
SEHEMU YA 31
ILIPOISHIA SEHEMU YA THERATINI
Naam hapo mzee Jacob alie kuwa anarudisha fedha kwenye begi, na kufunga zip, akamtazama mke wake, alie kuwa amesima anamtazama yeye, nikama walikuwa wanaulizana, juu ya kukubari mpango wa Sada au la, ambae wakati huo alikuwa amesimama anawatazama, huku akiomba wakubari, “asante nwanangu, itakuwa vizuri sana” alisema mzee Jacob, ambae, aliona nikitendo cha kifahari sana kwao kuzunguka mji wa songea kwa gari, “weee itakuwa safi sana, maana atutapata shida kututusa mizigo mpaka hapa stendi” alisema mama Peter, huku anaachia tabasamu pana, la furaha, “basi ngoja nisubirini hapa nikamweleze yule rafiki yangu, kama anatakiwa awasaidie usafiri” alisema Sada huku anaondoka kwa mwendo wa nusu mbo, kulifwata gari lililosimama karibu na duka, yani lile Toyota IST, na huku mama na baba Peter wakimsindikiza kwa macho, nakumwona akiishia kwenye lile gari la dereva mvuta sigara, na hapo ndipo wawili awa walipotazamana kwa macho ya mshangao, huku kila mmoja ikimjia kumbu kumbu ya tukio ambalo liliwai kumtokea kijana wao Peter, muda mreu uliopita alipokuja kumfwata Sada, ambapo alimkuta yupo na rafiki zake wakinywa pombe na kuvuta sigara, kisha walimshambulia na kumwibia kila alichokuwa nacho, na wakati wawili awa wakiwa wanatafakari ilo, mala wakashtuliwa na sauti ya dada muuza duka, “mama! we mama, mnamwamini huyo huyo mwanamke?” ilikuwa ni sauti ya chini, na yakunong’ona, na hapo ndipo ndipo walipo kumbuka tena kumtazama Sada ambae sasa alikuwa amesimama kwenye mlango wadereva ambae sasa alikuwa anaonekana kwa uwazim na wakafanikiwa kuona baadhi ya alama za michubuko usoni kwa kijana yule dereva, ambae alikuwa anamsikiliza Sada huku mala chache akiwatazama wao, kisha na wao wakatazamana tena, kabla mzee Jacob ajamjibu dada muuza duka, “kwakweli inatia shaka” alisema mzee Jacob, na yule dada akaeleza wasi wasi wake, “nime mwona anadalili za tamaa, asa baada ya kuona fedha zenu, ni vyema kama mkiondoka, alisema yule dada kwa sauti ya kunong’ona.
Hapo bila kuambizana chochote, mzee Jacob aliinua begi lake na kumfwata mke wake ambae tayari alikuwa anashuka ngazi kwa haraka kuondoka eneo lile, “baba! baba! mbona mnaondoka gari lenyewe ni hili hapa” alisema Sada huku anawakimbilia, “tumepigiwa simu kijijini, Peter amefika lakini anauwa sana, hivyo tunatakiwa kuondoka zetu” alijibu mzee Jacob, huku anaendelea kutembea, “lakini nimetoka kuongea na Peter sasa hivi, anasema yupo vizuri” alisema Sada, ambae sasa alikuwa amesha wafikia, wakina mzee Jacob.
Mzee Jacob, akatafakari kwa haraka, kuwa japo wao walidanganya kuhusu kuumwa kwa Peter, lakini muda mfupi uliopita, Sada alisema kuwa Peter aliibiwa kila kitu, inamaana ata simu iliibiwa, na pia yeye Sada aliibiwa simu jana jioni, sasa inakuwaje yeye aweze kuongea na Peter, niwazi kuwa ata mama Peter alikuwa anwaza hivyo huvyo, maana mama huyu alishindwa kuvumilia na kusimama, kisha akamtazama Sada kwa jicho kali, “we mwanamke, ukiendelea kutufwata, nakuitia mwizi, ili watu wavuruge usowako, unazani sisi ni wajinga, wewe umeongea saangapi na Peter, na muda mfupi uliopita umesema unahisi watakuwa kijijini, na atuja kuona ukiongea nasimu” alisema mama huyu kwa sauti ya juu iliyojaa hasira, kisha akageuka na kuendelea na safari yake, akifwatiwa na mume wake, huku Sada awakiwa amesimama anawasindikiza kwa macho, na watu wengine wakiwatazama kwa macho ya mshangao.
Kuona hivyo Sada akarudi kwenye gari, na kumweleza Janja kilicho jili, “lakini sikia shem, tuna weza kuwatuna vijana wako, ili wakawavamie, na kuwapola lile begi lao” alishauri Sada na Janja akaunga mkono, huku anatoa simu mfukoni, na kuanza kutafuta namba flani, na kabla aja zipata wakashuhudia kwa macho yao likiingia bus toka Mbeya, linaloenda masasi, likiingia pale stendi, ba wazee wale wakalisogelea mbio mbio, na liliposimama tu, nao wakaingia ndani, hapo Sada akaachia tusi la nguoni, kwa kutaja kiungo kama chake cha jinsia, “wamepona washenzi wale” alisema Sada, kwa sauti ya kujilahumu.***
Tayari Peter alikuwa amesha maliza kusimulia kilicho mtokea, kiasi cha kushindwa kulipia gharama ya hotel, huku akipoteza kila kitu, “pole sana bwana Peter, vipi kuhusu mkeo wako, unaweza kumsamehe endapo ata kuja kukuomba msamaha?” aliuliza Careen ambae alikuwa anaonekana kuudunishwa na simu lizi fupi ya maisha ya Peter, “mh! sidhani kama anaweza kufanya hivyo, inaonyesha tayari amelidhika na maisha yake” alisema Peter kwa sauti iliyo nyongea, “usijari kuhusu nauri ya kurudia nyumbani, nipo tayari kukupeleka mwenyewe mpaka nyumbani, lakini naomba ungekaa kwanza hapa nyumbani kwa sikuchache” alisema Careen kwa sauti tulivu ya upole yenye kuomba.
Nikama Peter alishtuka kidogo, na kumtazama Careen, ambae pia alikuwa anamtazama kwa macho tulivu, yenye kusubiri jibu, “nipazuri sana hapa, na ningependa kukaa ata sikuzote, lakini sijazowea kukaa bila kazi, alafu wazazi wangu lazima wata kuwa na wasi wasi juu yetu” alisema Peter, kwa sauti iliyo jaa upole pia, “nita kupatia kila kitu, utafanya kazi, utawasiliana na wazazi wako, tena ingekuwa vyema kama ungeishi hapa mjini mwanao aanze kusoma” alisema Careen, ambae macho yake ayakubanduka usoni kwa Peter, na kuya kwepesha kila Peter alipo mtazama, “malipo yake nitayawezaje, na mashamba yangu nani ata yalima?” aliuliza Peter, kama vile akukubaliana na swala lile, “kila kitu kinawezekana ukiwa na fedha Peter, tutaongea nikitoka ofisini, sasa unaweza kupumzika, ukiitaji chochote, kutakuwa na mfanyakazi kwaajili yako, na mwingine kwaajili ya Michael, vyumba vyenu mtaonyeshwa, pia nitakuletea simu uweze kuwasiliana na baba kijijini” alisema Careen kisha akainuka na kuondoka zake, akimwacha Peter kama amepigwa na butwaha, huku anamsindikiza kwa macho, na kuona jinsi alivyo kuwa anatembea kwa madaha, ata Careen alipofika karibu na mlango wa kutokea pale sebuleni, akasimama na kugeuka, kisha akamtazama uso wake ukiwa katika tabasamu flani afifu, “hupo huru kwa kila kitu, jisikie kama hupo nyumbani kijijini” ilikuwa ni sauti flani tulivu iliyojaa ukarimu, na upendo flani hivi, kisha akageuka na kuondoka zake, huku bado Peter akiwa ameduwaa.
Careen akiwa ameingia unyonge kwa kuona Peter anasita kubakia pale kwake, aliutembea kwa haraka kushuka ngazi, za kuelekea flow ya chini, ambako alimkuta yaya Groly, ambae ni kama alikuwa anamsubiri kwa hamu, “niambie Careen nime ona ukiwa unafuraha, na sasa umenyongea kulikoni, umeshindwa kuelewana na mgeni wako?” aliuliza mama huyu ambae, aliishi na Careen kwa miaka mingi sana, na anafahamu mambo mengi yaliyo mkuta huyu mwanamke mrembo, ambae akuwa na mwanaume yoyote kimapenzi, huku anamfata mwanadada huyu, ambae bado alikuwa anatembea kutoka nje, na mkoba wake mkononi, “yaya tafadhari naomba umfanye abakie hapa nyumbani, japo kwa week moja tu, pengine itafaa kumbadirisha mawazo yake, sitaki aondoke” alisema Careen kwa sauti ya chini, ya kuomboleza, akionekana kukosa amani kwa kiasi flani, huku wakitoka nje na kwenda kusimama karibu na gari la Careen, yani Range Rover Discover, “yanini kuudhunika wakati mtu hupo nae hapa nyumbani Careen, lazima atakuwa katika sintofahamu kidogo, ndiyo maana anashindwa kukubari kukaa hapa” alisema yaya Groly, kwa sauti ya kumtia moyo Careen, huku wakiwa wamesimama nje ya gari, “kwahiyo yaya utaweza kumfanya abakie hapa hapa” aliuliza kwa shahuku Careen, “ilo ondoa shaka, lakini Careen unataka kuniambia kuwa unahisia juu yake?” aliuliza yaya Groly, huku anatabasamu na macho yake amayaelekeza usoni kwa Careen, ambae pia alitabasamu kwa aibu usowake akiutazamisha chini, mi sijuwi, lakini nataka tu abakie hapa hapa” alisema kwa sauti flani ndogo iliyojaa aibu, huku akiachia kitabasamu flani hivi, kama vile mschana anae karibia kukubari tongozo la mwanaume anae mpenda, “sawa Careen, we nenda ofisini, ukirudi utamkuta ana kusubiri kwa hamu” alisema yaya na hapo Careen akashindwa kuzuwia tabasamu pana, kwa kujuwa hivyo aligeuka na kuingia ndani yagari lake, kisha akaondoka zake.***
Emmanuel Msengi au Pengo kama unavyoweza kumwita, alikuwa bado amejilaza kitandani, akitafakari mambo yaliyomtokea toka jana usiku, kule Makimakuluga, alikopokea kipigo bila kutegemea, na yeye kuja kulipizia kwa mwanamke wake Queen, alafu baadae anagundua kuwa mwanaume yule alie mshushia kipigo, ndie mwanaume wa Queen, ambae alimtaperi, na baadae kuibiwa fedha alizo iba kwa yule jamaa, na anayafahamu ayo ikiwa tayari amesha ibomoa sura ya Queen, na kama aitoshi, baadae akamwongezea kipigo cha maana, wakati huo boss wake akiwa amesha kasirika, kwa kile alichokiita ni uzembe wakuto kutekeleza majukumu yao vizuri.
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU