KIAPO CHA MASIKINI (79)

EHEMU YA 79

ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA NANE: alisalimia afisa msimamizi wa zamu, ambae kikawaida uwa na cheo cha insp au A-insp, “unatarifa yoyote ya askari kwenda kwenye nyumba ya Careen yule mwanamke wa #mbogo_land?” aliuliza RCO, ambae bado alikuwa amesimama barabarani, “ndiyo afande, tarrifa imetufikia sasa hivi, kuwa kuna askari oka kituo cha polisi wilaya, wanaenda hapo kwa Careen, maana kuna mshukiwa wa dawa za kulevya, ameonekana akiingia hapo” alijibu afisa wa zamu….……..Endelea…

Naam hapo RCO akahisi damu inachemka mwilini, na kufanya mwili wake usisimke, “uwezi kunichezea hakiri Peter, sasa mwisho wako umesha fika” alijisemea Mlashani, kwa sauti ya chini, iluyojawa na furaha kubwa, akihisi kuwa, hisia zake juu ya Peter zilikuwa ni zakweli, “na nilazima huyu kijana atakuwa mtu wa Kalonga, au mshirika wake wakaribu, katika mipango yao ya uuzaji wa dawa za kulevya na mimea korofi” aliwaza Mlashani huku akiwa bado amesimama pale pale barabarani.**

Yaap! mida hii kwa nchi ya kifalme ya #mbogo_land, katika jiji la Treanch town, lilikuwa lime changamka sana, taa ziliangaza kila kona, ya jiji ili, yani barabarani, pembezoni mwa majengo makubwa, mitaani na kwenye viunga mbali mbali vya jiji, pamoja na garden za jiji, maarufu kama city garden, ambazo mida hii, ungeweza kuwaona watu wakiwa wamekaa katika mikao mbali mbali, wakitazama manzari nzuri ya jiji inayoweza kuonekana nyakati hizi za usiku, unweza kuona waliokaa kifamilia, na wale walio kaa katika na wapenzi wao, na wapo waliokaa mmoja mmoja, au wili wawili na kuendelea, huku wengine wakipata vyakula na vinywaji walivyo uziwa na wafanya biashara mbali mbali, walio zunguka pembeni ya viunga.

Mida hii Careen na Peter, pamoja na wazazi wa Careen, walikuwa kwenye bustani nje ya jumba kubwa la kifahari, wanalo ishi wazazi wa Caren, ambao ni viongozi na wafanyaazi wa serikali ya kifalme ya #mbogo_laand, wakipata juice moja nzuri sana ya matunda mchanyiko yenye hasiri ya porini, yani siyo ya kupandwa kama tulivyo zowea, “mmepanga lini kufunga ndoa” aliuliza mama Careen ambae alikwa amekaa karibu kabisa na mume wake, yani baba Careen, bwana Martin, mlinzi wa mfalme, “mama jaman haeaka ya nini, tutawajulisha tukisha panga kila kitu” alisema Careen, ambae kwa muda mfupi aliokaa hapa Treanch Town, aliweza kumfanya Peter atambue kuwa Careen siyo tu kupendwa na kujaliwa na wazazi wake, ila pia alikuwa anadeka kupita kiasi, na wazazi pia walikuwa na uwezo mkubwa sana kifedha, ambao kwa nchi nyingine ungesema kuwa ni matajiri waubwa, siyo tu, kutokana na maisha ya kifahari wanayo ishi na magari ya kifahari waliyokuwa wanatembelea, pia walikuwa na fedha nyingi sana.

“Careen atuwaingilii mipango yenu, lakini hakuna aja ya kusubiri sana, mnaitaji kufunga ndoa” alisema mzee Martin, “kwa sauti tulivu, “baba tutajadiri mimi na Michael maana atukuwai kuongea ilo hapo mwanzo” alisema Careen, ambae alimoyoni mwake alikuwa anajuwa kuwa Peter asingekuwabari swala la ndoa, ghafla vile, kutokana na misimamo ya kijana huyu, kuto kupenda kuwa tegemezi, “sawa tuawapa siku 21 tu, kuanza leo, mume mme fumga ndoa” alisema mama Careen, na hapo Careen aka mtazama Peter ambae pia alikuwa anamtazama Careen, Peter katoa ishala ya kuitikia kwa kichwa, kukubariana na mama Careen, ikiwa pia ni kumpa matumaini Careen kwamba mambo yatakuwa sawa.***

Naam Songea Tanzania, nyumbani kwa Careen, wakiwa awajuwi ili wala lile, waliangaa Polisi kadhaa wakivamia pale nyumbani, na kuitaji kuonana na Careen, hapo akaiywa Jasmin, mlisimamizi wa ulinzi na usalama wa eneo lote la nyumba ya Careen na kampuni yake, “samahani mheshimiwa, “naweza kuona waraka unao waruhusu kuingia hapa, maana atukuwa na taarifa yoyote ya ujio wenu” aliuliza Jasmin ambae mida hii, aikuwa katika vazi lake lakawaida, yani gauni, na kandambili miguuni.

Hapo askari kiongozi mwenye cheo cha constabe, akatoa karatasi na kumpatia Jasmin, ambae alilipokea na kulisoma kidogo, kisha akamrudishia, huku ana mwuliza, “je tunaweza kufahamu anaitajika kwa ajiligani, au kuna kosa amelifanya?” aliuliza Jasmin huuku akiwa amekazia macho yule askari constable, “ni vyema ukiacha kuhoji, na ukamleta huyo muyo bwana Peter, tuondoke nae” alisema yule askari, kwasauti iliyojaa amri, “Peter Jacob na mke wake, wamesafari leo saa nne asubuhi, kwa ndege binafsi, kuelekea #mbogo_land, na ata kaa huko kwa muda wa week moja” alisema Jasmin na hapo yule askari kiongozi akaonekana kushtuka sana, akamtazama mmoja wao, na ambae pia likuwa pia ametoa macho kwa mshangao.

Naam nikama walionekana kukosa majibu, yule askari kiongozi akamtazama tena Jasmin, “usitutanie we mpuuzi, kama utaki tutaingia ndani na kwenda kumtoa sisi wenyewe” alisema yule askari kwa sauti kali, “sikia mheshimiwa sahamani tunaomba dakika moja” alisema Jasmin, kisha akamwita mtu mmoja kati ya wafanyakazi waliokuwepo pale, akamweleza jambo kisha yule mwanamke akaondoka zake kuelekea kwenye nyumba za upande wakulia, yani zile za wafanyakazi, “kwahiyo ina maana gani, tutaendelea kusubirimpaka saangapi?” aliuliza yule askari, kwa sauti ya ukali, “sina ufahamu mkubwa wa sheria, hivyo nime mwita mwanasheria, aje kuona tuna fanyaje” alisema Jasmin kwa sauti ya awaida tu, “sidhani kama kuna sheria ambayo inaweza kutuzuwia kumkamata Peter Jacob” alisema yule askari, na wakati huo akaonekana yule mfanyakazi alie tumwa, akiwa anarudi uku ameongozana na kijana mmoja mtanashati, alie valia bukta ndefu kidogo,na tishet, niwazi wawili awa walikutana njiani.

“Salaam mheshimiwa, naitwa Alpha nimwanashria wa madam Careen na familia yake, pamoja na kampuni yote ya #mbogo_land sonara” asalimia yule kijana ambae nazani ndie alikuwa mwanasheria, kwa sauti tulivu yenye nidhamu, huku anaweka mkono mmoja kifuani na mwingine mgongonikaribu na kiuno, “poa” aliitikia yule PC, “Alpha awa maafisa wapolisi wanmwitaji Mr Peter, sasa naomba uwa sikilize, ili ujuwe kama utaweza kuwasaidia” alisema Jasmin, huku anamtazama yule kijana, ambae alimwita Alpha, “nakara ya walaka wa wito tafadhari?” alisema mwanasheria kwa sauti ya tulivu, huku ananyoosha mkono, kwenda kwa yule askari Constable, “mnajuwa nyie acheni ahceni ubabaishaji, sasa hiyo arrest warrant tutaotoa mala ngapi” alisema yuleaskari kwa sauti ya ukari, huku anatoa ile karatasi ambayo mwanzo alimpatia Jasmin, na Alpha akaipokea kimya kimya, na kuanza kuisoma kimya kimya.

Naam baada ya kuitazama kwa dakika kama mbili tatu, akamrudishia yule askari, “samahani afisa, sijaona zumuni la wito” alisema Alpha, huku anamtazama yule askari wa jeshi la polisi, maeneo ya kifuani, kisha akamtazama askari mwingine alie kuwepo pembeni, alafu akamtazama na mwingine tena, “mh! aijaandikwa anakamtwa kwaajili gani?” aliuliza kwa mshangao yule yule askari, huku analikunjua lile karatasi, na kuanza kulitazama, kama vile analiona kwa mala ya kwanza “sababu siyo muhimu, huyu anaitajika kwa mahojiano” alisema yule Constable, huku analikunja na kuliweka mfukoni,

Hapo Alpha akamtazama Jasmin, kwa macho yaliyo eleza mashaka, juu ya jambo flani, nikama walielewana na Jasmin, maana Alpha akamtazama tena yule askari kiongozi, “samahani afisa, kwa sasa mr Peter yupo mbali sana, nizaidi ya kilomita mia mbili themanini, toka hapa, yani ni nje ya nchi” alisema Alpha, kwa sauti ile ile iiyo jaa nidhamu, kama ilivyo desturi yao, watu wa #mbogo_land, “msituletee sanaa hapa, sas tunaingia ndani kufanya ukaguzi sisi wenyewe” alisema yule askari kiongozi, kwa sauti iliyojaa ubabe, kisha akagaeuka kumtazama mwenzie “ebu ongozana na mimi” alisema yule askari, akimweleza mwenzie, huku anaanza kutembea kuingia ndani, “samahani afisa, waraka unakuluhusu kumkamata bwana Peter, na siyo kuingia na kukagua nyumba ya madam Careen, pia kuna taratibu tatu za kukamilisha ili uingie ndani ya nyumba hii” alisema mwanasheria Alpha, kwa sauti ile ile tulivu ya upole.
Kusikia hivyo yule askari akasimama na kugeuka kumtazama Alpha, “kuzuwia polisi wasifanya majukumu yao ni kosa kishria nazani unafahamu ilo” alisema askari kiongozi, kwa sauti ya ukali, “pia ni kosa kisheria, kutao kutimiza vigezo vya kutimiza majukumu yako, hivyo ukiwa kama ni msimamizi wa usalama na ma sheria, nivyema kama ukizingatia ilo” alisema Alpha kwa sauti ile ile ya upole, ungesema ni doctor anaongea na mgonjwa,

“vigezo gani unazungumzia, inamaana una nifundisha kazi?” aikuwa sauti ya chini, ilikuwa ni sauti kali yenye chukizo, “nivyema kama tunaogea na kuelewana afisa, kwanza unatakiwa ulekebishe waraka, uwe wa kukagua nyumba ya Careen na kumkamata Peter, pia waraka huo unatakiwa ukakaguliwe ofisi za barozi ya #mbogo_land, wao ndio tatoa kibari cha mtu kuingia hapa, mtatakiwa kukaguliwa kabla ya kuingia ndani kufanya upekuzi wowote, au kumkamata mtu yoyote” alisema Alpha, kwa asauti tulivu.

Hapo yule askari kiongozi akacheka kwa dharau, “unamaanisha nini, kukaguliwa, unataka kusema unatilia shaka vyombo vya dola?” aliuliza yule askari, kwa sauti yenye kuonyesha kuwa alichukizwa na maneno ya Alpha, “afisa, nina sababu kadhaa za kuzingatia utaratibu huo, ukiachilia kitendo cha jeshi ili kupuuzia malalamiko ya boss wangu, ambae alisha vamiwa mala kadhaa, na kufwatiliwa na watu wasio julikana, pia ata leo sioni namba zenu za kazi, wala name tag vifuani mwenu” alisema Alpha, na hapo yule askari akaachia tabasamu, ambalo lilitoka kwenye uso wenye hasira, na chuki ya wazi kabisa,

Hapo yule polisi akageuka kumtazama mwenzie, ambae alikuwa karibu yake, ambae pia alikuwa anamtazama mwenzie kwa macho ya kushangaa, kisha yule polisi kiongozi, akamtazama tena Alpha, “kuto kuwa na name tag, ni utaratibu wetu, tunapofanya kazi nyakati za usiku” alisema yule askari huku anaingiza mkono mfukoni na kutoa kitambulisho, “hiki ni kitamburisho changu” alisema yuale askari ambae akutumia ata sekunde moja kuonyesha kile kitamburisho, yani aliharaka na kurudisha mfukoni, yani siyo Alpha, siyo Jasmin, au wafanyakazi wengine waliokuwepo pembeni, alie weza kuona ata andishi moja, ndani ya kitambulisho kile,

Jasmin akatazamana na Alpha, wakabasamuliana, kabla Alpha ajamtazama yule askari, “afisa nivyema ukianza tena mwanzo kufwata utaratibu, huo nilio kueleza, ila kunajambo unatakiwa kulizingatia, nikwamba unaemwitaji yupo nchini Mbogo Land, na anatarajia kutumia week moja huko Mbogo Land” alisema Alpha, na hapo yule askari kiongozi akatoa simu yake na kusogea pembeni, huku anabofya simu na kuipiga kisha akaweka simu sikioni, sekunde chache wakaanza kumsikia akiongea….……..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata