KIAPO CHA MASIKINI (72)

SEHEMU YA 72

ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA MOJA : Hapo Kalonga akashtuka kidogo, maana akuitaji ufafanuzi toka kwa mtu yoyote, ili kuitambua ile sauti, ambayo alikuwa ametoka kuwasilina amida ya saa tano za asubuhi, na hapo ndipo alipo gundua kuwa, akuitazama namba ya mpigaji, kabla aja ipokea ile simu…. songa nayo…….

Hivyo akaitoa sikioni na kuitazama kwenye kioo, ilikuona namba au jina la mpigaji, ukweli ilikuwa ilikuwa kama alivyo zania, japo sauti tu ilisha tosha kumtambulisha pigaji alikuwa nani, maana jina lililonekana wazi juu ya kioo kwamba ni RCO, namba ambayo aliisave toka jana, mala baada ya kupewa namba hile na OCD Mwanauta, “huyu mshenzi, amejuwaje kama ni mimi?” alijiuliza Kalonga, kimoyo moyo, huku anarudisha simu sikioni taratibu, huku anawaza jibu la kumpa huyu bwana Mlashani, “we nani na unazungumzia mpango gani?” aliuliza Kalonga, kwa sauti tulivu ya kujiamini, wakati alikuwa amfahamu fika kuwa anaongea na RCO Mlashani, “siitaji maswali na majibu bwana Kalonga, hii namba umeitumia msaa macheche yaliyopita, hivyo unafahamu unaongea na nani” alisema Mlashani, kwa sauti ile ile tulivu, na kukata simu.

Hapo Kalonga akahisi mkono ulioshika simu yake, ukitetemeka kwanguvu, akijuliza imekuwaje RCO akajuwa kuwa yeye ndie anausika na jambo ili, ata simu yake iloita tena akashtuka na kutazama alie mpigia, akaona ni Mwanauta, yani yule OCD, akaipokea kwa pupa, “hallow mwanauta huyu jamaa yako sijuwi ni mchawi” alisema Kalonga kwa sauti iliyojaa uoga na wasi wasi, “ebu tulia kwanza Kalonga huyo jamaa ajuwi lolote alicho kifanya ni hisia tu, we usionyeshe kama una wasi wasi na ilo, cha msingi ingia whatsapp nimekutumia video ya mtu alie vuluga mpango mzima” alisema Mwanauta, akionyeha kujiamini sana, kwanza kanisa mpaka dakika hii ata ie namba ya bandia awakuikalili, maka gari linaondoka” aliongea Mwanauta, wakimalizia kwa kicheko cha ushindi.

Waliongea mawili matatu, Mwanauta akisisitiza kwa Kalonga kutokuwa na wasi wasi, juu ya simu aliyopigiwa na Mlashani, kwamba ni sehemu ya mtego na hisia zake juu ya yeye kuhusika na mpango huo.

Baana ya kumaliza maongezi yao huku wakipanga baadae wakutane wapange mpango unao fwata, Kalonga akafungua video ambayo, ilimshtua kwa kumwona Careen akiwa na kijana mmoja alie mtambulisha kuwa ni mume wake, “huyu Malaya anamume tokea lini?” alijiuliza kwa sauti ya mshangao na ghadhab, “na kama ni mume wake imekuwaje aingilie mpango wangu?”**

Baada ya kutika nyumbani ambako akukuwa na kitu chocho te cha upigka wala kula, Sada alitulia kwa muda mfupi, kisha akachukuwa simu ya Peter na kuweka betri, kisha akaiwasha, na kupiga kwa mama Kachiki, ambae akuchelewa kuipokea, “mambo mama Kachiki” alisalimia Sada kwa sauti ya upole yenye kuchekesha, usingefikilia kuwa ametoka kwenye dhahama ya kuwakataa wazazi wake na kumwona mwanae Michael, mtoto wa kushua, tofauti na alivyomwacha week iliyopita, “Sada poa tu Mambo” alisalimia mama Kachiki, “poa tu, hivi jana Peter aikuja huko kijijini?” aliuliza Sada, kwa sauti ya ile ile tulivu, “mh! kwani wakina mzee Nyoni awajakusimulia, si wamekuja huko mjini” aliuliza mama Kachiki, kwa sauti ya mshangao wa kimbea mbea, “hapana sija kutana na wakina mama, kwani wamekuja huku mjini kufanya nini?” aliuliza Sada, kwa sauti ya mshangao ungesema ni kweli alikuwa ajuwi kuwa wazazi wake wapo mjini, wamekuja kukuona wewe, na tatizo hawana simu vyema kama ukienda kuwa tafuta mjini, maana ata nauri wameazima kwa mzee Kabwenga, na wanategemea wewe ndie utakae wapatia ela ya kurudia, nakuja kulipa deni, pamoja na kuwanunuia vitu vingi vya kuja navyo kijijini” hapo Sada, akashtuka kidogo, maana ukweli akuwa na msaada wowote kwa wazazi wake, kuanzia nauri ata sehemu ya kuwaifadhi kwa usiku mmoja.

Lakini uwezi amini, licha ya kulijuwa ilo, Sada akuta ata kuwafikilia wazazi wake, “hao ni tawapata tu, ebu niambie kuhusu Peter ilikuwaje jana” alisema Sada, na hapo nikama alifunguia redio, “yani we acha tu, kijiji chote kiliamia nyumbani kwa mzee Jacob, yani pali jaa watu unesema pana sherehe, watu wamekunywa soda, wamekunywa bia mpaka usiku, hiyo yote kwaajili ya Peter” alisema mama Kachiki, akieleza kwa upana zaidi, kuliko ata alivyo uliza Sada mwenyewe, “yani Peter na mwanae wamependeza haooo, kwani wewe ujawaona huko mjini?” aliuliza mama Kachiki, lakini akukuwa na jibu lolote toka kwa Sada, ambae kiukweli alichanganyikiwa kwa kusikia hivyo, nakujihisi hasira moyoni mwake.

“hivi huyu Peter ela ya kufanya hivyo ameitoa wapi, si nilichukuwa bego lote la ela?” aliuiza Sada bila kutarajia, “inamaana ni kweli ulimwibia mzazi mwenzio?” aliuliza mama Kachiki kwa mshangao, na hapo Sada akashtuka kwa kugundua kuwa swali lile aliuliza kwa sauti, siyo moyoni kama alivyo kusudia, “ha…ha….hapana, siyo hivyo, yani nilisikia wamemwibia kila kitu” alisema Sada, kwa sauti ya kubabaika, “basi ata hivyo awaja mkomoa, yani amekuja na mwanamke wake, ni mzuri huyoooo, alafu Peter nae amependeza, yena wana gari zuri, alafu Michael, kila anakoenda kuna mschana anamwangalia, yani huyo ni yaya wake” alifafa nua mama Kachiki, ungesema anafanya makusudi, baada ya kuhisi Sada anavyo jisikia kwa taalifa hii.

Ukweli taarifa hii aikuwa nzuri kwa Sada, iliuchoma na kuusuta moyo wake, “kwahiyo umalaya wao ndio wanajifanya kumlea mwanangu?” aliuliza Sada kwa sauti kwa sauti ya ukali iliyojaa chuki, “weee Sada, sasa ulitaka wasi mlee wakati inasemekana wewe umemkataa mumeo na mtoto pia, kwaiyo ulitaka Michael ateseke au…..” kabla mama Kachiki ajamaliza kuongea Sada akakata simu, “yani huyu mpuuzi ameshaenda kuwaambia kijijini kuwa nimemkataa” alilalamika Sada, ambae mpaka sasa icha ya mazonge hayo yote, pia akujuwa sehemu ya kupata chakula, “ngoja nimtafute huyu mpuuzi, awezi kutamba hapa mjini wakati mimi nakufa na njaa” alijisemea Sada, huku anaweka simu pembeni, akachukuwa kikombe nakuchota maji kwenye ndoo, akayanywa ka pupa, kishaaka weka kikombe mezani na kujilaza kitandani asipo kujari vumbi alilo kuwa nalo miguuni.

Pale juu ya kitanda Sada alikuwa anawaza sehemu ya kumpata Peter, ambae aliamini kuwa, ata iweje, siku zote Peter anampenda yeye Sada kuliko mwanamke yoyote, “hakuna cha mwanamke mzuri waa nini, akinona tu, lazima huyo mwingine atimuliwe” alisema Sada, huku kichwani mwake, akiamini kuwa Peter alikuwa ameifadhi fedha nyingine nyingi, ambayo yeye akufanikiwa kuziiba siku ile, “ningejuwa nisinge mkatalia siku ile, ningejifanya namkubari alafu anaenda kumwibia ela zake zote alizokuwa nazo” ukweli Sada akuangalia anacho fanyiwa na Emma, yeye alipanga kumwibia Peter, “aiwezekani anizidi hakiri, yani eti Michael anapendeza vile, utazania wao ndio wapo mjini muda mrefu” alilalamika Sada, ambae roho ilimuuma kwa kumwona Michael akiwa katika hali ile sijuwi ni kwanini, alikuwa hivyo, na akupenda kuona kama amezidiwa hakiri.
Zaidi ya hapo Sada akuwaza juu ya wazazi wake, ambao leo hii amewaona ghafla wame kuja mjini, na ameambiwa kuwa wamemfwata yeye, na anategemewa kwa kila kitu, zaidi aliwaza juu ya kumnasa Peter, na pia namna ya kupata ata ela kidogo ya kula mchana huu, “hapa inabidi niende kwa Rose, angalau nikadowee ata chakula, najuwa awezi kuwa na fedha ya kunipa, lakini chakula akosi” aliwaza Sada huku anainuka na kwenda kuchukuwa maji ya kunawia miguu yake, tayari kwa safari ya bomba mbili kwa Rose.***

Emma na Janja ambao, walilazimika kusimama mita chache kabla ya kufika darajani Matarawe, walitulia sehemu hiyo wakisubiri gari walilokuwa nalo wakina Dullah, huku muda wote wakijadiri cha kumweleza Kalonga juu ya kile kilicho tokea kishindikana kwa mpango wao,

Pale darajani walitumia kama dakika ishilini hivi, mpaka walipo liona gari ilo aina ya Toyota Noah, likiibuka kwenye kilele cha mwinuko wa round about ya songea girls, “haoooo wanakuja, lakini tunaanzaje kumweleza boss kuwa, mchongo umebuma” aisema Emma, akionyesha kuwa na wasi wasi na hofu, “lakini kaka wewe wasi wasi wako nini, hakuna alie tarajia kilicho tokea” alisema Janja, akionyesha kutokuwa na hofu, yoyote, “we mpuuzi ukumbuki kuwa week iliyopita tume feli kwenye mpango wa kumkamata Careen, alafu leo tena tumeshindwa, unazani ata tuelewa kweli?” aliuliza Emma kwa sauti ya kumshangaa Janja.

Wakati huo wakina Dullah walikuwa wamesha sogea karibu na gari lao, nao wakapita kama awaja waona, “ebu wafwate haraka” alisema Emma huku anatoa simu yake na kuanza kuipiga kwa Dullah, huku wakilitazama gari lile, likiwa lina zidi kutokomea kwa mwendo mkali.

Janja nae akakanyaga mafuta kwanguvu, kulifukuzia, gali la wakina Dullah, ambalo sasa lilisha potea machoni pao, na mpaka simu ya Emma inapokelewa, Dullah alisema kuwa tayari walisha fika nyumbani kwa Kalonga, “mjinga wewe, kwa ni hamkutuona hapa darajani?” aliuliza Ema kwa sauti ya ukali, “samahani bro atukujuwa kama ndio nyie, sisi tulikuwa tuna wawai hapa kwa boss” alisema Dullah, kwa sauti ya chini, nikama akutaka asikike na mtu flani, “mme bugi nyie mafala, unazani boss akitoka nje mtamweleza nini hapo?” aliuliza tena Emma, na wakati huo na wao walikuwa wanapunguza mwendo mbele ya gate la nyumba ya Kalonga, ambao lilikuwa wazi, wakaingiza gari, huku macho yao yakishuhudia mlango wa nyumba kubwa unafunguliwa na Kalonga akatoka.

Siyo hasira, pia Sura ya Kalonga ilionyesha kuchanganyikiwa “Inamaana Emma boya kama huyu anaweza kuwa shinda hakiri na nguvu kweli?” aliongea Kalonga huku anamsogeea Emma aliekuwa ameshuka toka kwenye gari na kumpatia simu, ili aone kilichopo kwenye simu.

Emma anapokea ile simu, na kutazama kwenye kioo, ambao anakutana na video, inayo mwonyesha mtu ambae pale anapomwona tu, mapigo yake ya moyo yanashtuka, “Peter” alisema Emma, huku anamwonyesha Janja, ambae anapomwona pia anashtuka, nawote wanamtazama Kalonga, “umepataje huyu mshenzi?” aliuliza Emma kwa mshangao, wakati huo Dullah anae akisogea na kushungulia, “nimempaje inamaana ujuwi lolote?” aliuliza Kalonga kwa mshangao, na Dullah, ndie alie jibu, “huyu fala ndie alie ingilia mchongo mzima, yani nilikuwa naingia na mtoto kwenye gari, yeye akanivamia kwanguvu sana” alisema Dullah, ambae alionekana kuwa na jelaha kubwa usoni kwake, “inamaana Emma unamfahamu huyu mshamba, na unajuwa kuwa ndie mume wa Careen?” aliuliza Kalonga, huku akimtazama Emma………..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!