
KIAPO CHA MASIKINI (76)

SEHEMU YA 76
ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA TANO: Wakati anawaza hayo ndipo alipokumbuka kuwasiliana na Peter iliaweze kumwalika katika chakula cha jioni, kitu ambacho kinge saidia kuweka ukaribu zaidi kati yao, na yeye kuweza kumfahami vyema Peter, na pengine kung’amua ukweli juu ya kijana huyu, ambae endapo angekuwa maaarufu au mfanya biasharaflani, lazima angekuwa anamfahamu, au angesha wai kukutana nae ata mala moja.….ENDELEA…..
Hapo Mlashani akachukuwa simu yake, na kupiga kwa Peter, lakini bahati mbaya aikuwa inapatikana, “mh!inamaana alinipa namba ambayo aitumii” aliwaza Mlashani ambae alipania kupata ukweli, hapo akaomba namba ya ofisini kwa Careen, ambayo alipewa na msaidizi wake, akaipiga nayo ikapokelewa, nae akakutana na sauti nyororo na tamu yakike, “hallow #mbogo_land sonara huduma kwa wateja, nikusaidie tafadhari” hapo RCO akajiweka sawa kwa kusafisha koo lake, yani kama ile anakooa, “SP Cletus Mlashani, RCO Ruvuma naongea toka makao makuu ya jeshi la polisi, mkoa wa Ruvuma” ilikuwa ni sauti tulivu, iliyojaa hekima, ya kiutu uzima, “shikamoo mzee wangu, nikusaidie tafadhari, “marahaba, naweza kuongea na Careen au bwana Peter tafadhari? maana nimepiga simu ya bwana Peter, lakini aipatikani ” aliuliza Mlashani, “hoooo samahani mzee, kwa sasa auto weza kuongea nae, maana wameondoka saa nne, kuelekea #mbogo_land kwa ndege binafsi” ilisikika sauti ile ya kike.
Hapo RCO alishangaa kina kushtushwa na taarifa ile ya safari ya ghafla ya bwana Peter.***
Naam mwana dada Kadara, mida hii alikuwa anashuka toka kwenye gari dogo aina ya Toyota Noah, ambalo ufanya safari zake toka Namtumbo, kuja songea mjini, ndio usafiri pekee ambao, unapatikana muda wowote, asa nyakati za mchana, maana likijaa gari lina ondoka, huku jingine linapakiza, nalo likijaa linaondoka na kuingia jingine.
Kadara alichukuwa boda boda, kuelekea nyumbani kwake majengo, ambako aliondoka toka juzi, wakati huo kichwani mwake muda wote alikuwa anawaza juu ya kitumbacho ametoka kukiona kwenye simu yake muda mfupi uliopita, “jamani mbona Peter anakuwa maarufu ghafla hivi, alafu anapende huyo” alijisemea Kadara ambae kwa macho yake ameza kuona video ambayo inamwonyesha Peter, akielezewa kama shujaa, huku akionekana na amesimama na watu wenye heshima zao, huku mwanamke mrembo kuliko kikapu cha urembo, akimtamburisha kama mume wake, inamaana huyu mwanamke ndie alie enda na Peter kijijini?” alijiuliza Kadara kama vile akuyaamini macho yake, wala masikio yaliyo msikilisha maneno ya yule mwanamke mrembo sana, “hivi Sada kama ameona hii sijuwi atakuwa na hali gani huko?” alijiuliza Kadara huku akimalizia kicheko cha chini chini, bahati nzuri dereva wa boda boda akumsikia, maana angezania kuwa ni chizi.***
Taarifa hii ya kusafiri kwa Peter ilimshtua RCO, ambae alihisi kuwa pengine Peter kwa kujuwa atatafutwa, juu ya tukio la jana, ameamua kutengeneza safari ya uongo, “mbona ghafla hivi, kuna tatizo huko #mbogo_land?” aliuliza RCO, akitumia sauti tulivu, akificha mshangao, na mashaka yake juu safari ya Peter, “hapana akuna tatizo lolote huko nyumbani, ila madam anampeleka shemeji kwenda kumtamburisha kwa wazazi” alisema huyo mschana wa mapokezi wa #mbogo_land sonara, hapo RCO akaona atumie nafasi hii kumfahamu zaidi Peter, maana hapo mwanzo akuwa maarufu ata kidogo, na wala akuwai kumsikia, “hooo safi sana, wameona waanze kujitamburisha kwa upande wa mke, kisha waende upande wa kiume” alisema Mlashani, huku anacheka kidogo na yule mwanamke wa upande wapili nae akacheka kidogo, “hapana mzee, mbona kwakina Peter walishaenda juma mosi, tena walipokelewa kama wafalme, kijiji kizima kilikusanyika” alisema yule mwanamke, pokeaji wasimu, “hoooo! kumbe ni kijijini, hivi Peter anatokea kijijigani?” aliuliza Mlashani, “mh! sijuwi mwana…. mwana nini sijuwi, ni huko Namtumbo” alisema yule mwanamke ambae sasa alionekana kuanza kuchoka kujibu maswali yale binafsi, “samahani binti yangu, hivi, huyu bwana Peter kabla ya hapo aliwai kufanya kazi hapo, au ni mfanya biashara, yani nataka kufahamu walikutana vipi” alifunguka RCO kwa kusema duku duku lake, “japo siluhusiwi kuongea mambo ya watu, lakini kwa kifupi ni kwamba, Peter aliwai kumsaidia Careen mala mbili, alipovamiwa na majambazi, ndio urafiki wao ulipoanzia” alisema yule mwanamke.
Hapo RCO akashtuka kidogo, na kuhisi kuwa kuna jambo limejificha juu ya misaada ya Peter, yani Careen alikutana nae baada ya kumsaidia na ata yeye pia amekutana nae baada ya kusaidia, “hapana kuna kitu hapa, lazima nichunguze kwa kina” aliwaza mzee Mlashani, ambae alitupa swali jingine kwa mwanamke huyo, “kumbe ilikuwa hivyo, inasisimua sana lakini mbona hiyo taarifa aikufika polisi, waliliport kituogani?” aliuliza RCO ilikupata picha harisi, ya matukio hayo ya kuvamiwa kwa Careen kama ni yakupangwa na Peter, au nikweli walikuwa majambazi, “sidhani kama Careen atajisumbua kuja kutoa taarifa kwenu, amesha toa mala nyingi na hakuna kinacho tokea zaidi ya kupigiwa simu za kutishiwa” alisema yule mwanamke, na hapo kengere ya tahadhari ikagongwa kichwani kwa Mlashani.
Ukweli yeye akuwai kusikia taarifa yoyote ya kuvamiwa kwa mana mke huyu, maana utaratibu uliopo ni kwamba, tatizo lolote au tukio lolote likitokea tena ambalo lina mhusu mtu maarufu, na mfanyabiashara mkubwa kama Careen, uwa linaletwa kwenye kikao siku za jumatatu, na linajadiliwa kwa pamoja, ikiwa na kufahamishwa hatua zilizo chukuliwa, huku tayari staff officer anakuwa amesha pewa taarifa siku hiyo hiyo ya tukio, katika report zakila siku, lakini ukweli hakuwai kusikia taarifa kama hiyo, “unauhakika na unacho kisema?” aliuliza Mlashani kwa mshtuko mkubwa, aliuliza Mlashani, kwa sauti ya mshangao, na kushuku jambo la uongo, yani kama vile akumwani yule mwanamke anaeongea nae, “mh! baba kweli wewe ni polisi kweli, mbona madam alisha toa taarifa mala nyingi sana, nabaada yake ndio kwanza anapigiwa simu na vitisho juu, anaambiwa kuwa anajisumbua kutoa tarifa kituo cha polisi” jibu la yule mwanamke lilimshangaza sana Mlashani. ambae kiukweli, akutegemea kama kuna uzembe mkubwa kama huo unaweza kufanywa ndani ya jeshi la polisi.
“Samahani binti, unaweza kuniambia alikuwa anareport kituo gani cha polisi, na mala ya mwisho kureport ilikuwa lini?” aliuliza Mlashani, na nikama yule mwanamke akazinduka na kugundua kuwa alikuwa anatoa maelezo bila luksa ya boss wake, “samahani mzee kama unataka maelezo zaidi nivyema ukifwata utaratibu wakawaida, au ukikutana na madam wenyewe, maana hayo mengine siyo kwamba siyajuwi, ila nivyema kama utamsubiri Careen arudi” alisema yule mwanamke.
Ukweli ata RCO Mlashani pia aliona umuhimu wa kuongea na Careen, juu ya jambo ilo, “ok! sawa nitaongea nae, lakini atarudi lini toka huko #mbogo_land?” aliuliza Mlashani, hapo kidogo mwanake yule mwenye sauti nzuri kwenye simu, akaonekana kuvuta kumbu kumbu, kama mtu asie na jibu sahihi, “nazani watakaa week moja, maana wanasehemu nyingi za kutembelea” alisema yule mwanamke, “sawa na kama watarudi kabla ya week nitaomba uwaambie nina itaji kukutana nao” alisema Mlashani, kabla ya kukata simu.****
Yap! mwana dada Queen au Sada, kama tunavyo mwita kule mwanamonga, alikuwa amesha zunguka karibu mitaa yote ya mji wa songea, asa ile ya uswahilini akijaribu kumsaka Peter, lakini mpa mida hii akuwa amemwona Peter wala Michael
lakini akukata tamaa, maana alijuwa kuwa endapo atawapata wawili awa kuna fedha yake nyingi tu, na alipanga kutofanya makosa kama ya mwanzo, endapo ata fanikiwa kumwibia Peter, ambae aliamini kuwa akikutana nae, lazima Peter mwenyewe atalegea na kujipendekeza kwake, maana anafahamu kuwa Peter anampenda yeye kuliko mwingine yoyote, asa anapo kumbuka mambo yote alivyo mfanyia, lakini bado Peter anajipeleka tena kwake, maana angekuwa mwanaume mwingine, pale alipokutana nae, tayari angekuwa amesha mvunja mifupa yote ya mwili wake, kama siyo kumuuwa kabisa. ….……..
MWISHO SEASON THREE

