SEASON 2: KIAPO CHA MASIKINI (40)

SEHEMU YA 40

ILIPOISHIA SEHEMU YA THERATHINI NA TISA: kisha akamtazama tena Peter, huku analaza kinja chake cha mkono pale alipoguswa na Peter, na kufanya kama anaupapasa taratibu, mkono wake huo ambao ndio alioshikia ile juice, huku Peter nae aliekuwa anafinyanga kinganja chake kile cha mkono mfano wa mtu anae viliga chakula, akimtazama mschana huyu, na kufanya macho yao yakutane tena, wote waka tabasamuliana, “shangazi inamwagikaaa” alipiga kelele Michael, na hapo ndipo Careen na Peter, kwa pamoja waka tazama ile grass ya Michael………..Endelea…
Nakuona kuwa ni kweli ilisha jaa, na kuanza kumwagika, hapo Careen akatoa mkono wake haraka, na kwabahati mbaya akatikisa meza na kusabisha bakuli la kioo lililoja lost ya maini, na sahani ya chakula cha Careen mwenyewe, kuseleleka (kuteleza) kuelekea kwa mwanadada wa dhahabu ambae akuuweza kudanya lolote na kusubiri matokeo, yakile ambacho kinaenda kutokea, lakini fumba na kufumbua, tayari Peter alisha daka sahani na bakuri lile kubwa la kioo, akizuwia visiende kwa madada wa dhahabu, ambae alitoa macho kwa mshangao, “hoooo! asante sana Peter, hakika upaswi kukaambali na mimi” aliongea Careen kwa sauti iliyojaa asante toka moyoni, sambamba na tabasammu la kivutia.**
Yap kijijini mambo yakuwa bam bam, tayari nyumbani kwa mzee Jacob, palisha ongezeka wageni wengine kadhaa ambao nikama walikuwa wanapita njia, lakini walipoona kuna watu pale nje wanaendelea na kinywaji, nawao wakaenda na kujiunga, uzuri wa msimu huu wa malipo, ni wachache kama wakina mzee Nyoni ndio wenye kudowea pombe za watu, ila kikawaida, kila mmoja alikuwa na pombe zake, kama siyo bia basi ni ulanzi, maana lisha ya kuwa na fedha nyingi, lakini baadhi ya watu awakuweza kunywa bia, maana wangeweza kutapika mpaka nyongo, kutokana na kuto kuizowea.
Kila aliekuja kwa mzee Jacob, aliitaji kufahamu habari za Peter na Michael, maana tayari walisha pata dindoo ya kile kilichowapeleka mjini wazee awa, yani mzee Jacob na mke wake, niwazi walishapata taarifa za hawari ambazo zilisambazwa kwa hisani ya mama na baba Sada, yani mzee Nyoni na mke wake, “ni wasi wasi wetu, kumbe Peter yupo vizuri tu huko mjini” ilo ndilo lilikuwa jibu la mama Peter, na wale wageni ambao ni wenzao wakila siku, wange jikuta wanafunguka ukweli wa chanzo cha habari, “sasa mbona, mzee nyoni na mke wake wanasema kijana wenu amekutwa na mabalaha huko mjini?” ndivyo ambavyo mmoja wao angeuliza, na hapo mzee Ponera angeanzisha kicheko huku anajibu, “tume ongea na Michael sasa hivi, anasema kuwa wapo sehemu nzuri wanafaidi, na tena alipopewa simu alikuwa ghorofani” na hapo wakina mzee Ngongi na Jacob na mama Peter wangejiunga nae kucheka, huku mama Peter akiongezea neno, “nivyema mkimwambia akamtazame binti yake jinsi anavyo ishi huko mjini, na siyo kueneza habari asizo zijuwa” hapo wageni wal wange tazamana kwamacho ya viulizo, kabla awaja funga midomo yao, na kuendelea na unywaji wa pombe zao, huku wakiimba ule wimbo wao, wa tiuka lepa, mpaka timale ugimbi (tunaondoka hapa mpaka tukaimaliza pombe).****
Naam saa tatu iliwakuta Peter Careen na Michael wakiwa wamesha maliza kula na wafanyakazi wamesha ondoa vyombo pamoja na kumpeleka Michael chumbani kwake, wakibakia Peter na Careen wakiendelea kupata wine taratibu, na maongezi ya kuviziana, na waisha chamka kwa wine iliyotawala vichwani mwao, “hivi Peter uliwai kupenda mwanamke mwingine zaidi ya mama yake Michael” aliuliza Careen ambae kwawanao mfahamu leo ndio alikuwa amechangamka sana, “hapana sikuwai Sada nilimpenda sana” alijibu Peter, kwa sauti iliyopoa, huku jibu ilo likimshtua Careen, “lakini bado unampenda siyo” aliuliza tena Careen, huku anamtazama Peter kusikia atajibu nini, “mh! kwa maneno aliyo yaongea na kiapo alicho kitoa, sidhani kama moyo wangu naweza kumpenda ata kidogo” alisema Peter kwa sauti ambayo ilijaa machungu mengi, “hoooo! lakini moyo wako, si unaweza kumpenda mwanamke mwingine kwa sasa, siyo?” aliuliza Careen huku wakiendelea kupata kinywaji chao, ambacho kilikuwa kinaendelea kuwachangamsha, “ukweli moyo auwezi kuacha kupenda, aijalishi nini kimetokea hapo kabla, swala ni vipi kuhusu unae mpenda na yeye atakupenda, au atakuwa kama yule yule?” alisema Peter ambae sasa alisha pata uwezo wakuongea kwa kujiachia, maana kilevi kilisha panda vya kutosha, “nivyema kama utakuwa muwazi kwa unae mpenda, aijalishi amewakatalia wangapi pengine chaguo lake likawa ni wewe” alisema Careen kwa sauti flani ya kuvutia huku akimaliza kwa kicheko cha taratibu.
Hapo Peter ambae simu yake mpya ikiwa mezani, huku kila muda ulivyo zidi, kuona uzuri wa mwanamke huyu, ambao ni nikama ilikuwa unaongezeka kila dakika, akasema “kama ni hivyo basi ukweli aujawai kunisaidia kwenye mausiano, nilijieleza vizuri kwa Sada nabado akasema ni afadhari akilala na mbwa, kuliko kulala na mimi, bora afe kuliko kurudiana na mimi” safari hii Peter, aliongea kwa sauti iliyo changamka, kiasi chakumfanya mwenyeji wake ambae ni Careen ajikute anatabasamu, “lakini siyo lazima yeye, wanawake wapo wengi sana, tena wapo wengine kila mwanaume anasema ni wazuri, uwezi kuwaona wao?” aliuliza Careen, huku akimtazama Peter, ambae alicheka kidogo, labda na mimi niwe wa aina wanayo itaka, wanawake wanapenda mwanaume mwenye fedha nyingi zisizo za msimu” alifafanua Peter, huku anaichukuwa simu yake na kuibofya, kwa lengo la kutafuta sehemu ya kupigia.
Hapo careen amba bado akujuwa hisia za Peter zipo vipi juu yake akamtazama kijana huyu na kutafakari maneno yake, huku akiwaza kitu cha kumwuliza na alipo kipata aka mwuliza, “vipi kama huyo mwanamke mzuri, ana fedha zake mwenyewe?” Careen aliuliza huku anachukuwa chupa ya wine na kumimina kwenye grass, za wote wawili, “mh! mwanawake wenye fedha zao…..?” aliuliza Peter, na kusita kidogo, kisha akainua usowake na kumtazama Careen, ambae sasa alikuwa amesha maliza kumimina wine anamtazama pia, akionekana kusubiria kwa hamu jibu lake, “wamefanyaje, wanawake wenye fedha?” aliuliza Careen, kwa sauti tulivu pasipo tabasamu lolote, “sijawai kuwaza wala kufikilia juu ya ilo” alisema Peter, huku ana anaelekeza macho yake kwenye simu na kuendelea kuibofya bofya, kwa lengo lile lile la kupiga simu kwa baba yake, “vipi Peter unaitaji msaada wowote?” aliuliza Careen huku anatabasamu, akimaanisha kuwa pengine Peter anaitaji kuelekezwa jambo juu ya matumizi ya simu yake ile mpya, “ndiyo hii simu inanishida siioni sehemu ya kupigia” alisema Peter, huku anamkabidhi simu Careen ambae aliinuka na toka kwenye kiti alicho kuwa amekaa, huku Peter akimtazama mwana dada huyu, ambae alitembea taratibu kuzunguka ile meza, “ni lahisi tu, ebu nikufundishe, aisema Careen ambae sasa alikuwa amesha fika karibu na alipokuwa amekaa Peter na kukushika kiti cha Michael ambacho alikivutia, karibu na iti cha Peter, “unakuja hapa, alafu unagisa hapa, siunaona hizi namba?” alisema Careen huku anakaa kwenye kiti kile, na kusogeza simu karibu na Peter, kitendo ambacho kiliwafanya wawiawa wakaribiane zaidi, kiasi cha kila mmoja kusikia pumzi za mwenzie, “ebu taja namba za baba nimpigie” alisema Careen, na hapo Peter akaanza kutaja namba za simu za baba yake.
Naam hapo Careen akaanza kuziandika namba zile kwenye simu, huku akiwa ameisogeza simu karibu na Peter, ambae pia alikuwa ana chungulia kwa karibu ile simu, ilikona jinsi Careen alivyo kuwa anapyatila (gusa) kioo cha simu yake, kwa vidole vyake vizuri, akiandika namba alizokuwa anazitaja, na alipomaliza akabofya kialama cha kijani chenye mchoro wa mkonga wa simu…..……….

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!