilizo chomwa vizuri, “unataka kusema Erasto ndie alie sema kwa mama yako?” aliuliza Edgar kwa mshangao, “haa! inamaana ulikuwa ujuwi?, kwa hiyo siku zote ulikuwa unazani kuwa ni mimi ndie nilie kusema kwa mama?” aliuliza Monalisa kwa mshangao, huku Edgar ambae licha ya kucheza na mona lisa kipindi cha utoto lakini sasa aliona wazi kuwa, hakuwa nahadi ya kuwa na binti huyu, ambae amezidi kuwa mrembo, alishangaa zidi kusuhangaa pia, akihisi kuwa ata vitu vilivyo kuwepo ndani ya ile bahasha alivitoa na kuvitupa, maana mama Monalisa alipokuja kwao usiku wa sikuile, akuiona chupi, “hivi unajuwa kuwa Erasto ndie alie nishauri nikuandikie barua?” alisema Edgar kwa sauti ya kujilahumu sana, “basi mwenzio aliponipa tu, akaenda kumwambia mama, akaja mbio mbio kuni fumania na barua” alisema Monalisa huku anacheka, wote wakacheka.
Unajuwa mdau kunakitu utakuwa umesahau kuwa, wakati wawili hawa wana wana hukumiana kesi za uttoni, wale jamaa sita, yani wawindaji haramu, waliokuwa wamefungwa kamba, walikuwa wameitiwa na usingizi, wakisaidiwa na pombe aina ya ulanzi, “hivi Edgar, ningekukubari ungenifanya nini?” aliuliza Monalisa, huku anacheka cheka, Edgar nae akacheka kidogo, kabla ajajibu, “unge kubari ungejuwa ninge kufanya nini?” alijibu Edgar na wote wakacheka kidogo, “kwani umewafanya wanagapi?” aliza Monalisa, akimtazama Edgar, alie kuwa ana endela kuandaa mzigi wa nyama, ilikiwa ni swali la mtego, Edgar alicheka kidogo, huku ana mtazama Monalisa, “wewe unge kuwa wakwanza na wa mwisho” alisema Edgar kwa sauti tulivu, “mhhh! we! muongo mbona wanawake walikuwa wansema wanakupenda sana kule shuleni, inamaana uja mfanya ata mmoja” ali uliza Monalisa, ambae sasa alikuwa ana mwegemea mala kwa mala, kijana huyu rafiki yake wa zamani, ambae sasa alikuwa anamalizia kufunga nyama, kwaajili ya kesho safarini, Edgar akujibu kitu, zaidi alianza kuweka nyama kwenye begi lake, ambalo ndiyo kubwa kidogo kuliko begi la Monalisa, wakati huo huo wakawa wanawasikia wale walevi walio wa funga kamba wakiwa wana koroma, kwa usingizi, ulio zidiwa na ulevi.
“Eddy nikuulize kitu?” aliuliza Monalisa ambae nikama amesha zowea mazingira haya ya vurugu, na misuko suko ya toka jana, “sijawai kukuzuwia kuniuliza” alisema Edgar, ambae sasa alikuwa ananawa mkono yake, kwenye maji yaliyokuwepo kwenye ile ndoo waliyo ogea, Monalisa alicheka kidogo, kicheko kilichoonyesh kuwa, swali lake lina mpa wakati mgumu kuuliza, “hivi ile chupi uliyo ninunulia, ulitaka nivae wakati tunafanya nini?” aliuliza Monalisa na kumfanya Edgar ajisikie kitu kama aibu flani hivi, akatazama chini huku anakung’uta mikono yake, aliyo toka kunawa, “nijibu basi Eddy” alisema Monalisa, huku anaegemea kwenye bega la Edgar, alisema Monalisa, kwa sauti ya kubembeleza, “we unazani nilitakaje?” hapo Monalisa akajitoa begani kwa Edgar, na kumpiga kikofi kidogo cha begani, “lionekwanza, mimi nakuuliza na wewe unaniuliza” alisema Monalisa kwa sauti ya kulalamika kwa kudeka, **
Kingarame alikuwa ndani ya chumba namba saba kwenye ghorofa ya tatu, ya serena Hotel, akiwa ni mmoja kati ya watu walio kosa usingizi usiku huu waleo, lakinin yeye alikuwa anachupa kubwa ya pombe kali “hapa ningekuwa na mtoto mkali, ingependeza sana” alisema Kingarame, huku akiendelea kubugia pombe yake, pia alitumia muda huo, kukumbuka jinsi alivyo panga mipango yake na askari wake, kuhusu kumshambulia Kisona na kumteketeza kabisa, mana mtu huyu ni kikwazo na hatari sana, kwenye mpango mzima wa kuwaangamiza wakina Edgar na Monalisa,.
Mpango ulikuwa hivi, kesho mapema gari moja kati ya yale mawili waliyo kuja nayo wakina Kingarame, liende Makambako, waka chunguze wakina Kisona wanatoka muda gani kuelekea porini, wakati huo, tayari askari saba watakuwa wamesha jipanga kwenye sehemu itakayo chaguliwa, kwa ambush, wakiwa na silaha kubwa zilizopo kule porini, yani medium machiner gun, kwa wale wasiyo ifahamu silaha hiyo, ni bunduki zile za minyololo, idai yake mbili pia waliandaa makombola ya RPG, ambazo zilikuwa mbili, na waili wa mwisho wangekuwa na SMG.
Akika kwa mapango uo asinge toka mtu, maana hizo silaha ni zamangamizi.***
Kingarame aliwaza hayo pasipo kujuwa kuwa Kisona mwenyewe alikuwa chumba namba tatu, kwenye safu ile ile ya tatu katika jengo ili lenye ghorofa tatu, nayeye akipanaga yakwake, maana alikuwa ame itandika ramani yake kitandani, anajaribu kutazama maeneo ya misitu ambayo yana semekana kuwa Edgar na Monalisa wamekimbilia itaendelea ………. hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!