SEASON 3: TOBO LA PANYA (46)

SEHEMU YA AROBAINI NA SITA

ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA TANO: “mh!, huyu mzee noma, yani amesha niona na amejuwa namfwata yeye” alijisema kijana yule, huku anaachia tabasamu, “nikweli unajambo la kufurahisha kiasi cha kutabasamu, wakati umesha nijaza wasi wasi?” anauliza mzee Haule, akiwa anamfikia kijana huyu. . . . . ..Endelea…….

“bwana Mahundi amesema ni jambo zuri, sijuwi kwako litakuwaje?” alisema yule kijana, kwa sauti yenye uchangamfu, “sawa, nipe mchapo, kabla insi awajatuwa kwenye grass” alisema mzee Haule, akionyesha shahuku ya kutaka kusikia habari mpya.

“ni kuhusu SA-26, ameonekana kijana akipambana na vijana wa Tino Nyondo, maeneo ya chuo cha matogoro, amewauwa wote wanne, yani jamaa anamfanano mkubwa na yeye, kwa majibu wa maelezo ya jarida lake, anafanana kuanzia umbo mpaka matendo” alisema yule kijana mtanashati.

Kina pita kimya kifupi, tofauti na vile ambavyo kijana alitegemea kumwona mzee Haule akitabasamu, baada yake anamwona mkurugenzi huyu, anaonyesha hali ya kupooza na mashaka, “kwahiyo Mahundi amesha juwa SA-26, anaishi wapi?” aliuliza mzee Haule, kwa sauti tulivu yenye mashaka.

“mshukiwa alitoweka ghafla eneo la tukio, ilikuwa vigumu kumfwatilia, ameongozana na mschana Anastansia Antony, mtoto wa nje wa waziri mkuu mstaafu wa #Mbogo_Land, ambae aijulikani wanausiana vipi, cha kuzingatia ni kwamba ajamteka” alisema kijana mtanashati, huku anamtazama mzee Haule kwa macho ya tahadhari.

Zinapita sekunde tano, mzee Haule anatafakari, inampa mashaka kijana mtanashati, ambae anajuwa uweze mkubwa wa mhzee Haule, katika kushuku na kupapanua mambo.

“mzee mbona kama…., ujazipenda taarifa za kuonekana kwa huyu mtu, ambae anasakwa usiku na mchana?” anauliza kijana mtanashati, kwa sauti yenye mashaka na tahadhari kubwa, macho yake akiyaelekeza usoni kwa mzee Haule, ambae ni vigumu mkutafasiri.

Safari hii mzee Haule anatabasamu kidogo, huku anainua uso wake, kumtazama kijana mtanashati, “ulisha wai kumsikia huyu mtu hapo mwanzo, kabla ya kuanza msako huu?” aliuliza mzee Haule, huku anamtazama kijana huyu.

“hapana, sijawai kumsikia” alijibu kijana mtanashati, sasa ikiwa zamu yake kupoteza tabasamu lake, “mimi nime pata kumsikia mala nne” alisema mzee Haule na kutulia kidogo, akiachia sekunde kama nne hivi, kisha akaendelea.

“mala ya kwanza nilisikia habari zake alipo wachinja watekaji kumi na tano, waliomteka mtoto wa hakimu, kwa lengo la kushinikiza apindishe sheria katika huku” alieleza bwana Haule, kwa kituo, kama ilivyokuwa mwanzo.

“mala ya pili, nilisikia habari zake, wakati alipo uwa vijana nane, waliojaribu kumkaba kwaajili ya kumwibia, akiwa katika matembezi binafsi” alisema mzee Haule, na kuendelea, “mala ya tatu, nilimsikia SA-26, akiwa anatafutwa ili auwawe yeye” alisema mzee Haule, huku kijana mtanashati nikama alianza kumweleza boss wake.

“ni kweli mzee, leo tumemskia tena, ndani ya mkasaa matatu, amesha uwa watu watano” alisema kijana mtanashati, kwa sauti ya ung’amuzi, mzee Haule anacheka kidogo, “kumbuka walio uwawa ndio walikuwa na silaha, sijajuwa itakuwaje na yeye akishika silaha itakuwaje” alisema mzee Haule.

“lakini na uhakika tuta mnasa, kwa maana tuna watu wengi sana mtaani” alisema kijana mtanashati, akionekana kujipa matumaini, lakini mzee Haule anacheka kidogo, kicheko cha kukata tamaa, kiasi cha kumshangaza kijana mtanashati, ambae sasa alianza kumchukia mzee Haule kwa kujifanya mng’amuzi.

“mzee, unamaanisha hatuwezi kupata, yani yeye anaweza kuwa bora zaidi ya sisi wote?” aliuliza kijana mtanashati, huku akizuwia kuonyesha chukizo lake, juu ya mzee Haule, “nikazi sana kumwinda panya anaejuwa anawindwa” alisema mzee Haule akiwa mwenye uhakika wa kile anacho kisema.

“boss unataka kusema tayari SA-26 anajuwa kama anatafutwa?” anauliza kijana mtanashati, kwa sauti ya kumshangaa mzee Haule, ambae anaachia kicheko cha masikitiko.

“mbona ni lahisi sana, aiitaji antenna kuinasa hii, siuna ona amemchukuwa yule mschana, ambae ndie pekee ambae angeweza kutufikisha kwake, sidhani kama amefanya hivyo kwaajili ya Tino Nyondo, mtu ambae awezi kumtisha wala kumtia wasi wasi” alisema mzee Haule, huku kijana mtanashati akianza kubadirika sura, na kumakinika zaidi.

“tunapaswa kuelewa kuwa, SA-26, amefanya hivi kwaajili ya TSA, ambao ni maadui zake wakubwa” alisema mzee Haule, lakini kijana mtashati akatia shaka kidogo, “lakini yeye anamaadui wengi, pengine anawaofia wengine na TSA” alisema kijana mtanashati, akipingana na mzee Haule.

Haule anatikisa kichwa masikitiko, “kichwa chako kigumu sana, unashindwa kuelewa kuwa SA-26 anajuwa kuwa anasakwa na TSA, na kwamba anajuwa lile tukio alilolifanya jioni ya leo, lingeweka wazi uwepo wake ndani ya mji huu, na mtu pekee ambae angelahisisha kazi ni yule mwanamke” alifafanua Haule, na hapo kaacha mdomo wazi kwa mshangao.

“sasa mzee itakuwaje hapo, tuna lolote ambalo tunatakiwa kufanya ili tumnase?” aliuliza kijana mtanashati, na kumfanya mzee Haule atulie kidogo, kama atatafuta jibu sahihi.

“kijana, chakufanya nikuomba sana, SA-26, asipate wazo la kushika bunduki yoyote, pia omba sana siku ukikutana nae, kile kisu chake kikali, kisipite kwenye shingo yako, angalau akutoboe tumboni, pengine tunaweza kukuwaisha hospital Mwenyezi Mungu, akupatie nafasi nyingine ya kuishi ukiwa kilema” alisema mzee Haule, na kumfanya kijana mtanashati ashtuke na kushika shingo yake.

“boss, inamaana auna namna ya kuzuwia ili ilisitokee…” anasema kijana mtanashati kwa sauti ya uoga na kuchanganyikiwa, “acha kupoteza muda kijana, nenda kwa Mahundi, mwambie atumie akili anapomfwatilia huyu mwanaume, vinginevyo mpaka jua linatoka tutahesabu SA miongoni mwa wafu, watakao kuwepo” alisema Haule huku anaanza kutembea kurudi aliko waacha familia yake.

“miongoni mwa wafu, inamaana kuna vifo zaidi vitaendelea kutokea?” anajiuliza kijana mtanashati, ambae anatamani alipate jibu toka kwa mzee Haule, lakini tayari alisha fika mbali, na angeuliza kwa umbali ule, lazima usiri ungekosekana. . . . . . ..Endelea……. kufwatilia hadithi hii, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!