SEASON 2: KIAPO CHA MASIKINI (51)

SEHEMU YA 51

ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI: sijuwi wamesha pata jibu” alisema Sada huku anatoa simu mfukoni na kuipokea mala moja, bila kuangalia jina la mpigaji wala namba yake, akizania kuwa ni simu ya mama Kachiki, “hallow niambie” alisema Sada, kwa kujiachia kweli kweli, “habari za leo Sada amjambo huko” ilisikika sauti ya kiume iliyo changamka kiasi, hapo kidogo Sada alishtuka maana sauti aikuwa ya baba yake, “nani wewe?” aliuliza Sada kwa ukali, mimi baba Peter, naomba kuongea na Peter” nikweli ile sauti ilikuwa ni ya mzee Jacob, yani baba kwe wake wazamani……..Endelea…
Sauti ambayo Sada asingweza kuisahau ata kidogo, “nani kakuambia nipo na Peter, sijuwi ata habari zake huyo mpuuzi, siumtafute unakokujuwa” alisema Sada kwa sauti ya ukali kweli kweli, ungesema anaongea na mtoto mdogo, au mtu asie ma maana kwake, “lakini mwanangu mbona simu yake huponayo wewe” hapo ndipo Sada alipogundua kosa alilo lifanya, na kukata simu mala moja, alafu akatazama ile simu na kuina namba iliyompigia imeifadhiwa kwa jina la baba, “vipi wanasemaje?” aliuliza Emma, ambae alikuwa amesimama karibu na mlango wakutokea nje, na ndoo yake mkononi, “ni baba yake Peter huyo, eti anataka nimweleze Peter yupo wapi” alisema Sada, kwa sauti flani hivi yenye uchangamfu wa kulazimisha, akutaka Emma nae agundue kosa alilolifanya, “kwahiyo na wao awajuwi huyu bwege yupo wapi” alisema Emma huku anatoka nje kuelekea bafuni, “dah! sijuwi kwanini sikujuwa mapema” aliwaza Sada, huku amesimama anakodole vitu ambavyo inabidi avipike.**
Naam watu watatu wanafamilia mpya, yani Peter Careen na Michael, walikuwa mezani wanaendelea kupata kifungua kinywa, ambacho kwa milo yetu sisi wazawa, ingefaa kuwa ni chakula cha siku ya sherehe kubwa, tena ya watu wenye uwezo mkubwa wakifedha, muda wote wa chakula ilikuwa watu walikuwa kimya, huku wakisemeshana mala moja moja, inapo bidi, mfano ungesekia, “Peter unaonaje chakula, au kuna kitu kimepungua?” angeuliza Careen huku anachukuwa sambusa, na toka kwenye bakuri kubwa na kuiweka kwenye sahani ya Peter, “chakula kitamu sana, nazani wewe umekipenda pia” angejibu Peter, nakuendelea kula kimya kimya, wakishindwa kuzamana usoni, asa kila mmoja wao akikumbuka mambo yao ya chumbani, maana wakati Careen anawaza jinsi alivyojianika mbele ya mwanakaka huyu jana usiku, na vile alivyo amka huku dudu ya mpenzi wake huyu, akiwa ime kita eneo la kinena chake, na vile alivyo chukua uamuzi wa kuigusa gusa dudu ya mpenzi wake huyo, ambayo ukiachilia kuwa ilikuwa imesimama kweli kweli, japo yeye akuwai kutoa nafasi kwa dudu yoyote kuingia kitumbuani kwake, lakini niwazi ilikuwa kubwa, hapo Careen ange jaribu kumtazama Peter, ambae pia alikuwa anageuka kumtazama yeye, na macho yao yangekutana na wote wange tabasamuliana huku wanakwepesha macho yao ya aibu, maana Peter nae kabla aja chukuwa uamuzi wakumtazama Careen alikuwa anakumbuka kinsi maongezi yao yalivyokuwa jana usiku, huku wakikubariana kuwa penzi kighafla ghafla ghafla, na usiku huo huo kuweza kuuona mwili mwanana wa mschana huyo mrembo kuliko urembo wenyewe, na jinsi alivyo mwona asubuhi akimchungulia maungo yake na kuyagusa gusa, hapo ndipo alipoamua kumtazama huyo mwanamke ambae alifanya kituko hicho maa akuwa anafanania atakidogo, yani kwakifupi yeye Peter alijiona kwamba akustahili kufanyiwa yale yote, na mwanadada mrembo kama yule, basi hapo Careen ange jizugisha kwa kumwongelesha Michael, “Michael vipi chakula umekipenda?” angesema Careen huku, ana chezea nywele za Michael, ambae aliitikia kwa kichwa huku macho yakiwa kwenye TV, “aya kula basi huku unatazama TV” alisema Careen huku anachukuwa kijiko na kuchota rost ya maini kwenye bakuri kubwa la kioo, na kumwekea Michael kwenye sahani yake.
Naam wakati wakiwa wanaendelea kula kwa mtindo huo mala wakasikia simu inaita toka kwa mmoja wa waschana waliokuwa wamesimama pembeni, yani wahudumu, siyo Careen tu ata Peter mwenyewe akujuwa kama inayoita ni simu yake, maana alishasahau kama anasimu, nitokea jana usiku akuwa ameishika tena ile simu, “mimi ni mfanyakazi ndani ya nyumba ya dada Careen bwana Peter yupo mezani anakula, atakupigia baada ya kumaliza kula” alisikika mhudumu alie ongea kwa sauti iliyojhaa nidhamu ya hali ya juu, na hapo ndipo Peter na Careen waliposhtuka “hoooo! hapana, mwache aongee” alisema Careen ambae kikawaida meweka utaratibu wa kuto kupokea simu wakati wakula, ata kama ni yakazi au inatoka kwa wazazi wake, au mfalme wa nchi yao ambae ni rafiki yake wa utotoni, yani king Elvis wa kwanza, “kwani hiyo simu ni yakwangu, nani amepiga?” aliuliza Peter huku anainuka kuifwata simu, lakini Careen akamzuwia, “Peter upaswi kufwata simu, yeye ndie anaepaswa kukuletea” alisema Careen kwa sauti tulivu na yataratibu, na Peter akatulia kwente kiti, huku anamtazama yule mwanamke mhudumu, akileta simu, “lakini naona imekatika” alisema yule mwanamke, huku ananyoosha mkono kumpatia Peter simu, lakini Careen ndie alie wai kuichukuwa, na kutazama namba ya mpigaji, maana alisha sahau kuwa ndani ya simu ile kulikuwa na namba moja tu, ambayo ni ya baba yake Peter, na ndie mtu mwingine anae ijuwa namba ile, zaidi ya yeye mwenywe Careen, “hooo nibaba alipiga, tunaweza kumpigia tena” alisema Careen huku anapiga tena ile namba yam zee Jacob, ambayo ilisema kuwa aipatikani, “atakuwa amekasirika mbona amezima simu” alisema Careen kwa sauti yenye udhuni, “hapana nazani simu yake imesisha chaji” alisema Peter, wakati huo Michael anatazama TV ambayo walimwekea chanel ya cartoon, “kwanini muda mwingi simu ya baba yako inazima chaji, ni mbovu au?” aliuliza Careen huku anaweka ile simu ya Peter, juu ya meza karibu kabisa na alipokaa Peter mwenyewe, “hapana kule kwetu umeme hakuna na mzee bado ajaweka Solar, hivyo kuchaji mpaka aipeleke madukani” alisema Peter, huku anaendelea kula, “hoo hivyo nyumbani hakuna Solar” aliuliza Careen, “mafundi wapo, ata mimi mwenyewe kama nisinge ibiwa fedha zangu, nilitaka ninunue Solar” alisema Peter, na hapo Careen akaweka kiganja cha mkono wake mgongo kwa Peter, “usijari tuta nunua Solar kwaajili ya baba na mama” alisema Careen, na Peter akajuwa kuwa Solar inayo ngumziwa ni zile solar ndogo ndogo, akujuwa anacho kifikilia Careen kichwani mwake.***
Siyo kwamba mzee Jacob ndie alie piga simu, simu ilipigwa na mama Peter yani mke wa mzee Jacob, ni baada ya mzee Jacob kutoka kuongea na Sada, ambae alimkatia simu, huku akiwa amemjibu kwa dharau, “ni upuuzi sana huu, yani awa watoto wamekuwa jinga sana, ni tabagani hii, na huyu Peter anawezaje kumpatia simu huyu mtoto alie shindikana, alafu wanatuganganya kuwa imeibiwa, alafu ananijibu kama mimi mtoto mwenzie” alisema mzee Jacob alie onyesha kukasilika sana, huku akiweka simu juu ya kigoda, “baba Peter, uenda ni kweli huyu binti ameiba simu ya Peter, ebu piga kwenye ile namba ya jana, sialisema ni yakwake” alisema mama Peter, ambae sasa alikuwa anamilizia kunawa ili na yeye aanze kuifakamia supu ya kuku, “sipigi simu popote pale, nimesha choka na huu upuuzi wake” alisema mzee Jacob, huku anachukuwa bakuri lake la supu, “wacha kwanza nimpigie ili atuambie ukweli” alisema mama Peter, huku anajifuta mikono yake na kuchukuwa simu iliyokuwa juu ya kigoda na kuipiga ile namba ambayo sasa ilikuwa ni ya pili toka mwanzo, simu iliita kidogo sana ika pokelewa.
Hapo mzee Jacob akamwona mke wake akiwa ame tulia kimya akisilikiza alicho ambiwa, kisha akaonekana kushtuka wkanguvu sana, kiasi cha simu kumponyika na kuingia kwenye sufuria ya maji ya kunawa, “mamaa, simu ileee” alipiga kelele mama Peter, huku anaiwai simu toka kwenye sufuria lile, huku ikiwa imesha zima, “vipi kwani mbona kama umeshtuka sana?” aliuliza mzee Jacob huku anachukuwa simu toka kwa mke wake na kuitazama vizuri, nikweli ilisha zima, “eti amepokea mwanamke anasema yeye nifanyakazi kwa Careen, anasema eti Peter yupo mezani anakula atapiga baada ya kumaliza kula” alisema mama Peter, “siunaona huuni huo, usinge mpigia simu yangu singe haribika” alilalamika mzee Jacob, huku anafunua kizibo cha simu na kutoa betri, “lakini baba Peter, nimesikia sauti ya mwanamke mwingine anasema lete hiyo simu, aongee, tena ameongea kwa ukali sana, nazani ni yule mwanamke wajana usiku” alisema mama Jacob, ambae nikama alishikwa na sinto fahamu…..
MWISHO SEASON TWO..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!