
SEASON 2: KIAPO CHA MASIKINI (38)

SEHEMU YA 38
ILIPOISHIA SEHEMU YA THERATINI NA SABA: huku Sada ambae alisha juwa wanamzungumzia nani, akiwa anawasikiliza, “mh! awezi kuwa nyumbani kwa Careen, siunajuwa yule mwanamke nyumbani kwake awaingii wabongo” alisema Janja, na hapo Sada moyo wake ukashtuka kwa mshangao, “kwanini mnasema hivyo?” aliuliza kwasauti iliyo jaa mshtuko wamshangao, “watu wa Careen ndio waliomlipia pale Makimaluga, kisha wakaondoka nae” alisema Janja, na hapo Emma alionekana kukumbuka jambo, “alafu Queen siulisema umemwona jioni hii?” aliuliza Emma huku akimtazama Sada. Endelea…
Hapo Sada alishtuka alitabasamu kidogo, kwakuona kuwa hiyo ndiyo nafsi nzuri kwake kushilikishwa kwenye mambo ya wawili awaa, kiu ambacho aliona kuwa kitamwongezea upendo na kuaminiwa na Emma, “ndiyo nili mwona, yani shem pale uliponia chatu, na yeye huyu hapa, tena alikuwa peke yake, alikuwa amevaa nguo zile zile nilizo mwachia jana, aonyeshi dalili ya kuwa kwa Careen” alisema Sada akionyesha kuwa na uhakika kwa hasilimia mia moja, nilivyo mwona inaonyesha amekosa ata nauri, ndio maana aliwapigia simu wazazi wake waje kumchukuwa” alisema Sada ambae akujiuliza kwanini Peter hakuwa na Michael, “kwahiyo atakuwa anatanga tanga tu, unaonaje ukitoka hapa upitie mtini Pub ukamcheki?” alisema Emma akimweleza Janja, ambae akukaa muda mrefu sana akaondoka zake akitumia gari lile dogo aina ya Toyota Ist, ambalo walipewa na boss wao bwana Pitus Kalonga, kwaajili ya miznguko yao ya kikazi, akiwaacha Emma na Sada wakiwandelea kulewa.**
Yap! saa mbili kamili ya usiku, ndani ya jumba kubwa la kifahari, la mwanadada wadhahabu, upande wa nyuma wa nyumba ile, yani kwenye garden palikuwa ni tulivu sana, lililokuwa na wat wachache sana, ukiachilia mbali sauti ya music laini, na washana watatu, waliokuwa wamevalia nguo nyepesi, pia za maua maua, waliosimama pembeni ya meza kubwa yenye vyakula na vinywaji vya aina mbali, huku idadi kubwa ikiwa ni chupa za #mbogo_land coco wine, huku pembeni yake kukiwa na viti vitatu, huku kimoja kikiwa kimekaliwa na Peter, kingine Michael na kimoja kilikuwa wazi, Peter na mwanae Michael walionekana kupendeza kwa mavazi mapya, waliyokuwa wamevalia usiku ule, ukiachilia truck suit na tishet kwa Michael, pia Peter alikuwa amevalia bukta moja nyepesi, nyeupe na tisht jeupe lililokaa vyema kwenye mwili wake uliozowea kupambana na majari na visiki huko mashambani, na kuimiliki stearing ya baiskeri, miguuni alivalia sendo nyeupe, hakika ungekuwaona kwa kwa ghafla usingweza kuwatambua kwa jinsi walivyo badirika, na sasa wawili awa walikuwa wanapata vinywaji taratibu huku wakimsubiri mwenyeji wao, ambae bado alikuwa ajatoka ndani, wakati Peter alikuwa anakunywa wine ya nazi, toka Mbogo land, huku Michael alikuwa anapata juice ya dhabibu za kijani toka mbogo land, labda unaweza kushangaa kuona Peter ameamua kunywa kilevi ugenini, tena kabla mwenyeji wake ajafika.
Ukweli ulikuwa hivi, mala tu badaa ya kukaa pale mezani, wale waschana waliovalia magauni mepesi ya naua maua, walisogea na kuanza kuwa hudumia bila kuuliza, niwazi walifanya walicho elekezwa, mwanzo Peter alizania kuwa ile Juice, au soda flani, lakjni alipo ionja, aligundua kuwa licha yakuwa na radha flani ya utamu, lakini mwishoni ilikuwa ni chungu, ikiwa ni kiashilio cha Pombe, nikweli Peter alikuwa anakunywa pombe moja moja kule kijijini, lakini akuona vizuri kunywa pombe ugenini, sasa atafanyaje na amesha wekewa, hivyo akaona bora anywe hivyo hivyo, lakini kwa speed ndogo, huku anachezea simu yake, ambayo alisha pewa somo dogo la kupiga na kupokea, sambamba na maongezi yaliyojaa maswali ya kitoto, kati yake yeye na mwanae Michael, kama “vile baba hizi nguo amaetununulia shangazi mzuri mzuri?”.
Naam wakiwa wanaendelea kusubiri pale bustanini, huku wakitazama bwawa kubwa la kuogelea na bembea nzuri za kisasa, zilizo zungukwa na viunga vizuri ya bustani za maua, na vijitanda vidogo vidogo pembeni yta bwawa ilo, huku simu yake ikiWakaalionekana mwanadada Careen, akitoka nje ya jumba lake la kifahali na kuibuka uande wa Garden, akiwa amevalia gauni jeupe jepesi pana, miguuni akiwa amevalia viatu vya chini, yani sendo nazo nyeupe, kichwani aliwa amefunga nywele zake na kijibanio cheupe, hakika pasinge kuwa na mwanga hafifu wa taa zarangi rangi, basi tungeweza kujionea rangi ya nguo za ndani za mschana huyu, ambae toka amezaliwa akuwai kuuanika mwili wake kwa mwanaume yoyote, akija kwa mwendo wa taratibu, uso wake ukiwa mtulivu uliojawa na aibu, “poleni kwa kuwaacha peke yenu” ilikuwa ni sauti tulivu na tamu ya mwana dada Careen ambae alikuwa anakaa kwenye kiti cha upande wapili wa meza, akitazama na Peter, ambae kiukweli mwili wake ulikuwa unasisimka, kwa uzuri wa mwanamke huyu, ambae akujaribu kuwaza kuwa anaweza kuwa wakwake siku moja, kuwaza hivyo aliona atakuwa kama, mbwa anae tamani kukwea mtini.
Hapo hapo wafanyakazi wakasogea mezani na kuanza kuandaa chakula, na kumimina vinywaji zaidi kwenye grass, “samahani yanini dada Careen, mbona sisi atujakaa sana hapa” alisema Peter, kwa uchangamfu, hapo Careen akatabasamu kidogo, huku anachukuwa grass ya wine, “sawa lakini pengine Michael alikuwa anakuchangamsha” alisema Careen huku tabasamu pana lakuvutia, likiwa bado limeutawala uso angavu wenye nuru kama mbalamwezi, ya kiangazi, wa mdada huyu, “nimtundu sana Michael, tukiwa nyumbani utazani tupo kumi” alisema Peter na wote wakacheka, wakati Peter akicheka kwanguvu, Careen yeye alicheka kidogo sana, na kubakia akiwa anatabasamu, huku Michael yeye akiunga kicheko cha kitoto.
Kitendo cha Careen kucheka kidogo, kilimshangaza kidogo Peter, ambae sasa nikama alisha anza kufahamu, mwenyeji wake ni mtu wa aina gani, “nimeambiwa na yaya Groly, amesema leo amecheza sana, pia nime mletea vifaa vya kuchezea” alisema Careen akimtazama mtoto Michael, “asante sana, dada Careen sijuwi nikulipe nini kwa aya unayo nifanyia” alisema Peter kwa sauti ambayo kiukweli niwazi ilitokea ndani ya moyo, yani mfano wake, niile wanayo sema shukrani za dhati zimwendee flani, “usijari Peter, nyie ni watu muhimu sana kwangu, na ata ulicho kifanya kwangu, ni kikubwa sana, sidhani kama ninauwezo wakukulipa” alisema Careen huku akitabasamu, “lakini sikufanya kama deni, hivyo sistahili kulipwa” alisema Peter huku nayeye akijichekesha kidogo, hapo Careen alitulia kidogo akitabamu, huku wale wanawake wawili wakiendelea kuandaa vyakula, “lakini huo ni moyo wako, ila kwa moyo wangu, nina deni kubwa sana binafsi, naitaji kufanya kitu, ambacho moyo wangu utatulia” alisema Careen, kwasauti tulivu kama kawaida yake.***
Yap, twende Angon amrs hotel, mita chache toka nyumbani kwa Careen, ne ya hotel ile walio onekana watu wachache, wakiwa kwenye meza zao, tena meza moja unge kuta watu wawili yani wakike na wakiume, au mmoja, wakiendelea kupata vnywaji, siyo kwamba watu hawakuwa na fedha, hapana, swala nikwamba sehemu hii ni tulivu sana, na kamaujuwavyo walevi wa kingoni, upenda kulewa sehemu yenye kuchangamka, na wanawake wengi sana, siunajuwa hasiri yao, wakisha lewa uanza kuimba na kucheza, japo siyo kwenye bar za pombe za kizungu.
Tuachane na awawaliokaa nje, twende ndani ya vibanda vidogo vilivyo jengwa kwa namna ya kuvutia pale, kwenye viunga vya ile hotel kubwa ya kihistoria, na ndani ya kibanda kimoja wapo tuna wakuta watu wawili tofauti na wale waliokaa nje, mwanamke na mwanaume, awalikuwa ni wanaume wawili ambao walikaa kwa kutazama, juu ya viti vyao, wakitenganiswa na meza ndogo iliyo beba chupa kubwa ya #mbogo_land Queen Gin, na grass mbili zenye pombe ndani yake hii kali, toka nchi ya jilani, huku sigara zilizoshikiliwa kwenye vidole yao zikiendelea kufuka moshi, na kukijaza chumba kile, “kwahiyo bwana Kalo unasema kuwa mpango wako hivyo ndivyo ulivyo aribika?” iliuliza mmoja kati ya wale jamaa wawili, alie valia kofia ya duara kichwani mwake, “yani kaka nashindwa ata kuelekwa, hii ni mala ya pili, hapa nacho itaji nikumtia nguvuni, ilinimfundishe adabu” alisema huyu mwingine ambae kwa mwanga afifu uliokuwepo mle ndani ingekuwa vigumu kumtambua, ila sauti yake tunaitambua kuwa ni sauti ya bwana Pitus Kalonga, “kwahiyo umesha pajuwa anapo patikana huyo mpuuzi, ilituweze kumpatia kesi na kumtianguvuni, ili uweze kumchukuwa na kwenda kummaliza?” aliuliza yule mwingine, ambae katika mkasa wetu ndio anaonekana kwa mala ya kwanza, “bado sijajuwa, ila inasemekana nikijana toka shamba, uwa anaonekana kwa msimu, kama bado yupo hapa mijini, naamini tuta mpata tu” alisema Kalonga, kisha akachukuwa grass yake na kuipeleka mdomoni, akipiga funda moja kavu na kuirudisha mezani, kisha akazimulia kwa funda jingine la moshi wa sigara, kisha akaupuliza na kufanya kama gari moshi la henzi za vita ya pili ya dunia, “ok! kama utaiji msaada utanijulisha” alisema yule jamaa, ambae alionekana kuwa na wadhfa flani, katika serikali, “nakuaminia kaka, ila sasa nilicho kuitia hapa, nikwamba, kunamzigo naitaji kuingiza sokoni, nimzigo kubwa sana wa bangi” alisema Kalonga, huku wakiendelea kunywa pombe yao kali na kushushia sigara, “ok! sasa uliitaji msaada gani kwangu?” aliuliza yule jamaa, huku mdomo wake unafuka moshi kama jiko la kuokea mikate, “mpango nilio ufikilia, ni kwamba tutumie gari la polisi, maana mzigo nikama gunia hamsini, wewe toa gari la polisi, na askari wanne, mimi nitatoa mafuta na posho kwa askari wako” alisema Kalonga na yule jamaa ambae sasa naanza kupata picha kuwa, ni mkubwa flani wa jeshi la polisi, akaitikia kwa kichwa kukubaliana na Kalonga, “kwani mzigo wenyewe hupo wapi?” aliuliza yule jamaa,
mzigo bado hupo Linjumbwi, ndio unavinwa” alisema Kalonga, “akuna shida cha msingi waandae magunia kama kumi ya mkaa, ili yakae mwanzoni, na ukiwa tayari utanishtua” alisema yule jamaa, huku wakiendelea kupata kinywaji.
Huyu jamaa anaitwa Alphonce Clemnt Mwanauta, ni OCD wa songea mjini, akiwa na cheo cha ASP, kilicho tambulishwa na nyota zake tatu mabegani…..

