SEASON 2: KIAPO CHA MASIKINI (32)

SEHEMU YA 32

ILIPOISHIA SEHEMU YA THERATINI NA MOJA: alikopokea kipigo bila kutegemea, na yeye kuja kulipizia kwa mwanamke wake Queen, alafu baadae anagundua kuwa mwanaume yule alie mshushia kipigo, ndie mwanaume wa Queen, ambae alimtaperi, na baadae kuibiwa fedha alizo iba kwa yule jamaa, na anayafahamu ayo ikiwa tayari amesha ibomoa sura ya Queen, na kama aitoshi, baadae akamwongezea kipigo cha maana, wakati huo boss wake akiwa amesha kasirika, kwa kile alichokiita ni uzembe wakuto kutekeleza majukumu yao vizuri. Endelea…
Wakati anatafakari hayo, mala akasikia mlango wa chumba chake unagongwa, akajuwa kuwa ata kuwa Queen anarudi, japo aikuwa tabia yao kugonga mlango wachumba hicho, “fungua mlango hupo wazi” alisema Emmanuel, na mlango ukasukumwa, akaingia bwana Kalonga, “hoooo! boss karibu, karibu sana Boss” alisema Emmanuel huku anajaribu kujiinua, toka kitandani, lakini maumivu yalikuwa ni makali sana, ata hivyo alilazimika kuyashinda, maana asinge weza kuongea na boss wake akiwa amelala, “duuuuh! Emma, imekuwaje umebomolewa namna hiyo?” aliuliza Kalonga kwa sauti iliyo jaa mshangao wawazi kabisa, “yani boss ata atukutegemea kama yule fala atatuvamia, ilikuwa ghafla tu” alijitetea Emma, kwa sauti iliyoonyesha kuwa na maumivu, “dah! kwani huyo jamaa yupoje, na kwanini mna shindwa kumwingiza kingi ili afanyie anachostahili?” aliuliza Kalonga ambae sasa alikuwa anamkagua kijana wake, “ukweli sijuwi imekuwaje, maana alipotuvamia mala ya kwanza tulianza kumtafuta ili tumfanyie jambo, lakini atukumpata, nashangaa jana ameibuka tena, na kutuvamia” alisema Emma ambae alikuwa anajuwa fika kuwa Peter anatokea kijijini, na siyo mkazi wa hapa mjini, “bwana heee huyu lazima atafutwe na afanyie tohara bila ganzi” alisema Kalonga, ambae pia aliuliza kwanini Emma mpaka sasa ajaenda kutibiwa, “sina pf 3, niliogopa wanaweza kukataa kunitibu” alisema Emma, ambae pia alifafanua kuwa Janja ameenda kununua dawa kwa aajili yake, “ok! nitakuachia fedha kwaajili ya huduma, vipi lakini amja jaribu kumfwatilia asubuhi hii?” aliuliza Kalonga, na Emma akaelekeza kama alivyo elezwa na Janja, kilicho mtokea Peter pale Hotelin, ambako alikuwa anadaiwa fedha za chumba, “lakini Careen alituma watu kuja kumchukuwa, sijuwi wameenda nae wapi?” alisema Emma, na hapo Kalonga akakosoa, “janja akiri zake fupi sana, kwanini alishindwa kufwatilia, ebu hakikisha unawatuma watu wanamtafuta huyo mshenzi, ili alipie alichokifanya” alisema Kalonga ambae alitoa noti kumi za elfu kumi kumi, na kumpatia Emma, kisha akaondoka zake.***
Yah! akiwa ametulia pale kwenye ukumbi wa kikao, yani seating room, yeye na mwanae Michael, huku wadada wawili wakiwa wamesimama karibu yao tayari kupokea amri au maagizo toka kwa watu wawili wale, Peter alikuwa anatafakari kuhusu jinsi mambo yalivyo, kwamba yeye anaumuhimu gani kwa Careen, au ile kumsaidia mala mbili, ndio sababu ya kumuomba abakie pale kwake, sawa ni kwaida kwa mtu mwenye shukurani, kufanya vile, lakini yeye Peter na hali ya umaikini aliyokuwa nayo inawezekanaje akilimiwe na namna ile na mwanamke mrembo tajiri, asie mfahamu, kiundani, ambae yupo tayari kumsomeshea mwanae Michael, ikiwa mwanamke ambae amezaa nae, amaemfanyia ushenzi usio ambilika, kwa kumwibia fedha na kila tu, ikiwa nguo na fedha zote alizokuwa nazo, mpaka chenji, ambayo ingemsaidia nauri ya kurudia kijijini, pasipo kumkumbuka au kumjari mtoto alie mzaa mwenyewe, inakuwaje mwanamke mwingine ambae akuwa na undugu wala mausiano yoyote, ajitolee namna hii kwao.
Ukweli kuhusu hisia za mapenzi kwa Careen Peter, akufikilia kabisaaa, siyo kwamba akuvutiwa na Careen, hapana, ukweli nikwamba akuwa nawazo ilo sababu akuwai kuota kuwa na mwanamke wa daraja la Careen, ukichukulia mwanamke wakawaida kama Sada ameshindwa kummiliki, sasa itakuwaje kwa mwanamke mzuri kama wa kwenye video, na atampeleka wapi, atampa nini.
Wakati Michael anawaza hayo huku Michael anatazama cartoon kwenye TV, mala akaingia yaya Groly, “habari za za mida hii, mgeni wetu, naamini ume furahia maongezi yako na Careen” alisema yaya Groly, kwa sauti tulivu, akionyesha uso wa tabasamu, “asante sana, chakula kitamu sana, nime ongea na dada Careen, nimefurahi sana, japo anaonekana siyo mwongeaji sana” alijibu Peter, kwa uchangamfu, “tena kitu ambacho uwezi kuamini ni kwamba, uwepo wako leo umemfanya atabasamu, uwa hatabasamu kabisa, niwazi damu zenu zinaendana” alisema yaya Groly, huku akiwa amesogea karibu kabisa na Peter, “kweli inamaana pale ndiyo amefurahi?” aliuliza kwa mshangao, maana yeye alimwona akuwa kama yaya alivyosema, “ndiyo, napia nazani uwepo wako utasaidia sana” alisema yaya, kabla ajawatazama wale wanawake wawili, waliokuwepo pale ukumbini, “Georgina mchukue mtoto akabembee huko nje, mpatia kila atakacho itaji, au kile ambacho wewe utaona kinamfaa kuchezea” alisema yaya, na hapo mmoja kati ya wale waschana akamchukuwa Michael na kutokanae nje, “na wewe nenda tu, akiitaji kitu nitakuita” alisema yaya na yue mwanamke anaondoka zake, “hivi mama kwanini mna tufanyia haya yote, kuna ulazima wa kutufanyia hivi?” aliuliza Peter, na hapo yaya Groly akatabasamu kidogo, “nikawaida yetu kuwa karimu wageni wetu, japo wewe na mwanao, ndio wageni wetu wakwanza wenyeji wa hapa Tanzania kuingia hapa ndani” alisema yaya Groly, huku anakaa kwenye moja kati ya kochi kubwa la kifahari, lililopo pale sebuleni, “weeeee! inamaana mimi ndio wakwanza?” aliuliza Peter kwa mshangao, “ndiyo tena upande wa huku juu, akuna mgeni anaingia kabisa” aisema yaya Groly, ambae alikuwa anamsoma Peter na kuichezea hakiri yake ibadiri mawazo.****
mpaka wanaingia ndani ya Bus toka mbeya linaloelekea Masasi, mama na baba Peter, walikuwa wamana mwona Sada akiwa ana watazama kwa macho ya hasira na tamaa kama ya fisi, na sasa walimwona anaingia kwenye gari dogo, ambalo alilitaja kuwa ni la rafiki yake, “lakini baba Peter pengine akuwa na nia ya kutuibia” alisema mama Peter, kitu ambacho mume wake akukubaliana nacho, “hivi ulimwona kule usoni, alafu umeisikia ile sauti, na vipi yule kijana kwenye gari nayeye amepondekana kama dala dala la njia ya vumbi” alisema baba Peter, yani mzee Jacob huku safari ikiendelea, wakiwa wamekaa seat ya pili toka nyuma walibahatika kupata seat zinazo fwatana, “sasa kwanini Peter nae amefanya hivyo jamani” alisema mama Peter, kwa sauti ya masikitiko, “hapo mimi siona afadhari, najuwa ata kama angekuwa na huyo mshenzi lazima ange mwibia, pengine ange msakizia na watu wamvamie kama wakati ule, ninae mwonea huruma ni Michael tu” alisema mzee Jacob, ambae alikuwa na hamu kubwa ya kwenda kuongea na Peter kujuwa kilicho msibu mpaka akajiingiza kwa wanawake walio mwibia, “hivi unaamini kweli Peter amelewa kiasi hicho na kulala na wanawake wawili, ata wenye wake wanne awafanyi hvyo” alisema mama Peter, kwa sauti yenye uchungu, “alafu unashangaa eti anapiga simu, na kunieleza kuwa anatatizo” alisema mzee Jacob, ambae alitoa itimisho, hapa nikifika nikanunue bia zangu na ulanzi lita tano, kilo mbili za ngombe, ni kuchoma huku na jilewea zangu” alisema mzee Jacob, “kwahiyo atuendi kwanza kwa Peter?” aliuliza mke wa mzee Jacob, “niende mimi au aje yeye mwenyewe, kwani kuna chochote ninamdai” aliuliza mzee Jacob, ambae alionekana amekasirishwa na kitendo cha Peter, kama alivyo simuliwa na Sada, hapo kikapita kimya kifupi, ni kama mama Peter ailikuwa ana tafakari jambo, “lakini mwenzio kama nawasi wasi na maneno ya yule binti, hivi toka lini Peter akawa na hakili kama hiyo?” aliuliza mama Peter ani mke wa mzee Jacob, “toka lini Peter akawa na hakili ya kukataa tunacho mweleza, unakumbuka alivyo tugomea kuhusu swala la kukutana na huyu mwanamke?” kauri hii ilimfanya mama Peter kutulia na kuachana na habari za Peter.**
Naam Janja na Sada waliingia pale nyumbani kwa Emma, na kumkuta akiwa amejilaza kitandani, lakini usowake ikiwa umefarijika kidogo, maana ata katabasamu kalionekana, “mmepishana kidogo na boss, ametoka sasa hivi” alisema Emmanuel Pengo huku anajiinua toka kitandani, tayari kupewa matibabu, na mpenzi wake Queen, “amesemaje ajamaindi kilichotokea?” aliuliza Janja, “amemaindi kiaina ila amesema kuwa jamaa asakwe ili apewe somo” alisema Emmanuel, wakati huo Sada akianza kazi ya kupaka dawa, kwenye kidonda cha mpenzi wake, “tena bro, wazazi wake tume wakosa kosa kidogo sana, walikuwa na mkwanja wanguvu, tungendoka na lile begi, hakika sasa wange kuwa wananena kwa lugha” alisema Janja “duh! mliwakosa kosaje, simnge wavamia tu mnakwala begi kisha mnatimka na mia” alisema Emmanuel akisahau maumivu yake.
Na hapo Janja akaanza kusimulia jinsi ilivyokuwa, “kwahiyo mamito umeambulia hamsini?” aliuliza Emmanuel, huku anacheka kidogo, “yani nilijiliza mpaka wakaamini Peter amenipiga” alisema Queen ambae ndie huyo huyo Sada, wa mzee Nyoni, wote wakacheka, “ebu sada baadae ukanichukulie chupa mbili za #mbogo_land Queen Gin, nijitie ganzi” alisema Emmanuel, akimaanisha akaletewe chupa mbili kubwa za pombe kali toka mbogo land, “mh! jamani baada ya kuugulia kidonda wewe unataka pombe” alisema Sada ambae alimaliza kuweka dawa na kubadiri plaster kwenye kidonda cha Emmanule, “we kamanunue na chakula kabisa, ndizi na nyama choma” alisema Emmanuel kabla ajamweleza Janja ampatia sigara, maana alikuwa ajavuta toka jana usiku.****
Yap! Michael alikuwa anajiachia kwenye bembea zilizopo nyuma ya jumba ili la kifahari, akisimamiwa na mschana ambae, kama asingekuwa amevalia sale za kazi za wafanyakazi wanyumba hii, basi ungesema ni mtoto wa mwenyewe nyumba, kwa mwonekano wa sura ngozi na mwili ya mwanamke huyu, ambae alimtazama ungesema ni mwanae, mdogo wake au mtoto wa mwenye nyumba, maana alimfanyia kila kitu kwa ungalifu mkubwa na unyenyekevu, kilicho kuwa cha tofauti, sasa mwanake huyu alionyesha kuchangamka sana, kutokana na uchangamfu wa Michael.
Wakati hayo yanaendelea nje, huku ndani ukumbi wa maongezi, Peter bado alikuwa anaongea na yaya Groly, bwana Peter, sidhani kama itakuwa vibaya, kama ukibakia hapa, na mwanao akipata elimu nzuri hapa mjini, katika shule ya kisasa” alisema yaya Groly, kwa sauti iliyojaa ushawishi, “lakini mama, kukaa hapa siyo tatizo, mimi ndio kama unavyo niona, nimeibiwa kila kitu, kule kijijini kuna mashamba yangu, na msimu wa kuandaa unakaribia, nita mwachia nani, labda ningekuwa nimesha maliza kilimo” alisema Peter, lakini aikuwa jibu sahihi, “ilo siyo tatizo, kwani kule kijijini akuna watu ambao unaweza kuwalipa waka lima shamba lote, au kutumia tractor kulima?” aliuliza yaya, na hapo Peter alicheka kidogo, “mama usinichekeshe, mimi mwenyewe ndie ninae lima kwenye mashamba yawatu, sasa nitawezaje kukodi mkulima” alisema Peter, kwa sauti ya mshangao.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!