KIAPO CHA MASIKINI (83)

SEHEMU YA 83

ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA MBILI: Wakati huo ndani ya week hii, mipango yote ya Pitus Kalonga na OCD Mwanauta, ilikuwa imekamilika, huku wakipanga usiku wa siku hii ya jumapili wakauingize mzigo wote wa bangi, kwa kutumia gari la polisi, huku wakiwa wamesha fanikiwa kumchukuwa Peter. Wakati huo tayari wakina Emma, walikuwa Luhuwiko, njia panda ya kwenda Airport, wakisubiri kuona kama kweli wanarudi leo, ili wahakikishe wanatoa taarifa kwa Kalonga ambae pia ata mjulisha OCD Mwanauta, ili akamdabue Peter…..…..Endelea…

Nakumfanyia kile ambacho wangeona kina faa, kama malipizi ya uvurugaji wa mipango yao, na pia ukiachilia kumpteza RCO na makamanda wengine kuhusu muuzaji wa dawa za kulevya harisi, pia inge saidia wao kumpata Careen kilahisi.****

saa nane na nusu, ndiyo mida mbayo ndege ndogo binafsi, toka mbogo Land, ilipotuwa kwenye uwanja wandege wa Songea, na licha ya Careen, Peter, Michael yaya Glory na mfanyakazi mmoja kushuka toka ndani ya ndege, pia izilishushwa box kadhaa, za vitovya thamani, na vipodose pamoja na nguo za kisasa, ambayo Careena alivibeba kwaajili yake, Peter na Michael, pamoja na zawadi za wakwe zake, yani mzee Jacob na mke wake.

Baada ya kuhakikisha mizigo yote imepakizwa kwenye gari, la Careen ambalo liliachwa pale airport, na wao wakaingia ndani ya gari, kisha wakaanza safari ya kuelekea mjini, huku wakiongea kwa furaha na vicheko, wakisimuliana mambo ya huko mbogo land, ambayo kwa hasilimia mia moa yalikuwa ni ya kufuraisha na kupendeza, “mama lini tutaenda tena kwa bibi wakule” aliuliza Michael, ambae sasa alisha zowea kumwita Careen mama, “tutaenda week ijayo, kuchukuwa nguo na vitu vya harusi” alisema Careen, alie kuwa anaendesha gari taratibu.

Hapo nikama Caewwn alikuwa amemkumbusha kitu Peter “tena umenikumbusha Careen, inabidi tuliongee ili kwa kina, maana atuwezi kupuuzia maagizo ya wazazi wako, ila week tatu ni chache sana, bado sija jiandaa kwa lolote, inabidi niwe na kazi ambayo, itaweza kunifanya nimudu kuwa tunza wewe na Michael, ata wazazi wanapokuwa wanaitaji kitu, niwee kutoa bila kuangaika” alisema Peter kwa sauti ya kujiamini, ungesema anatania, ila kiukweli, alikuwa anamaanisha.

Yaya Glory na yule mfanya kazi mwingine waliachia midomo wazi kwa mshangao, huku Careen akiachia kicheko chepesi, “Peter nime kuelewa unacho maanisha, najuwa upendi kuwa tegemezi, si nimesema kuwa nitakufungulia mashamba kule kijijini, pamoja nakufungua kiwanda cha kusaga na kukoboa nafaka ili tuweze kuuza mikoani na nchi jilani, tena kule #mbogo_land atuwezi kukosa masoko, sababu mpaka sasa, wananunua bidhaa za mashambani toka nje ya nchi” alisistiza Careen, kwa sauti ya tulivu ya kubebeleza, huku anapunguza mwendo na kusimama mbele ya maungio ya barabara itokayo magharibi mwa mkoa wa Ruvuma, yani upande wa nyasa, mbinga na kitongoji cha Pelamiho, kuelekea Songea mjini, kisha akatazama kushoto na kisha kulia, huku akiwa amewasha taa za kuelekeza kuwa anaelekea kulia.

“Lakini week tatu asiwezi kukamilisha vitu vyote, na kuanza kuingiza fedha ambayo itanisaidia kuandaa harusi, na kufanikisha kile ninacho kueleza” alisema Peter, huku anamsaidia mke wake kutazama kushoto na kulia, “Peter jamani, kwani usichoelewa ni kitu gani, jukumu la harusi niachie mimi, hayo mengine tutakamilisha tu” alisema Careen huku anakanyaga mafuta taratibu kuingia baraarani, na kuelekea upande wa kulia, “sawa itakuwa vizuri sana, na kwa biashara hiyo tuta pata fedha nyingi sana” alisema Peter, ambae alikuwa na hamu kubwa ya kuliona gari lake jipya, alilopewa na Mfalme Elvis Mbogo, “kwahiyo Peter, tumesha kubariana tunafunga ndoa” aliuliza Careen, kwa sauti ya kujibebisha, huku anakanyaga mafuta kuelekea upande wa mjini, pasipo kujuwa kuwa, kwenye safu ya maduka, ya pale mtaa wa luhuwiko, kulikwa na watu wanne wamekaa ndani ya gari aina ya Toyota IST, wanawatazama kwa umakini mkubwa sana.

“ndiyo tumshakubariana, ila ujawajulisha wazazi wako, inabidi niende kwanza kijijini, nikawajulishe wakina baba, ili tuanze kufanya uratatibu wa kupeleka barua nyumbani kwenu” alisema Peter, na hapo Careen akaachia tabasamu pana, lenye kuonyesha kiwango cha furaha aliyokuwa nayo, “tutaenda wote Peter, au umesahau kuwa tume beba zawadi zao na inabidi mimi niwakabidhi, tena namba iwe kesho” alisema Careen kwa furaha, kisha akamgeukia yaya Glory, “ebu mpigie Jasmin mwambie aniandalie safari ya kesho nyumbani kwa wakwe” alisema Careen ambae alishindwa kuficha furaha yake akujuwa kuwa yajayo yanafurahisha, kama siyo kusisimua na kuuzunisha.****

Naam ASP Mwanauta OCD wa songea mjini, akiwa ofisini, alipokea simu toka kwa bwana Pitus Kalonga, nae akaiokea haraka sana, maana alikuwa wapo kwenye mapango mzito, ambao leo walipanga kuto fanya kosa lolote, “niambie Kalo, kuna habari mpya?” aliuliza OCD Mwanauta, kwa sauti ya chini, “kaka aina lemba, tayari wamesha toa AirPort na sasa wanaelekea mjini” alisema Kalonga kwa saut ya msisitizo, “ok! niachie mimi, nitakupgia baadae” alisema Mwanauta na kukata simu, kisha akapiga tena simu, ambayo aikuchelewa kupokelewa, “Panga hupo wapi sasa hivi?” aliuliza Mwanauta, kabla ata ya salamu, “tupo hapa nje ya ofisi afande, vipi tayari tuondoke?” aliuliza huyo Panga, “yes! tayari wamesha tua, wapo njiani wanakuja mjini, nazani watakuwa wanaelekea nyumbani kwao cha msingi nyie mkawasubiri, pale nyumbani kwao, hakikisha unamchukuwa huyo fala, alafu mnaenda kumfungia RMA (kampuni ya zamani ya utengenezaji wa barabara) alafu mida ya saa nne usiku, na baada ya hapo nita waambia cha kufanya” alisema Mwanauta kwa msisitizo na umakini mkubwa sana.

Ilo lilimshtua kidogo PC Panga, siyo kwamba akujuwa wanamkamata Peter kwa saabu gani, Panga alikuwa anafahamu kila kitu, “sasa afande, itakuwaje kama wakiitaji kumwona mshukiwa” aliuliza Panga, “watajuwaje kama tumemkamata, hakuna atakae mwulizia huyu mshenzi, mpaka tuwape taarifa kuwa tumesha mkamata, au umesahau kuwa hii operation ni yasiri, na wakisema kuwa wanaitaji kumwona, basi nitawaambiwa kuwa, ameifadhiwa sehemu siri anafanyiwa mahojiano” alisema Mwanauta kwa kujiamini, “sawa afande sisi ndio tuna ondoka hapa” alisema Panga, na kabla ajakata simu, Mwanauta akasisitiza jambo, “Panga akikisha hao askari watano ni wale wale tunaowatumia siku zote, na uhakikishe akuna kosa linafanyike” alisema Mwanauta.****

Naam, nusu saa baadae, tayari gari lakina Careen lilikuwa lina kata kona kulia kuacha barabara iendayo mitaa ya kusini, na kuingia barabara ya songea girls, kisha Careen akakanyaga mafuta kuifwata barabara hiyo, ambapo baada ya kutembea kwa mita kama hamsini hivi, wakiwa wamesha anza kuuona ukuta wa jumba la Careen, waka shangaa kuona gari la polisi, karibu na lango la kuingilia pale nyumbani kwao, wote wakazizima kwa mshangao na mstuko, maana yatari walikumbuka kuwa week moja iliyopita, polisi walikuja kumkamata Peter, na ilinionekana wazi kuwa, polisi walisha fahamu ujio wao, na walikuwa wanawafwatilia kwa kila hatua.

Lakini Careen akajipa moyo kuwa awawezi kumchukuwa Peter, ikiwa na sababu mbili, moja ni kwamba Peter akuwa nakosa lolote, pili nikwamba, tayari polisi walisha elezwa kuwa, wanatakiwa kufwata utaratibu wa kuja kumkamata Peter, ikiwa ni kuanzia kwenye barozi za mbogo Land, wawe na warrant inayoonyesha sababu za kukamata Peter, “naona awajaacha kutufwata fwata, sijuwi tume wakosea nini” alisema Careen ambae mpaka hapo akuwa ameliona gari lililokuwa lina wafwata nyuma yao, yani gari aina ya Toyota IST, ambalo lilisha wai kumfwatilia mala kadhaa, kwa lengo la kumdhuru.

Naam ile Careen anasimamisha gari mbele ya nyumba yake tu, na ata kabla gate alija funguliwa, tayari polisi watano, wenye bunduki zao, walisha lizunguka, na mmoja alisha shika kitasa cha mlango wagari, upande aliokaa Peter, na kujaribu kungua, lakini mlango ulikuwa umelokiwa, “kwa usalama wenu fungua mlango” alisema mmoja kati ya wale polisi, kwa sauti ya ukali iliyojaa kitisho,

Hapo Peter akajaribu kufungua yeye mwenyewe, lakini bado mlango uligoma kufunguka, “hapana Peter, uwezi kufungua mlango, sijaona mwanasheria wala watu toka ubarozini, siwezi kuluhusu wakuchukuwe” alisema Careen kwa sauti iliyo jaa uoga mkubwa, maana aliona kuwa wale polisi wamekuja kwa hali ya shari, na siyo maelewano, “Careen wacha nishuke wasije kuona tuna wabishia alafu wakapiga na bunduki zao” alisema Peter kwa sauti ya kunong’ona, “lakini Peter unauhakika gani na hao, maana mpaka sasa atujuwi kosa lako nilipi” alisema Careen, wakati huo mtoto Michael akiwa anashangaa tu, ajuwi chochote kinachoendelea.

Naam wakati huo huo lango la nyumba ya Careen likafunguliwa, lakini akuweza kuingiza gari ndani, maana tayari polisi wengine walikuwa mbele ya gari, “Careen ni bora kutii sheria, bila kulazimishwa, wacha nishuke nina uhakika nita rudi tu” alisema Peter, kwa sauti ambayo, ilificha uoga na wasi wasi wake, “nasema fungueni milango ya gari kabla atujavunja vioo” alisema askari alie onekana kuwa ni kiongozi wao, kwa sauti kubwa ya ukari, japo wote awakuwa na majinaifuani mwao, wala vyeo mabegani, “sawa Peter, lakini nawapigia simu watu wa ubarozini, na mimi namchukuwa mwanasheria tuka kuja huko kituoni” alisema Careen huku analegeza lock za milango na askari aliekuwa karibu na mlango akaufungua haraka na kumvuta Peter kwa nguvu, “mpuuzi wewe ulizania utatukimbia milele” alisema askari kiongozi, kwa sauri iliyojaa hasirra na chuki, huku anamvesha pingu mkononi mwake.

Baada ya hapo, kitendo bila kuchelewa, polisi watatu wakamshika Peter na kumnyanyua juu juu, kisha wakamtupia ndani yagari, kama furushi, hapo Mishael nikama aligundua kuwa baba yake akuwa salama kabisa, hivyo akaangua kilio kikubwa, akisaidiwa na Careen, “jamani kwanini mnamfanya hivyo, kwani amewakosea nini?” alisema Careen, kwa sauti iliyo jawa na uchungu, sambamba na kilio cha wazi kabisa, huku anashuka toka ndani ya gari na kulifwata gari la polisi, ambao sasa tayari askari walikuwa wameshaingia ndani yake, kisha gari likaondoka kwa speed kuifwata barabara ya kuelekea mikoa ya kusini, ata alipojaribu kulikimbilia, akajikuta ana shindwa kutokana speed ya gari lile.

Lakini akiwa analitazama lile gari la polisi huku anaangua kilio, na wafanyakazi wengine wakiwa wanatoka ndani ya gari, na ndani ya nyumba, mala akaliona gari dogo aina ya Toyota ist, lililokuwa lime simama mita hamsini, likigeuka na kuelekea kule lilikoelekea gari la polisi, kwa speed ile ile, ya gari la polisi.

Hapo Careen akaacha kulia ghafla, kiasi cha kumshangaza kila mmoja, asa yaya Glory, alie kuwa jilani kabisa na Careen, “yaya sasa nimeelewa kwanini aya yanatokea” alisema Careen kwa sauti iliyojaa hasira kubwa………..…

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!