
SEHEMU YA 30
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA TISA : wacha sasa niende kwanza ofisini” alisema Careen kama vile anajilazimisha kuongea, “nisawa dada Careen, lakini samahani, ninaomba unisaidie jambo moja” aliema Peter kwa sauti tulivu iliyo jaa nidhani, kiasi cha kumtia unyonge Careen, “mh! kwanini useme hivyo Peter, wala usiwe na wasi wasi, we nieleze chochote unacho itaji” aisema Careen huku anajaribu kutabasamu, “nilikuwa naomba uniazime shilingi elfu mbili na mia tano, ilinifike Namtumbo, toka pale nitatembea kwa miguu mpaka kijijini kwetu” alisema Peter, hapo akizungumzia kilomita tisa, toka Namtumbo mpaka Mwanamonga. …..Endelea…
Hapo Careen aliinamisha kichwa chini, kama vile anatafakari jambo, ila aikuwa hivyo ukweli nikwamba mwadada huyu alikuwa anaficha usowake, ambao, ulikuwa umesawajika kwa simanzi ya ghafla, kwa kusikia ombi la Peter, ambae pia aliliona jambo ilo, “dada careen naomba uniamini, nita kurudishia mala tu nikifika kijijini nita kutumia kwenye simu” alisisitiza Peter, kwa kuhisi kuwa Careen akuwa tayari kutoa fedha kwa mtu asie mfahamu, japo kiasi hicho cha fedha, kilikuwa kidogo sana kwa dada huyu, ukilinganisha na fedha alizo nazo, tena anaweza kutoa millioni moja, na asihisi kama ametoa fedha yoyote, lakini kwanini awaze juu ya elfu mbili mia tano.
Careen akainua usowake, huku akijaribu kutabasamu, “Peter ebu achana na hizo habari za kurudisha, labda nieleze kilichotokea mpaka ukapatwa na matatizo hayo yaliyokukuta wewe na mwanao Michael” alisema Careen ambae kiukweli kabisa kutoka moyoni mwake, akutamani kabisa kuacha Peter na mwanae Michael waondoke, “sijuwi nianzia wapi dada Careen, maana imekuwa kama movie zile za kina Tasha” alisema Peter akimtaja msanii mmoja wafilamu toka mkoa wa pwani, kisha akanza kumsimulia Careen, kuanzia maisha yake toka mwanzo akiwa na mke wake Sada, akubakiza kitu ata kimoja, mpaka leo hii aliponusurika kwenda kulala mahabusu ya polisi, kwakushindwa kulipia hotel ya ghari aliyo pelekwa na mke wahuyo, alie mtapeli.***
Naam bus dogo aina ya Toyota coster tayari lilikuwa limesha simama ndani ya stendi ndogo ya magari endayo mikoa ya kusini, maarufu kama stendi ya tunduru, abiria walikuwa ndio wanamalizikia kushuka, asa wale waliokaa seat za nyuma kabisa, kiwepo mzee Jacob na mke wake, yani mama Peter au bibi Michael kama walivyozwea kumwita watoto na majilani zao kule kijijini, “sasa tunaanzia wapi kumsaka?” aliuliza mama Peter, na hapo baba Peter akutumia nguvu nyingi kupata jibu la swali alilo ulizwa na mke wake, ebu tutafute sehemu tuchaji simu kidogo, alafu tumpigie kwenye namba yake, tukimkosa tuta mpigia kwenye simu ile aliyoitumia asubuhi” alisema mzee Jacob, huku akitazama kushoto na kulia, kutafuta sehemu ambayo inamwonekano wa kupata msaada alio uitaji, akisaidiwa na mke wake, amba endie alikuwa wakwanza kuliona duka la dawa ambalo, wange weza kuomba msaada wakuchaji simu yao, ili waweze kumtafuta Peter, “twende kwenye duka lile la dawa, nazani tuna weza kuchaji” alisema mama Peter, huku anaonyesha dula lile la dawa lenye maandishi makubwa, FARAJA DUKA LA DAWA, hapo awakujadiri wazo lile wote wakaanza kutembea kuelekea kwenye dula ilo la dawa, huku nyuso zao zikiwa katika hali flani ya unyonge, “sijuwi wamepatwa na nini awa watoto jamani” alisema mama Peter kwa sauti iliyo nyongea, “lakini mimi naona tuondoe mawazo mabaya, lazima watakuwa salama tu” alisema mzee Jacob, wakato huo wana zidi kulisogelea duka ilo la dawa, “yani mimi kutulia ni mpaka niwaone” alisema mama Peter, kwa sauti ile ile ya kinyonge.
Naam sasa walikuwa wamesha lifikia duka la dawa, ambalo mbele yake kulikuwa na gari dogo aina ya Toyota IST lilikuwa limesimama, huku dereva wa gari il akiwa kwenye seat yake anavuta sigara, iliyo tawanya moshi ndani ya gari lile kama jiko la kuni mbichi, za mti wa muembe, “inachefua sana yani jitu inapuliza mioshi kama linafukiza udi wa kutolea Mashetani, alisema mama Peter, huku anaongoza kupanda ngazi mbili za kuingilia kwenye duka la dawa, ambalo ndani yake kulikuwa na wateja wawili ambao ni wanamwake mmoja ni mama mtu mzima, na sana, kuliko ata mama Peter, na mmoja ambae icha ya kujitanda nguo mpaka kichwani lakini bado ungeza kuhisi kuwa ni mwenye umri wakati, yani miaka therasini na tisa au alobaini, na kitu, “alafu unadawa yoyote ya kupunguza maumivu” ilikuwa ni sauti ya kutetemeka ya yule mama mtu mzima, ambae mpaka hapo angeweza kuwa na wajukuu watoto wanao karibia kupata wajukuu, “mhhhh! kwa dawa nilizokupa nivyema kama ungetumiaaa…..” alisema muuza duka lile ambae ni mwanamke mdogo, wa kati ya umri wa miaka ishilini na ishilini na mbili, huku anageuka kutazama kwenye shelfu zilizopangwa dawa mbali mbali, lakini jambo ilo lilionekana kuto kumpendeza yule mwanamke alie jifunika nguo mpaka kichwani, “we dada ebu tuhudumie na sisi wengine kwanza, alafu ndio uendelee na huyu bibi” alisema yule mwanamke kwa sauti iliyo jaa chuki na dharau.
Hapo yule bibi akamtazama yule mwanamke, ambae akuonyesha kujari, “huyu bibi amemwacha mjukuu wake nyumbani anaumwa, namaliza sasa hivi kumhudumia, alafu nakuhudumia” alisema yule mschana muuza duka, huku anachukuwa dawa aliyo iitaji, “mjukuu kitu gani bwana, kwani mama wa mtoto yupo wapi, si angekuja mwenyewe” alisema yule mwanamke kwa nyodo, “mama yake ameenda kazini, yeye ndie anae tuhudumia nyumbani, awezi kuacha kwenda kazini” alisema yule bibi kwa sauti ambayo kama ungeisikia wakati huo, kwa jinsi sauti ile iliyo kuwa ya kinyonge, hakika machozi yangekunyemelea, machoni mwako, lakini hii aikusaidia kumtuliza huyu mwanamke mkorofi ambae aliwashangaza ata wakina baba Peter, ambao walishangaa insi maisha ya watu wamjini, yakuto kuheshimu wakubwa, kitu ambacho kiliwafanya wawe watulivu kidogo, wasubiri wawili awa wahudumiwe ndipo na wao waongee shida zao, mbele ya dada muhuza dawa, “bwanaee! ayanihusu ayo, kwanini yeye aangaike kwani baba wa mtoto yupo wapi?” alisema yule mwanamke wambae anamiliki sauti yenye mikwalizo, iliyo hasiliwa kwa pombe, “mwanangu, mwenzio alipotenza mume kwenye hajari kiwandani, hivyo analazimika kupigania maisha yake mwenyewe” alisema yule bibi, ambae aliwatia simanzi watu wote waliokuwepo pale dukani, yani muuza duka na wazazi wa Peter, “ndio tatizo la kuzaa mapema ilo” alisema yule mwanamke ambae sasa alikuwa ameshika elfu tano mkononi.
Ukweli iliumiza na kuchukiza sana, mbele ya mzee Jacob, na mke wake, lakini hawakuwa na lakufanya, zaidi walitulia wakitazama jinsi mambo yalivyoenda, na sasa yule dada muuza dawa alikuwa anamptia dawa yule bibi, “hii utampatia nusu kidonge, asubuhi mchana na jioni, kila baada ya masaa nane, kwa dawa hizi nilizokupa, mtoto atapona muda siyo mrefu, ila hakikisha anakula vizuri, na pia anywe maji kwa wingi” alielekeza yule muuza dula la dawa, ambae nikama akumjari yule mwanamke mkosa adabu, “asante mwanangu, mungu akubariki” alisema yule bibi, kwa sauti yake ile ile ya unyenyekevu na unyonge, kisha akaanza kuondoka, kutoka mle ndani akiwapita mama na baba Peter, ambao walikuwa wamesimama nje ya duka karibu na mlango, nao wakamsalimia, nae akaitikia huku anaondoka zake, “nipatie dawa za vidonda, na plaster zile za kubandika” alisikia yule mwanamke, mkosa adabu, ambae sasa alikuwa anampatia muuza duka ile elfu tano, mgonjwa ni nani?” aliuliza muuza duka, huku anageuka kutazama dawa, “sidhani kama inakuusu, we nipe vitu nilivyo kuagiza” alisema yule mwanamke, huku wakina zee Jacob, wakimtazama toka nyuma, na kusikiliza mangezi yao, “lakini nivyema nikijuwa kama mgonjwa ni mtu mzima au mtoto, ilinikupe maelekezo” alisema yule mwanamke muuza duka, ambae aionekana kuwa mwenye busara sana, “ni mume wangu” aijibu kwa mkato, yule mwanamke mkorofi, na hapo ndipo wakina mzee Jacob walipo gundua kuwa huyu mwanamke mkorofi ameolewa.
Muuza duka akutumia muda mrefu sana kumhudumia yule mwanamke, akimalizia kwa kumpatia chenji yake, kisha yule mwanamke aliipokea na kugeuka kwaajili ya kutoka nje, na hapo ndipo macho ya baba na mama Peter walipo shangazwa na macho yao, huku mwana mke yule akishtuka vibaya sana, kwsa kuwaona wazee awa wawili, “mama Michael, unamzungumzia mume gani unae mnunulia dawa za vidonda, inamaana Peter ameumia?” aliuliza mzee Jacob kwa mshangao, na wakati Sada anaendelea kushangaa, mama Peter nae akadakia, “vipi kuhusu Michael nae yupoje, mbona na wewe umeumia hivyo, au mlivamiwa na wezi?” mama Peter alionekana kuwa mwenye wasiwasi, mwingi na uchungu, kwa kile alicho kiona usoni kwa Sada.
Hapo Sada akaona anaweza kuumbuka, na akizingatia ametoka kufanya jambo baya kwa mtoto wa wazee awa wawili, hivyo akatazama kwenye gari lililokuwa limeegeshwa hatua chache toka dukani, akamwona Janja anaendelea kuvuta sigara yake, hakuwa na mpango wa kutazama kule dukani, Sada akapeleka mkono usoni, na kufanya kama anajifuta machozi, “yani mama sijuwi nikuambieje, Peter amenipiga sana jana usiku, sijuwi nini kime mbadirisha jamani” alisema Sada huku anajaribu kujiliza kilio cha chini chini, uso akiwa ameuinamisha chini, hapo mama na baba Peter wakatazama usoni, kwa macho ya mashangao, “jamani Peter amefanya nini tena huyu mtoto” aliuliza mama Peter, kwa sauti ya masikitiko na mshangao.
Hapo ndipo Sada alipotabasamulia tumboni, “yani mama uwezi amini, jana alinipigia simu, niende kumwafwata kwenye bar moja hivi mjini, nilipofika pale nikamkuta yupo na wanawake wengi wanao jiuza anakunywa nao pombe, nikamweleza kuwa wale wanawake siyo wazuri aachane nao, lakinia akaniambia kuwa nisimwingilie kwenye mambo yake kama nifedha yeye ndie alie zitafuta, nikamwambia basi nimchukuwe Michael nimpeleke nyumbani, hapo ndio yeye na wanawake zake, wakaanza kunipiga” alipofika hapo ajaanza kulia tena, huku akiinamisha kichwa chini, ili kuwazuwia wakina mzee Jacob wasione na kugundua kuwa kilio chake kilikuwa cha uongo, “yani mama walinipga sana, ndio maana umeona nimekuja kununua dawa, wameniumiza sana, wamenipotezea fedha na simu” alisema Sada kwa sauti yenye majonzi makubwa, kiasi cha kuziteka nyoyo za wakina mzee Jacob, ambao walitazamana kwa macho yaliyo jawa na simanzi na viulizo, jamani Peter, sijuwi kime mkuta nini, mpaka anafanya mambo ya ajabu kama hayo?” aliuliza mama Peter au bibi Michael, kwa sauti ile ile ya uzuni, “ata mimi nimeshangaa sana mama, yani alikuwa anafanya mambo machafu, alafu akaenda kulala nao kwenye hotel kubwa ya ela nyingi, na wanawake wawili, ambao wamemwibia ela zote, akaja kwangu nimempa nauri, nazani mme pishana nae, alikuwa anarudi kijijini” aliitimisha Sada kwa sauti yenye masikitiko makubwa, “bora wamemkomesha, cha msingi amerudi nyumbani” alisema mzee Jacob, kwa sauti iliyojaa hasira, “yani huyu mjinga anashindwa kujitambua na umri wote huu, bado anafanya mambo ya kitoto” aliongezea mama Peter, kwa sauti kama ya mume wake, yani iliyo tawaliwa na hasira, “yani tumejisumbua bule kabisa, bora elfu kumi tunayotumia kwa nauri, tunge nywea bia tu” alisema mzee Jacob, huku anaweka begi lake dogo chini na kufungua zip ya pembeni kisha akatoa burungutu la noti za elfu kumi kumi, zilizofungwa pamoja kwa rubber band, alafu akachomoa noti kadhaa na kuhesabu, noti tano za elfu kumi kumi, Sada alitoa macho ya uchu, akitamani alikwapu lile begi na kukimbilia kwenye gari, “pole sana mama, hii hapa utanunua dawa” alisema mzee Jacob, huku anampatia Sada zile noti tano za elfu kumi kumi, hakujuwa kuwa mwenzie ana panga la kwake kichwani, “asante sana baba, karibuni jamani, kuna gari la rafiki yangu, kama mna itaji liwatembeze kidogo, kuwapeleka sokoni na madukani kabla amja rudi kijijini” alisema Sada kwa sauti iliyojaa upole na unyenyekevu, kichwani mwake akiomba wazee awa wakubari kuambatana nae, ili akawaingize choo cha ward ya vichaa. . …..itaendelea…
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU