KIAPO CHA MASIKINI (86)

SEHEMU YA 86

ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA TANO: na hapo OC akaonekana kukubaliana na afande wake, “nisawa afande, lakini nivyema ukimjulisha Careen, mume wake yupo kituo gani” alisema OC na hapo kidogo RCO akashtuka, nakumtazama OC, inamaana mpaka sasa awajaambiwa Peter yupo wapi?” aliuliza RCO, kwa sauti ya shangao, “situ wao ata mimi pamoja na askari wa pale wilayani awajuwi mtuhumiwa yupo wapi” alisema OC, akitarajia kumwona RCO akishangaa…..…..Endelea…

Lakini ilikuwa tofauti kidogo, siyo kama alivyo tegemea “aina shida OC, siunajuwa kuwa hii ni peration ya siri, lazima watakuwa wapo sehemu wanafanya nae mahojiano, hivyo baadae tutapata jibu la kueleweka, maana najuwa lazima ataongea kila kitu” lisema RCO akionekana mwenye uhakika na anacho kisema.

Wawili awa walimaliza maongezi yao, na OC CID aashuka na kuingia kwenye gari lake, kisha kila moja akaondoka zake.***

Naam saa moja na nusu za jioni, ilimkuta Careen na wakina Jasmin, wakiwa nyumbani, wanaongea na vijana wawili, toka ubarozini, ambao mwanasheria aliwaeleza kila kitu kilicho tokea, kuhusu ukamatwaji wa Peter, muda mwingi Careen alikuwa anatokwa na machozi, kwa kumlilia Peter ambae mpaka sasa akukuwa na taarifa ya kituo gani alikuwa amepelekwa, na wale polisi, “imanaa huyo RCO anausika na ukamatwaji wa Peter” aliuliza mmoja kati ya vijana wale, “hatuna uhakika ila madam aliliona gari la watu ambao walishawai kuvamia mala mbili, lifwata gari la polisi lililombeba Pater” alisema Alpha, na hapo mmoja kati ya wale vijana toka ubarozini, akapata wazo, “Madam Careen swala ili inabidi tupate ufafanuzi toka kwa mkuu wa polisi mkoa huu wa ruvuma, inabidi tuwasiliane na afisa mausiano wetu, ili awasiliane na RPC akubari kukutana na sisi” alisema, alisema yule mmoja wao, na hapo Careen akadakia, “sasa kama nihivyo, tunasubiri nini, mpigie afisa mausiano wakati sisi tuliwa njiani, kuelekea nyumbani kwa RPC” alisema Careen huku anainuka na kuongoza nje ya jengo lile, akifwatiwa na wale vijana wawili Jasmin pamoja na Alpha.

“Sawa madam, ndio nampigia sasa hivi” alisema mmoja kati ya wale vijana wawili, aliekuwa anabofya simu yake, huku anatembea kutoka nje, na safari hii, waliingia kwenye magari mawili, yani wakina Jasmin wakaingia kwenye gari la Careen, ambae kutokana na hali yale, awakuweza kumwacha aendeshe gari mwenyewe, hivyo jasmine ndie alie endesha gari, huku wale vijana wawili toka ubarozini wakiingia kwenye gari ambalo walikuwa wamekuja nalo.
Kisha safari ikaanza kuelekea upande wa mabatini kwa RPC, wakati huo yule jamaa wa ubarozini akiwa anapiga simu, kwa afisa mausiano, wa ubarozi wa #mbogo_land, lakini kwenye gari alilokuwepo Careen, kunajambo zito lilizuka, nipale ambapo Careen alipopata wazo jipya, na wazo lenyewe ni kujaribu kuiiga namba ya simu ya Peter, ambayo ilianza kuita mala moja, “hiyo inaita” alisema Careen na kuwashangaza wakina Jasmin ambao awakujuwa Careen anampigia nani, “ninani huyo unampigia simu” aliuliza Alpha, ambae alikuwa amekaa seat ya nyuma peke yake, “naipiga simu ya Peter, naona inainaita, pengine polisi yoyote anaweza kuipokea, ili nijuwe yupo kituo gani” alisema Careen huku akisikilizia simu ambayo bado ilikuwa inaendelea kuita.***

Naam mambo yalikuwa yanaenda kama yalivyo pangwa, asa kwa upande wa OCD Mwanauta na bwana Kalonga, ambao mida hii walikuwa ndani ya hotel kuwa ya kisasa na tulivu, ya Kuchile, wakipata pombe kari kusherehekea mafanikio yao, maana waliamini kuwa ndani ya usiku mmoja watafanikiwa kutimiza mipango yao, “kaka kati ya siku ambazo nimekubari kazi zako, ni leo” alisema Kalonga kwa kusifia, huku anainua grass ya pombe kali na kuipeleka mdomoni, “nilikuambia kaka vijana wangu nawaamini, na hivi navyokuambia tayari gari lipo njiani linaenda kuwapitia wakina Panga, tayari wanaenda kuchukuwa mzigo” alisema Mwanauta kwa kujisifu, “alafu nime kumbuka kaka, kuna kitu bado sijafanya, inabidi nimpigie simu yule Malaya, nimsanifu” alisema Kalonga huku anatoa simu yake na kuanza kuibofya, huku Mwanauta akicheka kicheko cha ushindi.***

Naam mida hiyo hiyo naemeo ya luhila, mashariki mwa mji wa songea, lilionakana gari aina ya ashok layland rangi ya blue, lenye maandishi makubwa ubavuni mwake, yani Polisi, likipunguza mwendo karibu na njia panda ya songea boys, ambayo inaelekea upande wa kulia, lakini lenyewe likaingia upande wakushoto, kwenye mtaa wa majengo chakavu ya kampuni ya zamani ya matengenezo ya barabara TRM, ambako lili tembea kwa mwendo wa kika moja mpaka kusimama katikati ya majengo hayo chakavu, ambapo lilikungana na gari jingine dogo aina ya Toyota ist, lililokuwa lime simama mahari hapo sambamba na askari polisi mmoja na raia wanne, “Emma tutawaacha hapa sisi tutaenda kuchukuwa mzigo, nazani kwenye saa nne tano hivi tutakuwa tumesha rudi” alisema yule askari yani Panga, huku wanalitazama lile gari kubwa la polisi, ambalo licha ya kuwa lilikuwa limesimama, lakini bado lilikuwa linaunguruma, aina noma bro, nyie nendeni mtatukuta, chamsingi fanyeni faster, tukale bata” alisema Emma, huku wanaanza kutembea kuingia ndani, huku wakiwa awajuwi kilicho kuwa kinaendelea huko ndani, alikokuwepo Peter, alie fungwa pingu, kitambaa mdomoni, akiwa amelala chini, na kusimamiwa na askari wanne wenye bunduki zao mikononi.

Ambao sasa waliweza kuisikia simu ikiita, toka mfukoni kwa Peter, unaskia hiyo, kumbe tulikuwa atuja mpekuwa huyu mshenzi, alisema mmoja wao huku anaiwai pale alipokuwa amelala Peter, wenye maumivu makali na alama za majeraha sehemu mbali mbali za mwili wake, na kuichukuwa simu toka kwenye mfuko wa suruali ya kijana huyu, na kuitazama, alafu akacheka kwa kejeri, “demu wake anampigia simu” alisema yule askari, huku anasogea na kuwaonyesha wenzake, ambao walitazama na kuangua kicheko cha dharau na zihaka, “iweke pembeni hapo” alisema mmoja wao, na yule alie ishika simu, akaiweka kwenye dirisha, ambalo kiukweli lilikuwa wazi kabisa, ambapo simu iliita mpaka ikakatika yenyewe, na kusima mwanga.

Naam dakika chache baadae, Panga akaingia mle ndani, akiwa na wakina Emma Janja na Dullah, ambao, “oya mida yakazi hii, tunatakiwa kuondoka kuelekea shamba kuchukuwa mzigo, kisha tuje tule bata, na huyu bwege atabakia na wakina Emma, boss amesema tukirudi, tuta muuwa kwa risasi, tutasema alikuwa anajaribu kutoroka” alisema Panga, na hapo wale askari wanne wakatoka na kuelekea nje, “imekaa poa sana, najuwa boss leo atamwaga mkwanja kama wote” alisema Emma huku anawafwata wakina Panga, akiwaacha Janja na Dullah, mle ndani, “we fala kimbele mbele kime kuponza, yani boss ameangaika miaka yote hii, na kumkosa yule demu, alafu wewe unajibebea kilahisi” alisema Janja, huku ana mpiga teke la mgongoni Peter, ambae anaishia kuguna, kwa maumivu makali, maana akuweza kutoa sauti kutoa kelele kutokana na kitambaa alichofungwa mdomoni, “na mbaya zaidi unavuruga mipango yetu huyu mshenzi, anataka tukale wapi” alisema Dullah, huku ana yeye anamwongezea teke la mgongoni pia.

Wakati huo lilisikika lile gari kubwa la polisi, likiondoka, ikifwatiwa na Emma kuingia ndani ya lile jengo, “hoya Dullah, utabakia na huyu fala, wacha mimi na Janja tuka nunue bia za kusogezea muda” alisema Emma, kisha wao wakaondoka na kuingia kwenye gari wakimwacha Dullah, anamtazama Peter aliekuwa amesimama pembeni ya Peter aliekuwa amelala chini.***

Naam msafara wa Careen ulisimama nje ya nyumba ya RPC, na kuzungukwa na askari wawili wa jeshi la polisi, waliokuwa na silaha zao mikononi, Jasmini ndie alikuwa wa kwanza kushusha kioo, “samahani sisi ni watu wa kutoka #mbogo_land, ….” kabla ajamaliza kuongea Jasmin, mlango wa nyumba kubwa ukafunguliwa, na akatokea RPC, “karibu wageni karibu sana” alisema RPC, huku anasogelea kwenye gari, hapo wale askari wakasogea pembeni, kumpisha boss wao aongee na wagei wake ambao niwazi alisha juwa ujio wao.
Wakati RPC anasogelea gari, na wao wakina Careen wakashuka toka ndani ya gari, “karibu sana, nimepigiwa simu toka ubarozini, wamenijulisha kuhusu ujio wenu” alisema RPC wakati anasalimiana na wakina Careen, na wakati huo huo likaingia gari binafsi la staff officer, ambae alijiunga nao. na wote wakaingia ndani.

Naam baada ya kukaa kwenye makochi, hapo Careen akaanza kueleza kilicho mleta, ni kuhusu kukamatwa kwa Peter, ambae kwa habari zisizo lathmi, ameambiwa kuwa ni tuhuma za kupanga njama ya kumteka mkujuu wa RCO Mlashani, na tuhuma za kujiusisha na dawa za kulevya, “nikweli tunazo habari juu ya tuhuma za huyo mtu, ambae mwanzo atukumjuwa kwa jina, ila unasema tayari amesha kamatwa?” aliuliza RPC, ndiyo mzee wangu, lakini atujuwi yupo kituo gani” alisema Careen, ambae sauti yake bado ilikuwa aijakaa sawa, “atakuwa kituo cha wilaya, sababu wao ndio waliokuwa wanausika na operation hiyo” alisema RPC kwa kujiamini, “lakini mzee mpaka mala ya mwisho tunatoka pale kituoni, na wao walikuwa awana taarifa yoyote ya kukamatwa kwake, tumepiga simu ya Peter inaita tu aipokelewi” alisema Jasmin, na wakati huo simu ya Careen ambae mala ya mwisho alikuwa amepiga simu kwa Peter na aikupokelewa.

Hivyo Careen aaitoa simu yake haraka na kuitazama ile simu, ambayo namba yake ilikuja Kalonga, hakika moyo wa Careen ulishtuka sana, kiasi cha kila mmoja kumtazama Careen kwa mshangao, “huyooooo! anapiga simu” alisema Careen ambae alikuwa ametoa macho, akiwa tazama mmoja baaada ya mwingine, kama vile anawauliza apokee au sipokee, “ninani huyo?” aliuliza RPC, huku anamtazama Careen ambae alikuwa bado ameishika simu iliyokuwa inaendelea kuita, “ni Kalonga, naamini anausika na kukamatwa kwa Peter, maana nililiona gari la vijanawake wanalifwata gari la polisi, lililombeba Peter” alisema Careen, safari hii akiitazama simu yake, “pokea na uweke roud speeker, alisema RPC , na kisha wote wakatulia kimya kabisa.

Naam sasa Careen akabofya kitufe cha kupokelea simu, “hallow habari zajioni” alisalimia Careen kwa sauti ya upole, hapo kikasikika kicheko toka upende wapili wasimu, kilikuwa ni kicheko cha zarau, na kejeri, kilicho bebwa na sauti ya kiume, “pole sana Careen, kwakumpoteza mume wako” ilisikika sauti ya Kalonga ikiongea taratibu, na kwa dharau, “mume wangu ajapotea, mume wangu amekamatwa na polisi” alisema Careen akiwa na lengo la kumleta Kalonga kwenye uthibitisho.

Kwanza kabisa kikasikika kicheko chadharau, “Careen nanikakuambia kuwa Peter yupo kituo cha polisi, na kama unaamini hivyo basi niambie yupo kituo gani” alisema Kalonga, na hapo maaafisa waolisi na watu wote waliokuwepo wakatazamana kwa macho ya mshangao, asa ataff officer na RPC, ambao nikama walifumbuliwa masikio, “naenda kutoa taarifa polisi, kwamba wewe umeteka mume wangu” alisema Careen kwa sauti ya juu, lakini kika fwata kicheko kingine cha dharau, “Careen mimi ndie mwenye huu mji, unazani ni polisi gani ata kusikiliza wakati huyo fala wako anahesabika kama mtekaji na muuzaji wa dawa za kulevya” alisema Kalonga akimalizia kwa kicheko chake kile kile cha dharau, hapo Careen akakata simu, nikama alikumbuka jambo, afande nimegundua kitu, kuna polisi namjuwa anashirikiana na huyu Kalonga, ndio maana kila nipo toa malala miko yangu juu yake, uwa ayafanyiwi kazi” alisema Careen ha hapo RPC na RCO, waka tazamana kwa shahuku, “ebu telezee kila kitu Careen kwa nini umesema hivyo” alisema staff officer, na kisha wakatega sikio kwa makini kumsikiliza Careen ambae alieleza kitu toka wakati anatongozwa na Kalonga na kuanza kumchunguza kisha kugundua mambo machafu anayo yafanya Kalonga, “nikaamua kuachana nae, na hapo ndipo alipoanza kunitishia na kutuma watu wanivamie” alisema Careen, huku akiendelea kueleza jinsi alivyotoa taarifa polisi, ambao awakuchukuwa hatua yoyote zidi ya Kalonga, “ulisema kuwa unamfahamu polisi anae shirikiana na Kalonga?” aliuliza RPC, “ndiyo hakuna mwingine ni yule mzee ambae Peter alimsaidia kumwokoa mjukuu wake”

Naam RPC na staff officer waliposikia hivyo walishtuka sana na kutazamana “RCO Mlashani?” waliulizana wote wawili kwa sauti ya mshangao….. …..….. itaendelea…

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!