KIAPO CHA MASIKINI (85)

SEHEMU YA 85

ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA NNE: alisema yule askari wakike, hapo Careen akashangaa zaidi, “madawa gani yalevya, Peter anauza, ninani alitaka kumteka?” aliuliza Careen kwa hamaki, “ndiyo mumeo anatuhumiwa katika kupanga mpango wa majaribio ya kumteka mjukuu wa RCO” nazani hapo mwanzo Careen akuwa amesikia vizuri, ila sasa ndiyo alisikia vyema, “eti! unamaanisha yule mtoto mdogo, alie taka kutekwa jumapili iliyopita, pale NPF kids Coner?” aliuliza Careen kwasauti iliyojaa mshangao mkubwa, niwazi aliona kuwa kina jambo linaeendelea …..Endelea

“nazani sasa umesha elewa, nivyema kama mtaacha namba za simu, tukipata taarifa yoyote, tuwajulishe” alisema askari wakiume huku anachukuwa peni na karatasi, ili aweze kuanza kuandika namba za simu, “ok! ziro…” alisema yule askari akimtazama Careen, “ziro saba moja saba” alitaja Alpha, huku na hapo yule askari akageuza uso wake kumtazama Alpha, nikama akutarajia kitendo kile, japo aliandika ile namba, lakini niwazi aliitaji namba ya simu ya mwana dada Careen.

Muda wote OC CID alikuwa anafwatilia maongezi hayo, ambayo alitambua kuwa kama kweli Peter siyo basi kuna mchezo umetengenezwa kwaajili ya mkuu wake huyo wa upelelezi mkoa, “kuna umuhimu wa yeye kupata taarifa hiyo haraka, ili akae akijuwa ili” aliwaza OC CID, huku ana funga mlango na kuchukuwa simu yake na kuanza kuibofya.

Naam baada ya kumaliza kutoa namba, wakaaga na kuondoka zao, “hatua inayofuata maadam?” aliuliza Alpha, wakati wanatoka nje ya kituo, “kuna kitu akipo sawa, tunaitaji kuwasiliana na ubarozi, waje nyumbani, wanaitaji kulijuwa ili” alisema Careen huku anatembea kwa haraka sana kuelekea kwenye gari lake, na alipoingia akaliwasha na kuliondoa kuelekea nyumbani, huku kichwani mwake, ikimjia kumbukumbu ya gari lile dogo Toyota ist, ambalo ni la vijana wa Kalonga, ambalo mala ya kwanza lilimsakama na yeye kukimbilia kituo kile kile cha polisi, pia lilikuja sikuile pale ofisini kwake, na vijana wawili wakamvamia, kisha kusaidiwa na Peter, ni vijana wale wale, ndio walio shiriki kumshambilia pale hotelini, MAKIMAKULUGA.

Ukiachilia ilo, pia Peter ndie alie msaidia kumwokoa mjukuu wake, siku ya pili RCO anapiga simu kuulizia habari za Peter, na usiku wa siku hiyo hiyo, polisi wakaja nyumbani kwake kwaajili ya kumkamata Peter, kwa tuhuma za dawa za kulevya ambazo Kalonga ndie muusika, na kuhusu utekaji wa mjukuu wake, Peter ndie alie zuwia, “inamaana huyu mzee ndie anae shirikiana na Kalonga?” alijiuliza Careen huku anaendelea kuendesha gari lake.***

“dah! huyu boya ndie anae mla yule demu mkali” alisema mmoja kati ya askari wanne waliokuwepo ndani ya jengo chakavu na Peter, kwa sauti ya kuto kuamini, “sijuwi alitumia mbinu gani huyu mshenzi” alisema mwingine, huku wanamtazama Peter ambae sasa Peter alikuwa amelala chini, pingu mikononi, huku amefungwa kitambaa usawa wa mdomo, ili asiweze kuongea chochote, akuwa na lakufanya zaidi ya kuwatazama wale askari wanne, wenye bunduki zao mikononi.

Pia wakati huo huo, aliweza kumsikia askari alie itwa Panga anaongeana simu, “ndiyo afande tayari tumesha mfikisha RMA… ndiyo afande tuna siburi maelekezo….. ndiyo afande akuna shida, gari linaweza kutupitia hapa hapa… sawa sawa nita mwambia aondoke” Panga alimaliza maongezi yake, na kisha akasikika akiongea na askari mwingine, “oya! peleka gari kituoni, sisi tuta kuwepo hapa mpaka baadae kunakazi tunatakiwa kwenda kuifanya” alisema Panga, na sekunde chache baadae likasikika lile gari la polisi likiwashwa na kuondoka zake.

Wakati huo Peter akakumbuka kuwa alikuwa na simu mfukoni, mwanzo alitaka kutoa simu mfukoni, ili ampigie Careen, lakini akasita kidogo, maana akuwa na uhakika kama wange mluhusu kutumia simu hii.

Hapo Peter akawasikia wakina Panga na wale jamaa waliokuja kiraia, yani wakina Emma, wakiendelea kuongea mambo yao, ambayo yalimvutia sana Peter, huku awa askari wanne, waliokuwa ndani wakiongea maswala ambayo kwake yalikuwa ni kama masimango, “Dah! hivi sasa ni saa kumi” hapa tuna ondoka saa kumi nambili kwenda kushukuwa mzigo Linjumbwi” alisema Panga kwa sauti ya kulalamika, “lakini mpaka saa nne tayari mtakuwa mmesharudi, baada ya hapo ni bata kwakwenda mbele, najuwa boss lazima anamwaga kwanja wakumfa mtu” alisema Emma, na hapo nahapo Janja akawadakia, “hivi huyu fala mwisho wake nini?” aliuliza Janja, “huyu tuna mficha kwa muda, baade afande atatoa maamuzi, ni kifo cha aina gani kitamfaa huyu mjinga” alijibu Panga, kama vile anaongelea jambo la mzaha.

Kusikia vile hapo Peter akajuwa kuwa, tayari mwisho wake umefikia, hivyo anakwenda kumwacha Michael, ambae ata mama yake amesha mkataa, pia anawaacha baba na mama yake, pia anaacha maisha mapya aliyoanza na Careen mwanamke ambae anaonyesha kumpenda sana.**

Akiwa ndani ya gari la kazini kwake, anaelekea nyumbani kwake, RCO Mlashani, akiwa ajuwi chochote kilichotokea, akasikia simu yake inaita, alipoitazama akaona kuwa mpigaji ni OC CID, akaipoakea kwa haraka, akiwa mwenye shahuku kubwa sana, “iambie CID, kuna jipya lolote” aliuliza RCO Mlashani, kwa shahuku, “afande hii nizaidi ya mpya, niyema kama tunge kutana” alisema OC CID, kwa sauti ya chini, iliyoonyesha niwazi alikuwa ofisini na akutaka watu wengine wajuwa anaongea na nani na anaongelea nini, nilikuwa naelekea nyumbani, vipi naweza kukupata wapi, “ok! natoka hapa ofisini, naomba tukutane barabara ya viwandani” alisema OC CID, na hapo kabla ajakata simu, RCO akamtazama dereva wake, “ebu geuza gari, uelekee barabara ya SIDO” alisema RCO, huku simu bado ikiwa hewani, “OC sasa hivi naelekea huko” alisema RCO kisha akakata simu, huku tayari dereva wake alikuwa anakata kona kuelekea barabara ya magereza, ili akazunguke kufwa barabara ya Iringa, huku RCO akiwa mwenye shahuku kubwa sana, ya kujuwa kile anachoenda kuambiwa.***

Yap! baada ya kuona wakina Careen wameondoka, ndipo askari wale watatu wa ale mapokezi, walipoanza kujadiri, “hivi inawezekana kweli wanachosema wakina Careen?” aliuliza yule askari wakike, “inawezekana ikawa kweli, maana ujuwe operationi ya kumkamata huyu jamaa, ni yasiri, pengine wamempeleka kwenye mahojiano kule shimoni, polisi mkoa” alisema askari mmoja wa kiume, na wakati huo OC CID akawa anakatiza pale mapokezi, na kutokomea nje, nao wakasitisha maongezi yao, soyo kwamba awakuitaji ofisa huyu asikie maongezi yao, ila ni kwaajili ya kumogia saluti.

Na baada ya kufanya hivyo, OC CID alitoka nje na kuingia nani ya gari lake, kisha akaondoka zake, kueeka upande wa SODECO, na wao wakaendelea na maongezi yao, “nazani nimuhimu afande OCD, maana itakuwa mbaya endapo ata pata habari hizi kwa mtu mwingine wakati sisi tuponae hapa hapa ofisini” alisema askari wakiume, ambae umri wake ni mkubwa kuliko wale wengine, huku anainuka na kuelekea ofisini kwa OCD.

Naam wakati yule askari akiwa anaenda ofisini kwa OCD, na yeye OCD mwanauta wakati huo alikuwa anaongea na simu, “sawa Panga nyie subirini hapo hapo, gari lita wapitia hapo hapo RMA, hakikisheni huyo fala, ana anabakia chini ya ulinzi mkali wa hao vijana wa Kalonga wakati nyie mnaenda kuchukuwa mzigo Linjumbwi” alisema OCD, kwa sauti ya chini, “lakini afande huyu jamaa mwisho wake tuta mfanyaje?” aliuliza Panga, “ilo siyo la kuuliza Panga, huyo kazi yake ni ndogo, maana atuitaji akutane na mtu mwingine yoyote na kuongea nae, maana kila kitu kitakuwa hadharani, cha msingi nikwamba, huyo bwana atajaribu kutoroka na polisi wakamshambulia kwa risasi, bahati nzuri mmoja ilimpata kisogoni, kasi hiyo itafanyika usiku baada ya kurudi linjumbwi” alisema OCD na hapo wite wakacheka, na wakati huo huo ikasikika hodi mlangoni kwa OCD.

“Nani?” aliuliza mwanauta, huku anatoa simu sikioni, “mimi PC Chima afande” isikika sauti toka nje ya ofisi, “ok! ingia” alisema Mwanauta, kisha akasogeza simu sikioni, “Panga nitakupigia baadae kuweni makini” alisema Mwanauta, kisha akakata simu, na kumtazama polisi contable Chima.

ambae alikuwa anaingia mle ofisini, akapiga saluti na kuanza kueleza juu ya ujio wa wakina Careen pale kituoni, “ok! kama umechukuwa namba yao ya simu, basi kama ata letwa hapa kituoni, utawajulisha mala moja” alisema OCD Mwanauta, na PC Chima akapiga salut na kutoka nje ya ofisi, hapo Mwanauta akapiga simu kwa Kalonga, ambae alikuwa ametoka kuongea nae muda mfupi uliopita, akimpatia taarifa ya kufanikiwa kwa kukamatwa kwa Peter, “niambie mzee baba?” alsema Kalonga kwa sauti iliyochangamka, akionyesha wazi kuwa, alikuwa amelewa, “kaka tayari wameshaanza kuangaika kumsaka vituoni, chamsingi tukutane kwajili ya kula bata huku tuna subiri vijana wakachukuwe mzigo na kumaliza kazi ya kumpoteza yule fala, kisha mambo mengine yaendelee” alisema Mwanauta, kwa sauti yenye furaha, “usijari kaka, nazani pale Kuchile pana tufaa sana” alisema Kalonga kabla awakata simu.***

OC CID alisimamisha gari mita chache, toka kwenye gate la SIDO, ni baada ya kuliona gari la RCO, likija mbele yake, nalo likasimama pembeni ya gari la OC CID, ambae alishuka mapa moja toka kwenye gari lake, na kuingia kwanye gari la RCO, “niambie kuna kitu gani kipya kilichotukutanisha” alisema RCO ambae alonekana kuwa na hamu kubwa ya kumsikiliza OC CID, “afande unajuwa lolote juu ya kukamatwa kwa bwana Peter Jacob, mume wa bi Careen Martin, yule mwanamke mmiliki wa #mbogo_land sonara?” aliuliza OC, ambae alikuwa amekaa seat ya nyuma ya gari lile la polisi lenye namba za kiraia.

Swali lile lilimshtua RCO Mlashani, ambae alimtolea macho OC, akionyesha wazi alikuwa anamshangaa, “hapana sijapata habari hii, lakini wamefanya kazi nzuri, maana huyu mshenzi naitaji asema anashirikiana na nani, na kwanini walitaka kumteka mjukuu wangu” alisema RCO, na hapo OC ikiwa zamu yake kushangaa, “afande hivi huyu Peter Jacob ni yule ambae alipambana na yulemtekaji wa mjukuu wako?” aliuliza OC CID, kwa sautui tulivu lakini yenye mashaka, “ndiyo, lakini imegundulika kuwandie mpangaji wa mango wa utekaji” alifafanua RCO, kwa sauti yenye uhakika, “afande ulisha wai kufikiri mala mbili juu ya ilo, maana yule mwanamke ameonekana kuwa na mashaka makubwa sana, na hivi sasa anawasiliana na ubarozi wa nchi yao, ili walisimamie swala ili” alisema OC CID, “kwani ilo lina kutisha, cha msingi tuhakikishe mtuhumiwa anahojiwa, na kueleza kila anacho kijuwa” alisema RCO, na hapo OC akaonekana kukubaliana na afande wake, “nisawa afande, lakini nivyema ukimjulisha Careen, mume wake yupo kituo gani” alisema OC na hapo kidogo RCO akashtuka, nakumtazama OC, inamaana mpaka sasa awajaambiwa Peter yupo wapi?” aliuliza RCO, kwa sauti ya shangao, “situ wao ata mimi pamoja na askari wa pale wilayani awajuwi mtuhumiwa yupo wapi” alisema OC, akitarajia kumwona RCO akishangaa…..…..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!