
SEHEMU YA 89
ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA NANE: Naam hapo ndipo Mlashani alipo shtuka, na kuanza kukumbuka maneno ya mke wake, maana licha ya kulitambua gari la mkubwa wake wakazi, lakini pia aliyatambua magari mawili yaliyo ongozana na gari lile la RPC, kwanza kabisa ni gari la Careen, ambalo lilikuwa lina julikana na kila mmoja, maana lilikuwa peke yake pale mjini songea, na pengine mkoa wa ruvuma kwa ujumla, hiyo ilikuwa wazi kuwa ujio ule ni kwaajili ya ukamatwaji wa kijana Peter, ambae mpaka sasa anashutumiwa. ENDELEA
Pili alishtuka baada ya kuona gari lenye namba za ubarozi wa #mbogo_land, inamaana sasa inshu ipo kimataifa, kwamaana ni wazi kama inshu ni kama alivyo sema mke wake, kwamba Peter ausiki na chochote, basi taarifa lazima ziende ikulu na kumfikia rais ambae lazima ashushe kwa wariri wa mambo ya ndani, na hapo ni mammuzi mazito yange fwatia, lakini aikumtisha sana, maana yeye alikuwa na uhakika akuhusika na ile opereation, ya kumkamata Peter Jacob, yani mume wa Careen Martin, wakati huo Careen alikuwa amepiga simu na kuweka loud speeker nab ado ilikuwa inaendelea kuita, kwa sauti ya wazi kabisa.
RCO aliona milango ya magari yote inafunguliwa, na wakashuka watu kutona na magari waliyo yapanda, huku RPC akiongozana na askari wawili, “Jambo afande” alisamilimia RCO, huku amebana mikono yake usawa wa pindo ya suruali yake, “jambo RCO” aliitikia RPC, ambae ni wazi kabisa usoni kwake, alionekana kushindwa kujuwa aanze wapi, maana kwa jinsi anavyo mfahamu RCO Mlashani siyo mtu wakufanya kile alicho kishuku Careen, “karibu afande, kunajambo gani usiku usiku huu?” aliuliza RCO kwa sauti ambayo licha ya kuficha wasi wasi wake, lakini kwambali ungeweza kuona kuwa Mlashani alikuwa anamaswali mengi kichwani kwake, “RCO, kianzia sasa hupo chini ya ulinzi, unashuukiwa kushirikiana na muharifu ambae ni bwana Pitus Kalonga kupanga njama za kumteka bwana Peter Jacob” alisema RPC, japo ilikuwa ni sauti ya chini, lakini sauti ya RPC, ilikuwa ni kavu na ya kikamanda.
Hapo RCO akashtuka na kwanguvu na kumtazama Careen, ambae bado alikuwa ameshikilia simu yake iliyokuwa inaita, “inamaana mmeweza kuni tega na kuniingiza kwenye mtego, ndio kile mlicho niahidi baada ya kunipigia simu?” alisema RCO Mlashani kwa sauti ya mshtuko yenye kulalamika, wote wakamshangaa, akiwepo RPC, “afande naweza kufanya hivyo, hii ni njama ya kunizuwia nisiendelee na upelelezi” alisema RCO kwa sauti ya kulalamika, “Mlashani ata sisi tuumeshangaa, lakini kutokana na maelezo tuliyo yapata kutoka kwa mlalamikaji, niwazi unausika na swala ili, hivyo utaongozana na sisi mpaka kituoni ukachukuliwe maelezo, pamoja na kutaja sehemu alipo Peter Jacob, atutaki swala ili, lifike ikulu, maana umeona watu waubarozi wao, wanataka kupeleka taarifa hizi nchini kwao” alisema RPC, wakati huo wanaendelea kusikia mwito wa simu ya Careen, ambae akuchoka kupiga namba ya Peter.
Hapo RCO akazidi kushangaa, kwamba yeye anausikaje na swala lile, “samahani afande, naomba kujuwa mimi nausikaje na swala ili, “samahani afande naomba mneleze mimi nausikaje na swala ili wakati hii operation anausika OCD wa songea mjini?” aliuliza RCO ambae nikama alikubari yaishe, lakini ajulishwe kwanza juu ya uhusika wake, “bwana Mlashani, kwa mujibu wa maelezo ya bi Careen, ni kwamba ulipiga simu mchana wa tukio la kwanza la jaribio la kukamatwa kwa Peter Jacob, ulipiga simu mbogo land sonara, ukijaribu kupata habari za bwana Peter, na leo moja ya sababu za kukamatwa kwa Peter Jacob, ni jaribio la kutekwa kwa mjukuu wako….” wakati RPC anaendelea kueleza sababu ya kuusishwa kwa RCO na tukio la utekaji wa Peter.
Mala Careen akasikika akiongea kwa mshtuko, “wamekata!! wamekata simu” wote wakamtazama Careen ambae alipiga tena simu ile, na kuweka loud speeker kama kawaida yake, safari hii ilipokelewa mala moja, “hallow mmempeleka wapi mume wang…” aliuliza Careen kwa sauti ya ukali na jazba, lakini kabla ajamaliza, tayari upande wapili Peter akasikika, “Careen ….. Careen ni mimi ni mimi Peter, nime watoroka, kumbe ni wauwaji, siyo polisi, wamesema wanataka kuniuwa…” alisema Peter kwa sauti ya chini kama vile ananong’ona, kanakwamba, akutaka asikike kwa mtu yoyote, “Peter hupo salama, hupo wapi mume wangu awajakuumiza, niambie hupo wapi nije nikufwate Peter” alisema Careen kwa sauti kama ya kupagawa, “Careen ata sijuwi nipo wapi, kuna majumba chakavu, na nyasi nyingi” alisema Peter kwa sauti ile ile, ya chini, hapo ghafla RPC akadakia, “bwana Peter, ebu elekeza vizuri, hupo wapi, tuje tukufwate” alisema RPC ambae alikuwa ameisogelea simu, “sipajuwi sipajuwi kabisa, ila panaonekana kama vile porini, kuna vichaka vingi sana” alisema Peter, na staff officer akadakia kwa haraka, “ok! tuambie nikitu gani unakiona zaidi ya hizo nyumba chakavu na vichaka, ilituweze kuijuwa hiyo sehemu” alisema staff officer, wakati huo RPC anamtazama RCO, piga simu kwa afisa wa zamu, mwambie askari wa doria waje hapa haraka sana” alisema RPC na hapo RCO akachukuwa simu yake na kuanza kuipiga.
Wakati huo Peter akaendelea kusikika, “kuna magari ya kubeba mchanga, na magreda yaliyo aribika” alisema Peter kwa sauti ile ile ya chini, na hapo staff officer akamtazama RPC, huku akionekana kufahamu eneo usika, “afande huyu atakuwa TRM” alisema staff officer, na RPC sogelea tena simu, “Peter ni kweli hao waliokukamata ni polisi”” aliuliza RPC, na hapo wote wakatega sikio kusikiliza jibu la Peter, “Ndiyo ni polisi, wameva nguo za polisi, na walikuwa na gari la polisi, tena sasa hivi wameondoka wameenda kuchukuwa mzigo, huko Linjumbwi, wamesema watarudi tena kuniuwa” hapo kidogo RPC akaingiwa na mashaka, kwamba inakuwaje wamteke alafu wamwache peke yake, kisha wapange kurudi tena ili wamuue, “kijana kama wameondoka na kukuacha peke yako na wewe umetoroka, kwanini usifwate barabara, kutokea mtaani ambako unaweza kuulizia hupo sehemu gani” aliuliza RPC, huku swali lake likiwa ni kama mtego, kwa Peter, ilikubaini kama amejiteka au ametekwa, “mzee siyo kwamba waliniacha peke yangu, nilikuwa nalibdwa na mtu mmoja, ni yule ambae alitaka kumteka mtoto wa yule mzee, wenzake wameenda kununua bia, bado awajarudi, nime msukuma yule jamaa amejibamiza ukutani, nimemwacha amelala chini, sijuwi kama mzima au amekufa, fanyeni haraka kabla awajarudi watanikamata tena” alisisitizia Peter.
Na sasa RPC nikama alikuwa bado ajamwamini Peter, ndio maana akaamua kutupa swali jingine, wakati huo RCO akiwa anamaliza kutoa maagizo, “umemtambua mtu mwingine zaidi ya huyo mtekaji wa mtoto RCO?” aliuliza RPC, “ndiyo nime watambua wale vijana wawili walioenda kununua bia, ni wale waliomvamia Careen, kule hotelini” alisema Peter na hapo Careen akadakia, “ni watu wa Kalonga, washenzi sana hao” alisema Careen kwa sauti ya kukupayuka huku ana mgeukia RPC, nakuendelea kumweleza “baba yangu, naomba twendeni tukamchukue Peter, kabla awaja mpata, nitalipia mafuta ya magari yenu” alisema Careen safari hii akimtazama RPC, kwamacho yaliyokuwa yanalegwa na machozi, hapo RPC akamtazama staff officer, “fanyeni haraka hao askari waje haraka hapa, na waje akari wengi, ikiwezakana doria zote za hapa mjini zije hapa, na wasimbiwe tunaenda wapi” alisema RPC kisha akainamia simu ya Careen, ambayo bado ilikuwa hewani, “kijana tafuta sehemu ambayo awata kuona kwa urahisi, sisi tunakuja sasa hivi” alisema RPC, na kukata simu.
Naam wakati wakina RPC wanapanga namna ya kufika pale na kuzingira, na kuwamkamta wausika ambao lazima wange rudi, ndipo walipo wakayaona magari matatu ya polisi yakija pale kwa RCO.***
Naam, msafara wa magari mawili ya liyokuwa yana elekea luhila, hii sasa ulikuwa umefika mahenge, Kalonga akiwa mbele, na gari lake, akifwatiwa na OCD Mwanauta, ambae alikuwa mita kama hamsini, nyuma ya Kalonga, huku bwana Kalonga akonekana ana endelea kunywa pombe yake, kwakutumia chupa moja kwa moja, “alafu sija mjulisha Emma, kama naenda huko TRM, alisema Kalonga, huku anaweka chupa yake ya pombe kali kwenye sehemu ya kuifadhia chupa kati kati ya sea yake na abiria, kisha akapapasa kwenye dash board na kuchukuwa simu.
Baada ya hapo Kalonga aka akaanza kubofya simu yake kupiga simu kwa Emma, simu ambayo iliita kwa muda mrefu, mpaka ikakatika bila kupokelewa, lakini Kalonga akuishia hapo akaendelea kupiga tena na tena, lakini hali ilikuwa ni ile ile, ata mwisho simu ya Kalonga ilizima ghafla ata alipo jaribu kuiwasha ikagoma kuwaka kabisa, “hoooo! kum… make kumbe sijachaji simu” alisema Kalonga huku ana vuta waya wa kuchajia na kuchomeka kwenye simu yake, ambayo betri ilisoma ziro, wakati simu inaanza kuchaji, “lakini kwanini awapokei simu awa wapuuzi au wanatatizo” alijisemea Kalonga, huku anaongeza speed, kueleka mashariki mwa mji wa songea.****
Naam mida hii kule Luhila stendi, bado Emma na Janja wanaendelea kunywa bia zao kwenye ile bar, “hoya Emma, mida hii, unajuwa jamaa, watakuwa karibu wanarudi” alisema Janja, huku anaonyesha muda kwa saa ya simu yake, “ni kweli kaka ebu tuwai, ata hivyo sehemu yenyewe aina watu kabisa” alisema Emma kisha akachukuwa chupa ya bia yake ambavyo ilikuwa nusu chupa, na kuipeleka mdomoni, na kuinywa kwa awamu mbili, na kuwa amesha imaliza, “twenzetu” alisema Emma huku anainuka toka kwenye kiti, na kuongoza nje, akifwatiwa na Janja ambae tayari alikuwa amesha maliza bia yake.
Dakika chache baadae tayari walikuwa ndani ya gari, wakawasha nakuondoka, Janja akiwa kama dereva, safari ya kuelekea TRM ikaanza, “awajama nao wafanye haraka ili tumalize swala ili, ukaendelee na bata” alisema Emma, huku safari inaendelea, alafu ujambebea bia jamaa yako Dullah” alisema Janja huku anacheka kidogo, “achana nae, ataenda kunywa bia baadae tukitoka hapa, tena sijuwi kama ajatupigia simu” alisema Emma huku anachukuwa simu yake, na kutazama kama Dullah aliwapigia simu.
Naam nikweli Emma aliona miseed call, lakini azikuwa zinatoka kwa Dullah, zilikuwa zinatoka kwa Boss Kalonga, “khaaa! hivi kwanini sikukumbuka kutazama simu, yani boss amepiga kishenzi” alisema Emma huku anabofya ile namba na kuipiga simu ya Kalonga, ambayo ilisema kuwa bamba ya simu unayoipiga aipatikani kwa sasa, “boss apatikani, sijuwi kwanini” alisema Emma huku anaiweka simu mfukoni na wakati huo walikuwa wamesha karibia kufika TRM.**
Naam OCD Mwanauta akiwa mita chache nyuma ya gari la Kalonga, anaendesha gari lake, huku anakunywa pombe yake, akiwa ajuwafika kuwa ni kosa kisheria, na huo ndio wakati aliosikia simu yake ikiita, alipotazama ilikuwa ni namba ya afisa wa zamu, wa polisi wilaya, “anataka nini huyu mpuuzi, ajuwi kama huu ni muda wa bata” alijisemea OCD, huku anapunguza mwendo kidogo, na kuipokea simu yake, “hallow habari za jioni” alisema Mwanauta. kwa sauti tulivu, akijitaidi asionekane kama amelewa, huku analitazama gari la Kalonga ambalo lilikuwa linaongeza mwendo kuelekea mashariki ya mji huu, wa songea, “afande za jioni ni salama, lakini siyo salama sana, maana jioni hii, imepigwa simu kuwa askari wa doria wanaitajika kwa RCO, na alie piga simu inasemekana ni RPC mwenywe sijajuwa kuna inshu gani” alisema afisa wa zamu, wa polisi wilaya, “unasema awajasema kuna inshu gani?” aliuliza OCD, kwa sauti ya mshtuko, huku analitazama gari la Kalonga ambalo sasa lilikuwa limesha potea kwenye upeo wa macho yake.. …..…..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU