
SEHEMU YA 29
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA NANE: alisema Careen kwa sauti ya upole, huku akitabasamu kidogo, “asante sana dada Careen” alisema Peter na Michael nae akuwa mbali, “asante shangazi” ilikuwa sauti ya kitoto iliyo changamka, na kumfanya “lakini dada Careen hivi tuwezi kupata vyombo ya bati au plastic maana sizani kama tuna weza kulipa endapo Michael atavunj…” alisema Peter kwa sauti ambayo ilionyesha wazi kuto kumwamini, mwanae Michael, lakini Careen alimkatiza kwa kicheko, “hooo! bwana Peter wala usiwe na wasi wasi, hapa ni kwake, mwache atumie vyombo ambavyo ata kuwa akivitumia kuanzia leo” . …..Endelea…
Alisema Careen japo alikuwa bado anaendelea kucheka, lakini ni kicheko flani chepesi na tulivu, huku anamtazama Peter, kijana ambae mpaka sasa akuamini kama yupo nyumbani kwake, “sikudanganyi dada Careen huyu ajawai kutumia sahani za hivi, bora mimi nilitumia nilipokija umisenta” alisema Peter, huku anamtazama Careen, na macho yao yakakutana, wakati huo Careen alikuwa ametabasamu, kwa maneno ya Peter, kwamba bora yeye alisha wai kutumia sahani za hivyo.
Naam hapo ndipo Peter alipopata nafasi ya kumtazama dada huyu kwa ukaribu na kuweza kumwona vyema kabisa, na kuubaini uzuri uliopitiliza wa mwanamke huyo, alie kuwepo mbele yake, kiasi cha kujikuta akiduwaa kabisa, na kuutafakari uzuri wa mwanamke huyu kimoyo moyo, huyu dada ni mzuri jamani, nikweli na yeye ni mwanamke kama wakina Sada?” alijiuliza Peter, huku akiendelea kumtazama Careen ambae nikama aliona jinsi alivyo shangaliwa, maana taratibu aligeuza usowake na kumtazama Peter huku anatabasamu, na kufanya vile vijisima vyake vya mashavuni kuonekana vyema, “Peter tunaweza kuanza kula sasa” alisema Careen huku tabasamu likiwa bado limeshamili, usoni kwake, lakini moyoni alikuwa anajisemea, “ananishangaa, itakuwa nimependeza machoni mwake” hapo wote kwa pamoja wakaanza kula vyakula vile ambavyo asilimia sabini na tano, vilikuwa vipya machoni mwa Peter na mwanae Michael, huku Peter mwenyewe akiwaza namna ya kuomba nauri ya kufika mwanammonga na pasipo kukumbuka kuwa alisha mpigia simu baba yake kumweleza shida yake iliyomkuta kule hotelini.**
Naam saa tano ikiwa inaelekea saa sita kasoro, mwana dada Queen yani Sada, kama anavyoitwa kule mwanammonga na Janja, yani kijana Hussein, walikuwa ndani ya gari, wakielekea mjini kwenye moja ya duka kubwa la madawa, ambalo waliitaji kununua dawa kwaajili ya kidonda cha bwana Emma ambae alikuwa anaitwa pengo, wakati anapengo moja sijuwi sasa ataitwaje, “unazani duka la Faraja linaweza kuwa na dawea tunazo itaji?” aliuliza Janja, wakiwa wana karibia njia panda ya mkuu wa mkoa, wenyeji wa mkoa wa Ruvuma sehemu hii wanaiita junction, “mimi nazani duka ra faraja pale stendi ya Tunduru” alisema Sada, yani Queen, shemeji yake Hussein, “kweli bwana yani sijuwi nilisahau vipi” aliusema Janja, aliekuwa anaendesha gari, akinyoosha kuifwata barabaa ya viwandani, ya Sido, alafu ambako mita mia tano toka hapo kuna hiyo stendi ya magari toka wilaya ya tunduru, na vijiji vya jilani, huku wakiongozana na bus moja dogo aina ya Toyota coster, lililokuwa linatokea wilaya ya tunduru, kupitia walaya ya Namtumbo.***
Yap! bwana Pitus Kalonga akiwa wenye hasira kali sana, alionekana ametulia ndani ya gari lake alilokuwa anaendesha mwenyewe, anapandisha kipando cha Mateka, kueleka mjini, na alipoingia kwenye round about ya songea girls aka fwata uelekeo wa kulia, yani barabara ya shule ya majimaji, “niupuuzi huu, wanashindwaje kumkabiri mtu mmoja, na huyo mtu ni nani?” aliwaza Pitus Kalonga, huku anakanyaga mafuta, kuelekea upande huo ambapo alipita mtaa angoni arms ambapo kuna nyumba ya Careen, au mama wa dhahabu, ambapo kila alipo paona roho ilimuuma sana, “inawezekana ameleta mlinzi wa siri toka nchini kwao?” alijiuliza Kalonga, ambae alipungaza mwendo kuingia barabara kuu iendayo mikoa ya kusini, ya Lindi na Mtwara, kupitia Tunduru na Masasi, “kama mtu huyo ni mtanzania ata kuwa analiwa au anajipendekeza tu?” alijiuliza swali la tatu pasipo ajibu, zaidi ya kuzaliwa maswali mengine, “kama anajipendekeza kwanini nisi mlipe huyo mpuuzi na yeye ndie akaja kunifanyia kazi ninayo itaji, maana naona huyu Emma sasa amechoka sana” safari alijiuliza hivyo huku anapunguza mwendo na kukatakona kushoto, akiwa anaingia barabara ya mashujaa ya makumbusho ya maji maji, iliyopo mtaa wa Mahenge, “wacha kwanza nika kutane na huyu pengo kisha tutajuwa la kufanya” alijisemea Kalonga huku ana endelea kukanyaga mafuta, kulekea mtaa huo anao patikana kijana Emanuel Msengi.***
Naam tayari walikuwa wamesha maliza kupata chakula ambacho kwa muda ule tungeita kuwa ni chai, lakini kwa mwonekano wa chakula kile, mimi mwenyewe ningesema kuwa ni chakula cha mchana ambacho kingefaa kiliwe katika afla au sherehe kubwa sana, iliyoandaliwa na mtu tajiri sana, “asante sana kwa chakula dada Careen” alisema Peter ambae, huku akimtazama Careen, ambae muda wote wa chakula, Peter alikuwa ana mtazama kwa macho ya wizi mwanadada huyu, na kustaajabia uzuri wake, ungesema ndio kwanza anamwona, kuanzia kule kwenye ukumbi wa chakula mpaka kwenye sebule ya kikao, (seat room) ambako sasa walikuwa wameamia, “Peter upaswi kunishukuru, ni hakiyako kupata chochote kwangu” alijibu Careen kwa sauti tulivu, nzuri na tamu, huku tabasamu laini liki tawala usoni mwake, kiasi cha kuwashangaza ata wafanyakazi wawli wakike, ambao walikuwa wamesimama pembeni yao, kuwahudumia vitu mbali mbali, kama vile juice ya matunda ambayo ilikuwa mezani, wanakunywa wakiendelea kunywa, kitu ambacho Peter hakukijuwa ni kwamba, Careen aliona jinsi alivyokuwa anamtazama kwa macho flani yaliyoshindwa kuongea ukweli wa kile anacho kiona, “siwezi kuacha kukushukuru dada Careen, ina kikubwa nilicho kufanyia, ambaho kina nistahili kutendewa haya yote” alisema Peter, kwa sauti ya unyenyekevu, wakati huo Michael alikuwa anatazama vikaragosi (cartoon) kwenye television, “hooo! Peter acha hizo bwana, umenifanyia makubwa sana” alisema Careen huku akiachia tabasamu laini, na kitu ambacho unatakiwa kujuwa, tabasamu la Careen lilikuwa ni laini, kwa maana ya kwamba alikuwa anachezesha mdomo kidogo sana, huku macho na yake yakionyesha na furaha, na mashavu yake yakionyeha vijisima (dimples) ambayo vilimfanya azidi kupendeza mala dufu, na kumchanganya kijana wawatu, ambae siyo kwamba alidondokea kwenye tamaa ya mapenzi, hapana, yeye asinge weza kuwaza juu ya penzi wala ngono na mschana huyu, ambae achilia utajiri alionao, ila fikilia uzuri wake, ukweli ni kwamba yeye alikuwa anashangaa vitu ambavyo wakubwa wanafaidi.
Upande wa Careen, ambae akujuwa Peter anamchukulia kama mschana ambae, kwa yeye ni ndoto ya mchana tena, leo hii alikuwa anajisikia furaha sana moyoni mwake, ata yeye mwenyewe ukimwuliza chanzo cha furaha hiyo sizani kama angekueleza kiufasaha, ila kwakifupi alitamani kukaa pamoja na wageni wake muda wote, “bwana Peter, nazani tutaongea kwa kirefu jioni, wacha sasa niende kwanza ofisini” alisema Careen kama vile anajilazimisha kuongea, “nisawa dada Careen, lakini samahani, ninaomba unisaidie jambo moja” aliema Peter kwa sauti tulivu iliyo jaa nidhani, kiasi cha kumtia unyonge Careen, “mh! kwanini useme hivyo Peter, wala usiwe na wasi wasi, we nieleze chochote unacho itaji” aisema Careen huku anajaribu kutabasamu, “nilikuwa naomba uniazime shilingi elfu mbili na mia tano, ilinifike Namtumbo, toka pale nitatembea kwa miguu mpaka kijijini kwetu” alisema Peter, hapo akizungumzia kilomita tisa, toka Namtumbo mpaka Mwanamonga. …..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU