
SEASON 2: KIAPO CHA MASIKINI (35)

SEHEMU YA 35
ILIPOISHIA SEHEMU YA THERATINI NA NNE: na wapo walio mshangaa kwa kumng’ang’ania mwanamke alie pondeka usoni kama Sada, na wapo pia walio mshangaa Peter kwa kubembeleza mwanamke, ambae baadhi yao walikuwa wanamfahamu kama mwanamke anae uza sukari yake,
Peter akamdaka mkono “mama Michael naomba usinifanyie hivyo nipo chini ya miguu yako..” kabla Peter ajamaliza kuombolea, Sada akamkatiza, “nimesema niache mbwa mkoko we sikutaki” alisema Sada huku anamsukuma Peter kwa nguvu….…. Endelea…
na kumfanya Peter ambae akujiandaa kwa tukio lile, ayumbe mala kadhaa kabla ajajiweka sawa na kusimama vizuri, kisha akamtazama Sada kwa macho ya mshangao, wa kuto kuamini, “Sada una uhakika na unacho kisema?” aliuliza Peter huku akiwa anamkazia macho mzazi mwenzie, “sidhani kama nimeongea kichina, najuwa umenielewa vizuri tu, sikutaki na sitaki kusikia habari zenu wewe na mwanao” alisema Sada wa sauti iliyojaa nyodo, “Sada hivi unayaongea hayo ukiwa na hakiri zako timamu kabisaaa, kuwa utorudi nyumbani na Michael?” aliuliza tena Peter, na hapo ndipo alipopewa jibu ambalo lilimfanya aondoke zake, pasipo kudai chenji, “ebu nisikilize vizuri we mbwa koko usie taka kuelewa, na ukawasimulie wote huko kijijini pamoja na mizimu ya babu zako walio lala makaburini, sikutaki, sina mtoto, na kamwe sito kaa kurudiana na wewe labda nife, nahapa kwa miungu yote ile, nikirudiana na wewe niwe kichaa hapo hapo” alisema Sada ambae baadhi ya boda boda walikuwa wanamfahamu kwa jina la Queen, na kuanza kuanza kuondoka zake, akimwacha Peter anamsindikiza kwa macho, mpaka alipopanda boda boda na kuondoka zake, akitokomea upande wa Mahenge.
Hapo Peter alishusha pumzi ndefu, kisha akaanza kutembea taratibu, kuelekea upande wa majengo, huku akiwa ana waza kile kilicho mtokea, muda mfupi uliopita huku baadhi ya maneno ya Sada, ambayo yaliuchoma moyo wake, “nahapa kwa miungu yote ile, nikirudiana na wewe niwe kichaa hapo hapo” “sijuwi nilimkosea nini, au amepata mwanaume mwenye bola zaidi yangu?” alijiuliza Peter, huku anatembea pembeni ya barabara, machozi yakikaribia kumdondoka machoni mwake, “sawa anitaki sasa kwanini alinidanganya na kuiba vitu vyangu vyote pamoja na fedha?” alijiuliza tena Peter, ambae sasa alikuwa anakaribia njiapanda ya Msogeze Pub, iliyopo karibu kabisa na mtaa wa Jengo mwisho wa lami, “sijuwi nitawaeleza nini kijijini, kwakweli hii niaibu kubwa sana” aliwaza Peter huku anasimama pale njia panda, na hapo ndipo alipogundua kuwa alikuwa anaelekea sehemu ambayo akuwa anaifahamu, hivyo katazama kushoto na kulia, huku akijuliza aelekee wapi.***
Saa kumi na moja na robo, ikiwa nilisaa limoja tu, toka mzee Jacob aache simu yake pale dukani, sasa alimtuma kijana mmoja akamletee, ili aweze kuwasiliana na kijana wake, na akiwa anaendelea kutafuna minofu ya ng’ombe ya kuchoma, huku bado mawazo yake yakiwa kijana wake, japo kuna wakati alikuwa anatamani kudharau, jambo lile, kutokana na ubishi wa kijana wake Peter, waking’ang’ania kwenda mjini kukutana na Sada, lakini bada ya muda mfupi ilishindakanda, na kujikuta akiwaza tena upya, “hooooo bwana Jacob, naona una punguza uchovu wa safari” mzee Jacob na mke wake walishtuliwa na sauti yam zee Ponera, wote waka geuza shingo zao kutazama upenda ilikotokea sauti, wakawaona mzee Ponera mwenyewe akiwa na mzee Ngongi, wakiwa na dumu la lita tano lililosheheni ulanzi, “karibu bwana karibu sana” alisema mzee Jacob, huku anajiweka sawa kwenye kiti chake, na wakati huo mke wake alikuwa anainuka na kuingia ndani kutoa viti viwili, “asante sana bwana Jacob, naona tuna mguu zuri” alisema mzee Ponera, huku anaonyesha pande la nyama lililokuwa jikoni, wote wakacheka, zilikuwa kilo mbili hizo, nime ikang’anda weee, mpaka meno yanauma.
Naam baada ya kupewa viti na bilauri za kunywea ulanzi ambao sasa waliuchanganya na bia, story zikaanza, “bwana Jacob nashindwa kukuelewa kwakweli, nilitegemea ningekukuta umejikunyata kwa mawazo, lakini naona una shindilia bia na minyama kama una sherehe” alichombeza mzee Ngongi, huku akicheka na kufanya alichokiongea kiwe kama ni utani, “uzuni ya nini bwana Ngongi, wakati msimu wa mavuno umetukuta na afya njema?” aliuliza mzee Jacob ambae kiukweli alisha juwa anachomaanisha mzee Ngongi, “haaaa! bwana Jacob, mbona kijiji kizima kina fahamu kuwa kijana wako amepatwa na matatizo, huko mjini” alisema mzee Ponera, safari utani waliacha pembeni.
Hapo mzee Jacob akaweka ukimya mfupi huku akishusha pumzi ndefu, “ukweli atujajuwa lolote mpaka sasa, kama nikweli Peter anatatizo huko mjini au la, maana atuja onana nae, ila sasa tuliyoyakuta huko, ndiyo matatizo kweli kweli” alisema mzee Jacob, na wakati huo huo akaingia kijana mmoja akiwa na baiskeri, “mzee anasema imeingia chaji nusu” alisema yule kijana huku anampatia simu mzee Jacob, “asante sana kijana” alisema mzee Jacob huku anaipokea simu na kuiwasha, huku yule kijana akaondoka zake, “kwahiyo mlivyomkuta huko mjini akafanyaje?” aliuliza Ngongi, ambae nika alikuwa na hamu kubwa ya kusikia habari za huko mjini, “unazani huyo Peter mwenyewe tulimwona basi, tulikutana na binti wa mzee Nyoni” alisema mama Peter, wakati huo mzee Jacob akiwa anafungua ujumbe ulioingia kwenye simu yake, “unamaanisha Sada?” aliuliza mzee Ponera, huku Ngongi akidakia, “tena nilisikia wanarudiana na Peter, “hakuna cha kurudia hapo jamani, yani nauhakika kama ….” alitaka kuongea mama Peter na hapo hapo mzee Jacob akaingilia, “jamani Peter huyu hapa katuma meseji” alisema baba Peter, na wote akatulia kumsikiliza, “Peter anasema kwamba alikutana na Sada, ambae amemwibia kila kitu, kuanzia fedha, simu, mpaka nguo zao na viatu yao, kisha amtoweka” hapo mama Peter akadakia “na akome kwa kimbele mbele chake” kisha mzee Jacob akaendelea, “ila kwasasa anasema yupo sehemu nzuri tu yeye na Michael wamepata mwenyeji, na watakaa kwa muda wa week moja” alimaliza kusoma ile messeji mzee Jacob, “hapo afadhari, nazani atakuwa ameshaamini kuwa yule mwanamke siyo mtu mzuri” alisema mzee Jacob mwenyewe kisha wakaanza kuwasimulia wakina Ponera, jinsi walivyo nusurika kuingia kwenye mtego wa binti huyo, “ebu! mpigie kwanza tujuwe huyo mwenyeji wake ni nani, maana sidhani kama anarafiki au ndugu ambae anaweza kukaa kwake week moja” alishauri mama Peter, ambae alitamani kuongea na mwanae Peter, mzee Jacob aliafiki wazo la mke wake, na kupiga ile namba, aliyotumia sms, ambayo ilianza kuita mala moja, na aikuchelewa kupokelwa, “habari ndugu ni yaya Groly hapa nyumbani kwa madam Careen” ilisikika sauti tulivu ya mwanamke mtu mzima, upande wapili wasimu, “habari za jioni mama” alisalimia mzee Jacob, kwa sauti tulivu pia, akijizuwia asionyeshe kama alikuwa nakilevi cha kutosha kichwa mwake, “salama baba yangu, nikusaidie tafadhari” aliongea yaya Groly, “samahani mama yangu, kuna kijana alitumia simu yako kututumia messeji, anaitwa Peter, sijuwi nina weza kumpata niongee nae?” aliuliza mzee Jacob, kwa sauti ile ile tulivu, huku akiwatazama wakina mzee Ponera walio kuwa wakifwatilia maongezi yale kwa umakini mkubwa sana, “hoooo! unamzungumzia baba Michael, ameenda kutembea kidogo, akirudi nita mwambia akupigie, ila sijajuwa wewe ninani kutoka wapi?” aliuliza yaya Groly, “mimi ni baba yake nipo na mama yake, tulitaka kujuwa anaendelea je huko, yeye na mwanae Michael” alisema mzee Jacob, huku akimkonyeza mke wake, kwa jicho moja, “wapo salama kabisa, tena Michael yupo ghorofani anacheza na kijakazi wake” alisema Groly, ambae akuishia hapo, “ngoja nimfwate aongee na babu yake” ilikuwa ni sauti ya uchangamfu ambayo ilimfanya mzee Jacob angundue kuwa mwenyeji wa Peter ni marimu sana, “itakuwa vizuri sana, ila samahani wewe ni nani na mme fahamiana vipi na Peter?” aliuliza mzee Jacob, huku akisikia vishindo vyepesi upande wapili wa simu, ikionyesha mwanamke mtu mzima alikuwa anapanda ngazi, “mimi ni yaya Groly, mlezi wa rafiki yake Peter, ambae anaitwa Careen, mschana kiongozi wa duka la vito vya thamani na nguo za kila aina, la #Mbogo_land Sonara, jinsi walivyo fahamiana watawaeleza wenyewe” alisema yaya Groly huku anaangua kicheko. ***
Naam upande wa mwanadada Careen, akiwa njiani huku anawaza juu ya wapi alipoenda Peter, huku akiwa katika hali ambayo ata yeye akujuwa ni kwanini yupo hivyo, kwamaana alikuwa na wasi wasi na hofu ya kumpoteza Peter, sijuwi kwamaana gani, tayari alisha pita mitaa kadhaa, pasipo kumwona kijana wake huyo ambae ni wazi akuwa anaifahamu vyema mitaa ya Songea mjini, alilifahamu ilo kutokana na simulizi aliyosimuliwa na Peter mwenyewe, tayari alisha tembea msokoni na madukani, huku watu wakimtazama kwa macho ya mshangao, siyo kwamba awakumjuwa au alikuwa anakitu cha ajabu, ila ukweli ni kwamba, kama ulikuwa unaitaji kumwona Careen, basi nipale dukani kwake pekee ndiyo sehemu ambayo ungemwona tena akiwa anapita au anaangalia toka ghrofani, ilikuwa ni agharab, kumwona mtaani kama hivi.
Mwisho Careen alipata wazo la kwenda kule MAKIMAKULUGA Motel, ambako jana Peter alikuwepo, na wakati anakaribia mitaa ile ndipo alipomwona Peter akiwa anapotelea upande wamajengo mwisho wa lami, ndipo alipo ongea zamwendo kuelekea upande ule, na kila alipozidi kumsogelea kijana huyu, aliweza kubaini kuwa Peter alikuwa akatika mawazo mengi sana, tena mazito, kiasi cha mkumshangaza Careen ambae alipomfikia pale njia panda ya Msogeze Pub, akasimamisha gari na kupiga honi, Peter akatazama gari, huku usowake ukiwa katika uzuni kubwa sana, lakini mala macho yake yalipo kutana na macho ya Careen yenye uzuni kubwa, hapo Peter akaonekana kutabasamu kidogo, “hoooo! dada Careen, unatokea wapi huku?” aliuliza Peter akijitaidi kujitabasamulisha, huku anatembea kulisogelea gari lile la kifahari.
Swali ilo lilikuwa gumu kidogo kwa Careen ambae aliingia uzuni kubwa kwa hali aliyomkuta nayo mgeni wake, ambae ni shujaa wake, akisema kuwa alimfwata yeye lazima kijana huyu amshangae, na kumwona anajilahisisha kwake, “nili… nime … mhhh! nilikuwa napita tu” alisema Careen kwa sauti ya kubabaika, huku akiachia tabasamu laini, ambalo lilimchanganya Peter, na kubakia amekodoa macho huku amesimama nje yagari, karibu na mlango wa dereva aliokaa Careen mwenyewe, “vipi wewe unatokea wapi?” aliuliza Careen, ambae alishaona mshangao wa Peter,
Naam swali ilo lilikuwa ni zito kwa Peter, siyi kwamba akuwa na jibu, ila ukweli nikwamba, jibu lilikuwa ni la aibu, asa kwa kile kilicho mtokea, “haaa! mhhhh! nilikuwa natembea tembea tu, hapa nilikuwa najiuliza ni elekee wapi” alisema Peter, huku akijitaidi kucheka cheka, “ok! usijari, nitakutembeza week end, kesho kutwa, sasa twende nyumbani” alisema huku anashuka na kwenda kumfungulia Peter mlango wa abiria wa mbele, Peter nae akaingia bila kusema neno, nakufunga mlango kwanguvu, kiasi cha Careen kuuma meno kwa uchungu, alitaka kuongea neno lakini iliishia kooni, na kujitabasamulisha, huku anaondoa gari, wakiingia upande wa kushoto wa njia panda ile, wakifwata barabara ya Songea Girls sekondari, safari ikiwa imeanza kimya kimya, kila mmoja akitafakari la kwake, wakati Peter alikuwa anawaza juu ya kile kilicho mtokea, yani kukataliwa adharani, na mzazi mwenzie, ambae amemkataa na mtoto wao pia, huku Careen alikuwa anajiuliza kwanini shujaa wake yupo katika hali kama hii, “au amekutana na mke wake, na wamegombana” alijiuliza Careen, akihisi kuwa Peter atakuwa amekutana na Sadam, kitu ambacho kiukweli “umekutana na mke wako Peter” aliuliza Careen kwa sauti tulivu ya upole, “ndiyo nimekutana nae” alijibu Peter kwasauti tulivu, huku akiwa kama amekumbushwa machungu, “umesha msamehe?” aliuliza Careen ambae jibu la Peter liliushtua moyo wake, “yes nimesha msamehe” alijibu Peter, huku akijaribu kujiweka katika hali ya kawaida na siyo ya udhuni, lakini aikuwezekana, Careen alijikuta akipunguza mwendo, sijuwi kwanini jibu lile lilimkosesha amani kiasi kile.…. Itaendelea…..

