KIAPO CHA MASIKINI (91)

SEHEMU YA 91

ILIPOISHIA SEHEMU YA TISINI: “tumekwisha” alisema Panga kwa sauti ya chini, huku simu yake ikiendelea kuita, na wote wakatazama yake magari, ambayo sasa yalikuwa yamesha ingia mahali pale, huku magari matatu ya polisi yakisimama kwa kuwazunguka, huku askari waliokuwa kwenye magari yale wakishuka wka haraka, na kuzunguka huku wakiwa na silaha zao mikononi, “Panga nini kinaendelea, inamaana Mwanauta amenizunguka?” aliuliza Kalonga kwa sauti ya kushangaa na mshtuko. …..…..Endelea…

Huku akimtazama Panga, ambae alikuwa amesimama bunduki yake akiwa ajuwi cha kufanya huku simu yake mkononi, ikiendelea kuita, “inamaana afande analifahamu ili?” alijiuliza Panga, ambae sasa alikumbuka kuwa simu ya OCD Mwanauta ilikuwa inaita, basi akaipokea mala moja, huku macho yake yakiwa kwenye magari mengine yaliyo jipanga kwenye barabara ya kutokea.

Naam ile Panga, anaiweka simu sikioni, akasikika OCD mwanauta, “Panga msiende kule TRM, telekezeni mzigo porini haraka sana” alisema mwanauta kwa sauti yenye wasi wasi wingi na haraka nyingi sana, wakati huo tayari Panga alisha waona RPC staff officer na RCO, wakiwa wanasogelea pale walipokuwepo, wakiongozana na askari wengine wawili wenye silaha, “waliokuwa kwenye gari wote washuke chini na muweke silaha chini” alisema RPC mwenyewe, kwa sauti kali ya kikamanda.

Naam Panga akatoa simu yake sikioni, na kuweka silaha chini, huku Kalonga akiwa anatetemeka asijuwe la kufanya, wala wakumwomba msaada, “inamaana wakina Emma walilijuwa ili toka mwanzo, kwanini wasinge nijulisha sasa” aliwaza Kalonga, huku akikodoa macho kwa RCO, akisubiri kifwatacho, akamwona RCO anamtazama na kutabasamu.

Wakati huo askari wa nne pamoja na dereva wa lile gari kubwa walikuwa wanashuka kiunyonge toka kwenye lile gari, “staff askari wakague kwenye majengo, yote kama kuna wengine wamejificha, wawe makini, maana wanabuduki awa wapuuzi” alisema RPC, na hapo ataff officer aka toa amri mbili, moja ni yakuwaweka chini ya ulinzi askari wote walioshiriki kwenye uarifu, pamoja na bwana Kalonga, pili alitoa amri ya askari kukagua majengo yote manne yaliyo wazunguka, mala moja utekelezaji ukaanza, “lakini afande sisi atuhusiki na chochote, sisi tumekuja kukamata bangi ambazo zilikuwa zina safarishwa na bwana Peter Jacob” alisema Panga, wakati anafungwa pingu ambazo walifungwa wawili kwa wanne, yani pingu moja waliveshwa watu wa wili, na kuunganishwa mikono na wengine wawili, hiyo ilimhusu pia bwana Kalonga.
RPC alishindwa kuvumilia, “kaa kimya we mjinga, unazani utaenelea kutufanya sisi wajinga, na utamtaja mkubwa anae ongoza huu ujinga” alisema RPC huku anamuwasha kufi zito la usoni PC Panga, ambae aliyumba na kuanguka chini, na kuzii kuwabana wenzake kwa zile bangiri zenye meno meno, ambazo muda mfupi uliopita walimfunga Peter, ambae bado alikuwa kwenye maficho.

Sekunde chache baadae askari waliokuwa wanakagua nyumba zile wakaibuka na watu wawili, mmoja wao akiwa nai Dullah alie kuwa ametoka kuzindika muda huo, na bwana Peter, alie kutwa na pingu mkononi, na hapo ndipo Careen alipo jitokeza na kumkimbilia Peter ambae alikuwa ameshikwa na polisi huku na huku, maana bado walikuwa awaja mtambua kuwa siyo mtuhumiwa, “jamani Peter awajakuumiza popote mume wangu” alisema Careen wakati anamfikia Peter na kumkumbatia pasipo kujari polisi waliomshika, “huyo mwacheni, na mfungueni hizo pingu” alisema RPC, na wakati huo RCO alikuwa anamsogelea Kalonga, “kaka nazani sasa maigizo yako yameisha, utaenda kuishi unapostahili, na kuhakikishia kuwa kesi yako itaenda haraka sana, kuliko kesi nyingine yoyo iliyowai kutokea” alisema RCO, mala baada ya kumfikia Kalonga ambae akuweza kujibu kitu, na kubakia akitazama chini, “mtupieni kwenye gari lake lililobeba bangi, huyu mshenzi” alisema RCO huku anamzibua teke la kwenye makalio bwana Kalonga, na kumfanya mwamba huyu wa muda mrefu yani bwana Kalonga ayumbe kidogo, na kupepesukia mbele,

Wakati huo ndio wakati ambao Careen nae, limwona Kalonga, akiwa anadakwa na askari, juu na kuanza kukokotwa kupelekwa kwenye kalandinga, lililosheheni bangi, nae akamwachia Peter na kumsogelea Kalonga, ambae sasa alikuwa amesha fikishwa kwenye lile kandinga bado kupakizwa, “nilizania upo juu ya jeshi lote la polisi kama ulivyo kuwa unajinadi kumbe ulikuwa unategemea awa waharifu wenzako” alisema Careen kwa sauti tulivu, japo ilijawa na hasira, lakini ilikuwa na sanifu za kutosha, kitu ambacho ni kama kilimjaza hasira Kalonga, ambae alicheka kicheko cha kujilazimisha, “we malaya kama ulizani imeisha, sasa nakuambia bado aijaisha, huu ni mwanzo wa kurasa mpya, ambayo unaiandika wewe mwenyewe..”

Naam kabla Kalonga aja maliza kuongea utmbo wake, aishtuka kitako cha buduki, kikitua mdomoni mwake, na kugongonga lips zake za juu, na kupitiliza mpaka kwenye meno yake ya barazani, ambayo yalishondwa kuimili msukumo ule wa kitako cha bunduki, ikasikika gu!, ukweli Mwanauta alishindwa ata kupiga kelele, maana jino lilisha tangulia kwenye koo, sambamba na damu kama nusu lita hivi, akabia anakoo na kutema damu na kile kipande cha jino, “unamuda wakuongea upuuzi wako ebu panda kwenye kwenye gari mjinga wewe” alisema askari alie mtwanga na Kalonga, akimsindikiza na teke la kwenye makalio, lilimsukuma mpaka kwenye kuta ya gari na kujipigiza usawa wa kipanda uso, kisha akaanguka chini, “mimi sipandi kwenye gari mpaka mwanashria wangu aje hapa” alisema kwa sauti ya juu, kalonga, akiwa bado yupo pale chini.

Na hapo nikama alifungulia hasira za RCO, askari huyo mpuuzi apande mwenye kwenye gari bila kushikiliwa na mtu yoyote” siyo Kalonga pekeee na wakina Peter, ata mimi sikuamini kama mtu alie fungwa pingu, alafu mwenye kitambi kikubwa kama cha Kalonga, anaweza kupanda gari refu kama lile, lakini nilijionea mwenyewe, ndani ya dakika tatu, ambazo zilimpa uwezo Kalonga wa kuinuka pale chini na kupanda kama speer man, kwenye lile gari.

Maana ile RCO anamaliza amri yake, sijuwi ata ni uharaka gani ulitumika kukata fimbo za miti ya mwarobaini, ambazo ziliishia mwilini mwa Kalonga, kila mmoja akitandika sehemu yake, bila kujali ni wapi fimbo inatua, fimbo ambazo zilimwinua Kalonga pale chini, na kusimama haraka, kisha akakimbia kufwata mlango wa wanyuma Kalandinga, huku fimbo zikiendelea kutua mgongoni mwake, na yeye akitoa miguno ya maumivu.

Sasa kwenye kupanda ndio ikawa mazingaombwe, maana Kalonga akiwa amini kama anaweza kulukia pale juu, aka bakia pale ana mlangoni ana subiri kupakizwa, kamaa alizania kuwa kauri ya RCO, ilikuwa niyautani tu, hapo fimbo ziliendelea kulindima kwenye mwili wa Mwanauta, bila kuchagua, mpaka alijikuta ana piga kelele kama mtoto, “mtaniuwa jamaniiiii! naomba mnisameheee” lakini aikusaidia, fimbo ziliendelea kulindima. hapo Kalonga alipo, sijuwi alipata wapi uwezo wa kudaka imlango wa gari, na kujivuta mpaka juu, kisha akajiangushia kwa ndani, na huo ndio ulikuwa mwisho wa viboko kwake, na dakika chache baadae, wakaondoka zao, ni baada ya kupolisi kuhakikisha wamekagua eneo lote, na kwamba hakuna mtu alie salia. awa kuacha magari yale mawili yani lile la Kalonga na lile la Emma.**

Wakati aya yanaendelea Emma na Janja walikuwa njiani wanautwanga kwa mguu, kuelekea mjini, “kaka hapa twende mahenge tukajichimbie ghetto, mpaka tumpate boss, tumweleze kilichotokea, vinginevyo hatuna ujanja” alisema Emma, wakati huo wanavuka mto wa luhila wa daraja la kwanza, na kuvukia kwakuchile kijijini, “ila Emma, sikunyingine tuwe tuna chagua watu wenye akili zao timamu, sasa Emma amewezaje kuzidiwa ujanja na fala kama yule” alisema Janja, kwa sauti ya kulaumu, “nani alijuwa kuwa Dullah anaweza kufanya uzembe wa namna ile, ile yule jamaa nae nikama mwanga, siunakumbuka amesha wai kutuzidi ujanja mala mbili, na ile ya NPF ya tatu” alisema Emma, huku wakiendele kuchanja mbuga, kueleka mjini, ambako ingewagharimu masaa kama tatu na nusu au manne hivi, mpaka kufika mahenge nyumbani kwa Emma, ambako waliamini wata kumta Queen, ambae ndie wata kuwa wanamtuma nje na kuwaletea maitajio yao mbali mbali.****

Yap! ASP Mwanauta, alisikia kila kilichoendelea kupitia simu yake ambayo likuwa amempigia Panga, wakati huo tayari alikuwa amesha rudi nyumbani kwake na kulala, kichwani mwake akipanga majibu ambayo atayao ayanafaa kwa yeye kuwajibu wakubwa wake, ili kujichomoa kwenye janga ili, ambalo kwa sasa akuwa na uwezo wowote wa kumwokoa mtu yoyote, iwe askari wake wakina Panga, au wakina Kalonga, ambao ni washiriki wake wakubwa, “sasa ni wakati wa kila mmoja kufa na lake, mimi nilisha jaribu kumwokoa, lakini yeye alikuwa amezima simu” alijisema Mwanauta ambae usingizi ulimkataa kabisa.***

 

Baada ya kufika kituo kikuu cha polisi mkoa wa ruvuma, na kuwasweka ndani wakina Panga, na askari wenzake pia Kalonga na Dullah, wakiwekwa kwenye selo yao, peke yao. wote wakiwa wamesha kaguliwa na kunyang’anywa kila kitu, RPC akawaluhusu wakina Careen waondoke na kwamba kesho yake Peter angetakiwa kuja kutoa maelezo yake pale kituoni, lakini RCO pia akatumiamuda huo kuongea na Peter, “kwanza nataguliza samahani bwana Peter kwa kukuto kutilia maanani kile walicho kupakazia awa jamaa, maana ili swala lisinge fikia huku lilikofika” alisema RCO kwa sauti tulivu, huku wakina Careen na wakina RPC wakisikia, “pia niombe msamaha kwa Careen, najuwa umeniona sina shukrani, lakini kumbukeni kuwa mimi ni binadamu pia, na siwezi kuwa mkamilifu kwa asilimia mia moja, hivyo naomba mnisamehe” alisema RCO Mlashani.

Baada ya hapo wakina Careen wakaondoka zao kueleka nyumbani kwao, wakiwaacha makamanda awa watatu, yani RPC staff officer na RCO, walipo itana pembeni na kuanza kujadiri, juu ya swala ili, “hapa bado atujamaliza, kuna viongozi pale wilayani waliosimaia upuuzi huu, na mshukiwa wa kwanza ni OCD mwanauta” alisema RPC, na kueleza kwanini alisema vile, “sababu yeye ndie alie tueleza juu ya operation ya siri anayotaka kuifanya, na alifanya hivyo ilikumsingizia kijana huyu, na kuficha maovu ya huyu mshenzi Kalonga, kumbe mala ya kwanza awakujuwa kama Peter amesafiri, ndio maana wakaenda na kumkosa, na walipojuwa amesafiri, wakaamua kumvizia airport, na umteka mala tu alipokaribua nyumbani kwake” alisema RPC, kabla ajatoa maagizo ya kukamatwa kwa OCD mwanauta, na pia peleka taarifa makao makuu ya jeshi la polisi, kueleza juu ya tukio ili” alisema RPC wakati akimaliza kutoa maelekezo yake.

Wakati RPC ana maliza ndipo staff officer alipokumbuka jambo….…..….. itaendelea…

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!