KIAPO CHA MASIKINI (78)

SEHEMU YA 78

ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA SABA : maana atoa simu yake haraka na kuanza kuipekuwa, “kwani na wewe ulikutana nae mpaka ukampiga picha?” aliuliza Sada huku anasogealea karibu kabisa pale alipokuwepo Kadara kwa lengo la kutazama anachotaka kumwonyesha, kwenye simu yake, “kwani ujuwi mwenzio Peter amekuwa maarufu siku hizi, ukiatazama tu face book unamwona” alisema Kadara ambae sasa alikuwa amesha ipata ile video na kuiweka, huku Sada aambae nikama alishindwa kuelewa anachomaanisha Kadara akiwa amekodolea macho kwenye simu ile……….…..Endelea…

Ambayo ilikuwa mkononi kwa Kadara, alie ibofya na kuicheza ile video, ambayo ilianza kwa kumwonyesha Peter mwenye kuonekana katika mwonekano, mzuri wa kijana ambae ungesema amezaliwa mjini na amekulia mjini, tena katika maisha mazuri, alie onekana anamwinua binti mtoto wakike, ambae Sada anamkumbuka kuwa alimwona siku iliyopita, akicheza Michael, na baadae anasogea kumchukuwa yule binti, huku sauti za watu zikisikika kumsifia Peter kwa kile alicho kifanya, “he! Peter amewezaje kuwa hivi?” aliuliza Sada kwa sauti ya mshangao, huku anatazama ile video, “unashangaa yeye mwenyewe, ebu subiri umwone mke wake” alisema Kadara, huku wanaendelea kutazama ile video kwenye simu.

Naam wakati video inaendelea, Sada alikuwa makini kuifwatilia, na kila alicho kiona kilikuwa cha kushangaza kwake, lakini kilichomvutia zaidi ni mwonekano wa Peter wakati huu, ni mabadiriko ya ghafla na haraka sana, Peter alionekana handsome, ukiachilia utanashati, pia Peter alikuwa na mwili mzuri wa kiume, ni kutokana na shughuri zake shamba, “yani amenidanganya ananipenda, alafu anashindwa kunitafuta” alisema Sada, na hapo Kadara akashangaa kidogo, maana siku chache zilizo pita, Sada alihapa kuwa atoweza kurudiana na Peter, ata kitokee nini, yani bora afanye mapenzi na mbwa, kuliko kurudiana na Peter, na kama hiyo aitoshi alisema kuwa endapo ikitokea aka rudiana na Peter, basi ageuke kuwa kichaa.

Sada alizidi kushangaa, pale alipomwona mwanamke mrembo, akimsogelea Peter, nakusimama pembeni yake, “huyu ndie mke wake, sasa” alisema Kadara akimwonyesha Careen kwenywe simu, “mh! kumbe na wewe bado mshamba, huyu si Careen yule mwanamke wa #mbogo_land sonara, anawezaje kuwa mwanamke wa Peter?” aliuliza Sada, huku macho yake bado yapo kwenye simu akitazama video ile ambayo sasa ilizidi kumshangaza, “we ngoja uone huko mbele, ata mimi mwenyewe nimeshangaa” alisema Kadara, akiwa na uhakika wa kuwa kuwa lazima kuna jambo lita mshangaza Sada.

Nikweli, dakika nne sekunde kadhaa, ya ile video, ambayo sasa ilikuwa inamwonyesha RCO Mlashani akiwa amesha fika na anaanza kuhoji kuhusu Peter, na Careen akawai kujibu, “huyu ni mume wangu” yani kkama kunasiku Sada alishangaa, basi ni siku hii ya leo, tena ni wakati huu, aliokuwa anatazama hii video, ghafla alipatwa na wivu wa ajabu, “usini tanie we mwanamke, mumeo nani, kwani ajakuambia kuwa anamke, huyo au unazani huyo mtoto alimzaa yeye mwenyewe” alisema Sada, huku anaondoka zake na kuelekea kule kule alikokuwa anaelekea mwanzo, bila ata kuaga kwa Kadara, ambae alikuwa anacheka kimoyo moyo.**

Yap! Mlashani akiwa na sababu kadhaa za kumshuku Peter, juu ya tuhuma za kuhusika na utekaji wa mjukuu wake, ikiwa pamoja na safari ya ghafla ya siku hii, ambayo kuna taarifa ya tukio la kuingizwa kwa dawa za kulevya, “sasa huyu Careen atakuwa anausikaje, au kuna tishio ambalo lime mlazimu kushiriki kwanguvu?” alijiuliza RCO Mlashani, huku anabofya simu yake kwenda kwa OC CID wa songea mjini.

Simu iliita kwa sekunde kadhaa kisha ikapokelewa, “jambo afande” alikuwa ni CO CID mwenyewe ndie alie pokea simu hiyo, “jambo OC CID, hupo wapi kwa sasa?” aliuliza RCO Mlashani, “nipo ofisini afande” alijibu OC CID, “ok! kuna jambo naitaji kulifahamu toka hapo wilayani, hivi ulisha wai kusikia taarifa yoyote, ya kuvamiwa kwa Careen hapo kituoni kwenu?” aliuliza Mlashani, ambae mpaka hapo, bado alikuwa anahisi kuwa kuna mchezo umetengenezwa ili kuficha ukweli wa jambo flani, na siyo kweli kwamba Careen amevamiwa na kutoa taarifa kituoni, “yah! nilisha wai kusikia kitu kama hicho ila ni muda mrefu sana” alijibu OC CID.

Jibu la OC lilimshtua kidogo Mlashani, “una uhakika, kuwa taarifa kama hiyo iliwai kuletwa hapo kituoni?” aliulizaMlashani, kwa sauti ya kutia shaka, “ndiyo afande nimuda siwezi kusahau, na kumbuka vizuri sana” alijibu OC CID, kwa sauti yenye kuonyesha alikuwa na uhakika, “ilikuwa lini, je alimtaja mtu anae mshuku, na hatua gani ilichukuliwa?” aliuliza RCO Mlashani, “lakini inakaribia mwaka sasa, ni wakati ule nikiwa A-Insp (akiwa na nyota moja), niliona Caeen akija na gari lake na kugesha hapo nje, kisha akaingia ndani na kutoa hiyo taarifa ya kufukuziwa na gari dogo ambalo niliweza kuliona toka ddirishani, sikufahamu lanani, ata hivyo taarifa ilipelekwa kwa OCD Mwanauta, na zani yeye ndie alie chukuwa hatua” alijibu OC CID.

Hapo RCO akatulia kwa sekunde kadhaa akitafakari jambo, kisha akauliza, “vipi kuhusu taarifa yoyote ya mtu anaeitwa Peter, aliwai kurepotiwa kwa tukio lolote la kiarifu hapo kituoni?” aliuliza Mlashani, na jibu la OC CID likwa ni hapa, “na vipi kuhusu mshukiwa wa kuingiza dawa za kulevya anae tarajiwa kukamatwa leo, una mfahamu kwa jina?” aliuliza Mlashani, “mh! afande ata mimi nimesikia tu kuwa kuna kikundi kimeandaliwa kitaenda kumkamata huyo muarifu, lakini sija juwa ni wapi na wala sijamjuwa huyo mwarifu ni nani” alijibu OC CID.

Hapo RCO kengere ya tahadhari ika gonga kichwani mwake, maana kama ni siri sasa hakuna tena, maana karibu askari wote wa jeshi la polisi hapa mkoani wanafahamu, japo hakuna anae fahamu jina la mshukiwa, lakini ni wazi kama kuna mshirika wake ndani ya jeshi, tayari atakuwa amesha mweleza juu ya zoezi la siri linaloandaliwa kwaajili yake, “sawa OC, ukipata taarifa yoyote ni julishe mala moja” alisema Mlashani na kukata simu.***

Sada akiwa mwenye hasira za ghafla, ambazo akujuwa ata zie tokea wapi, alitembea kwa haraka, mpaka mtaani kwao mahenge, na kuingia ndani ya nyumba anayoishi na mpenzi wake Emma, kisha akajilaza kitandani, pasipo kuangalia vumbi miguuni mwake, huku kichwani mwake akiwa na mjadara mzito, ambao ulikuwa unakisa majibu na suluhisho, “amwezaje kunifanya mimi mjinga kiasi hiki, yani mimi nashinda na njaa, alafu yeye analifwa lile limwanamke” aliwaza Sada, ambae kila mala alikuwa anajigeuza geuza pale kitandani.

Ukweli kama usinge juwa alicho kifanya Sada hapo mwanzo, basi ungeamini kuwa Peter ndie alie mtelekeza Sada, ni kutokana na kile alicho kuwa anakilalamikia Sada, “hapana awezi kunifanyia hivi, anasababisha mwanangu ananiambia kuwa niliwaibia nguo zao, hiyo yote mtoto anione mbaya, kwani ange kaa kimya angepungukiwa na nanini” aliwaza Sada, huku uchungu mkubwa ukimshika moyoni mwake, na kuona kama ametendewa jambo flani baya la uthariti, na Peter, “inaonyesha alikuwa nae toka zamani, alafu mimi akawa anazugatu” aliwaza Sada, kwa machungu makubwa.

Ukweri mimi binafsi sikujuuwa ni kwanini Sada anawaza sana juu ya Peter, wakati yeye ndie alie mkataa kijana wetu, pamoja na mtoto wao, Michael, sasa kwanini leo namwona Peter ndie mthariti.**

Naam toka saa nne walipoingia Mbogo Land, mpaka mida ya saa kumi na mbili za jioni, Careen na Peter walikwisha tembea baadhi ya maeneo ya mji wa Treanch town, ikiwa ni kama kuwaonyesha wakina Peter maeneo ya mji huu mdogo wa umbo la kini ni mkubwa kwa fahari zake na na mambo yakifahari na yakuvutia yanayopatikana ndani ya viunga vya jiji ili lenye mita chache za mraba, kuliko majiji yote duniani, na sasa walikuwa wanaelekea nyumbani kwa wazazi wa Careen mtaa wa viongozi wa nchi.

Na wakiwa wanakaribia nyumbani kwa kina Careen, huku wakiwa wenyewe na Michael pamoja na mfanya kazi wakike mmoja, mala simu ya Careen ambayo ina namba za nchi hii, ikaanza kuita, alipo itazama akaona ni namba ya ofisini kwake, yani #mbogo_land sonara, ikiwa ni namba ya huduma kwa wateja, nae akaipokea mala moja, “salaam mdam Careen” ilikuwa ni sauti tulivu ya kike toka upande wa pili wa simu, “salaam” aliitikia Careen ambae alikuwa anaendesha gari, “madam kuna mtu alipiga simu, akajitambulisha kuwa ni RCO Mlashan, alikuwa anamwulizia shemeji” alieleza yule mwanamke, wa kutoka ofisi za Mbogo land, ambae alieleza kuhusu simu iliyopigwa na Mlashani, na maswali aliyo uliza, “eti anasema ajuwi kama uliwai kuvamiwa, na hakuna taarifa yoyote aliyo ipata” alieleza yule mwanamke, kitu ambacho akikumshangaza sana Careen ila alishangazwa na maswali mengi yaliyo ulizwa juu ya Peter.***

Naam! saa tatu na nusu, giza nene lilikuwa lime tanda RCO alikuwa nje ya nyumba yake anahakikisha kama kila kitu kipo sawa, na sehemu ambazo ziliitajika kufungwa zilikuwa zime fungwa, lakini kabla ajarudi ndani, akaona gari moja aina ya land rover defender, mali ya jeshi la polisi, likipita mita chache usawa wa barabara, inayoenda upande wa shule ya msingi maji maji, kukutana na barabara inayotoka songea girl sekondari kwenda kukutaa na barabara iendayo mikoa ya kusini, likiwa limebaba askari watano nyuma yake, kwa tabu aliweza kuona baadhi ya askari hao wakiwa wamebeba bunduki aina ya SMG.

Sijuwi kwanini mzee Mlashani alivutiwa, kulitazama lile gari, ambalo lilionekana likikamata barabara ya songea girls na kukata kushoto, kuelekea upande wa barabara ya kuelekea mikoa ya kusini, na hapo Mlashan akataka kuingia ndani, lakini akasita ghafla baada ya kuliona lile gari la polisi, kwa kutumia taa zake za nyuma, likianza kupunguza mwendo na kusimama nje ya gate la nyumba ya mwanamke wa #mbogo_land sonara, yani Careen, kisha kuanza kupiga honi kwa fujo, “mh! kuna nini pale” alijiuliza Mlashani, huku anatembea kusogea barabarani, maana akuweza kuona vizuri, maana sasa alizuiwa na majengo ya angon arms hotel.

Naam RCO alipofika barabarani akweza kuona gari lile la polisi, likiwa lina ingia ndani ya uzio wa jengo lile la kifahari, baada ya gate kufunguliwa, ilimshangaza sana Mlashani, maana jengo lile, ukiachilia kuto kuingia mtazania yoyote asie na kazi maalumu, pia akukuwa na biashara yoyote kati ya polisi na miliki wa jengo lile, asa ukichukulia kuwa mmilikiwa jengo lile alikuwa amesafiri na mtu alie mtaja kuwa ni mume wake, “hapana lazima nipate ukweli wa jambo ili” alijisema RCO huku anatoa simu yake na kumpigia afisa msimamizi wa zamu, “ambae akuchelewa kupokea simu, “jambo afande” alisalimia afisa msimamizi wa zamu, ambae kikawaida uwa na cheo cha insp au A-insp, “unatarifa yoyote ya askari kwenda kwenye nyumba ya Careen yule mwanamke wa #mbogo_land?” aliuliza RCO, ambae bado alikuwa amesimama barabarani, “ndiyo afande, tarrifa imetufikia sasa hivi, kuwa kuna askari oka kituo cha polisi wilaya, wanaenda hapo kwa Careen, maana kuna mshukiwa wa dawa za kulevya, ameonekana akiingia hapo” alijibu afisa wa zamu….……..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!