
SEHEMU YA 34
ILIPOISHIA SEHEMU YA THERATINI NA TATU: “ameenda wapi, na nani, yani ….. yani….. amepelekwa nani?” aliuliza Careen kwa mshtuko, “yeye ni mwenyeji huku, ameenda peke yake, ila mwanae yupo juu” alisema yaya Groly, kwa sauti iliyopoa kidogo, maana aliona mabadiliko ya Careen, “namaanisha ameenda na gari gani?” aliuliza tena Careen, sasa kwa sauti ambayo ilikuwa kama inawasi wasi, “ameenda kwa mguu” alijibu yaya Groly kwa sauti ambayo ilizidi kupoa, “hapana yaya atakiwi kutembea kwa mguu, amesema anaenda wapi, niambie yaya, nimfwate” alisema Careen huku anageuka na kuanza kutembea kutoka nje…. Endelea…
Huku mawazo yake yakiwa kwa Peter, akiamini kuwa kwa sasa Peter akutakiwa kutembea kwa miguu, na kuzurula akiwa peke yake, Careen aliitoka nje na kuingia kwenye gari, lake aina Land Rover discovery jeusi, la kisasa, na kuanza kuliondoa kuelekea kwenye geti la kutokea nje, huku mlinzi akiangaika kulifungua geti ilo, Careen akaendesha gari kwa speed kuelekea upande wa mjini, huku akijitaidi kutazama kushoto na kulia kama ange mwona mgeni wake, yani kijana wetu Peter Jacob.***
Naam turudi kijijini mwanamonga, ambako, habari za kurudi kwao toka njini zikianza kusambaa, huku wanakijiji wenzao wakiwa awajuwi lolote juu ya kilochotokea huko mjni, na vipi kuhusu vijana wao yani Peter na mjukuu Michael, huku mzee Nyoni na mke wake wakiendelea kutembea sehemu moja mpaka nyingine, asa zile ambazo, zilikuwa zinapatikana ulanzi, na kuanza kusimulia habari ya Peter kuingia katika matatizo.
Siyo mbaya kwa wanakijiji kupata habari za mwanakijiji mwenzao, lakini ni namna ya mwanadoa awa walivyo zifikisha zile habari kwa wanakijiji mwenzao, “ndio mjifunze, mkitaka kwenda mjini mntuambie sisi tuwape namba ya Sada, ili awapokee na kuwasaidia kuwaonyesha mitaa, sasa ona kilichomkuta mtoto wa mzee Jacob” alisema mzee Nyoni, na mke wake ange dakia, “tatizo ni ushamba, aliona aibu, kumpigia Sada ampokee, mwenzie yule mjini amefika zamani” waliongea hayo huku wakipewa ulanzi na kuendelea kunywa, “nimesikia mzee Jacob na mke wake wameelekea mjini, hivi hakuna taarifa yoyote ya huko” aliuliza mzee Ponera, ambae alishtuliwa na taarifa ile, “nimewaona walipita na pikipiki, ila awakuwa na Peter wala Michael” alisema mzee Ngongi, hakuna shida nitaenda kuwaona ili tupate taarifa za huko mjini, maana sikuhizi imani imekwisha, binadamu ni zaidi ya chui au simba, asa pale anapoitaji kitu toka kwako” alisema mzee Ponera, akijiinua tayari kwa safari, “tutaenda wote bwana Ponera ebu tumalize kwanza hii nusu” alishauri bwana Ngingo, na mzee Ponera akakaa tena, “nyie mnazani ata kuwa na lolote jipya, mji mkubwa huo, sidhani ata kama amesha mwona” alisema mzee Nyoni ambae kwa mala ya kwanza akupenda mapokeo ya taarifa zake, juu yam zee Jacob, pale kwa kina bwana Ponera,.***
Naam kijana Peter Jacob, katika tembea tembea yake kweli alitokea eneo la soko kuu, ambapo aliweza kupakumbuka, na kuamua kushika uelekeo wa upande wa kusini, ambako jana alipelekwa na boda boda, ambapo mita kama mia mbili mbele, akajikuta ameibukia kwenye lile jengo kubwa la ghorofa tatu, ambalo jana alilala ndani yake, jengo ambalo lilimkumbusha jinsi alivyo tapeliwa na Sada, na hapo akajikuta anashikwa na uchungu mkubwa sana.
Ukweli uwezi amini, uchungu ambapo aliupata Peter siyo kwaajili ya fedha alizopoteza ila ni kwakuona mpaka siku ya jana, bado Sada akuwa na mpango wa kuwa nayeye au mtoto wao Michael, “au alikabwa na kuumizwa sana, kiasi cha kushindwa kujitambua” aliwaza Peter huku anatembea kusogelea mtoini Pub, “aiwezekani kuwa amekufa, lazima ningekuwa na weweseka mala kwa mala” aliwaza Peter, huku akiendelea kutembea kusogelea pale mti pub.
Naam wakati anataka kuingia mtipub, ambayo ilikuwa na watu wengi kiasi, mapa akamwona Sada akiwa ameshika mfuko wenye mzigo flani ndani yake, na kwa haraka usinge shindwa kuona kuwa vilikuwa ni vyupa vya bia, akiwa amesimama kwenye jiko la kuchomea nyama, hapo Peter akatabasamu kidogo, na pasipo kuamini macho yake, ukiachilia kumwona mwanamke huyu akiwa mzima wa afya nasiyo kama alivyofikilia kwamba alivamiwa na wezi, hiyo ilikuwa ni furaha yake ya kwanza, na pili Peter alitaka kujuwa kilichomkimbiza na kumfanya asirudi pale hotelini, akiwaacha wenzake awana mbele wala nyuma.
Hapo bila kujiuliza lolote, Peter akaanza kutembea, kumsogelea mwanamke huyu, ambae toka ameenza nae mausiano, akuwai kupunguza upendo wake kwake.Yap! mpaka Peter anamfikia Sada alie simama pale mbele ya mchoma nyama wa jiko la pale Mtini Pub, Sada akuwa amemwona wala kuutambua ujio wake, “mama Michael, mbona jana hukurud….” kabla ajamaliza kuongea alichotaka kuongea, Sada akaonekana kugheuka kwa ghafla akishtuka kwanguvu, na kumtazama Peter alie kuwa anaongea huku anajichekesha, “weeee, unanijuwa mimi?” aliuliza Sada kwa sauti ya mshangao, huku anamtazama kuanzia chini mpaka juu, kisha akashusha tena macho yake, huku akikunja mdomo, kama ameona taka kata, na hapo ndipo Peter alipoweza kuona uso wa Sada ulipondeka kwa madonda na mikwaluzo ya ajabu, sambamba na vimbe za aja, “he! kumbe ulipata hajari, kwanini hukurudi kutujulisha, au ulivamiwa na vibak…” aliuliza kwa mshangao Peter, lakini Sada akumpa nafasi ya kumaliza swali lake, “we kaka ebu nikome, mbona una vamia watu usio wajuwa, ebu niondokee hapa” alisema Sada kwa sauti iliyojaa ukali, huku amekunja sura kwa hasira na chuki ungesema ana ugomvi mkubwa na kijana huyu.
Ukweli nikwamba, Sada alikuwa na wasi wasi wakudaiwa fedha alizo ondoka nazo, fedha ambazo ata yeye akuwana ata seti moja, maana zote zilisha ibiwa, na watu ambao ata yeye hawakuwajuwa, hapo Peter akatazama kushoto na kulia akawaona watu wanawatazama, akajicheksha kidogo, “mama Michael tunaitaji kuongea” alisema Peter kwa sauti ya kunong’ona, “weee koma kabisaaa, uongee na nani, alafu mume wangu akitukuta itakuwaje?” aliuliza Sada na hapo Peter alishikwa na mshtuko mkubwa sana, “mume wako nani, inamana…. yani… yani.. unataka kusema umeolewa?” aliuliza Peter, huku akianza kuona miguu yake inaanza kukosa nguvu taratibu, “sasa je kama uja sikia sema niongeze sauti, tena naomba uondoke mbele yangu” alisema Sada kwa sauti iliyojaa nyodo, hapo Michael akamtazama Sada kwa macho ya mshangao, huku upande mwingine ukimweleza kuwa Sada ata kuwa anamtania, maana ni yeye ndie alie mtafuta kwenye simu na kumweleza kuwa anaitaji warudiane, “kwahiyo ulikuwa na maana gani uliponiambia kuwa umejirekebisha na unataka tumlee mtoto pamoja?” aliuliza Peter, kwa sauti ambayo nikamaaikuwa inaamini amini, “tena ondoa wazo kuwa ulizaa na mimi we fala, ebu endelea na mambo yako, na itakuwa vyema kama utarudi kijijini, maana wazazi wako wanakutafuta” alisema Sada ambae sasa alikuwa anapokea kijifuko chenye vyakula alivyo agiza, toka kwa jamaa wa jikoni, na kuanza kuondoka huku Peter akimfwata, “Sada nivyema ukiacha utani, unajuwa huo ni utani mbaya sana” alisema Peter, huku akijaribu kujitabasamulisha, wakati huo walikuwa wamekaribia kwenye kijiwe cha boda boda, mbele ya mtini Pub, huku watu wakiwafwatilia kwa macho.
Kusikia hivyo Sada akasimama na kumtazama Peter kwa macho ya dharau, akamtazama juu mpaka chini, akirudia mala mbili, kisha akacheka kwa dharau akimaliza kwa kutema mate, “kwahakili zako, wewe uwe na mimi, hivyo ulivyo, tena usije ukaota kabisaaaa, kwamba nita rudi kwako, bola nilale na mbwa kuliko wewe taka taka, naomba ukae mbali na mimi, yani iwe kama atujuwani na atuja zaa kabisaaa, mimi ni mke wamtu” alisema Sada kwa sauti ya chini iliyojaa dharau na majigambo, “lakini Sada hivi mimi nime kukosea nini mke wangu, mbona unanipa adhabu kali kama hii?” aliuliza Peter, huku akihisi uchungu mkubwa moyoni mwake, kiasi cha kutamani kumwaga chozi, “kwahiyo unataka niwe na wewe masikini mshamba, unisaidie nini, mbona nyie watu mnapenda kuziba liziki za watu, nasema sikutaki mimi ni mke wamtu, alisema Sada kwa sauti ya juu safari hii, na kuwa fanya ata wale jamaa waboda boda waliokuwa umbali mdogo toka kwao, wawatazame kwa mshangao, “Sada kumbuka tulikotoka mke wangu, nakuomba rudiane, nipotayari kufanya chochote, iliukubari kuwa na mimi, uje tumlee mtoto wetu” alisema Peter kwa sauti iliyotia huruma, “ebu acha ujinga we mbwa, nasema hivi sikutaki! sikutaki! sikutaki! na unikome kabisa, siwezi kurudiana na wewe bola nife kuliko kufanya ujinga kama huo” alisema Sada, kwa sauti ya juu, yani ya kupayuka, kisha akaanza kuondoka, kuelekea upande wenye boda boda, huku vijana waboda boda wakianza kushangilia kwa kumdhiaki Peter, wapo waliomdhiaki kwa kumwona mdhaifu, na wapo walio mshangaa kwa kumng’ang’ania mwanamke alie pondeka usoni kama Sada, na wapo pia walio mshangaa Peter kwa kubembeleza mwanamke, ambae baadhi yao walikuwa wanamfahamu kama mwanamke anae uza sukari yake,
Peter akamdaka mkono “mama Michael naomba usinifanyie hivyo nipo chini ya miguu yako..” kabla Peter ajamaliza kuombolea, Sada akamkatiza, “nimesema niache mbwa mkoko we sikutaki” alisema Sada huku anamsukuma Peter kwa nguvu….….
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU