SEASON 2: BINTI MDUNGUAJI (24)

SEHEMU YA ISHILINI NA NNE

ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA TATU: kutazama kama atamwona yule dada mwenye begi dogo jeusi, huku akitowa simu mfukoni kwake, baada ya kuangaika kwa dakika kadhaa alifanikiwa kumwona Jackline kwa mbali, akiwa anatokomea, kwenye chocholo za mitaa ya buguruni, kuelekea upande wa barabara ya ilala na kaliakoo, hapo mala moja Busungu alijaribu kupiga simu kwa Johnson, endelea…..
Simu iliita kwa mda mrefu kidogo ndipo ilipo pokelewa na Johnson mwenyewe, haraka sana PC Busungu akamwambia alicho kiona, huku akiwa na uakika kuwa ndie mwanamke anae shukiwa, kuhusika na mauwaji ya nayoendelea, hapo mala moja insp Johnson, ambaye alikuwa mbali kidogo slimwambia awaambie askari waliopo karibu wamfwatilie huyo dada wakati yeye anakuja hapo alipo, akiwa na polisi wake wengine, Busungu akafanya hivyo, akiwaomba askari watatu, kati ya askari polisi, ishilini wa kituo cha pale buguruni, waliokuja pale msibani, kuangalia usalama, mala moja wale askari wakaelekea kule aliko elekea Jackline wakiwa wamesha ambiwa jinsi alivyo vaa, dakika tano mbele Johnson na vijana wake wanne, maana wengine walikuwa wamejipanga upande mwingine, walisha mfikia pc Busungu, akaanza kuwapa repot ya kile alicho kiona na jinsi huyo dada alivyo, baada ya maelezo awakuchelewa, wakaanza kumfwailia huyo mwanamke huku insp akipiga simu kwa yule sajent wake, awakusanye vijana waliobaki, wachukuwe magari wapitie barabarani wakutane mbele, ** wale polisi watatu walio tangulia, wakiwa awana silaha zozote mikononi, zaidi ya virungu, waliweza kumwona kwa mbali Jackline akiingia kwenye jengo moja kubwa la gholofa tatu, Baraka shopers ni jengo ambalo utumiwa kwa shuguli mbali mbali za biashara, Busungu akuwa ame wahabarisha vyema juu ya dada yule, kwani ata yeye kwa jinsi alivyo muona akuamini kuwa ndie muuwaji wenyewe, kabda ni kibaraka wa muuwaji, Baraka shopers ni gholofa moja kati ya mengi yaliyopo eneo lile, kumbe Jackline alisha chunguza kuwa, jengo lile ndilo linalo onekana vizuri toka kwenye viwanja vya kanisa la Daraja la uokovu, alipokuwa ame simama mzee Masinde, na waomboleji wengine, Jackline baada ya kumtoroka yule kijana ambaye alimchukulia kama kijana mzinzi, pasipo kujuwa kuwa ni polisi mpelelezi, alielekea moja kwa moja kwenye jengo la Baraka shopers, alilo lichaguwa kwa kazi yake, akapanda juu kabisa ya jengo hilo, kwenye paa ya mwisho kabisa, top ruff, ambako alikuta kupo kimya kabisa, kukionyesha hakutumiki mara kwa mara, aka weka chini begi lake dogo jeusi, na kuilifungua, ile anaingiza mkono kwenye begi tu! akasikia, “tulia hapo hapo, usitikisike,” ilisika sauti ya kuamrisha toka nyuma yake, aliongea polisi moja kati ya wale watatu mwenye cheo cha koplo, hapo Jackline akajuwa kuwa amekwisha, kwani akujuwa hao walio mtolea amri hiyo walikuwa wana silaha gani, “mamaaaa” Jackline akajifanya kupiga kelele za uoga, akijifanya kustuka kwa uoga kama wafanyavyo wanawake wengi wanapo shtuliwa, kama vile ajuwi chochote, kinachoendelea labda amevamiwa na vibaka, japo Jackline alijuwa fika kuwa, ile amri ni ya polisi, lakini akazuga, “samahani kaka naomba usuniuwe, wechukuwa kila kitu” aliongea Jackline pasipo kutazama nyuma, polisi waka duwaa, wakimshangaa Jackline kwa mambo mawili, la kwanza ni kwamba, mtu walie mfwatilia ni mdada mrembo mwenye mwili wa kutamanisha, kiasi kwamba polisi wenyewe walitamani kuomba namba za simu, na pili dada mwenyewe ni muoga kiasi cha kuogopa vibaka, hapo taratibu polisi wale, waka jilegeza, na yule koplo akianza kumsogelea Jackline “unafanya nini huku we mwanae utabakwa huku, haya simama juu” alisema yule koplo, akizidi kumsogelea, Jackline, na ilo lilikuwa kosa kubwa sana, ** Wakiwa ofisini Denis na Mahadhi, Mahadhi alikuwa amekaa pembeni akisinzia, yeye Denis alitulia kwenye kiti chake, akionekana kuwaza jambo flani kichwani mwake, alikuwa akiunda maneno mazuri, na jinsi ya kuyatamka mbele ya Jackline, wakati akimwomba radhi, kwatukio la jana usiku, kuna wakati alijikuta anaongea peke yake kwa sauti, baada ya kuangaika muda mrefu sana Denis akapata wazo, ambalo aliliona litamsaid, akainuka haraka na kwenda moja kwa moja ofisini kwa Jeni, “niambie Jane, hupo freshi?” Jane aliacha kutazama tv ndogo ya ofisini, iliyokuwa ikionyesha, tukio la kuaga miili ya marehemu wachungaji, nakumtazama Denis “hoo poa, vipi wewe mzima?” alijibu Jane kwa uchangamfu, akiwa anaachia tabasamu la ukweli, maana sikuzote Janeth alionyesha kumtamani sana Denis, lakini tabasamu lile, alikumvutia kabisa Denis ila na yeye akazuga kutabasamu, lakini kitu hajabu, tabasamu ilo la uongo lilimvutia sana Jane, “freshi ujuwe nini Jane, kuna jamaa yangu amekosana na demu wake, sasa anaomba ushauri, akamwombaje msamaha,” aliongea Denis huku akijitaidi kuonyesha kuwa muhusika siyo yeye, Jane naye kama mwanamke ambae alisha wai kuwa na mpenzi na kukosana nane, akamwelekeza Denis vitu ambavyo wanawake wengi, wanapenda kufanyiwa iwapo wamekosewa na waume zao ili wawasamehe, hapo hapo Denis akionyesha kupata matumaini, akamwambia Jane kuwa atamuagia kwa boss kuwa amepatwa na zarula, kisha yeye akachomoka akimpita Mahadhi pale ofisini kwao, akimwacha bila kumstua pale alipo kuwa bado kasinzia, hapo moja kwa moja Denis akaelekea wanapo egesha magari, kwa mwendo wambio, akishuka ngazi haraka sana na huku nyingine akiziruka, mbio mbio, akaingia kwenye gari na kutambaa na mia kuelekea kaliakoo, akiwa na lengo la kwenda kutafuta vitu ambavyo vinge msaidia kuomba msamaha kwa mgeni wake, ambae amemwachisha kazi za mama ntilie, ** Jackline baada ya kuambiwa ainuke juu, hapo moja kwa moja akajuwa kuwa hii ndio nafasi ya pekee kwake kujinansa toka kwa polisi awa, ambao kutokana na vishindo vyao, alijuwa kuwa wapo zaidi ya mmoja, Jackline akahesabu atuwa za polisi aliekuwa anamsogelea, huku analikamata gauni lake kwa mkono wa kushoto, mkono wakulia ukiwa umekamata begi dogo jeusi, ni kitendo bila kuchelewa, aliinuka na lile begi dogo jeusi, na kulivulumisha kichwani kwa koplo wa polisi ambaye alipiga kelele za uchungu, huku akipepesuka na kwenda kujigonga ukutani, ambapo ailikosa nguvu ya kujiwai, na kuelekea chini kama mzigo, huku wenzao wakiwa wanashangaa ilo, walistuka wakikutana na mapigo mseto, ambayo awakuamini kama yanatoka kwa mwanamke huyo mrembo, kila walipo jaribu kujihami, lakini walikutana na vipigo vya kwenye video, waka huo huo, chini kidogo ya jengo ilo la gholofa tatu, Insp Johnson alikuwa anapandisha ngazi mbio mbio, akiongozana na vijana wake wa nne, wakiwa na silaha zao aina ya smg mikononi mwao, walikuwa wakipanda ngazi mbio mbio, macho juu juu, wakiangalia kwenye ngazi wanazo pandisha, wakiamini kuwa mtu wanae mtafuta yupo kule juu, ni kweli alikuwepo kule juu, maana ile wana ifikia ghlofa ya mwisho kabisa, walishuhudia polisi wa mwisho kati ya wale watatu aliebakia, akijitaidi kupigana ndiyo anaanguka chini kama kifurushi, akiwa amepoteza fahamu kamawenzake, huku mwanamke mmoja mzuri mtata, akiinama na kuokota begi dogo jeusi, wote wakainuwa silaha zao, nakummwelekezea, na kuanza kufunguwa kizuwia mapigo, (usalama) iliwawenze kukoki na kupiga, endapo mwanamke huyu asinge tii amri, “tulia hivyo hivyo” haaaa wapi! walisha chelewa, ndio kwanza kama walikuwa wanamstua, na kumjulsha uwepo wao, maana Insp Johnson, aliweza kushuhudia yule dada mzuri wa sura na mwili, anaefaha kuwa mchumba au mke wa mtu, akiwa hewani kama chui akija upande wao, na kabla hawaja weka risasi kwenye chemba zao, kwa wepesi wa hajabu yule mwanamke ambae mwili wake ulio umbwa vizuri, alikuwa amesha wafikia, na kutuwa kifuani kwa askari mmoja, akiutanguliza mguu wa kushoto, uliokita kifuani kwa yule askari, na kumpeleka chini, akitengana na silaha yake smg, pia akajigeuza juu kwa juu nakurusha mguu wakulia, ukatuwa kichwani kwa askari mwingine, huku yule mwingine akipatanafasi ya kuweka risasi chemba, tayari kumtandika mwanamke huyu, mrembo lakini hatari, wakati anaanagaika kumlenga, alistuka akigongwa kichwani na lile begi jeusi alilo beba yule mwanamke, alipatwa na maumivu makari sana, kwani begi lilikuwa na kitu kigumu sana ndani yake, misili ya chuma chapua, yule askari akajikuta akizidiwa na maumivu, yaliyo sababisha kizungu nzugu, kilicho mchanganya na kujikuta ameminya trigger (kifyatulio cha risasi) hapo sasa ndani ya sekunde tatu alisha maliza risasi selathini, toka kwenye kimkebe kimoja cha kwenye silaha yake, ambazo zilitoka mfululizo bila mwelekeo maalumu, na kusababisha tahaluki eneo lile, insp Johnson ambae alikuwa amebonyea chini, kupunguza uwezekano wa kupigwa na risasi zile, macho yake yaliweza kuona askari watatu, mmoja akiwa ni askari wake na wawili ni kati ya wale walio tangulia mwanzo, yani askari wa kituo cha buguruni, ambao mddawote walikuwa wamepoteza fahamu toka mwanzo, walionekana damu zikianza kuwachuluzika toka maeneo mbali mbali ya miili yao, ikionyesha wameingiwa na risasi toka kwenye siraha ya yule askari alie changanyikiwa, wakati insp Johnson naye amepigwa na bumbuwazi, akashangaa kumwona yule dada akitokomea kushuka ngazi akiwa na begi lake mkononi, insp Johnson paipo kuzubaa akaanza kumfwata mbio mbio kule chini, Jackline baada ya kushuka ngazi chache, Jackline akatazama chini kule anakoelekea, akaona polisi wengine watano wanapanda ngazi wakiwa na silaha mikononi mwao, Jackline akageuza na kurudi alikotoka, ile kutazama juu akamwona insp Johnson akiwa ame mwelekezea bastora, “tulia hapo hapo, auna ujanja wowote, Malaya mkubwa we” aliongea insp Johnson kwa sauti iliyo jaa hasira na ghazab, kitu cha hajabu yule dada, akamtazama Insp Johnson, nakuachia tabasamu lake lile la hajabu, ambalo uliachia kipindi akiwa na hasira, Jackline huku mkono mmoja kashika beg na mwingine kiunoni (kumbuka gauni lilikuwa limepanda na kuhachia paja lake lakulia lionekane na sehemu ndogo ya kipensi cha jinsi), usoni akionekana kama hakuwa na wasiwasi wowote, kiasi cha kumchanganya, Johnson nakumfanya aanze kutafakari, kuwa huyu dada anatakakufanya nini, huku akiutazama uso wake, ambao alishindwa kujuwa kama anatabasamu au mekasirika, wakati anamtazama usoni dada huyu, ndipo alipo gunduwa kuwa, ni yule alie mwona kwenye picha, zilizo okotwa, full dose pub, “husirudie tena kuniita jina kama hilo” Johnsoni aliisikia sauti nyololo na tamu ya kike, toka kwa mscha huyu ambae, leo amepata kumwona muuwaji wake, akati anajiandaa kujibu, ghafla alistukia akimwona yule dada mrembo akiwa hewani kama mcheza mpira wa kikapu, na kujipindua kwa ujuzi mkubwa sana, kuelekea chini, huku akichomoa bastora yake, toka kwenye kikaptula kifupi cha jinsi, ambacho alikuwa amevalia ndani ya gauni lake, sasa alimwona akiziruka ndazi kadhaa na kwenda kukamata mabomba ya chuma yaliyowekwa na kutumika kama kingo za ngazi, akipishana na askari polisi watano waliokuwa wakipanda juu mbio mbio, insp Johnson alinyoosha bastora yake ilimpige risasi Jackline, lakini akuwai, kwani aliweza kumwona, yule dada akiachia tena kingo za ngazi na kurukia ngazi nyingine huku akijigeuza na kumtazama Johnson alichokuwa anataka kufanya, hapo bastora ya yule dada ikaonyesha alama kama ya mwaga wa moto, kimya kimya pasipo kutoa mripuko, akiilenda bastora ya Johnson, ambae alitukia bastora yake ikipigwa na kitu kama shot ya umeme, na kurushwa pembeni, akamwona yule dada akituwa chini kama mcheza sarakasi kisha huyo, akatokomea kwenye gholofa ya chini kabisa, Ensp akatowa amri kwa wale askari wa tano, kuwa wageuke na kumfwata yule dada, huku yeye akipiga simu kituo kikuu kuja eneo lile kuwaangalia wale askari waliopigwa risasi kwa bahati mbaya na mwenzao, na wale waliozimia, Jackline alikuwa ameshafika kituo cha taxi na kuchukuwa taxi, mara moja na kuondoka kuelekea upande wa kaliakoo na ilala, polisi wakiwa pamoja na mkuu wao insp Johnson, walifika kwenye kituo cha taxi huku wakijaribu kuulizia kama amesha onekana mdada mwenye mwonekano wa Jackline, madereva wa taxi, walimtambua kwa arama ya begi dogo jeusi, wakaelezea kuwa amefika na kuchukuwa taxi, na kuelekea upande wa kaliakoo na ilala, hapo bila kuchelewa gari la polisi, sasa likiwa moja lingine lilikuwa lina wangojea wale waliopigwa na risasi, safari ikaanza kwa mwendo wa kasi sana, kama zima moto, likatimka kuelekea upande waliko elekezwa, kuwa Taxi alilopanda yule mwanamke limeelekea ** Denis baada ya kumtoroka Mahadhi, akaelekea moja kwa moja Kaliakoo kutafuta vitu alivyoelekezwa na Jane kwa ajili ya kuombea msamaha, mpaka dakika hii alikuwa amsha nunua baadhi ya vitu hivyo, kama mauwa na gauni zuri sana, akaingia kwenye duka moja kubwa sana la pipi na chocolate, akanunuwa pipi na chocolate moja kubwa iliyo tengenezwa kwa mtindo wa love, akaona huu ndiyo wakati wakurudi nyumbani mapema, kwenda kuyajenga, ** wakati huo kumbe Jackline alisha karibia maeneo ya shule ya uhuru, ambako palikuwa na foleni kubwa kidogo, ya magari yanayo subiriana pale round about, huku ya msimbazi, Jackline akiwa set ya nyuma ya gari hilo alilokodisha, alianza kuvisikia ving’ola vya gari la polisi vikisogea kwakasi sana sehemu walipo, alipo jaribu kugeuka na kutazama nyuma, akaona polisi nao wamekwama kwenye foleni, wakiwa nyuma ya agari machache toka gari lao lilipo, na sasa akawaona polisi wanashuka nakuanza kutembea kwamiguu, huku wakitazama magari yaliyo kuwa yame kwama kwenye foleni, hapo Jackline akajuwa moja kwamoja polisi wale wanamuusu, akamtazama dereva wa taxi, huku anapeleka mkono wake kwenye kitasa cha mlango wa gari hilo, bahati nzuri wakati huo magari ya mbeleyao yakaanza kutembea baada ya kuruhusiwa na taa ya kijani, ya barabarani, wakati magali yaliyo kuwa yame simama mbele ya gari la polisi yakianza kuondoka taratibu, ndipo Isnp Johnson alipo liona lile taxi, ambalo lime tokea buguruni, akimaanisha ndilo alilo panda Jackline, kutokana na rangi yake na namba za usajiri, na za ubavuni, hapo poisi waliokuwa wameshuka kwenye gari wakapewa amri ya kulikimbiza lile gari kwa miguu, lakini kabla awaja lisogelea waokaona gari zikiwa zimesha changanya nakuongeza mwendo, wao wakapanda kwenye gari lao ambalo lilikuwa linawafwata kwa kasi, huku insp Johnson akipiga simu kwa polisi wenzao wa mbele akitumia redio call, akiomba walizuwie gari, ambalo alilielezea lilivyo pamoja na mnambazake za gari na za ubavuni, tukio hilo liliwashangaza sana raia wa eneo lile, *** dereva wa taxi akiwa anaendesha gari lake huku akipiga mahesabu ya kuomba za simu namba kwa mteja wake huyu, maana alisha mtamani sana, kutokana na uzuri aliokuwa nao, asa ule msambwanda wake, yani alikuwa tayari kumsamehe kumdai nauli, lakini tu awe mpenzi wake, wakati akijiandaa kuongea neno, akashangaa ghafla, akisongwa songwa na gari la polisi, 110 defender huku polisi waliokuwepo ndani yake wakimwonyeshwa asimamishe gari lake pembeni, na yeye bila ubishi, akapaki pembeni mala moja, wale askari wa kwenye Defender wakaruka wakiwa na silaha zao na kulizunguka lile Taxi “zima gari haraka” ilisikia amri toka kwa insp Johnson, dereva akazima gari “wote shukeni nje, mikono ikiwa juu”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!