KIAPO CHA MASIKINI (94)

SEHEMU YA 94

ILIPOISHIA SEHEMU YA TISINI TATU: Japo gari liliwaka, lakini Nusu busara alishtuka gumi, ikigonga kwenye kioo cha upande wake wa dereva, lakini kioo akikuvunjika, na hapo Mzee huyu, akaona wazi hatari iliyopo mbele yake kwamaana aliona kile anachofanyiwa Sada, ambae sasa alikuwa anapigwa kama wizi, pale alipoanguka, mzee wanusu busara akaondoa gari kwa speed kuelekea mbele yani kule iliko nyumba ya Emma, kule ambako alikuwa anafahamu kuwa, kuna njia ya kutokea upande wapili wa mtaa ule. ..…..Endelea…

Lakini basi muda huo huo, akasikia jiwe zito likituwa kwenye kioo cha nyuma cha gari lile, likipitiliza ndani huku kioo kikimwagika kama mchanga au changalawe ilizo mwagwa kwenye bati, lakini aikumfanya asimamishe gari lake, alizidi kukanyaga mafuta kutokomea zake, huku nyuma akiuacha msala wote kwa Sada, ambae alipigwa na kukanyagwa kama mbwa alie lamba keki ya birth day, mpigaji akiwa ni Emma mwenyewe, ambae akujari kilio alicho kuwa anakitoa Sada.

Hakika kilikuwa ni kilio kikali sana, kilichosababishwa na kipigo cha mbwa koko, maana Sada butuliwa teke la uso, na kabla ajakaa sawa akakanyagwa mkono ambao aulitoa mlio wa mvunjiko kisha akaakabigwa teke la mbavu, na kabla ajakaa sawa, akabigwa mateke mfululizo ya tumboni na mbavuni, huku mwisho Emma akishusha kwanguvu mguu wake, juu ya mguu wa Sada, akikita mala kadhaa, bila kujari matokeo yake.

Kipigo kitakatifu kilikoma pale ambapo, kilio cha Sada kilipo koma ghafla, na mschana huyu kuanza kuhema juu juu, huku akitanua midomo kama samaki alie tolewa nje ya maji, “kufa hapo hapo, wewe ndie nuksi kabisa, katika maisha yangi, yani toka nimekutana na wewe nimekuwa na mikosi mingi sana” alisema Emma huku ana mpekuwa Sada na kuchukuwa funguo ya nyumba yake, kisha kuanza kutembea kurudi upande iliko nyumba aliyopanga, “Emma tuna mwacha hapa?” aliuliza Janja, huku anamfwata Emma, “achana nae aliwe na mbwa, yani anatomb… kama paka shume” alisema Emma kwa hasira, huku wanaendelea kutembea kuifwata nyumba yao pasipo kujuwa kuwa kama wana wageni usiku ule.

Naam wawili awa, walifika nyumbani na kuingia ndani lakini kabla awaja fungua mlango wa chumba cha Emma, mala wakasikia vishindo nyuma yao, ile wanageuka, wanakutana macho kwa macho na polisi kadhaa wenye silaha mikononi, na mitutu ya bunduki zao ikiwa ina waelekea, “tulie hivyo hivyo, msijaribu kufanya chochote cha kipumbavu” ilikuwa ni sauti ya juu iliyo jawa na amri, toka kwa askari mmoja kati ya wale walioingia mle ndani, “tumekwisha” alisema Emma, kwa sauti ya chini, “wekeni mikono vichwani mwenu kisha pigeni magoti” aliamrisha yule askari kwa mala nyingine, “kaka lazima tufanye jambo, atuwezi kwenda jela kilahisi hivi” alinong’ona Emma, kwa sauti yachini huku wanaweka mikono kichwani na kupiga magoti, “Emmanuel na Hussein mpo chini ya ulinzi, kwa kushiriki utekaji nyala, na usafirishaji wa dawa za kulevya” alisema askari yule mwenye cheo cha sajent, ambae sasa alikuwaanawasogelea wali wale, kwa lengo la kuwafunga pingu wakina Emma.

Yap! ile alipowakaribia tu, Janja na Emma wakainuka ghafla na kumsukuma yule polisi, kwanguvu sana, ane ambae akuwa amejiandaa, aliyumba kwanguvu na kuwasukuma wenzake, ambao walikosa uelekeo, na ile wanakaa sawa, tayari wakina Emma walikuwa wamesha fika mlangoni, na kukimbilia nje, ambako walikutana na polisi kadhaa waliokuwa wamelekeza mitutu yao mlangoni, lakini kwa kuofia kuwapiga risasi, wenzao, wale polisi walishindwa kufytua risasi.

Nahapo ndipo wakina Emma walipo zania kuwa hiyo ndiyo nafasi pekee kwa wao kukimbia, na kutokomea zao, maana walichomoka mbio kuifwata chocholo iliyokuwa karibu yao, pasipo kujuwa wanafanya kosa kubwa sana, maana kitendo cha kukimbia toka mlangoni, ambacho kilikuwa lazima wakifanye, kama wanaitaji kutoroka, kiliwatoa kwenye usawa wa malengo ya bahati mbaya ambayo yangetokea kwa askari wengine, waliokuwa wanatokea ndani.

Hivyo basi, ile wanagusa chocholo, nikama polisi waliambizana, maana walimimina risasi mfululizo, ambazo zilichakaza miguu ya wakina Emma na Janja, ambao walianguka chini kama vifulushi, huku miguu yao aitamaniki kwa matundu ya risasi, yaliyokuwa yanavuja damu kwa wingi, “aya jamani wabebeni tuwapeleke hospital haraka, nilazima wapone ili wajibu mashtaka yao” alisema yule sajent na hapo askari wakawaburuza wakina Emma mpaka kwenye gari, na uwatupia ndani ya magari hayo, huku vijana awa wakitoa vilio kama nguruwe wenye njaa kari, na hapo safari ya kuelekea hospital ya mkoa ikaanza, huku sanjet wa polisi akipiga simu kwa RCO kutoa taarifa ya operation yao, na hatua walizozichukuwa.****

Naam siku ya pili mida ya saa kumi na moja alfajili, Sada aliokotwa na watu waliokuwa wanawai makazini na kutoa taafa kituo cha polisi, polisi walifika eneo la tukio mida ya saa kumi na mbili, wakimkuta Sada amepoteza fahamu, japo mivunjiko ya wazi ilionekana kwenye mguu wake na mkono wake, walimpeleka hospital ambako alifikia kwenye chumba cha wagonjwa maututi.***

Saa nne za asubuhi, Peter alieamka na uafadhari, akiwa na mpenzi wake Careen, walikuwa wamesha toa maelezo yao kituo cha polisi, na sasa walikuwa nyumbani kwao, ambako tayari walisha ona gari la kisasa toka #mbogo_land kwa king Elvis, kisha wakaingia ndani na kuanza kujadili juu ya biashara mpya kwaajili ya Peter, huku mipango yao wakiitaji ianze mapema sana.

Awakuishia katika mipango hiyo pekee, pia walipanga kuhusu harusi yao, ambayo waliitaji ifanyike mapema, “ujuwe tukisha maliza swala la kufunga ndoa, tuta kuwa huru kufanya mambo mengine ya biashara zetu” alisema Careen ambapo kauri hiyo ungeichukulia kama ndiyo lengo kuu, ila ukweli, Careen alikusudia kuwa, afunge ndoa haraka na Peter, kabla aja gaili, kumuoa kutokana na mambo yaliyo mkuta, kitu ambacho alikiweka wazi baada ya kumaliza kupanga mipango yao ikiwa ni pamoja na safari ya kesho yake kwenda Mwanamonga, kuwajulisha wazi wa Peter kile walicho kikusudia, kisha wa peleke taarifa #mbogo_land, “hivi Peter, unaweza kuniacha kwaajili ya kuwaogopa wakina Kalonga?” aliuliza Careen kwa sauti tulivu ya chini kabisa, “mh! yani hapo maana yake nimekuachia matatizo yako mwenyewe, kwa kukukimbia, kitu ambacho siwezi kukifanya ata siku moja, nina juwa maumivu ya kukimbiwa” alisema Peter, kwa sauti iliyojaa upendo wa hali ya juu, ulitoka moyoni, Careen akaachia tabasamu pana, la raha.***

Naam Kituo cha polisi cha mkoa wa Ruvuma, mambo yalikuwa mazito, maana watuhumiwa walihojiwa mmoja baada ya mwingine, wakiwa tayari wamesha chukuliwa maelezo yao, huku askari wadogo yani wenye vyeo vya chini, kama vile Panga na wenzake, wakidai kuwa walipewa amri na mkubwa wao, ambae walimtaja kuwa ni OCD Mwanauta, bahati yao mahojiano ya leo aya kuwa kama yale ya jana usiku, waliyofanyiwa wakina Kalonga na Dullah, “kwahiyo Panga, ulikuwa tayari kufanya chochote, ata kama unajuwa kuwa kufanya hivyo nikosa?” aliuliza RCO kwa sauti tulivu yenye mtego, huku akimtazama PC Panga, ambae katika hali ya kushangaza akatoa jibu, “afande nimesema kuwa ni amri, na sikuzote tuna ambiwa, kupokea amri zilizo tolewa na zitakazo tolewa na wakubwa” alijibu, anga kwa kujiamini, “hivi unazani kwa kusema hivyo unaweza kukwepa kukutwa na hatia, labda nikukumbushe kitu Panga, kazi yako siyo kupokea amri za kutekeleza uarifu na uvunjaji wa sheria, ila jukumu la polisi ni, kulinda usalama wa raia na malizao, kulinda na kusimamia sheria zinafutwa” alisema Mlashani kwa sauti tulivu.

Hapo nikama Panga hakuwa na lolote la kujibu, maana alikaa kimya huku akitazama mezani, “ok! panga ebu tueleze ulianza lini kupokea amri zilizo kinyume na maadili ya kazi” aliuliza RCO Mlashani, huku anamtazama Panga usoni, “afande siku zote nilizania ananipa amri sahihi, kama ile ya kumkamata Peter, ila kuhusu bangi, jana ndiyo siku ya kwanza” alijibu Panga, huku akijitaidi kukwepesha macho yake, yasikutane na macho ya Mlashani, ambae aliandika kitu kwenye karatasi zake juu yameza.

Maswali hayo yalikuwa karibu kwa askari wote, kasoro bwana Mwanauta, ambae mapaka sasa, tayari alisha ondolewa katika madaraka yake ya ukuu wapolisi wilaya, na sasa yeye nawenzake walikuwa wanaandaliwa barua za kusimamishwa kazi, na badae kufukuzwa kazi mala tu watakapo fikishwa mahakamani, maana kwa mujibu wa jeshi la polisi, linaamini, polisi ashitakiwi, ukishitakiwa wewe siyo polisi, “Mwanauta, unaweza kutuambia, kwanini ulitumia magari na ya polisi na askari kufanya uarifu, ukishirikiana na Kalonga na wenzake?” aliuliza Mlashani, kwa sauti ile ile tulivu, huku akimtazama Mwanauta usoni, “afande mimi sijashiriki uarifu wowote, huyo aliekuambia alizania akinitaja mimi anaweza kupata unafuu, katika kesi hii inayo mkabiri” alisema Mwanauta, kwa sauti ya kujiamini na kwamba anachokisema ni kitu cha kweli kabisa.

Mlashani akacheka kidogo, huku anamtazama Mwanauta usoni, “Mwanauta, inamana ata ile operation yako ya kumkamata Peter Jacob, nayo ilikuwa ni ya kusingiziwa?” aliuliza Mlashani, na hapo Mwanauta alitulia kidogo kama vile anatafuta jibu, kisha akajibu, “afande ilo siyo tatizo langu, nikwamba tulipewa taarifa na mtu tusie mfahamu, akimtaja Peter kuwa ndie mhusika wa dawa za kulevya, ndio maana tuka mfwata kumkamata” alisema Mwanauta, kwa kujiamini, hapo RCO akaandika kitu kwenye karatasi zilizokuwepo mbele yake juu ya meza, kisha akamtazama, Mwanauta, “na vipi kuhusu taarifa alizowai kuzitoa bi Careen pale kituoni, zilizi fanyiwa kazi yoyote, au uliamua kuungana na rafiki yako Kalonga?” aliuliza Mlashani, kwa sauti ya kusanifu, “hizo taarifa sizijuwi kabisa” alisema Mwanauta, huku anakwepesha macho yake, yasikutane na macho ya Mlashani. “uwezi kuzijuwa kwa sasa, ila askari walio kupigia simu na kukujulisha juu ya ilo ndio ambao watakutaja mahakamani” alisema Mlshani kabla ya kuwai ta watuhumiwa wengine, ambao Kalonga na Abdallah, japo Kalonga mwanzo alikuwa mbishi lakini baadae akatoa maelezo ambayo yange saidia kutia hatiani, huku Dullah, akiofia kupatwa na vile vilivyo mpata jana, na kuamia kusema yote, kama mjamzito anavyo tapika shombo ya samaki.***

Saa saba mchana, ilimkuta Sada akiwa na lisaa limoja, toka akiwa amezinduka, na kujikuta akiwa amefungwa bande mwili mzima, katairi jipya linavyo viligiwa karatasi, na kubakizwa sehemu za aja na macho pua na mdomo, huku akihisi maumivu makali, katika sehemu mbali mbali za mwili wake, ikiwepo mkono wake wa kulia na mguu wa kushoto, sehemu zambavu, na kichwani.

Sada alikwua katika mawazo mengi sana, asa juu ya kile kilicho mtokea, Sada aliwaza maisha ya shinda na vipigo aliyo kuwa anaishi kwa Emma, ambae mpaka sasa akujuwa kama alikuwa pale pale hospital, ward inayo fanana na ile aliyo lazwa yeye, tofauti ni kwamba, Emma alikuwa upande wa wanaume,

Sada alikumbuka maisha ya raha aliyokuwa anaishi na Peter, akipatiwa vitu vingi bila jasho, lakini sasa alikuwa anaishi kwa gharama kubwa sana, gharama ya kubadirishana chakula na utu wake, alilazimika kuzowea mchozo wa kurukwa ukuta kwaajili ya sehemu ya kulala na chakula, hakika sasa aliuona umuhimu wa Peter.

Na Sada akiwa kati kati ya mawazo akasikia“mgonjwa amesha amka, lakini bado ajajitokeza mtu yoyote, kama ndugu yake” Sada alisikia sauti ya kike akiongea, akajitaidi kutazama upande wa mlangoni, ilikumwona anae ongea, na hapo ndipo alipogundua kuwa alikuwa ameumia shingo pia, maana alipojaribu kutazama akasikia maumivu makali, huku kitu kama mbao iliyo fungiwa shingoni kwake, ikimzuwia kufanya hivyo, “mimi naona hakuna shida, kwakuwa amesha amka, basi ata tueleza mwenye, kama kuna ndugu zake sehemu, basi tutaenda kuwa taarifu” ilisikika sauti nyingine ya kike, sambamba na vizindi vya viatu, vya watu wawili vikisogelea kitanda chake.

Naam sekunde tatu baadae tayari Sada aliweza kuona doctor mmoja wakike alie ambatana na afisa mmoja wa polisi, mwenye jinsia ya kike pia, “pole sana, dada jina lako nani?” aliuliza yule polisi wakike ambae mwonekano wake ni kuwa mama mtu mzima, mwenye cheo cha SP, “a s ante, na I twa Sa daa” alijibu Sada, ikiwa ni mala ya kwanza baada ya muda mrefu akijitambulisha kwa jina lake harisi na siyo Queen, “hooo! dada Sada, naona sasa umepata nafuu kidogo, maana asubuhi ulipatikana ukiwa hoi” alisema yule Polisi.

Naam baada ya hapo yule mama akauliza swali kusudio, “Sada mpaka sasa hakuna ndugu alie kuja kukuona, niwazi kuwa ndugu zako, hawana taarifa za kwamba hupo hapa, unaweza kutueleza ndugu zako wako wapi, au kutupatia namba zao za simu, ili tuwajulishe, maana nimuhimu ukipata mtu wa kukuhudumia hapa hospital” alisema yule askari wakike, na hapo bila kujiuliza mala mbili, “Pe ter” alisema Sada kwa shida, “Peter ni nani wako na anaishi wapi?” aliuliza yule Polisi………..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!