
SEHEMU YA 95
ILIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NNE: Naam baada ya hapo yule mama akauliza swali kusudio, “Sada mpaka sasa hakuna ndugu alie kuja kukuona, niwazi kuwa ndugu zako, hawana taarifa za kwamba hupo hapa, unaweza kutueleza ndugu zako wako wapi, au kutupatia namba zao za simu, ili tuwajulishe, maana nimuhimu ukipata mtu wa kukuhudumia hapa hospital” alisema yule askari wakike, na hapo bila kujiuliza mala mbili, “Pe ter” alisema Sada kwa shida, “Peter ni nani wako na anaishi wapi?” aliuliza yule Polisi………..Endelea…
Ukweli Sada akaelekeza vyema nyumbani kwa Careen ambako sasa alikuwa anapahamu, na kamba mume wake anaishi hapo, “mh! huyu baba sinndie alie tekwa jana usiku, una uhakika yeye ni mume wako?” aliuliza yule polisi kwa mshangao, na Sada akathibitisha ilo kwa kueleza kuwa, Peter ni mume wake na wanamtoto mmoja, na kwamba Peter alimtelekeza kijijini, na yeye amekuja toka kijijini kumtafuta mume wake huyo, ndio yaka mkuta matatizo aya yaliyo mkuta, hakika hadithi hii, ilimuuzunisha sana yule polisi, wa dawati la jinsia, “huyu Peter anastahili kulipia kwa hili” alisema yule mama kwa sauti iliyojaa uchungu mkubwa sana, huku anatoa kijitabu kidogo cha kuandikia dondoo, yani note book, kisha akaanza kuandika alicho kijuwa yeye mwenyewe, ambacho kwa haraka nazani ni taarifa za Peter Jacob.
Alipo maliza kuandika, akamtazama Sada, “dada umezaa watoto wangapi na huyo mwanaume?” aliuliza yule SP, kwa sauti tulivu, “m mo jaaa” ukweli Sada alikuwa anaongea kwa shida kweli kweli, kutokana na maumivu aliyokuwa nayo mwilini, “moto anaitwa nani na yupo wapi?” aliuliza yule mama alie valia mavazi ya jeshi la polisi, na Sada alie kuwa anaongea kwa shida, akaeleza kuwa mtoto anaitwa Michael, na yupo na baba yake, ambae aliondoka nae akwa kuaga kuwa anakuja mjini kufanya manunuzi.
Ukweli mpaka yule polisi wa kike, anaondoka pale hospital, alikuwa anaonekana mwenye kusikitishwa na maelezo ya Sada, alimchukulia Peter kuwa ni mwaume mkatili, alie tawaliwa na tamaa ya fedha na uthariti, hivyo polisi yule alipanga kusimamia swala ili mpaka haki itendeke kwa Sada, na ikiwezekana Peter achukuliwe hatua kali za kisheria.**
Naam taarifa za kukamatwa kwa Kalonga pamoja na OCD Mwanauta zilianza kusambaa taratibu, mwishoe zikawafikia wanaandishi wa habari, ambao, waliomba mahojiano na RPC, ambae alieleza tukio zima, kwamba licha ya kukamatwa kwa bwana Kalonga sambamba na polisi kadhaa walioksa uadirifu, waliokuwa wanajaribu kusafirisha bangi, pia jeshi la polisi limefanikiwa kumwokoa kijana Peter Jacob aie tekwa nyala na polisi waliokosa maadiri, wakishirikiana na wauzaji wa dawa za kulevya., huku RPC huyo akitangaza siku ya kuanza kusikilizwa kwa kesi yao.
Baada muda mfupi wa mahojiano, na RPC, habari zilisambaa kwa haraka sana, kupitia vyombo mbali mbali vya habari, namba moja ikiwa ni mitandao ya kijamii, huku redio na television vikifwatia, wengi walishtushwa na ushirika wa OCD kwenye swala ili, maana licha ya kutambua uharifu wa Kalonga, lakini awakufikilia kama kuna Mwanauta nyuma yake.
Naam saa nane na mchana, iliwakuta Careen, Peter na Michael, wakiwa upande wa nyuma ya jumba lao la kifahari, wakiwa wamejipumzisha kwenye bustani, ile ambayo sikuzote wamekuwa wakizowea kuiona usiku, asa kwa upande wa Peter, maana Michael alisha wai kuletwa huku mala kadhaa, kwaajili ya kubembea.
Wanafamilia awa walikuwa wamejila za kwenye vitanda vyao, huku wakilitazama bwawa la kuogelea, “Peter inabidi ufikie wakati baba na mama waje mjini, japo wakae na sisi kwa miezi ata mitatu au zaidi” alishauri Careen alie valia gauni fupi jepesi sana, lililoangaza mpaka chupi yake ya ndani kabisa, “awawezi kukubari kukaa mbali na nyumba yao kwa muda wote huo, labda siku mbili au tatu, yani siku watakayo kuja, washinde siku moja wakizunguka mjini, na siku ya tatu waondoke zao” alisema Peter, ambae alikuwa amevaa bukta yenye kitambaa chepesi sana, ila aikuonyesha ndani, “lakini wewe umekuwa ukiwajibia watu sivyo walivyo itaji, hivi unaweza kuniacha na mimi nije nikae na wakwe zangu?” aliuliza Careen katika hali ya utani.
Hapo Peter, akageuza shingo lake kumtazama Careen alie kuwa anamtazama huku anatabasamu, “unazani na kutania Careen, baba na mama awawezi kukubari, mimi nawajuwa vizuri sana, kwanza awaja zowea kuishi ghorofani” alisema Peter akionyesha akuwa anatania, hapo akamfanya Careen aanze kucheka, kwa jinsi Peter alivyo jifanya yupo serious, Careen alicheka kiasi kwamba ata Peter mwenyewe akajikuta anaanza kucheka.
Naam wakiwa katikati ya kicheko chao, mala akatokea Jasmin, ambae toka asubuhi akwenda kazini, aliambatana na wakina Careen, kwenda kituo cha polisi, “samahani dada Careen, kuna jambo ni muhimu kama ukilisikia wewe na shemeji” alisema Careen kwa sauti tulivu ya upole kama ilivyo kawaida yao.
Ukweli Careen na Peter walishtuka, maana kiukweli toka lile tukio la jana litokee, awakuwa na amani iliyo kamilika mioyoni mwao, “kuna nini tena Jasmin, nilazime nikasikie?” aliuliza Careen huku anajiinua na kukaa kubakia amekaa kwenye kitanda, wakati huo Peter tayari alisha inuka toka kitandani na kusimama akimtazama Jasmin alie kuwa anatoa ujumbe, “siyo jambo geni kwako, naweza kumwambia aje huku huliko, ni polisi wakike” alieleza Jasmin kwa sauti ile ile iliyojaa nidhamu na unyenyekevu, “sawa mwambie aje” alisema Careen huku akiinuka na kuchukuwa tauro, kisha akajifunga kiunoni, alafu yeye na Peter wakaelekea kwenye viti vilivyopo chini ya mwamvuri, ni vile ambavyo wakati wmingine utumia kwaajili ya chakula chajioni na vinywaji.
Dakika chache baadae, walionekana polisi watatu, wawili mmoja wakike na wawili wakiume, waliokuja na kuunga na wakina Peter pale mezani, huduma ya vinywaji ilitolewa kwa wale polisi, ambao nikama hapo mwanzo walikuwa na hasira kali sana, hapo maongezi yakaanza, “mimi SP Shanie Mohamed, toka kituo cha polisi mkoa, nime kuja hapa kuchukuwa maelezo toka kwa bwana Peter Jacob, nazani ndie wewe bwana” alisema yulemwanamke, ambae hapo mwanzo tulimwona kule hospital kwa Sada, “ndiyo ni mimi..” alisjibu Peter, na kabla ajamaliza akadakia Careen “ndiyo ni huyu hapa, yeye ni mume wangu mtarajiwa” alisema Careen.
Hapo SP Shanie, akawatazama wawili awa kwa zamu, huku macho yake yakionyesha hasira, kiasi cha kuwashangaza wakina Careen na Peter, “labda niwafahaishe kuwa, mimi ni mkuu wakitengo cha dawati la jinsia, labda nianze na wewe unaesema kuwa huyu ni mume wako na unatarajia kufunga nae ndoa, je unafahamu kuwa anamke na mtoto?” aliuliza SP Shanie, kwa sauti ambayo ilikuwa inashindwa kuficha hasira zake.
Hapo Careen katazama Peter kwa mshangao, “Peter una mke mwanamke mwingine zaidi ya Sada?” aliuliza Careen kwa mshangao, huku Peter nae akionekana kushangazwa na hoja ile, aliyokuja nayo afisa huyu wakike, swali la Careen lilimshangaza pia SP Shanie alionekana kushangaa, “inamaana bibie unafahamu kuwa anamke anaitwa Sada?” aliuliza Shanie kwa mshangao ulio changanyika na hasira, “ndiyo nilisha wai kusikia kuhusu huyo mwanamke, na wazazi wake niliwasafirisha juzi, week moja iliyopita, baada ya yeye Sada kuwa kataaa adharani” alisema Careen, ambae alionekana kuwa na wasi wasi wa juu ya Peter kuwa na mke zaidi ya Sada, “unamaanisha nini kuwa kataa hadharani, wakati Sada ndio kwanza ameingia mjini, kutoka kijijini?” aliuliza SP Shanie, akionekana kuingiwa na sinto fahamu.
Hapo Peter akaohisi kuwa SP Shanie amechanganya jambo, “pengine mheshimiwa umechanganya, huyo siyo Sada ninae mfahamu, maana Sada ambae niliwai kuishi nae na kupata nae mtoto mmoja, ambae aliibia fedha zangu na kukimbilia mjini, mwaka mmoja uliopita, ajawai kwenda kijijini hivi karibu, na awezi kwenda kijijini, maana kitendo alicho wafanyia wazazi wake week moja iliyopita, nikibaya sana, aliwakana adharani, kwamba siyo wazazi wake” alisema Peter kwa sauti ambayo, ilionyesha kuwa alikuwa na uhakika yule SP Shanie, amemfananisha na mtu mwingine, “sija kuelewa Peter, unamzungumzia Sada Nyoni, au mwanamke mwingine?” aliuliza Shanie, kwa mshangao, “ndiyo mama yangu, huyo ndie Sada au mama Michael, nina mfahamu mimi, yupo hapa mjini mwaka sasa umekatika, na ataki ata kutuona mimi na mwanae Michael” alisema Peter, na kuzidi kumshangaza SP Shanie, ambae aliomba maelezo kamili juu ya mkasa huo wa Sada.
Peter nae akaeleza kila kitu, yani mwanzo mwisho, kuanzia siku ya kwanza Sada ameiba fedha zote, na kutoroka kijijini, akimwacha yeye na mtoto wa mwaka mmoja na nusu, pia alimweleza Sadari yake ya kwanza kuja mjini kumtafuta, na mwishoe kukutana na majanga ya kuvamiwa na wakina Sada na wenzake, kisha kupoeza fahamu na kujikuta akiwa mtaroni.
Peter alieleza pia kuhusu Safari yake ya pili, ambayo hii, ilikuwa ni kama sikio la kufa, sililo sikia dawa yoyote, maana licha ya kwamba yeye alikuwa anakuja mjini, kwa malengo ya kununua vifaa ya ujenzi wa nyumba yake, lakini wazazi wake, walimtahadharisha juu ya kukutana na mwanamke huyo, kitu ambacho yeye akutaka kuwasikiliza, na kuja kuona matokeo yake.
Kwakifupi mpaka mwisho wasimulizi, ambayo ilieleza kitu mpaka tukio la kumwibia fedha kwa mala ya pili na kumtelekeza kwenye hotel, akiwa hana fedha yoyote ya kulipia, pia alieleza tukio la kukataliwa hadhari siku yapili, pale mtini pub, huku Sada akihapa kuwa bora alale na mbwa kuliko kurudiana na yeye, na endapo ata rudiana nae ata kwa bahati mbaya, basi na ageuke kichaa, walieeza kuhusu kijitendo cha Sada kuwakataa wazazi wake hadharani mbele ya lango la hospital ya mkoa, hakika SP Shanie, alifadhaishwa sana na hadithi ile, inayo mhusu Sada, “Peter una uhakika na unacho kisma, kwamba tukiitaji ushaidi unaweza kuuleta?” aliuliza SP Shanie, huku anamtazama Peter, “siyo shahidi mmoja, ni kijiji kizima nilicho tokea, wanaweza kuthibitisha” alisema Peter, kwa kujiamini.
Naam akiwa mwenye kusikitishwa na kile alicho kisikia, SP Shanie, aliwaeleza wakina Peter kilicho mtokea Sada, “amekutwa amepoteza fahamu, ni matokeo ya kupigwa, na kuingiliwa kinyume na maumbile” alisema SP Shanie, ambae akufahamu kuwa kitendo cha kuingiliwa, kilikuwa ni kwa kupenda kwake, “sasa yupo ward ya mifupa pale hospital ya mkoa, ila alisema kuwa jana ametoka kijijini kuja kukutafuta wewe na mwanae” alisema SP Shanie,
Ata hivyo Shanie aliaga na kuondoka zake, akiahidi kulifwatilia swala ili kiundani zaidi, na kubaini nani mkweli kati yao, yani kati ya Sada na Peter, wakiwaacha Peter na Careen wanajadiri juu ya kile kilicho mkuta, Sada.****
Naam lisaa limoja baadae, SP Shanie, alisimamisha gari mtaa wapili wa maenge B, mita chache toka alipo okotwa Sada, mapema leo, akashuka toka kwenye gari la polisi, akiwa na askari wawili wakiume, wakaenda moja kwa moja kwenye moja ya nyumba zilizopo karibu na eneo lile, nyumba ambayo kuilikuwa na watu wamekaa kibarazani, wanawatazama kwa macho ya mashaka, nazani walikuwa wanajiandaa kwa maswali toka kwa polisi awa, maana walijuwa ujio wao ni kwaajili gani……..….
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU