
SEASON 2: KIAPO CHA MASIKINI (28)

SEHEMU YA 28
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA SABA: alisema Janja, na hapo Emma akamweleza, “hivi unajuwa kuwa huyo mjinga ni mzazi mwenzie na Queen?” taarifa hii ilimshangaza sana Janja, “dah! sasa boss akujuwa si atazania Queen anaweza kuwa kikwazo?” aliuliza Janja, “tena anaweza kutoa amri zake za ajabu, ila unajuwa nini, hi inakuwa siri yetu, hakuna kujuwa Queen wala boss” alisema Emma, huku akimwelezea Janja, kiasi ambacho Queen anafahamu juu ya wao kuvamia Peter jana usiku. …..Endelea…
Naam wakati wanaendelea na maongezi yao, ndipo Sada au Queen aliingia akiwa na mazaga yake mkononi, hapo Emma akashukuru kimoyo moyo, kwakuona kuwa sasa pata pikika mle ndani, “hoooooo shemeji naona ulienda kukusanya mazaga” alisema Janja, ungesema kuwa akujuwa kilichomtokea shemeji yake huyo asubuhi hii, “ndiyo shemeji siunajuwa tena asubuhi hii” alisema Queen huku anaweka mezani vitu alivyokuja navy, na kuchukuwa palest, akasogea nayo alipo kuwa mpenzi wake Emma, huku akijiuliza kimoyo moyo, kama ata kubari kuwekewa ile plast au bado anahasira naye, lakini mpaka anamfikia tayari Emma alisha jiweka sawa kwaajili ya kutibiwa, na Queen akambandika plast juu ya mdomo wa Emma, “ila kiukweli bro, shem anakupenda sana” alisema Janja, alikuwa anafahamu kilichotokea, mapema ya leo, “ata mimi nampenda sana, ila wakati mwingine anazingua” alisema Emma, akijifanya kama vile bado amekasirika Sada, yani Queen, ambae aienda kuendelea na shuguri zake, za upishi, wa kifungua kinywa ambacho mpaka mida hii kilikuwa bado akijapita midomoni mwa watu awa, “ila bro licha ya kuweka hiyo plast, mimi nitatoa fedha uende hospital ujuwe hichi kidonda ni kikubwa sana” alisema Janja, ambae kiukweli niwazi alikuwa anamaanisha anacho kisema, “hivi janja unazani nitawaambiaje kituoni, yani kama boss angekuwa ajakasirika ningekuwa na uhakika wa kutibiwa bila pf 3, sasa unazani itakuwaje” alilalamika Emma, na hapo nikama Jania aielewa shida ya mwenzie, “poa basi, ngoja nimsubiri shemeji afanye yake akujari zaidi ya hapo alienda kufanya mfanya mipango ya kupika, alafu nongozana nae, akanunue dawa, maana hivyo hivyo na plast akitopona, gari lako nitakurudishia jioni” alishauri Janja na Emma akaunga mkono.**
Naam mida hii mzee Jacob na mke wake, ndio walikuwa wanaingia Namtumbo mjini, wakalipa pikipiki na kisha kusogea barabarani ambako awakukaa sana, walipata gari na safari ya kuelekea songea mjini ikaanza, huku njiani, wakijaribu kufikilia kuwa wataanzia wapi kumtafuta Peter, “ngoja kwanza tukachaji simu alafu tupige ile namba aliyotupigia asubuhi” alisema mzee Jacob, huku safari inaendelea, wakikatiza mtwango mtwara pachani, nakuzidi kuyoyoma kuelekea songea mjini.**
Naam Peter na mwanae Michael wakiwa wameoga tena kwa mala ya pili, wali vaa nguo zao zile zile walizokuja nazo, “baba nasikia njaa” alisema Michael, huku anashika tumbo lake, hapo ndipo Peter alipo kumbuka kijijini kwao Mwanamonga, isingefikia hatua ya mwanae kulalamika njaa, maana tayari angekuwa ameshaingia jikoni na kufunua sufulia, ambalo lingekuwa limejaa viazi vitamu, au mihogo, mchna pia ingekuwa hivyo hivyo, maana muda wote sufuria lilikuwa limejaa wali wa mtama au kande za maindi mabichi na maharage mabichi, hivyo muda wowote angeweza kufunua na kuchukuwa chakula, ukweli licha ya kuwa ndani ya chumba ambaho akuwai kuota kuwa angewai kuingia ata kwa bahati ambaya, “Michael ata mimi nina njaa sana, lakini …. sasaaaa….” wakati Peter anawaza kitu cha kumdanganya mwanae, mala mlango ukagongwa, na Peter ndie alie wai kwenda kufungua mlango.
Akaonekana mmoja wa wale wamawake wazuri machoni pa Peter, waliosema kuwa, watakuwa nje ya chumba kusubiri kuwahudumia, ambae aliinamisha kichwa kwa unyenyekevu, na kusema, “wageni karibu ni kwa chakula Madam Careen anawasubiri” kusikia hivyo wote wawili yani Peter na mwanae Michael walitabasamu kwa furaha, huku Michael akiongoza kutoka nje ya chumba kile kikubwa cha kupendeza, na alipofika kolidoni akakutana na yule mwanamke mwingine alie kuwa anawasubiri nje, nawakaungana wote wanne safari ya kuelekea kwenye ukumbi wa chakula ambao hupo kule kule kwenye ghorofa ya pili, mala zote ukumbi huu utumika pale tu Careena anapo pata wageni toka maalumu, kutoka kwao #mbogo_land.
Sekunde chache baadae wakaibuka ndani ya ukumbi mdogo, wenye vitu vichache lakini vya thamani kubwa, pamoja nameza kubwa yenye viti sita iliyobeba vyombo mbali mbali viliyo beba vyakula vya aina mbali mbali, kilicho mvutia Michael ni TV kubwa iliyokuwepo hapo ukumbini, wakati Peter akitoa macho kumtazama Careen ambae alipowaona wakiingia tu alisimama, ikiwa ni ishara ya kuwakaribisha, “karibu wageni wangu” alisema Careen kwa sauti ya upole na tulivu, huku tabasamu afifu likionekana usoni mwake, huku anainamisha kichwa chake, “asante sana dada yangu, kumbe muda wote huu ulikuwepo humu ndani” alisema Peter huku anamsadia mwanae Michael kukaa kwenye kiti na yeye akakaa kwenye kiti cha jilani na Michael, “nilikuwa kazini, lakini nime rudi mala moja kwaajili yenu” alisema Careen, kwa sauti ile ile tulivu, na tabasamu lile lile afifu, lakini lilikuwa ni tabasamu kubwa sana kwa wafanyakazi wanne ambao walikuwepo pale ukumbini wakisubiri kuhudumia, “pole sana, kwa usumbufu, ni bora kama ungetuambia sisi tuje huko, kazini kwako, kulikowewe kusumbuka hivyo” alisema Peter, huku anajitaidi kumzuwia Michael asipeleke mkono kwenye vyombo vilivyosheheni vyakula, “hooo! usijari, ni bwana nani vileeee” aliuliza Careen, ambae aliona jinsi Peter anavyo angaika kumzuwia mtoto huyu, kujisevia chakula, na kumfanya acheke kidogo, lakini ni kicheko afifu sana, “peter naitwa Peter Jacob, na huyu ni Michael” alisema Peter na hapo akiwa mwenye uso wa uchangamfu, huku wafanyakazi wakimtazama Careen kwa mshangao, kwajinsi alivyoonekana kuwa na furaha, na uchangamfu muda “ok! karibuni sana, Peter na Michael, pia poleni kwa tatizo lililowakuta” alisema Careen, huku anawatazama wale wafanyakazi wake wanne, na kuwapa ishala ya kwamba wafanye jukumu lao, nao wakaanza kuangaika haraka haraka, kuandaa vyakula, kwenye sahani, “asante sana, dada yangu” alisema Peter, na hapo Careen akadakia “niite Careen” alisema dada wadhahabu, kwa sauti tulivu na tamu sana.
Wale waschana waliandaa vyakula na walipo maliza waliwakaribisha kwa sauti zao zilizo jaa nidhamu, “sawa mnaweza kwenda kila kitu nita shughurikia” alisema Careen kwa sauti yake ya upole, na wala ewaschana wakaondoka zao, wakiwaacha watatu awa, “karibuni chakula wageni wangu” alisema Careen kwa sauti ya upole, huku akitabasamu kidogo, “asante sana dada Careen” alisema Peter na Michael nae akuwa mbali, “asante shangazi” ilikuwa sauti ya kitoto iliyo changamka, na kumfanya “lakini dada Careen hivi tuwezi kupata vyombo ya bati au plastic maana sizani kama tuna weza kulipa endapo Michael atavunj…” alisema Peter kwa sauti ambayo ilionyesha wazi kuto kumwamini, mwanae Michael, lakini Careen alimkatiza kwa kicheko, “hooo! bwana Peter wala usiwe na wasi wasi, hapa ni kwake, mwache atumie vyombo ambavyo ata kuwa akivitumia kuanzia leo” . …..

