
SEHEMU YA 45
ILIPOISHIA SEHEMU YA 44: “lazima nirudi, ili nikuletee chakula, ila usiondoke hapa” alisema Edgar, na Monalisa akaitikia kwa kichwa, lakini nikama machozi yalisha anza kumlenga lenga, huku Edgar akiinuka na kuelekea kwenye kambai la muda la polisi, kwenda kufwata chakula, na wakati huo huo waka ona msafara mdogo wa magari una elekea mjini, endelea……….
Edgar alisimama kidogo na kuya tazama mpaka yalipo potelea upande wa mjini, yalikuwa magari sita mchanganyiko, yani land rover mia nakumi ma tatu na toyota land crucer tatu, yakiwa na akasri kama wawili kila gari, Edgar akatazama kule alikokusudia kuelekea, aka ona bado pilika zina endelea, lakini akukuwa na mwonekano wa kuwepo kwa walinzi, hivyo akaanza kutembea kwa tahadhari akizungukia upande wa nyuma ya eneo la polisi, ambako ndiko kulikuwa na nyasi nyingi sana, akimwacha Moalisa kwenye kichaka akimsindikza kwa macho, mpaka alipo tokomea kwenye kichaka na giza nene.
Monalisa akiwa amechuchumaa, huku ameshikilia SMG, akatazama kushoto na kulia, kote kulikuwa ni vichaka na giza, hivyo akatulia kimya kabisa, macho akayaelekeza kule kwenye kambi la muda la polisi.**
Baada ya maongezi mawili matatu ya kupena moyo, na kuondoana wasi wasi, juu ya mgonjwa, huku Isaya akipiga mahesabu na mna ya kumwondoa mle ndani, mke wa Mapombeka, iliyeye afanye kazi yake, aliyotumwa na Kingarame,
“dada nazani ungeenda kumwelea yule doctor, kuwa nataka ni mhage, mana ninataka niondoke” alisema Isaya, kwa sauti ambayo iilionyesha kuwa amechoka sana, akimalizia na muhayo wa uchovu, “ni kweli kaka, wacha nika mwite ili umuage, ukapumzike” alisema mke wa Mapombeka huku anainuka toka kwenye kitanda alichokuwa amekaa, jilani kabisa na kijana mpole mwenye moyo wa ubina damu Isaya, ambae amejitolea kuja Hospital kumtazama mume wake,
Isaya alimtazama mke wa mapombeka, alie tembea taratibu, huku tumbo likiwa limetangulia mbele, akielekea kwenye mlango wa kutokea nje ya hile ward, Isaya aka ingiza mkono wake ndani ya mfuko wa koti la suit, huku macho yake yakiwa mlangoni, yana mtazama mke wa Mapombeka, alie kuwa ana potelea nje ya ward hile,
Yani ile anaptea tu! Isaya akainuka toka pale alipo kaa, huku mkono wake ukiibuliwa toka mfukoni, na bomba la sindano na kichupa kidogo cha dawa, hapo haraka sana aka chana lile kasha la bomba la sindano ambalo liliambatanishwa na sindano yenyewe, akaziunganisha na kuichoma kwenye kifuniko cha ile chupa, kisha aka nyonya ile dawa yote iliyo kuwa ndani ya ile chupa, kisha aka ikamata drip na kusogeza sindano iliachome.
lakini kabla haja choma, “vipi naoma matibabu yanaendele” ilikuwa sauti yakiume, iliyo mstua sana Isaya, ambae alistuka wazi wazi na kutazama ilikotokea ile sauti, yani kwenye mlango wa kuingilia, mle wardini.
Naam macho yake yakakutana uso kwa uso na kijana mmoja mdogo, kwa umri, alie valia mavazi ya kijeshi, na cheo cha ukanali, kikionekana mabegani mwake.
Huyu alikuwa ni kanal Joseph Kisona mutu mbaya, ambae aliingia hapa dakika chache zilizopita, akiwa na wenzake, yani baba Edgar koplo Katembo na wale askari wanne, wa jeshi la ulinzi, “nisubirini hapa nika waone mala moja, alafu tuondoke zetu” alisema Kisona huku ana iweka bunduki yake kwenye seat na kushuka, toka kwenye gari, kisha akaelekea kwenye mlango wa kuingilia kwenye jengo la hospital, ambalo usiku huu apakuwa na watu wengi, kwakifupi mahali pale alikuwa tulivu, “hoo! afande Kisona, naona umekuja kuwatazama wagonjwa wako” alisema doctor wazamu ambae wakati huo alikuwa anatokea kwenye lile jengo, “ndiyo bwana siunajuwa kuwa hao ni watu muhimu sana kwetu, ili kupata ushaidi” alisema Kisona wakiwa wame simama na yule doctor, “tena kuna watu wame kuja kuwatembelea wagonjwa” alisema doctor, na hapo nywele za utosini za Kisona, zika sisimka, “watu gani hao?” aliuliza Kisona, kwa sauti ya mashaka, na doctor akaeleza kama alivyo elezwa, zaidi alieleza kuwa, “nikijana mstaharabu, amevalia suit yake nzuri tu!” lakini maelezo hayo haya umfanya Kisona kuondokewa na mashaka, “ok! doctor wacha nika waone mala moja, kisha niende Njombe nika pumzike” alisema Kisona, huku anaanza ktembea kuelekea ndani ya jengo la hospital, akimwacha doctor anaelekea aliko kujuwa yeye.
Lakini Kisona akufika mbali, akamwona mwanamke mjamzito, akija usawa wake, “samahani kaka, umemwona doctor huko nje?” aliulizamwana dada huyu, baada ya kusalimiana na Kisona, “yupo hapo nje, vipi unaitaji msaada?” aliuliza Kisona kama vile alitaka kufahamu kitu kwa dada huyu, “kaka yangu anataka kuaga ili akapumzike” alisema yule dada, huku anaanza kutembea kuelekea nje, hapo kisona akusubiri kuambiwa mala mbili, nikama hakiri ilimtuma kuwa kule ndani, waliko lazwa askari majeluhi.
Nandipo alipo mkuta Isaya ana ana taka kuchoma sindano kwenye drip ya Mapombeka, “vipi naoma matibabu yanaendelea” ilikuwa sauti yakiume, iliyo mstua sana Isaya, ambae alistuka wazi wazi na kutazama ilikotokea ile sauti, yani kwenye mlango wa kuingilia, mle wardini.
Naam macho yake yakakutana uso kwa uso na kijana mmoja mdogo, kwa umri, alie valia mavazi ya kijeshi, na cheo cha ukanali, kikionekana mabegani mwake, Isaya alisha mtambua huyu jamaa, kuwa ni kanal Kisona, hapo akajuwa mchezo ulisha ungua, aka tazama kushoto na kulia, akuona pa kutokea, zaidi ya pale alipo simama Kisona, ambae alisha ona wasi wasi wa kijana huyu, alie utilia mashaka ujio wake, na kiukweli hakuwa doctor wa hospital hii, sababu waganga wazamu uwa katika mavazi ya kijeshi, kisona aka mtazama Isaya huku anatabasamu, akijuwa kuwa amesha mpata.
Lakini ghafla akamwona ana mjia mbio mbio na bomba la sindano mkononi, ameliinua tayri mdunga, lakini kama uliwai kumskia Kisona, una weza kupata picha ya kilicho tokea, maana kamanda huyu ali nesa kidogo, kama anaangukia nyuma, na kumfanya Isaya apitishe sindano hewani, huku akipokea ngumi moja nzito iliyo tuwa shavuni kwake nakumpeleka kwenye kingo ya flem ya mlango, huku kiongezewa teke languvu, kwenye chemba ya moyo, lililo mrudisha ndani ya ward, akifikia kujibwaga chini kama kifurushi, huku ile sindano ikimtoka mkononi na kusambaa mapaka uvunguni mwa kitanda kimoja wapo cha wagonjwa, ile Isaya ana inuka haraka haraka, akakutana na teke la usoni, lililo veshwa buti la kijeshi, lililo mrudisha chini na kujibamiza kisogo, Isaya alihisi kitu kama kizungu zungu flani, na wakati aja kaa sawa, kisona alimdaka na kumwinua na ku sogeza ukutani akim,bamiza kwa nguvu, na kumkandamizia ukutani pale, “nani ame kutuma?” aliuliza Kisona kwa sauti yachini iliyo jaa hasira, lakini Isaya hakujibu kitu, zaidi alijitaidi kujipapatua toka kwenye mikono ya Kisona,
Isaya aka waza hraka haraka na kufikiri kuwa endapo ata mtandika ngumi moja tu Kisona, ana weza kumwachia na yeye akapata nafasi ya kuondoka mahali hapa, ambapo kwa sasa alipaona padogo, nikama Isaya alikuwa anahesabu, maana alitulia kidogo kisha akirusha ngumi mija mzito sana, kuelekea shavuni wa kisona, lakini kama vile Kisona alijuwa anacho kiwaza Isaya, maana ali mwachia Isaya, na kuikinga ile ngumi, kisha kitendo bila kuchelewa, kisona akiaachia ngumi mija matata iliyo tuwa kati kati ya kifua na tumbo, hapo nikama Isaya pumzi zilikata, ila kabla haja vuta pumzi, aka ona ngumi ya pili ikishuka pale pale, aka weka viganja vya mikono yake, na ngumi ya tatu ika tua juu ya viganja vya mikono yake, yani pale alipo zuwia, na kumtekenya vidole na chembe ya moyo, akajikuta anaahia mwenye, kwa maumivu makali aliyo yapata.
Kilicho fwatia hapo sasa, ni mvua ya ngumi, mfano wake ni sindano ya celeani, kwa kati ya ngumi mfululizo zilizo tua kifuani kwa Isaya, ambae alijihisi ana kosa nguvu, Isaya alitamani kusema kitu kwa Kisona, na kujikuta ata pumzi zina shindwa kutoka, mwisho akapata wazo, aka nyosha mkono mmoja juu akiomba poo! lakini jibu alilo pata, ata yeye akutegemea, “na juwa amekutuma Kingarame, auna faida kwangu” hapo kisona aliyasenma hayo huku anakikamata kichw cha kijana huyu, na kukipeleka upande wa kushoto kwanguvu, ikasikika sauti kama ya milio wa kijiti kikavu kinacho vunjika, kisha Isaya katulia, huku ametumbu macho, uhai umeacha mwili, Kisona aka kimbilia mlangoni na kumttazama kama mke wa apombeka anakuja, maana akutaka ajuwe kama kuna tukio kama lile lime tokea, akuona kitu, hapo Kisona aka msachi Isaya aka mkuta na kitambulisho cha polisi, aka kisoma na kukirudisha kmfukoni kwa Isaya, Kisha aka akarudi tena mlangoni.
Safari hii, aka waona doctor wa zamu na mke wa Mapombeka, wana kuja kule aliko kuwepo yeye, yani wardini, Kisona aka rudi kwenye mwili wa Isaya na kuishika miguu ya Isaya, alafu aka ukokota mwili wa kijana huyu, na kuuweka kwenye uvungu wa kitanda cha mwisho kabisa, “kaka doctor huyu hap…….” ilisikika sauti ya mke wa Mapombeka, alieshindwa kumalizia kauri yake, baafa ya kuona kaka yake hayupo, “hooo! shameji bwana Isaya ameona una chelewa na yeye ame amua kuondoka, kuna sehemu ana wai kidogo” alisema Kisona, ambae alisha juwa alicho kifanya, “hoo! sawa lakini ame ondoka mapema, sababu doctor mwenyewe nio huyu hapa” alisema mke wa Mapombeka, huku wote wawili wakimtazama doctor wa zamu, aliekuwa anasogelea kitanda kimoja cha pembeni ya kile alicho lala MAPOMBEKA, “afande hii chupa ume kujanayo?” aliuliza doctor huu akiichukuwa chupa ndogo ya dawa kitandani, “hapana kwani ni chupa ya nini hii?” aliuliza Kisona akitaka kupata uakika waile chupa, “hii ni brack Mamba snake venon, (sumu ya nyoka) sijuwi ime kuja vipi humu ndani” alisema doctor hukwa sauti iliyo jaa wasi wasi. na kumshangaza mke wa Mapombeka, **
Edgar alitembea kwa umakini sana, na kwenda kijibanza nyuma ya kichaka flani, karibu kaisa na hili kambi la muda la polisi, akatulia na kutazama shughuri za pale, huku akitafuta sehemu inayo tokea arufu ya chakula, akika sehemu hii haikuwa na ulinzi, maana askari wote walionekana wakitembea hovyo hovyo, wengine wakizunguka mito, na kupunguza baridi, huku wengine wanywa pombe ya ulanzi, waliyo itoa kwa wakulima, Edgar aka endelea kutazama na kupanga jinsi ya kuingia sehemu ambayo jiko lilipo.
wakati anapanga hayo, mala akamwona akskari polisi mmoja ana sogea kichakini kujisaidia, ni mmoja kati ya wale waliokuwa wanaota moto, huku wana kunywa ulanzi, Edgar akamvizia yule askari ambae SMG yake ilikuwa mgongoni, lakini ile ana mkaribia nikama yule askari alichezwa na machale maana aka geuka na kumtazama Edgar, itaendelea…….. hapa hapa
…….
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU