SEASON 2: KIAPO CHA MASIKINI (37)

SEHEMU YA 37

ILIPOISHIA SEHEMU YA THERATINI NA SITA: alisema Peter kwa sauti yenye kumaanisha, hapo Careen akachia tabasamu pana, huku wanaingia ndani na kupandisha ngazi kuelekea ghorofani, “ambako walikutana na yaya Groly, alie kuwa anashuka ngazi, “yaya tuandalie bustani, chakula cha jioni mimi na Peter tuta kula huko” alisema Careen, ambae baada ya kufika kule juu akaagiza Peter na Michael wapewe zile nguo alizokuja nazo, “Peter utavaa bukta na tishet zipo huko ndani” alisema Careen huku anaelekea chumbani kwake, “asante sana” alisema Peter huku akimsindikiza kwa macho mwana dada huyu mrembo ajapata kuona mfano wake…..Endelea…
Peter alimtazama Careen alie yembetembea taratibu kuelekea upande wa vyumba vyake, ambae alipoufikia mlango wa chumba chake akasimama nakutazama kule alikokuwepo Peter, ambae bado alikuwa amesimama amekodoa macho, ata macho yao talipokutana Peter alishtuka vibaya sana, akiona kuwa sasa anaumbuka kwa ushangaaji wake, lakini alishangaa kuona Careen anatabasamu na kuingia chumbani kwake, Huku akijisemea kimoyo moyo kuwa “kuna watu wanafaidi jamani dah! sisiwengine tumejawa nagundu tu”aliwaza Peter huku anaelekea chumbani kwake, kule alikoelekezwa nyakati za mchana, ambako alikuta kuna nguo nyingi za kila aina, viatu na vitu vingi ambavyo yeye angeviitaji, katika matumizi ya kila yake ya siku, ukweli Peter siyo tu kushangaa, alifikia hatua ya kuogopa kabisa, “au amenifananisha na mtu flani, yani kumsaidia tu ndio anifanyie haya yote” aliwaza Peter, huku anatazama vile vitu kitandani.**
Yap! tukirudi kijijini Mwanamonga, mambo yalikuwa ngoma drow, kwamaana ya kwamba, mama na baba Sada yam zee nyoni na mke wake, wakiwa wamesha zunguka huku na huku, wakieleza kilicho mtokea Peter na Michael huko mjini, kwa kile walicho kisema kuwa ni ushamba wa kijana huyo wa mzee Jacob, huku wakiwa wamesha lewa kwa kiasi flani, waliamua kwenda kwa mzee Jacob, kupata matokeo ya safari ya mzee huyo na mke wake, ambao walienda mjini kufwatilia kilicho mkuta kijana wao.
Wawili awa walitembea kwa haraka wakifwata njia ya kuelekea nyumbani kwa mzee Jacob, huku njiani wakiongea ili na lile, ikiwa ni kuwa simanga mzee Jacob na mke wake, “awa walipoona binti yetu ameenda mjini na anaishi huko, na wenyewe wakaona ni kazi lahisi, sasa kijana wao yame mkuta” alisema mama Sada, na mume wake akaunga mkono, “unazani nini kinacho wasumbua zaidi ya wivu” alisema mzee Nyoni, ungesema uwepo wa Sada mjini ulikuwa na manufaa kwao, awakuwaza toka Sada aende mjini, amefanya nini na anaishi vipi.
Dakika chache baadae, tayari walikuwa wanaingia kwenye mji wa mzee Jacob, ambapo walishangaa kuona watu wanne wakiwa wana kunywa pombe huku wanaongea kwa furaha na vicheko vya uchangamfu wa ulevi, “yani mtu analala ghorofani nyie mnahaha kumtafuta” mzee Nyoni na mke wake waliisikia sauti ya mzee Ngongi, wote wawili wakasimama na kutazamana kwa mshangao, siyo kwamba walishangaa kumsikia mzee Ngongi, hapana maana uwepo wa mzee Ngongi, na Ponera kwa mzee Jacob, walikuwa wanaufahamu, kilicho waduwaza ni kile walicho kisikia.
Lakini wakajipa moyo kuwa, kile walicho kisikia akikuwa kina mhusu Peter, hivyo bila kusema lolote waka aanza kutembea kuingia kwa mzee Jacob, wakilenga pale walipokaa wenyeji hao na mke wake, ambao kila walipowasogelea waligundua kuwa wazee awa walikuwa katika hali ya uchangamfu mkubwa, “yani Michael amechangamka kweli kweli eti tupo kwa shangazi mzuri mzuri” safari hii ilisikika sauti ya mzee Ponera, na hapo wakasimama tena.
Msomaji tambua kuwa kutona na giza na umbali waliokuwepo wakina mzee Nyoni, ilisababisha mpaka wakati huo, wakina mzee Jacob wasiwe wamewaona, “hivi awa wanaongelea nini lakini” aliuliza mzee Nyoni, kwa sauti ya kunong’ona hku anamtazama mke wake, ambae pia alikuwa anamtazama, “we kwani ata najuwa basi, au Peter amefikia kwandugu huko mjini?” aliuliza mama Sada, huku anatega sikio vizuri kusikiliza kinachoongelewa kule kwa mzee Jacob, “ila ni lazima niongee na Peter, ndio roho yangu itulie” alisema mzee Jacob, kwa sauti yenye kisisitiza, huku wakina mzee Nyoni wakisikiliza kwa umakini ilikufahamu kilichokuwa kinaongelewa, “bwana Jacob acha wasi wasi, kijana anafaidi upepo wa ghorfani” alisema Ngongi, na wote wakacheka, hapo hapo mama Peter akadakia, “jamani msiseme hivyo, yani nimuhimu sana kufwatilia maisha ya watoto huko mjini, kuna watoto wameenda huko wakiwa vizuri tu, lakini sasa ukiwaona utazani majambazi, ndio maana wanazamiaga moja moja” kusikia hivyo kila mmoja kati yao, yani mzee Nyoni na mke wake wakasisimka na kujionja, japo mke wa mzee Jacob akutaja jina, lakini walipo kumbuka kuwa binti yao, toka alipoondoka mwaka jana msimu wa malipo ya tumbaku, akuwai kurudi tena kijiji, na awakujuwa anafanya nini na anaishije, wakatazama kwa sekunde kadhaa, nikama waliambizana waondoke zao, maana waliheuka na kurudi walikotoka, huku masikio yao yakiendelea kusikia maongezi ya furaha na shangwe, za wakina mzee Jacob na wageni wao, “watu wengine kwa kujishauwa, sasa kukaa ghorofani ndio nini?” alisema mama Sada, kwa sauti iliyojaa chuki na hasira.***
Naam wakati peter akiwa bado, yupo chumbani anatazama nguo na baadhi ya vitu alivyo vikuta chmbani kwake, mala akasikia mlango wachumba hicho ukigongwa na kabla aja sema lolote, mlango ukasukumwa, akaingia Michael, akiwa mwenye furaha kubwa sana, akiwafwatiwa na yaya Groly alieshikilia box la simu, mkononi mwake, “baba ona!! ona!!! nimepata nguo nzuriiiinaviatu vingine” alisema Michael huku anaonyesha kwa mikono yake, nyuo na viatu vipya alivyo valia, kwamacho yake, Peter aliwezakuona na kukili kuwa, mwanae alikuwa amependeza kweli kweli, akamtazama kwa sekunde kadhaa huku akizidi kujiuliza inakuwaje mwenyeji wake amhudumie kiasi kile, kwalipi asa jema alilo lifanya, “bwana Peter, simu yako hii hapa utapata maelekezo jinsi ya kuitumia” alisema yaya Groly, huku ana mkabidhi Peter box la simu, Peter akuwa na kusema zaidi ya kupokea lile box pana la simu, ambalo lilikuwa na picha ya simu nzuri ya kisasa, ilimshangaza sana Peter, japo ilikuwa ni moja ya vitu alivyopanga kuvinunua huku mjini, lakini kiukweli akuona kama anastahili kununuliwa simu kama ile na mwanadada huyu mrembo, kwa hakili yake ni kwamba, kama ni kutokana na msaada Peter aliona kuwa nguo na viatu, vilitosha kabisa, ila angeongezewa na elfu mbili na mia tano kama nauri ya kufikia namtumbo, kisha ange mbeba mwanae Michael na kutembea kwa miguu mpaka mwanamonga, ambapo angeitajika kutembea kwa mwendo wa kilomita zaidi ya sita, “alafu tumeongea na baba yako, aipiga kwenye simu yangu, nazani utampigia kwa simu yako, baada ya kuelekezwa namna ya kuitumia” alisema yaya Groly, ambae sauti yake ilikuwa imechangamka kidogo, tofauti na wale wengine, “kweli basi alicha soma messeji yangu, sasa atokuwa na wasi wasi” alisema Peter akionyesha kufurahishwa na taarifa ile, “ndiyo, ila wazazi wako ni wacheshi sana” alisema yaya Groly, ambae alianza kutembea kutoka nje huku akimsisitiza Peter kuvaa kama alivyo agizwa na Careen.****
Naam kijana Hussein au dogo Janja, baada ya kumwacha shemeji yake Queen pale mtini pub, alianza kwa kutembelea baadhi ya vijiwe vyao vya kuuzia dawa haramu za kulevya, kama vile bangi, milungi, cocein na mengine mengi ambayo ni kati ya biashara zao za kila siku ukiachilia, kazi nyingine walizo kuwa wanazifanya kamavile wizi, ukabaji, utaperi na ujambazi wakuvamia na kuvunja majumba na maduka yawatu.
Lakini kijana Janja wakati anaendelea kuzunguka na kukagua vijiwe vyako vya biashara, kazi ambayo mala nyingi uifanya Emma, pia alikuwa anaendelea kumtafuta kijana aliewashikisha adabu jana usiku, pale Makimakuluga Motel, huku kila anapopita akiwa anatoa kazi kwa vijana wake, kwamba wamsaidie kumtafuta bwana Peter, ambae siyo yeye Janja peke yake alie mwona, pia kuna baadhi ya vijana aliokuwa nao asubuhi, pale Makimakuluga, nao walimwona, wakati ule anadaiwa fedha, lakini maka mida ya saa mili kasoro, bado akuwa amemwona, wala kupata habari kumhusu, ndipo janja alipo amua kurudi nyumbani kwa Emma, kwenda kumweleza juu ya matokeo ya msako.
Janjaa alipofika pale nyumbani kwa Emma alimku Emma na mpenzi wake Sada, ambae wanamwita Queen, wakiwa wanaendelea kupata bia zao taratibu, huku wakiwa wameshaanza kulewa, walikuwa wanaongea na kucheka kwa furaha, usinge hisi kuwa asubuhi Sada alishushiwa kipigo cha mbwa mwizi, labda nizile ngeu usoni kwa Queen, ata hivyo ukimtazama Emma ungesema pengine walipata hajari au walivamiwa na wezi, “niambie Janja, kuna lolote?” aliuliza Emma, ambae alikuwa amekaa kwenye kitanda akiegemea pillow, lililoegemeshewa ukutani, “mambo yanaenda fresh bro, vijiwe vyote vinapiga kazi, na wajasumbuliwa na mtu yoyote, ila kuhusu yule fala, mpaka sasa ni giza tu” alisema Janja, akimaanisha kuwa akuwa amepata lolote juu ya Peter, “atakuwa amejichimbia wapi huyu mshenzi, ulijaribu kumfwatilia nyumbani kwa Careen?” aliuliza Emma kwasauti ilionyesha dalili za hasira, huku Sada ambae alisha juwa wanamzungumzia nani, akiwa anawasikiliza, “mh! awezi kuwa nyumbani kwa Careen, siunajuwa yule mwanamke nyumbani kwake awaingii wabongo” alisema Janja, na hapo Sada moyo wake ukashtuka kwa mshangao, “kwanini mnasema hivyo?” aliuliza kwasauti iliyo jaa mshtuko wamshangao, “watu wa Careen ndio waliomlipia pale Makimaluga, kisha wakaondoka nae” alisema Janja, na hapo Emma alionekana kukumbuka jambo, “alafu Queen siulisema umemwona jioni hii?” aliuliza Emma huku akimtazama Sada.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!