SEASON 2: KIAPO CHA MASIKINI (27)

SEHEMU YA 27

ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA SITA: “yeye aliambiwa na Sada, kwamba akifika ampokee, lakini yeye akajifanya mjanja, ndio kwanza akamkimbia mwenzie, na kujifanya mwenyeji, kilicho mkuta niaibu kwa kijiji kizima” alisimulia mama Sada, yani mke wa mzee Nyoni, huku huku mzee Nyoni mwenyewe akisakafia kwa juu, “yani leo hii ukifika mjini usije ukajitambulisha kuwa unatoka mwanamonga, utaonekana nawewe mshamba tu” watu wote waliokuwepo hapo kilabuni, saa nne hii ya asubuhi, waliangua kicheko.** Endelea…..
Naam gari aina Toyota V8, liliingia ndani ya lango kubwa la chuma lenye rangi ya dhahabu, na kwenda kusimama mbele ya jumba kubwa la ghorofa mbili, lenye viunga vya kupendeza vilivyo safishwa vikasafika, huku vikipambwa na mauwa aiya waridi, ya rangi mbali mbali, kisha wale watu watatu wakashuka toka kwenye gari, wakimwacha Peter, Michael, na Dereva, Peter ambae alizania kuwa bado safari inaendelea, na kwamba hapa wanapita tu, kuelekea huko wanakoitwa, lakini baada yake akamwona yule mscha anae onekana kuwa ndie kiongozi wake, akisogea usawa wa mlango wagari, usawa wa seat aliyokaa yeye, kisha akaufungua, na kwaheshima na tahadhima akainamisha kichwa chini, “Ewe kaka muungwana tunashukuru tumesha fika salama sasa mnaweza kushuka toka kwenye gari” alisema Jasmini, kwa sauti tulivu iliyojaa hesma na unyenyekevu, huku akiwa amesimama pale pembeni ya mlango, huku ameinamisha kichwa chake kwa heshima.
Hapo bila kusema lolote Peter akamshika mwanamke Michael mkono na kutoka nae nje ya gari, mlango wagari ukafungwa, baada ya hapo wakatokea wascha wawili, toka nyumba kubwa, nao waka inamisha vichwa vyao kwa heshima, “salaam muugwana” walisalimia ka sauti ya unyenyenyekevu kama alivyo fanya Jasmini, sasa Peter nikama alihisi anachotakiwa kufanya, “salama tu” aliitikia huku anainamisha kichwa kidogo, “karibu ndani” walisema wale waschana wawili ambao uzuri wao, ulimfanya Peter angae kidogo, na kujipa imani kuwa kati ya wale wanajamii, hapakuwa na mwanamke mbaya, japo walizidiana na awakumzidi boss wao, yani yule mwanamke wajana usiku, alie lala chumbani kwake, na kuondoka bila kuaga, wale waschana wawili, waliovalia nguo nyeupe kama sare, wakawaongoza Peter na Michael kuingia ndani ya jumba kubwa la kifahari, na ata walipoingia ndani, na kuvua viatu mlangoni, lakini badi Peter alihisi kuwa anachafua kila alipo kanyaga, huku ndani wakipokelewa na harufu nzuri ya chakula, arufu iliyoleta shida tumboni kwa Michael ambae kiukweli alikuwa na njaa kali, awakujuwa kule nje, kuwa Jasmin alikuwa anapiga simu kwa Careen kumweleza kuwa tayari wageni wamesha wasiri nyumbani.
Naam wawili awa waliongozwa mpaka ndani ambako walikutana na mama mmoja mtu mzima, ambae Michael alihisi kuwa ni mama wa yule mschana ambae alitajwa kuwa ni Careen, “shikamoo mama” alisalimia Peter, na Michael anae akatoa salam yake “shikamoo bibi” huku ananyosha mkono kushika kichwa na mama huyu mtu mzima, ambae alitabasamu kwa furaha, “marahaba wanangu” aliitikia yule mama, huku anainamisha kichwa chake kumwezesha Michael akiguse kwa kiganja chake cha mkono, “karibuni sana mimi enyi wa ungwana wa kitanzania, naitwa yaya Grory, nipo kwaajili yenu” alisema yule mama mtu mzima, ambae alionekana kupendezwa na wawili wale, asa kwa salamu waliyo itoa, “asante sana” aliitikia Peter, wakiwa wamesimama katikati ya sebule kubwa lenye vitu vya thamani kubwa, “nazani mnaitaji chakula kilichoandaliwa na Careen, naomba mnifwate” alisema Grory, kisha akaanza kuongoza kufwata ngazi, zakueleka ghorofa ya pili, huku kichwani mwake, akiwaza kuhusu ile salam.
Dokezo, ni kwamba yaya Grory anaifahamu hii salamu ya shikamoo kwa namna ya pekee kabisa, ikiwa ni salamu ya watu wenye hasiri ya bainiani, toka nchini India, kikawaida siyo salamu, ila ni kitu kinachofanyika wakati wa mtu anapokaribishwa sehemu, au anapoaga, kwamaana ageinamia miguu ya mtu mkubwa mwenye hesima kubwa katika familia ukoo au jamii, na kusema shikamoo, huku anashika mguu wa mtu yule, akiwa na maana ya kusema chini ya miguu yako, ni kitendo cha kuomba baraka, za mtu yule, ambae kama yupo tayari kutoa baraka zake, basi angesema marahaba, huku anakushika kichwa wewe ulie mshika miguu, nahapo baniani, uamini kuwa huko anakoenda mambo yake yatakuwa safi kabisa, sasa ka yaya Grory, nazani niile kuto kutembea tembea hapa songea, maana angeamkiwa mpaka angechoka na roho yake.
Naam safari yao iliendelea mpaka walipoibukia kwenye korido moja fupi lenye milango minne tu, nasebule moja kubwa upande wa kushoto, nao wakaunga na wanawake wengine wawili ambao, licha ya kuvaa magauni meupe na vikofia kama vya wahudumu wa mikate, lakini walionekana kupendeza na kushamilisha uzuri wao, nao wakainamisha vichwa vyao na kutoa salam, “salaam wageni wa madam Careen” safari hii Peter akushangaa kuitikia, “salam” aliitikia na kisha akaendelea kumfwata yule mama mtu mzima, yani yaya Grory, alie tembea kufwata korido, upande wa kulia, wa jengo lile kubwa la kisasa, huku wale wanawake wakiwafwata nyuma, mpaka mwisho wa safari yao ambayo iliishia kwenye mlango wa chumba cha tatu, hapo yaya Grory akatoa funguo za chumba kile na kufungua mlango, kisha akawaambia wakina Peter, “karibu sana wageni wetu, sasa mnaweza kuoga na kujiandaa kwa chai” alisema yaya Grory, alafu akawatazama wale wanawake, ambao kiukweli Peter akuweza kujaribu, kuwa linganisha na mschana yoyote kule kijijini kwao, ata mzazi wake Sada ambae anamwangaikia kila siku, “hakikisheni wageni wetu wanapata kila wanachoitaji” nao wakaitika kwa nidhamu kubwa sana, huku wakiinamisha vichwa yao kwa unyenyekevu, ukweli aya mambo yalimshangaza Peter, ambae alihisi pengine yupo ndotoni, au ni mpango wa Sada kumshangaza yani surprise, yani inawezekanaje alale usiku akiwa ameibiwa mamilioni, na kuamka akiwa ana karibishwa kwenye jengo moja kubwa kama ili, linalo onekana kumilikiwa na matajiri, ambao wanawaonyesha ukarimu mkubwa, hesima na nidhamu ya hali ya juu.
Peter na Michael wakakaribishwa ndani ya chumba hicho ambacho usingeweza kukifananisha na chumba walicho lala jana usiku, kilikuwa ni kizuri zaidi, kuliko kile ambacho kilifanya wadaiwe laki moja, “wageni wetu sisi tupo hapo nje, kama kuna lolote mnaweza kutuambia” alisema mmoja kati ya wale wanawake wawili, kisha wakataka kutoka mle chumbani, na wakati huo yaya Grory alikuwa amesha ondoka, hapo Peter akawawai wale wanawake kabla awajatoka, “samahani dada, mimi sijaomba humba chochote, nyie wenyewe mmenileta humu, siyo baadae nmaanza kunidai fedha” alisema Peter, kwa sauti ya kutahadharisha, kama isingekuwa nidhamu ya hasiri waliyonayo wale wanawake, basi wangecheka mbele ya peter, lakini baada yake wakainamisha vichwa kwa nidhamu, na huku mmoja akimjibu Peter, “usiwe na shaka mgeni wetu, madam Careen ni mkarimu sana” baada ya kusema hayo waliotoka nje na kufunga mlango kisha wakaangua vicheko vya chini chini.***
Naam nikama nilivyokudokeza kuwa Sada hakuwa na mpango wa kupanda boda boda, (pikipiki) basi achana na boda boda, ukweli nikwamba Sada hakuwa na mpango wa kwenda ata hospital wala dispensal, baada yake, alienda moja kwa moja kwenye duka la sawa, ambako alininia plast ya mia tano, na kubandika juu ya mdomo, akibakiwa na fedha ya kitanzania shilingi elfu kumi na tisa, na mia tano, ambayo aliingia nayo magengeni na kuanza kusanya vitu vya kwenda kujipikilisha, ikiwa ni mboga kidogo, nyanya, vitunguu na vitu kama hivyo, bila kusahau vitumbua kwa ajili ya chai, pia alinunua plast nyingine sikujuwa ni kwaajili gani, pamoja na pakiti moja ya sigara, sijuwi alikuwa anafanya hayo kwa maana gani, ila nilimwona anaelekea mahenge, kule kule alikotoka asubuhi.**
Yap! akiwa ofisini kwake mwanadada Careen, alionekana mwenye kujiamini kuliko kawaida, huku moyoni mwake akiwa mwenye furaha nusu, furaha ambae ingekamilika endapo kijana alie msaidia jana usiku, angekuwa karibu yake, ukweli akuwa katika husia za mapenzi, ila alimini angejiona salama kama angekuwa na kijana huyu, ambae jana licha ya kuwa alilewa sana, lakini pale alipomshika na kumwinua ili kumwingiza chumbani, alihisi msisimko mkalimwini mwake, “lakini nitawezaje kumbakiza nyumbani kwangu, au numwambie na mwajiri, kama mlinzi wa ngu binafsi?” aliwaza Careen au mama wa dhahabu kama wengi wanavyo mwita, na alikuja kukatizwa mawazao yake mala alipo sikia simu yake inaita, akaitazama na kuona kuwa mpigaji alikuwa ni Jasmin, msimamizi wa walinzi wake na usalama wa kampuni yao, Careen akaipokea haraka ile simu, “Ndiyo Jasmin” aliongea Careen kwa sauti tulivu na ya chini, “madam tayari wageni wapo nyumbani, lakini walipatwa na tatizo, la kuibiwa kila walicho kuwanacho na pia tulikuta wanadaiwa fedha ya chumba walicho kitumia jana usiku, lakini tulisha lipa fedha toka mfuko wa dharula” ilisikika sauti ya Jasmin, ambayo iliongea nidhamu na heshima, “ok! asante” aliongea Careen kwa sauti ile ile ya kama ataki maongezi mengi, kisha akakata simu, na kuinuka na kukusanya kila kinachomhusu na kuweka kwenye mkoba wake, kisha akatoka ofisini akimpitia msaidizi wake pale mlangoni, “natoka nitarudi baadae” alisema Careen pasipo kusimama, akaelekea kwenye kolido, na kuzifwata ngazi.
Sekunde chache baadae alikuwa amesha zifikia ngazi za kushukia chini, ambako Caareen alishuka kwa haraka, kama vile alikuwa na haraka sana, huku akiwa ana waza jambo flani kichwani mwake, ni kwamba, licha ya kitendo cha kijana yule mwokozi wake wa mala mbili, kuibiwa kila alicho kuwa nacho, yeye akupanga kumbebea chochote cha kumsaidia yeye na mwanae Michael, akuwaza kuhusu mama wa mtoto wake, yeye aifikilia kumshawishi kijana yule abakie nyumbani kwake.
Careen alikatiza eneo la chini la jengo lile kubwa, lenye safu ya maduka, yake mengi ambayo yalijaliwa na wateja wengi sana, ambao nusu yake waliacha kufanya manunuzi, wakimshangaa mwanamke huyu, ambae kiukweli hakuna aliewai kumzowea kwa uzuri wake na kumwona wa kawaida, ata yeye Careen alijuwa kuwa wateja uwa wanamshangaa sana, ndio maana uwa anakaa juu na kutazama maendelea kwa chini, ata sasa alijuwa wanamshangaa, hivyo alitembea kwa haraka kutoka nje, ambako aliingia kwenye gari na kuondoa gari kwa speed ambayo, lazima ungejuwa kuwa mwanadada huyu wa dhahabu, alikuwa anawai jambo muhimu.**
Janja baada ya kuona simu anazopiga kwa Emma azopokelewi, akapata wasi wasi kidogo, maana hali waliyo kuwa nayo jana usiku, zilizotokana na kipigo walichokipata toka kwa yule kijana, hazikuwa nzuri, ata yeye mwenyewe alikuwa bado anahisi maumivu baadhi ya sehemu za mili wake, hivyo akaamua kuwasha gari, na kuelekea mahenge nyumbani kwa Emma, ambako alimkuta Emma bado amejilaza kitandani, anaugulia maumivu, “kaka vipi, bado umelala” alisema Janja, mala bada ya kuingia ndani, akiwaacha wale wenzake wawili, nje ya nyumba hii ya kupanga, anayoishi bwana Emma, “dah! nilikuwa nimejiegesha tu, yani hapa nahisi njaa kali, maumivu ya mwili, dah! yani shida tu” alisema Emma kwa kulalamika, “unasikia njaa kivipi, kwani Queen bado ajarudi mpaka sasa?” aliuliza Janja, “alirudi, lakini amezingua hivyo nime mpa kipigo kibaya sana, mpaka ameondoka zake” alisema Emma, huku anajaribu kujiinua ka kukaa, aliweza lakini kwa tabu kidogo, “ila bro inabidi tufanye mpango uende hospital” alisema Janja, baada ya kuona kuwa hali ya mwenzie nimbaya kuliko yakwake, “sina vyanzo (fedha) ebu nipe report, vipi umefanikiwa?” aliuliza Emma ambae alikuwa amevimba mdmo na jelaha lake linaonekana wazi kabisa, “kaka tulicho kikuta MAKIMAKULUGA ni noma, yani kama tunge rudi usiku usiku ule ule, tulikuwa tuna mchomoa kilahisi, alafu tuna mfanyia kitu ambacho asingeweza kusahau” alisema Janja ambae alimsimulia Emma mambo yaliyo mtokea Peter, “inaonekana yule fala alijichanganya na Malaya pale hotelini, amemkomba kila kitu kisha akamwachia msala, sema wakaja jamaa wa #mbogo_land Sonara, wa yule malaya Careen, wakamlipia na kuondoka nae, ila polisi walisha timba yani tungeenda kumchomoa polisi, alafu tungempeleka mafichoni kumfinya” alisema Janja, na hapo Emma akamweleza, “hivi unajuwa kuwa huyo mjinga ni mzazi mwenzie na Queen?” taarifa hii ilimshangaza sana Janja, “dah! sasa boss akujuwa si atazania Queen anaweza kuwa kikwazo?” aliuliza Janja, “tena anaweza kutoa amri zake za ajabu, ila unajuwa nini, hi inakuwa siri yetu, hakuna kujuwa Queen wala boss” alisema Emma, huku akimwelezea Janja, kiasi ambacho Queen anafahamu juu ya wao kuvamia Peter jana usiku. …..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!