
SEHEMU YA 84
ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA TATU: Lakini akiwa analitazama lile gari la polisi huku anaangua kilio, na wafanyakazi wengine wakiwa wanatoka ndani ya gari, na ndani ya nyumba, mala akaliona gari dogo aina ya Toyota ist, lililokuwa lime simama mita hamsini, likigeuka na kuelekea kule lilikoelekea gari la polisi, kwa speed ile ile, ya gari la polisi, hapo Careen akaacha kulia ghafla, kiasi cha kumshangaza kila mmoja, asa yaya Glory, alie kuwa jilani kabisa na Careen, “yaya sasa nimeelewa kwanini aya yanatokea” alisema Careen kwa sauti iliyojaa hasira kubwa………..…..Endelea…
“unamaanisha nini Careen, umejuwa sababu ya kukamtwa kwa Peter?” aliuliza yaya Glory, akionekana mwenye wasi wasi mwingi, lakini Careen akujibu swali la yaya, baada yake aliongea kitu kingine kabisa, “yaya mchukue Michael, mwingiza ndani, wapigie mwanasheria na Jasmin na Alpha, wanifwate kituo cha polisi haraka sana” alisema Careen huku anatembea kulifwata gari lake, “lakini Careen.. nivyema kama uta tulia kwanza ili.. ili..” alisema yaya Glory ambae sasa alikuwa anamshika mkono Michael ambae tayari alikua karibu yake, “hapana yaya, aipo kama unavyo fikilia, Peter yupo kwenye hatari kubwa sana, lazima nimsaidie haraka” alisema Careen huku anaingia ndan yagari, na pasipo kushusha mizigo waliyo kuja nayo toka Mbogo Land, akaondoa gari kuelekea mjini, akipita barabara ya upande wapili, siyo kule liliko elekea gari la polisi.**
Yap mida hii, Kalonga alikuwa nyumbani kwake anasubiri kusikia matokeo ya mpango wake, mala akasikia simu yake inaita, akaichukuwa haraka toka mezani na kutazama jina la mpigaji, maana sasa hivi alikuwa makini sana kutazama anae mpoigia, akaliona jina la Emma Pengo, akaipokea haraka, “niambie Emma vipi kuna jipya?” aliuliza Kalonga mala baada ya kuiweka simu sikioni, “boss mambo yapo fresh, jamaa wapo mbele yetu, wamempakiza huyu fala, hivi sasa tupo njiani tuna elekea RMA” alisema Emma kwa sauti iliyojaa furaha, “safi sanaaaaaaa, sasa kilicho bakia ni kitu kimoja tu, tufanikishe kutoa mzigo kule Linjumbwi, alafu tushereheke” alisema Kalonga kwa sauti ya shangwe, iliyojaa furaha kubwa, kisha akakata simu.
Baada ya kukata simu Kalonga akapiga kwa OCD, kwa lengo la kumpa taarifa ambazo aliamini kuwa bado ajazipata, bahati nzuri simu aikuchelewa kupokelewa.****
Naam Peter akiwa nyuma ya gari lile la polisi, akiwa amezungukwa na polisi wanne wenye bunduki, ame lazwa chini pasipo kuweza kuona anakopelekwa, sasa alianza kuelewa maana ya kile alichoambiwa na Careen kwamba asishuke toka kwenye gari, maana dakika kumi baadae gari lilisimama mbele ya majengo chakavu, ambayo ayakuwa na mwonekano wa kutumika hivi karibu, kwa kifupi nikama yalikuwa yametelekezwa muda mrefu.
Ile kusimama tu, Peter alinyanyuliwa juu juu na kutupiwa nje, ambako alijibwaga kama kiroba, nawakati anasikilizia maumivu, wale polisi tayari walisha shuka wote na kumsogelea “inuka wewe fala” alisema mmoja wao, huku anamzibua teke la tumboni, ambalo liliongeza maumivu mala dufu kwa Peter, ambae sas aliona wazi kuwa akuwa katika mikono salama, alithibitisha ilo dakika chache baadae.
Maana baada ya kuzibuliwa teke la tumbo, akainuka haraka ili kuepuka teke jingine, lakini alikuwa amejidanganya, maana alikutana na kofi zito la mgongoni, tembea bwana, unazani hupo kwa Malaya wako hapa” alisema mwingine huku anamsukuma Peter, kueleka ndani ya jembo moja kubwa, ndipo alipoguneua kuwa kuna gari jingine linaingia kwenye eneo lile, lililozungukwa na magari makubwa ya kubebea mchanga na vifusi, na mitambo ya kutengenezea barabara, lakini halikuwa gai la polisi kama lile walilokuja nalo wao.
Nabaada ya kusimama tu lile gari, wakashuka watu nne, ambao akuweza kuwaona vizuri, maana alikuwa anasukumwa kuingia ndani, “Panga, naona mpango umekaa sawa” alisema mmoja kati ya wale vijana waliokuja na gari la kiraia, “sasa je, atunaga kazi mbovu, tuna subiri bss acheke, ili watu baadae tukafanye yetu” alisema askari kiongozi, alie tajwa kwa jna la panga, huku awakifwata ndani ya jengo ambako aliingizwa Peter, huku ameshikwa huku na huku, na mkono yake ikiwa imevishwa pingu.
Peter akiwa ajaelewa kinachoendelea, aliingizwa kwenye chumba kikubwa sana, ambako ni kama ukumbi mkubwa sana, wenye madirisha makubwa yaliyokuwa wazi, ilionyesha wazi kuna watu waling’oa, baada ya kuona majengo aya yametelekezwa, wakati anangaa ilo, akashtuka akizolewa mtama na kujibwaga chini, ambapo aligonga kwenye sakafu ya saruji, na kutoa mguno wa maumivu, “jamani nime wakosea nini, mbona mna nifanyia hivi?” aliuliza Peter kwa sauti iliyogubikwa na maumivu makali, “kaa kimya we mpuuzi, siunajifanya bingwa wakuingilia mipango ya watu” alisema askari mmoja huku anampiga teke jingine la kwenye mbavu, teke ambalo lilimpata Peter barabara, na kumfanya ahisi kama pumzi ina bana kwa sekunde kama tano hivi, na kushindwa ata kutoa ukelele wowote, “anataka kujuwa amekosea nini?” ilikuwa sauti toka mlangoni, na hapo Peter alie kuwa bado yupo chini, akainua uso wake na kutazama, kule sauti ilikotokea.
Naaam!!! macho ya Peter aya kuamini yalicho kiona, ni baada ya kuwaona watau watatu, kati ya wale wanne waliokuja na gari la kiraia kuwa anawafahamu vyema kabisa, na siyo kuwa fahamu kwa urafiki, ila ukweli nkwamba ni watu ambao, wawili kati yao, aliwai kupambana nao mala mbili, akiwapiga kweli kweli, na huku yule mmoja akimpiga mala moja, siku akijaribu kumteka mtotoJasmin, mtoto wa mtu alie jitamburisha kuwa ni kamanda wa upelelezi wa makosa ya jinai, sasa kwanini watu awa wanamteka tena kwa kutumia jeshi la polisi, “inamaana waliomvamia Careen ndio waliotaka kumteka, mtoto wa yule mzee, na kwamba wanashirikiana na polisi wenyewe” alijiuliza Peter, huku anamtazama Dullah, alie kuwa anamsogelea kwa haraka, huku amekunja uso kwa hasira, na alipomfikia akavuta mguu wake kwanguvu na kuachia teke la kwenye makalio, “mshenzi wewe kum….mak.. leo utalipa ulichonifanyia” alisema Dullah, huku ana ongeza tena teke jingine, na wakati huo huo Emma na Janga nao wakasogea na kuanza kushushusha vipigo, alicho kifanya Peter aliekuwa amefungwa pingu ni kuziba uso tu, akiacha jamaa wajipigie wanavyotaka.
Naam baada ya kipigo kama cha dakika mbili tatu, waka mwacha, huku tayari Peter akiwa anaunja damu baadhi ya sehemu alizo chubuka, “ebu mfungeni kitambaa mdomoni” alisema Panga, alie shika simu yake mkononi, huku anatoka nje ya jengo lile chakavu, akifwatiwa na wakina Emma, na wezake watatu, huku wale polisi wakibakia ndani, “wacha nipige simu kwa…” alisema Panga, na kabla ajamalizia akasikia simu yake ikivuma kwa mtetemo, kiashilio cha kwamba ilikuwa inaita, na alipoitazama tu, akaona kuwa jina la mpigaji ni OCD.**
Naam Careen alisimamisha gari lake, mbele ya jengo la kituo cha polisi, na wakati huo huo, akaliona Toyota V8 analotumiaga Jasmin, likisimama nyuma ya gari lake, kisha akashuka Jamsin mwenyewe na kijana Alpha, ambao walimkimbilia Careen alie kuwa anaingia ndani ya jengo la kituo hiki, wakati huo awakuwa wameona dalili yoyote ya uwepo wa lile gari lililokuja kumkamata Peter, “karibu tuwasaidie tafadhari” alisema askari wakike, akiwa ni mmoja kati ya askari watatu waliokuwepo pale mapokezi, wakati huo wakina Jasmin na Alpha nao walikuwa wanaingia pale mapokezi,
Wakati huo huo, OC CID alie kuwa anatoka ofisini kwake, aliuona ugeni huo ukiingia pale kituoni, hivyo akarudi haraka ofisini kwake na kuacha mlango wazi, iliaweze kusikia kinachoendelea juu ya wageni wale, ambao tayari tetesi za kusakwa kwa Peter mume wa Careen alikuwa nazo, na zile taarifa za kuvamiwa kwa Careen pia alikuwanazo, na zilisha wai kukosa maelezo yakinifu.
“salaam enyi watendaji wa serikali” alisalimia Careen, kwa sauti tulivu yenye unyenyekevu, huku yeye na wakina Alpha wakiinamisha vichwa vyao, na mkono mmoja kifuani, akijitaidi kuzuwia hali yake harisi kwa muda ule, wale askari wawili wakiume, walikuwa wamekaa wana mtazama Careen, kwa macho ya mshangao na uchu, “salama dada nikutasaidie tafadhari” alisema yule askari wa kike, kwa sauti iliyojaa ukarimu, ambae mshangao wake aukuwa mkubwa, “nimekuja kujuwa sababu ya kukamatwa kwa mume wangu, bwana Peter Jacob” alisema Careen kwa sauti ile ile tulivu, wale askari watatu wakatazamana, kwa mashangao, kabla askari mmoja wakiume ajamjibu Careen, “mh! unamzungumzia yule mtuhumiwa wa dawa za kulevya na utekaji wa mtoto wa RCO, mbona bado ajakamatwa” alijibu yule askari, na hapo Careen akamtazama Alpha, kwa macho ya mshangao, na kuhamaki.
Alpha ambae alisomea sheria, akajuwa kwa sasa akimwachia Careen peke yake, basi kuna uwezekano wakukosa kile wanacho kiitaji, na kusabaisha matatizo kwao, hivyo akamwonyeshaishala ya kutulia, “samahani afisa, mimi ni mwanasheria wa #mbogo_land, ni kwamba juma tatu iliyopita mida ya saa tatu usiku, maafisa wa polisi wasio pungua wa tano, toka kituo cha polisi wilaya, walikuja nyumbani kwa madam Careen, kumkamata mume wake, kulikuwa na mapungufu katika ujaji wao, na pia awa kumkuta bwana Peter Jacob, hivyo wakaondoka tukiwa tumesha wapa utaratibu, leo mteja wangu akiwa amelejea toka nchini mbogo land, wamefanikiwa kumkamata oasipo kufwata utaratibu ata mmoja, hivyo tumeona tuje hapa kujuwa sababu za kumkamata na kama tuna weza kumuwekea zamana” alisema Alpha, kwa sauti ile ile tulivu.
Hapo maafisa wale wakatazamana tena, nikama walikuwa wanaulizana kinachoendelea, kabla yule askari wakike ajatoa maamuzi, “naomba muelewe, huyo mtu nikweli anatafutwa na jeshi la polisi, kwamakosa ya uuzaji wa dawa za kulevya, na utekaji, ila hapa hayupo, kama amekamawa basi ata kuwa kituo kinginena siyo hapa” alisema yule askari wakike, hapo Careen akashangaa zaidi, “madawa gani yalevya, Peter anauza, ninani alitaka kumteka?” aliuliza Careen kwa hamaki, “ndiyo mumeo anatuhumiwa katika kupanga mpango wa majaribio ya kumteka mjukuu wa RCO” nazani hapo mwanzo Careen akuwa amesikia vizuri, ila sasa ndiyo alisikia vyema.
“eti! unamaanisha yule mtoto mdogo, alie taka kutekwa jumapili iliyopita, pale NPF kids Coner?” aliuliza Careen kwasauti iliyojaa mshangao mkubwa, niwazi aliona kuwa kina jambo linaeendelea …..…..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU