
SEHEMU YA 73
ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA MBILI: “nimempaje inamaana ujuwi lolote?” aliuliza Kalonga kwa mshangao, na Dullah, ndie alie jibu, “huyu fala ndie alie ingilia mchongo mzima, yani nilikuwa naingia na mtoto kwenye gari, yeye akanivamia kwanguvu sana” alisema Dullah, ambae alionekana kuwa na jelaha kubwa usoni kwake, “inamaana Emma unamfahamu huyu mshamba, na unajuwa kuwa ndie mume wa Careen?” aliuliza Kalonga, huku akimtazama Emma………..Endelea…
Ambae nikama alikuwa katika wenge, “ndiyo boss huyu ndie Peter, yule alie vuruga mpango wa kumkatama Careen, nashangaa kuona na leo amevuruga tena mpango huu” alisema Emma, na hapo Kalonga akashtuka vibaya sana, “eti, unasemaaa ndie mshenzi ambae tunamtafuta, sasa mmeshindwaje kujuwa kuwa, siku zote hizi huyu bwege yupo kwa Careen?” aliuliza Kalonga kwa sauti ya ukali, bahati nzuri mke wake alikuwa ameenda kanisani, na alikuwa bado ajarudi, “boss mtu tulie mtuma, alishindwa kutambua Peter, hivyo akaleta jibu tofauti, lakini sasa kwakuwa tumesha juwa kuwa yupo nae, basi inabidi tufanye mipango ya uwa teketeza wote wawili” aliema Emma, kwa sauti ya utiifu mkubwa, “ebu sikia Emma, sitaki mfanye jambo lolote la kijinga, kuanzia sasa nyie tulieni mtakuwa nmasubiri maelekezo, swala la kumkamata huyu fala namwachia Mwanauta” alisema Kalonga, kaba ajawapatia fedha, kiasi cha tsh laki tatu, wakina Emma na kuwaambia waondoke zao, wakasubiri maelekezo, nao wakaingia kwenye gari moja yani IST, lawakina Emma, wakipanga kwenda sehemu wakapate chakula na kinywaji, huu wanatafakari, juu ya ushindikana kwa mpango wao wakumteka Jasmin Mlashan, “twendeni msogeze pub, pale anachakula kizuri” alisema Emma, na safari ya huko Msogeze ikaanza.
Wakati huo, Kalonga aliingia ndani, huku anapiga simu kwenda kwa Mwanauta, na kumweleza kuhusu mtu anae onekana kwenye video, ya pale NPF, yani kijana alie mwokoa mjukuu wa Mlashani, kuwa ndie kijana ambae wanamsaka kwa udi na uvumba, “kaka usijari huyo tunae, ila atuwezi kumfanyia leo leo, maana watashtukia mchezo” alisema Mwanauta.****
Yap! saa tisa za jioni, iliwakuta Careen na Peter kwenye ofisi za ubarozi wa #mbogo_land, wakiongea na mkuu wa idara ya uamiaji, kwaajili ya kupata kibari cha Peter na mwanae kuingia nchini humo, kwa mpango wa vibari vya VIP, ambavyo uwahusu familia za watu wakaribu wa mfalme, yani ukoo wote wa mfalme, viongozi wakuu wa nchi, wajumbe wa baraza la wazee, mabarozi na mawaziri, hao wote ikiwa na familia zao, kama ambavyo hipo kwa Careen mtoto wa mzee Maltin, ambae ni mlinzi wa mfalme, na mke wake ambae ni waziri wa Afya jinsia na watoto.
Huku wakipanga safari kuifanya siku inayofwata, muda ya saa nne za asubuhi, ambapo wangeondoka wa wafanya kazi wawili, pamoja na yaya Glory, jumla wangekuwa sita, na wangeondoka kwa ndege binafsi, ambayo ingeisingia lisaa limoja kabla ya kuondoka zao.
Na baada ya kumaliza swala ilo la upatikanaji wa kibari, nao wakaondoka zao kuelekea nyumbani kwaajili ya kwenda kupumzika, kabla Careen ajaelekea kazini kufunga hesabu, “Careen ninawazo nimelipata namba unisaidie kulitekeleza” alisema Peter wakiwa njiani wanaelekea nyumbani kwa Careen.
Kwanza Careen akatabasamu na kumtazama Peter, “wazo gani ile baba, naimani litakuwa zuri sana” alisema Careen akionyesha kuwa amefurahi, sana kusikia Peter anawazo, “naomba uninunulie pikipiki, niendeshe boda boda, kwa mkataba, nikitimiza hesabu yako, pikipiki inakuwa yangu, alafu naendelea kuzalisha ela nyingine” alisema Peter na hapo Careen, alimtazama Peter kwa macho ya uzuni, “Peter unawezaje kupata wazo kama ilo, nikukoe fedha kama nani, wakati wewe ni mume wangu mratajiwa?” aliuliza Careen kwa sauti iliyojaa simanzi, “ujuwe Careen sijazowea kukaa bila kazi, na kama ujuwavyo msimu wa kilimo bado aujafika, na mimi kwa sasa sina fedha kabisa” alisema Peter, kwa sauti tulivu, huku akionekana wazi kutambua kuwa alikuwa amememuuzunisha Careen, “Peter najuwa kuwa wewe ni mkulima, lakini tunapaswa kukifanya kilimo chako kuwa cha kisasa, nitakugea fedha uongeze mashamba, ununue mtrector na vifaa vya kisasa vya kilimo, utalima mazao mbali mbali kisasa zaidi, pia utanunua, magari ya kubebea mazao kutoa shambani, na kupelekea sehemu yoyote liliposoko la uhakika” alisema Careen, na Peter akaupenda mpango huo.****
Saa kumi za jioni, ndio muda ambao Sada alifika nyumbani kwa Rose, kule bomba mbili, jaa ilikuwa ina mchamanda kweli kweli, bahati ilikuwa kwake, alimkuta Rose, ambae leo alikuwa katika siku ambazo asingeweza kunyanduliwa, maana nisiku za matumizi, hivyo alikuwa nyumbani na hakuwa na moango wa kutoka, “weeee queen, bola umefika, yani kuna fedha nilikuwa na ikosa hivi hivi?” alisema Rose, kaba ata awaja salimia, akimaanisha kuna jambo ambalo yeye ameshindwa kulifanya kutokana na hali yake, hivyo Sada ingemfaa. “mhhhh Rose, yani hapa siwezi kufanya lolote, mpaka nile kwanza” alisema Sada yani Queen kwa sauti iliyoonesha wazi kuwa alikuwa na njaa kali, wala usijari kuna wali na maharage nilipika mchana, umebakia hapo kwenye sufuria” alisema Rose na hapo Sada akusubiri maelekezo, akavamia sufuria la wali, na kuchanganua maharage ndani yake, kisha akaanza kufakamia, huku anapewa mpango kamili.
Mpango ilikuwa hivi, kwamba kuna mteja wake toka mlila yoyo, anakuja namwenzake, ambae alikagiza amtafutia mwanamke, wa kupuzika nae, kaba ajaelekea kijijini mlila yoyo, kwa maana alikuwa anakuja ana kuondoka zake, “huyo anatoaga ela nzuri, we kula ujiandae anakuja hapa hapa” alisema Rose, akimweleza Sada ambae kiukweli alikuwa na shidakubwa ya fedha.***
Saa mbili za usiku nyumbani kwa mzee Jacob, watu walikuwa wengi kama jana, wanatazama video, ndio wakati ambao gari la abiria liliingia toka mjini, na wakina mzee Nyoni wakashuka na kuelekea moja kwa moja kwa mzee huyo, kila alie alishkwa na viulizo, maana licha ya kubeba mizigo mbali mbali, ikionekana kuwa walifanya manunuzi, huko mjini, wakati walienda na nauri, lakini nyuso zao zilionekana kupwaya kwa kwa uzuni.
Ata walipofika nyumbani kwa mzee Jacob, ambae walimkuta akiwa na wazee wenzake wake kwa waume, wakinywa ulanzi, na kutazma video, wakamwomba, mzee Jacob na mke wake, waongee pembeni kidogo…..…….
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU