KIAPO CHA MASIKINI (82)

SEHEMU YA 82

ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANIN NA MOJA… Hapo Mlashani akashusha pumzi ndefu, kisha akatulia kama sekunde tano hivi, anatafuta swali la kuuliza, maana aliona kuna utofauti mkubwa wa jinsi hadithi yenyewe ilivyo, ukichukulia kuwa, yule mwanamke jana alimweleza kuwa amevamiwa mala mbili, na zote ameokolewa na Peter, na hiyo ni baada ya kuacha kutoa taarifa kituoni, kwakuona kuwa polisi hawakuwa na msaada wowote kwake, “OCD nivyema kama utakuwa unasema kile unacho kiamini, kuwa unauhakika nacho, vinginevyo nakushauri utafute jibu, maana hii ni kashfa kwa jeshi la polisi na wizara nzima ya mambo yandani, kwakushindwa kusimamia usalama wa raia, tena wakigeni” alisema RCO………..Endelea…

Kisha akakata simu, pasipo kusubiri jibu la OCD. Baada ya hapo RCO akatulia kidogo, kuchanganua majibu ya OCD “inawezekana vipi mtu akaacha kutoa taarifa kituo cha polisi, baada ya tukio moja kukosa ushaidi?” alijiuliza Mlashani, ambae alikuwa amekaa kwenye kiti chake ofisini kwake, “hapana kunajambo linaendelea, lazima nifwatilie na nimjuwe mshukiwa wa uvamizi huo” aliwaza RCO Mlashani, huku anachukuwa moja kati ya majirida yaliyokuwepo mezani kwake, kwenye kisaani kilicho andikwa kwa maandishi ya in, kisha akaanza kulipekuwa.****

Naam Baada ya mwadada Queen au Sada kutoka pale #mbogo_land sonara, alitembea kama mita mia moja hivi, kisha akasimama na kutazama kile kijikaratasi alichokuwa amekishika mkononi, yani kile alichopewa kule dukani, ambacho alikuwa amekifinyanga finyanga mkononi mwake, kisha akakifungua na kukitazama, kilikuwa kime andika, 23 loyar street in Trench Town, Mbogo Land, kitu ambacho Sada akukielewa kabisa.

Hapo Sada akageuka na kulitazama lile jengo la #Mbogo_land Sonara, kwa hasira, lakini akajikuta anapoa baada ya kuona maandishi ya Mbogo land Sonara kwenye jengo lile, “watakuwa na duka jingine” alijisemea Sada, huku anatazama tena kile kijikaratasi, ambapo bado akuambulia kitu, ukweli alijilahumu sana, kuondoka mle ndani bila kusoma kile kikaratasi, pengine engepewa maelekezo sahihi.

Hivyo Sada, ambae leo akuitaji kujuwa Emma yupo wapi, aka tazama kushoto na kulia kama angeona mtu wakumsaidia, mala akamwona mlinzi mmoja pale nje ya mbogo land Sonara, ambae alikuwa karibu na maegesho ya magari, hivyo aka msogelea kwa ajili ya ufafanuzi zaidi, awezekufika kule anakoweza kumpata Careen, ambae yeye anamtaja kuwa ni mwanamke walie mchukulia mume wake.

“mambo” alisalimia Sada, kwa sauti flani yenye swaga za kisister do, mala baada ya kumfikia yule mlinzi, “Salaam mgeni wetu, nikusaidie tafadhari” alisema yule mlinzi kwa sauti iliyojaa nidhamu, huku anainamisha kichwa chake, kwa heshima, “poa tu, eti anko, unapafahamu hapa?” aliuliza Sada, huku anamwonyesha yule askari, kile kijikaratasi, mlinzi akakitazama kwa sekunde chache kisha aka mtazama Sada, “unataka kwenda huko, au unataka kujuwa ni wapi?” aliuliza yule mlinzi kwa sauti tulivu, iliyoficha mshangao wake, “vyote vyote” alijibu Sada, kwa swaga zile zile za kujisexisha, na kujipa daraja flani la kipisi kali, akukumbuka kuwa mavazi chavu aliyovaa yalimtamburisha vyema kuwa ni mwanamke mwenye hadhi ya chini, au aliepishana na maisha mzuri, toka mwanzo.

Hapo mlinzi niwazi akaona kuwa Sada akuwa anakifahamu vyema alicho andikiwa kwenye karatasi, “hapa 23 unaitaji kufika au unaitaji kujuwa hipo sehemugani?” aliuliza tena yule mlinzi, safari kwa umakini zaidi, nikama swali lile lilimuuzi Sada, maana ni mala ya pili anaulizwa, “hivi unaelewa wewe, nataka nikamwone boss wenu, aya sasa umenielewa?” aliuliza Sada, na hapo ata yeye aliweza kuona mshangao usoni kwa yule mlinzi, ambae alimtazama Sada, kuanzia juu mpaka chini, kisha akarudisha macho usoni kwa Sada, ambae alikuwa anamtazama kwa macho ya mkumshangaa pia, “mbona unanitazama, au unaniona sina hadhi ya kuonana na huyu mwanamke?” aliuliza Sada kwa sauti yenye ujeuri ndani yake.

Mpaka hapo tayari Mlinzi alikuwa amesha fahau anaongea na mwanamke wa ainagani, “ok! huo ni mtaa ambao hupo kaskazini mwa jiji la Trench Town, huko nchini Mbogo Land, ambako Madam Careen na mume wake na mtoto wao, wameenda huko jana” alisema yule mlinzi, huku anamtazama Sada, “kumbe anamume, sasa Peter anamtakia nini?” aliuliza Sada kwa sauti iliyo jaa chuki, “Peter ndie mume wake, na ndie alie enda nae” alifafanua yule mlinzi

Kusikia hivyo Sada akatoa macho kwa mshangao, huku mdomo ukiwa wazi, “inamana Peter ….. amewezaje kufanya hiyo…. yani…. yani….” ukweli Sada ni kama akuamini alicho sikia, mawazo yake yali mtuma kuwa fedha walizo tumia kuendea huko Mbogo Land ni fedha za Peter, ambazo ata kama angekuwa nazo bado, basi ni kidogo sana, kiasi cha kwamba endapo ange fanikiwa kurudi, basi fedha zake zingekuwa zimesha kwisha, na yeye ange kosa kabisa fedha toka kwa Peter, “Peter ameamua kuchezea ela na huyo mwanamke, wake, anawezaje kuliia nauri ya kwenda huko, ata bakia na kitu kweli?” aliuliza Sada kwa sauti iliyojaa chuki, “mh! unamfahamu Peter yule mume wa madam Careen?” aliuliza yule mlinzi kwa sauti ya mshangao, “ndiyo yule ni mume wangu, yani ametoroka na mtoto, amekuja kutumia fedha na huyo Madam wenu” alisema Sada, kwa sauti yenye hasira na machungu, siyo ya kuigiza ni machungu toka moyoni.

Hapo mlinzi alionekana kushtushwa kidogo, “dada lakini mbona huyu bwana Peter, yeye aliibiwa na mzazi mwenzie, na kutelekezwa hotelini, ilibakia kidogo apelekwe polisi kwa kushindwa kulipia chumba, bahati nzuri alikuwa anafahamiana na Madam Careen, na sasa ndie mume wake, na wameondoka jana kwa ndege binafsi wameenda huko mbogo land, kuwasalimia wazazi wa Careen” hadithi hiyo ilimshtua zaidi Sada, na kumfanya aone aibu mwenyewe, kabla ajafanya maamuzi yoyote, akabandikwa swali jingine, “je unamfahamu huyo mzazi mwenzie alie muibia Peter?” aliuliza mlinzi.

Hapo Sada akujibu swali ilo, ambalo aliliona ni lakizushi, baada yake akageuka na kuondoka zake, akimwacha yule mlinzi akimsindikiza kwa macho, ya mshangao, huku yeye akiwa anahisi kichwa kina muuma, kutokana na kile alicho kisikia toka kwa mlinzi, “inawezekana vipi, yule mwanamke tajiri vile tena mzuri, akampenda Peter na ushamba wake” aliwaza Sada huku anaendelea kutembea, “kwahiyo sasa hivi ndio watakuwa wanafaidi tu, kupandege, kutembelea magari mazuri, kuvaa vizuri, kula vizuri, na kuishi vizuri pia, huku Peter analala na yule mwanamke mzuri” mawazo hayo yalizidi kumuumiza kichwa Sada, ambae aliendelea kutembea huku hasira na chuki zidi ya Careen na Peter, zikizidi kuongezeka kila dakika, pasipo kumuwaza tena Emma.***

Yap, week ilikatika, RCO akiangaika pasipo mafanikio, akuweza kufahamu, ukweli juu ya uvamizi wa Careen, ukweli juu ya maisha ya Peter ya mwanzo, akuweza kumjuwa mtu alie usika kwenye jaribio la utekaji nyala wa mjukuu wake, pia akujuwa chochote juu ya mtu anae usika katika kutoa habari za mipango ya jeshi la polisi, kila wanapo kumkamata bwana Kalonga, wala uhusika wa Peter kwenye usafirishaji wa dawa za kulevya.

Wakati tayari wakina Peter Careen walikuwa wamesha zunguka nchi nzima ya Mbogo land, ikiwa na golden Castle, kwa king Elvis Mbogo, ambae kiukweli alifurahi sana kuwaona wawili awa, ambae licha ya zawadi ya pete za gharama za harusi, pamoja zawadi kadhaa, wakadhaa, pia aliagiza gari mpya la kifahari aina ya Range Lover toleo la kisasa kabisa, ambalo mpaka mida hii, lilikuwa njiani juu ya Volvo semi terrela, linaelekea songea Tanzania, ikiwa mali ya bwana Peter, ambae mpaka sasa akuwa na ufahamu wowote wa juu ya uendeshaji wagari, pia mfalme Elvis aliaidi kuwafanyia sherehe kubwa ya kupendeza ndani ya ikulu yake, na mida hii ya saa saba mchana, walikuwa wanaelekea uwanja wandege wa wakimataifa Trench Town, kwaajili kuelekea Songea Tanzania.

Wakati huo ndani ya week hii, mipango yote ya Pitus Kalonga na OCD Mwanauta, ilikuwa imekamilika, huku wakipanga usiku wa siku hii ya jumapili wakauingize mzigo wote wa bangi, kwa kutumia gari la polisi, huku wakiwa wamesha fanikiwa kumchukuwa Peter.

Wakati huo tayari wakina Emma, walikuwa Luhuwiko, njia panda ya kwenda Airport, wakisubiri kuona kama kweli wanarudi leo, ili wahakikishe wanatoa taarifa kwa Kalonga ambae pia ata mjulisha OCD Mwanauta, ili akamdabue Peter…..…..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata