KIAPO CHA MASIKINI (87)

SEHEMU YA 87

ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA SITA: “nikaamua kuachana nae, na hapo ndipo alipoanza kunitishia na kutuma watu wanivamie” alisema Careen, huku akiendelea kueleza jinsi alivyotoa taarifa polisi, ambao awakuchukuwa hatua yoyote zidi ya Kalonga, “ulisema kuwa unamfahamu polisi anae shirikiana na Kalonga?” aliuliza RPC, “ndiyo hakuna mwingine ni yule mzee ambae Peter alimsaidia kumwokoa mjukuu wake” Naam RPC na staff officer waliposikia hivyo walishtuka sana na kutazamana “RCO Mlashani?” waliulizana wote wawili kwa sauti ya mshanga…..…..Endelea…

Nakabla awajapata jibu, staff officer akauliza tena, “inawezekanaje, wakati familia yake ndiyo ilinusurika kutekwa” alisema staff officer, kwa sauti ya kuto kuamini kile kilicho semwa na Careen, “ndiyo, tena Peter ndie alie msaidia mjukuu wake asitekwe” alisema Careen kwa msisitizo.

Hapo RPC na staff officer wakatazamana kwa mala nyingine, huku macho yao yakionyesha wazi kuto kuamini anacho kisema Careen, “Careen ili swala linaitaji maelezo yakina ili kulithibitisha, maana nijambo la kisheria zaidi” alisema RPC na staff officer akadakia, “maana hayo maelezo yako ayawezi kutoshereza kumuusisha Mlashani na tuhuma hizo” alisema staff officer, na hapo mwanasheria Alpha akashindwa kukaa kimya, “mhesimiwa, niwazi mnajaribu kukingia kifua mshukiwa wetu, sisi tumefika hapa, siyo kutoa shutuma juu ya mtu huyo ambae tayari tunaamini anausika moja kwa moja kutokana na dalili alizo zionyesha hapo mwanzo, sisi tume fika hapa ili kuomba ushirikiano wenu tumpate Peter, na taarifa hizi tayari zinaandaliwa ili zitumwe nchini kwetu, na baadae king elvis amjulishe raisi wa Tanzania” alisema mwana Sheria Alpha, kwa sauti tulivu, “sasa kijana unajaribu kuongea nini, inamaana unataka tukubariane na wewe kwamba Mlashani, anausika na kile kinacho mtokea Careen na Peter?” aliuliza RPC kwa sauti ya ukali.

Hapo sasa Careen akutaka kubakia kimya, “nimezowea kuona mkiwalinda waharifu, leo ametumia polisi kuja kumteka mume wangu, labda kama mna nufaika kwa hizo shughuri zake haramu, lakini nawahakikishia kuwa, kwa jambo hili sito kaa kimya, nitapaza sauti dunia nzima ifahamu kinachoendelea” alisema Careen, kwa sauti iliyo jaa uchungu.

Hapo RPC akamtazama staff officer wake, “ebu piga simu kwa afisamkuu wa week, ambae ni RTO, akueleze kama kweli huyo mtu amekamtwa na polisi, na kama amekamatwa yupo kituo gani” alitoa maagizo RPC na hapo staff officer akatoa simu yake na kuanza kupiga simu, Trafick officer wa mkoa, huku RPC wenyewe akiandika ujumbe kwenye simu yake na kuutuma sehemu.***

RCO Mlashan akiwa na furaha kwa kiasi flani, furaha ambayo ilitokana na kusikia kuwa mtuhumiwa wa mpango wa utekaji nyara mjukuu wake ameshakamatwa, alitulia nyumbani kwake huku mala kwa mala akitazama simu yake, akitarajia kupokea simu aidha kutoka kwa OCD au OC CID, akimweleza juu ya mahojiano na mtuhumiwa, “yani alitaka kunizidi akili mimi, sasa amesha juwa kuwa mkono wa serikali auchezewi” alijisemea moyoni RCO Mlashani, ambae alikuwa anaitazama simu yake, kila baada ya dakika tano, akitarajia kupokea taarifa yoyote, juu ya kukamatwa kwa mtu alie amini kuwa ndie mpangaji wa utekaji wa mjukuu wake, yani kijana Peter Jacob, “baba Sophy, mbona kama unafuraha sana leo, si tuambizane jamani” alisema mke wa RCO, kwa sauti iliyojaa utani.

Hapo RCO aka tabasamu zaidi, “ninafuraha kweli siyo utani, ujuwe kuna watu wanajifanya wajanja sana, hivi unafahamu kuwa yule kijana aliejifanya anamwokoa Jasmin sikuile ndie mpangaji wa utekaji nyala?” alisema RCO, huku anachukuwa simu yake na kuitazama, kisha anairudisha mezani, “acha utani baba Sophy, sasa afanye vile ili iweje, yani amteke yeyewenyewe, alafu amwokoe mwenyewe, na afanye hivyo akiwa na familia yake, inawezekana kweli?” aliuliza mke wa RCO kwa sauti ya kawaida ambayo, iliyoshesha kutokuzingatia swala lile, “kwanini ashindwe, ujuwe wauzaji wa dawa za kulevya wanaweza kufanya kitu mpaka unajiuliza kama anawaza kwa kutumia kichwa kama sisi au anasehemu nyingine ya kufikiri kabla ya kutenda” alisema Mlashani, akimalizia kwa kicheko, na mke wake akacheka kidogo, “yani katika upelelezi wako wote safari hii umeferi kabisaaaaa!” alisema mke wa Mlashani, akionyesha kuwa na uhakika na kile alicho kisema.

Lakini upande wa Mlashani, yeye akampuuzia mke wake, akiamini kuwa mke wake akuwa na sababu za msingi za kusema vile, “kwa taarifa yako imeshibitishwa na sasa tayari yupo mbaloni” alisema Mlashani na hapo mke wake akashtuka na kumtazama, “baba Sophy, hivi nikweli uwa mna wasingizia watu makosa, kweli yule kijana amekuwa muuzaji wa dawa toka lini?” aliuliza mke wa RCO, kwa sauti ya uchungu na kushangaa, ata mume wake Mlashani, akamshangaa mke wake, “we mama Sophy, kwanini unaongea kama unamfahamu yule mtekaji, kwa taarifa yako amesha wai kufanya hivyo kwa yule mwanamke Careen, alitengeneza matukio ya uvamizi na yeye akamsaidia ili ampate” alisema RCO, akionyesha anauhakika na anacho kisema, wakati huo huo akasikia simu yake ikitoa mlio wa kuingia kwa ujumbe, “lakini nilimsikia akiongea na mwenzie derea wa boda boda, ilionyesha kijana wawatu amefika mjini sikuchache zilizo pita, maisha yake yalikuwa huko kijijini” alisema mke wa RCO.

Ukweli licha ya maelezo yale ya mke wake, lakini Mlashani akuonyesha kuamini kuwa Peter akuwa mwalifu, “utakuja kuniambia mama Sophy, watu wanambinu chafu sana, na amaefanya hivyo ilikunivuta upande wake nipotezee kesi nayoichunguza sasa hivi ya dwa za kulevya” alisema Mlashani huku anachukuwa simu yake na kufungua ujumbe, ambao ulikuwa unatoka kwa RPC, akajuwa tayari mambo yapo wazi, “hupo wapi?” aliuliza RPC, nae akajibu “nipo nyumbani vipi kuna lolote?” kisha akaiweka simu pembeni, lakini azikupita ata dakika mbili akasikia ujumbe unaingia, “nikukute hapo” ndivyo ulivyo sema ujumbe ule, ambao ulimshangaza kidogo RCO, “kuna nini tena, baada ya mimi kwenda kwake yeye ndie aje kwangu” aliwaza RCO huku anaandika ujumbe, “ndiyo afande” kisha akautuma kwenda kwa RPC.****

Sada au Queen yeye mida hii alikuwa amejilaza kitandani, huku akipiga hesabu zake namna atakavyo enda kumvaa Peter kesho, na kusema kuwa ni mume wake, hakika mpaka sasa alikuwa anaumia rohoni, kwa kujiuliza kwanini Peter anamfanyia hivi, sasa akuwa anawaza juu ya Emma, ambae ndani ya week hii, alikuwa amelala siku moja tu pale nyumbani, na wala akumwuliza alikuwa wapi, na akutaka kujuwa alikuwa wapi, yeye mawazo yake yalikuwa kwa Peter, “kama vipi wanipe mwanangu, na wanifunulie duka kama la Kadara” aliwaza Sada, huku ana jigala gaza kitandani, maana akuwa na usingizi kabisa, ni kutokana na njaa iliyokuwa inamchamanda, baada ya chakula kidogo alichokula mchana, kuisha tumboni mwake, “yani kesho mapema tu, nafika pale madukani kwa yule mwanamke, alafu nalianzisha mpaka kila mmoja ajuwe kuwa Careen ameniibia mume” aliwaza Sada huku hasira na chuki izidi kumpanda kichwani mwake, usingesema kama yeye ndie alie kula kiapo kuwa awezi kurudiana na Peter, huku akimkana mumewake huyu, pamoja na mtoto wake, wakumzaa mwenyewe.***

Yap! Mashaliki mwamji wa songea, maeneo ya luhila TRM, lilionekana Toyota ist, likiwa linatembea taratibu, toka kwenye majengo ya kampuni ya zamani ya matengenezo ya barabara, na kuelekea kwenye makutano ya barabara ya songea boys na ile ya kuelekea mikoa ya kusini, “sasa ndio wakati wakula ela ya boss” alisema Emma, akimwambia Janja, ambae alikuwa nae ndani ya gari, maana walikuwa wawili tu, “dah! yani kaka hapa tuombe mzigo uingie salama, tunaenda kuta chetu, alafu tunaenda zetu Msogeze” alisema Janja, aliekuwa anaendesha gari.

Nahapo nikama alimkumbusha jambo flani “enheeee umenikumbusha, ebu wapigie wale mademu mwanangu, unajuwa ile ya sikuile ilikuwa nzuri sana” alisema Emma, na Janja akaseka kwanguvu sana, “unamanisha wale mademu wasikuile?” uliza Janja, wait huo wanakaribia kufika, Luhila stendi, “umeona hen, ilikuwa tamu kishenzi, na leo tutakuwa tuna badirishana mademu kama kwenye video” alisema Emma, ambae anaonekana alifuraia sana mchezo huo, “kwani Dullah, tutamwacha wapi?” aliuliza Janja, huku anakata kona kushoto, akielekea upande wa stendi wenye maduka mengi pamoja na bar, “achana na huyo mshamba, ataenda kwenye viwanja vyake” alisema Emma, kwa sauti ya dharau, Janja akacheka kidogo, “kijana wako huyo” alisema Janja huku anasimamisha gari pembeni ya bar moja iliyo kuwa na watu wachache, kati ya bar kadhaa zilizopo pale, “kha kimpango wake, yani tukitoka shamaliza hii inshu, tunamfikisha mjini kisha tunachana nae” alisema Emma huku anafungua mlango, na kushuka chini.

Yap! Janja alizima gari, na kutegua kitufe cha kufungulia mlango wa boot la gari lile, “sasa tuna chukuwa ngapi?” aliuliza Janja huku anashuka toka kwenye gari, tunaharaka gani bwana hapa tuna masaa kama manne au zaidi, wacha kwanza tupige bia za kutosha, mwachae Dullah apanmbane na hali yake” alisema Emma huku anaongoza kwenye bar, akufikilia kama kumwacha Dullah peke yake kule TRM, pengine kuna weza kubadiri matokeo muda wowote, maana mtu siyo shati, kwamba ukilitundika sehemu unalikuta hapo hapo, “imekaa vizuri hiyo boss” aliunga mkono Janja, huku anafunga gari na kumfwata Emma.***

Naam tayari ilisha timia saa tatu na nusu za usiku, sasa turudi nyumbani kwa RPC, ambako sasa, staff officer alikuwa amesha ongea na RTO ambae alisema kuwa akukuwa na taarifa yoyote ya kukamatwa kwa mtu anaeitwa Peter Jacob, ila akaahidi kujulisha endapo atapata taarifa hiyo, ukweli iliwachanganya wakuu awa wangazi za juu za jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma.

Nao wakatulia kidogo kama wanawaza jambo, huku RPC akiwa amesha panga kwenda nyumbani kwa RCO, akaongee nae juu ya jambo ili na pengine kumrudisha kijana wa watu, “jamani naomba muende nyumbani kwenu, mimi nafwatilia swala ili, nita wajulisha kinacho endelea” alisema RPC, na hapo mwanasheria, aka jibu, “mzee sisi tunaomba tuachana na wewe tukiwa tumesha juwa ukweli, maana atuwezi kusubiri zaidi wakati atujuwi polisi wamempeleka wapi Peter” alisema Alpha, na hapo RPC alitaka kutumia nguvu, lakini akaona aitakuwa na maana, pengine na yeye akaonekana yupo pamoja na RCO Mlashani.

Hivyo basi RPC, akaona wacha tu aende nao kule nyumbani kwa RCO, ili wakamsikie mwenyewe anasemaje, ok! staff waambie askari wawili na silaha zao, tuongozane kwa RCO, tutatumia gari langu” alisema hivyo na staff officer akatoka nje, huku akimwacha RPC anawakabiri wakina Careen, “naamini kuwa Mlashani awezi kufanya kitu cha kijinga kama hiki, maana nimtu anaefanya kazi yake, kwa umakini na uhadilifu mkubwa sana” alisema RPC, kwa sauti tulivu ya kirafiki, “lakini ni mtu gani anae kosa shukrani, kwa mtu alie msaidia kumwokoa mjukuu wake, siku ya kwanza polisi walifika mapema saa mbili, baada tu ya yeye kupiga simu, kumwulizia, na leo naambiwa eti kosa lake ni kupanga njama ya kumteka mtoto huyo huyo alie mwokoa, aya sasa aitoshi kukubari ukweli baada ya Kalonga kunipigia simu na kujitapa” alisema Careen, kwa sauti yenye machungu makubwa.

Ukweli kama unge mtazama RPC, usingefikilia kuwa alikuwa anawaza jambo gumu sana kichwani mwake, maana muda wote alikuwa anatabasamu, na kuonekana kawaaida, “sawa mama twendeni, nyumbani kwa RCO, yeye ndie ata tuambia Peter yupo wapi” alisema RPC na hapo wakainuka na kuelekea nje ambako waliingia kwenye magari kama walivyokuja, huku staff officer na askari wawili wenye bunduki zao, wakiingia kwenye gari aina ya Nissan safari, pamoja na RPC mwenyewe, safari ikaanza akiongoza RPC, aliekuwa anenda gari lake mwenyewe, “kaka unajuwa sijaelewa hiki kinachotokea, yani naona kama vile huyu mwanamke anauhakika na anacho kiongea” alisema RPC kwa sauti ya mashaka, “ni kweli kaka, kama kweli huyo kijana ndie alime mwokoa mjukuu wake, inakuwa iwe yeye ndie aliepanga kumteka?” aliuliza staff officer, lakini awakupata jibu. .. …..…..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!