KIAPO CHA MASIKINI (96)

SEHEMU YA 96

ILIPOISHIA SEHEMU YA TISINI TANO: Naam lisaa limoja baadae, SP Shanie, alisimamisha gari mtaa wapili wa maenge B, mita chache toka alipo okotwa Sada, mapema leo, akashuka toka kwenye gari la polisi, akiwa na askari wawili wakiume, wakaenda moja kwa moja kwenye moja ya nyumba zilizopo karibu na eneo lile, nyumba ambayo kuilikuwa na watu wamekaa kibarazani, wanawatazama kwa macho ya mashaka, nazani walikuwa wanajiandaa kwa maswali toka kwa polisi awa, maana walijuwa ujio wao ni kwaajili gani……..…..Endelea…

Kama siyo tukio la kukamatwa kwa wakina Emma, basi ni tukio lililotokea jana usiku, tukio ambalo habari zake zime samba mtaani kote, “habari zetu jamani” alisalimia SP Shanie, kwa sauti iliyojaa urafiki, ni mbinu moja wapo ya kipolisi, kumvuta raia karibu yako, pale unapoitaji habari flani, toka kwake, salama shikamoo” waliitikia wale raia ambao walikuwa jinsi mchanganyiko, huku salamu zikigongana kwa mpigo, “marahaba, samahani kwa kuwakatisha maongezi yenu” alisema SP Shanie, ambae alikuwa amesimama karibu yao kabisa, mitachache toka kibarazani, “bila samahani sisi tupo tu hapa tunapiga story za kawaida” alisema mmoja wao.

Kusikia hiyo SP Shanie, akaanza kwa kujitamburisha, “naitwa SP Shanie Mohamed, toka kituo cha polisi mkoa, ni mkuu wa dawati la jinsia, nime kuja hapa kwaajili ya kuuliza mawili matatu, ambayo yatasadia katika uchunguzi watukio lililomtokea bi Sada Nyoni, usiku wa kuamkia leo, ili kusaidia mwanamke yule kupata haki zake na pengine kumkamata mtu alie mfanyia kitendo kile” alisema Shanie, kwa sauti flani, japo iliyochangamka, lakini pia, ilikuwa ya kirafiki.

Lakini akashangaa kuona wale raia, wakitazamana kwa mshangao, ata yeye mwenyewe Shanie, aliuona mshangao huo, na yeye kuanza kuwashangaa wae raia, “mbona kama mna nishangaa, au amkusikia kilichotokea usiku wa kuamkia leo, kwa bi Sada, ambae aliokotwa hapo pembezoni mwa barabara” aliuliza Shanie, ambae aliona kitu kama dalili ya kuto kupata ushirikiano toka kwa wale raia, “hapana afande, siyo kwamba atujasikia, ila nikama umechanganya majina, maana dada alie okotwa hapo anaitwa Queen, na alie mpiga tayari amesha kamatwa usiku ule ule, tena ni muda mfupi tu baada ya kumpiga Queen, sasa huyo Sada unae mzungumzia sisi atumfahamu” alisesema mmoja kati ya watu wale, akielelezea jinsi tukio zima lilivyokuwa jana usiku, wakati wakina Emma wanakamatwa, na kwamba Queen alikuwa anaishi na kijana huyo ambae mala kwa mala amekuwa akimpiga kipigo cha jibwa jizi.

Hapo SP Shanie akawatazama wale askari aliokuja nao, “inawezekana Queen akawa ndie Sada, na kwamba wale watuhumiwa wa kesi ya utekaji, wakawa ndio hao wanao zungumziwa?” aliuliza Shanie, kwa sauti ya chini, “afande, kwa mujibu wa maelezo aya, nazani Sada baada ya kuja mjini, na kuishi na huyu bwana, alibadiri jina, na kujiita Queen” alisema askari amoja kati ya wale wawili mwenye cheo cha sajent, “kwahiyo bwana Peter yupo sahihi, na huyu mwanamke ni mshenzi, na pengine kilicho mtokea ni uthariti kaika mapenzi, kama alivyo mthariti Peter na kumkataa mtoto wake Michael” alisema Shanie, kabla ajaaga na kuondoka zake pamoja na wale askari, kuelekea ofisini kuandika report yake, juu ya kile ambacho amekigundua juu ya Sada ambae anajiita Queen.***

Naam!! Careen na Peter, wakiwa pale nyumbani kwao, walijadiri sana kuhusu Sada, “Sada ni mama mzazi wa Michael nivyema ukasahau alicho kufanyia na kumsaidia kwa huduma, na malipo ya hospital, ili akisha pona arudi nyumbani kule mwanamonga” alisema Careen ambae kichwani mwake, alikuwa anajuwa kuwa endapo Sada ata ona na kurudi kijijini, basi wao watapata nafasi nzuri ya kuishi kwa amani na furaha, vinginevyo ataanza kuwa sumbua, na kudai kuwa Peter ni mume wake, “Careen achana na huyo mwanamke, tena tusijaribu kuwa nae karibu kabisa, ujuwi baada ya kupona atafanya nini, maana hii akili yake sikuizi anaijuwa mwenyewe” alisema Peter akionekana wazi kuwa, hakutaka kabisa kujiusisha na na swala lile linalo mhusu Sada, “lakini Peter, unazani anaweza tena kufanya lolote wakati, umeambiwa kuwa hali yani mbaya, uoni kuwa akisha pona ataenda kijijini na kukuacha uishi kwa furaha, ebu ona amepatwa na tatizo sasa anasema wewe ndie mume wake” alisema Careen kwa sauti ya kubembeleza.

Hapo Peter akatulia kidogo, akitumia sekunde sitini, kama vile anatafakari kile alichoelezwa na Careen, “sawa tunaweza kufanya hivyo” alisema Peter, kwas sauti ambayo ungetambua wazi kuwa, ilikuwa ni kishingo upande, “lakini Peter, swala ili, tuta mwachia Jasmin, sisi atuto kutana kabisa na Sada, ilo naomba unielewe” alisema Careen, ambae licha ya kuamua kumsaidia Sada lakini akutaka ukaribu wowote kati ya sada na mchumba wake Peter, “ata bila kuniambia Careen nisinge taka kukutana na huyu mwanamke, siyo kwamba kuna kitu nitajisikia juu yake, ila ukweli nikwamba, sitaki kumsogeza karibu yangu, aliyo yafanya yanatosha” alisema Peter, akimwakikishia Careen.

Naam hapo napo Careen alipiga simu kwa Jamin na kumpa jukumu ilo la kuhakikisha anachagua mtu ambae ata simamia matibabu ya Sada, huku yeye mwenyewe Jasmin akimtembelea mala kwa mala, kumuona na kujuwa maendeleo yake.****

Naam Sada saa kumi nambili jioni, ndio muda ambao Sada alianza kupatiwa huduma za daraja la kifalme, kwanza picha linaanza aliwaona wanawake watatu, wakiiingia kwenye ile ward ya watu wenye matatizo ya mifupa ambayo mpaka sasa Sada akuwa anajuwa mle ndani kuna watu wangapi, walio lazwa kama yeye, zaidi alikuwa anasikia sauti za wagonjwa wengine, maana yeye akuweza ata kugeuza shingo yake kutazama pembeni, “salaam bi Sada, sisi ni wahudumu toka #mbogo_land, tupo hapa kukuhudumia, katika kipindi chako cha ugonjwa, tatizo lolote shida yoyote utasema na kuhudumiwa kwa wakati” alisema mmoja wao alievalia suit yeusi ya kike.

Na kwa maneno hayo moja kwa moja Sada aliwatambua watu awa kuwa wametumwa na Peter, kuja kufanya hivyo, na kwamba tayari SP Shanie, amesha enda kumweleza Peter, ambae baada ya kupewa taarifa za kulazwa kwake, amechanganyikiwa na kutuma wafanya kazi, “nilisema Peter ananipenda na awezi kuniacha ata iweje, sasa huyo awala yake atajibeba, ngoja kwanza nipone aone mchezo” aliwaza Sada, huku ana akisikia wale wanawake wanapanga mipango ya kumwamishia kwenye ward ya daraja la kwanza, kitu ambacho kilifanyikamala moja, kwa msaada wa wauguzi.

Na baada ya hapo, ndipo Sada alipo ona akihudumiwa kama malikia wa #mbogo_land, yani alipewa kila alichotaka, pia ata matibabu alikuwa alikuwa anapewa kwa namna ya pekee, lakini uwezi amini alichokuwa anakiwaza, “hivi Emma anajuwa kama nimelazwa hapa, we ngoja tu, nikijipatia ela zangu kwa Peter yeye mwenyewe atajileta, na kusahau kila kilichotokea” ayo ni baadhi ya mawazo ya Sada.***

Naam siku zilienda Peter na Careen wakiendelea na mipango yao, ya kufungua kampuni ya kilimo, napia kufunga ndoa, walienda kijijini kutoa taarifa ya maamuzi yao ya kufunga ndoa, ambayo wazazi wa Peter awakuwa na kipingamizi chochote, pia Peter alipeleka taarifa ya kulazwa kwa Sada pale Hospital ya mkoa, kwa wazazi wa Sada, ambao awakuonyesha kushtushwa na taarifa hiyo, zaidi ya kumshangaa Peter kwa moyo aliokuwa nao, kwa kuchukuwa majukumu ya kumsaidia Sada, mwanamke ambae fai ata kuwa wanyongeza.

Hivyo mzee nyoni na mke wake awakujisumbua ata kutafuta nauri ya kwenda mjini, zaidi walikuwa busy na maandalizi ya mashamba yao, kwa ajili ya msimu ujao, na licha ya kutopanga kwenda mjini kumwona Sada, pia awakupanga kumpokea pale nyumbani, endapo angerudi.

Siku zilisogea, harusi ilitangazwa, watu wengi wakaalikwa, ata pale wanakijiji, walichaguliwa wachache ambao wata wakilisha mjini, huku pale kijijini pakiandaliwa sherehe kubwa sana, ambayo ingefanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mwanamonga.

Ukiachia kijijini, Mwanamonga, pia pale mjini, habari zilisambaa, na shrehe ikipangwa kufanyakika kwenye viwanja vya songea Club, huku mialiko ya watu mashuhuri toka pande mbali mbali za dunia, kuanzia mbogo land, mpaka nchi nyingine, za jilani na zambali, huku wakiarikiwa viongozi na watu mahashuri wa nchini Tanzania, pamoja na washereheshaji mbali mbali, na wamusic toka mbogo land na Tanzania, pia ilipangwa maharusi waktembelee nchi Mbogo land, ambako wataandaliwa chakula cha jioni, na mfalme Elvis na mke wake.***

Naam sikuzilikatika atimae ilibakia week moja tu, kabla ya siku ya harusi ya Careen na Peter, harusi ambayo ambayo siyo tu kutikisa Songea, ila ingetikisa Tanzania nzima na mbogo land kwa ukubwa wote, ikitajwa kuwa ni harusi ya rafiki wa utotoni wa mfalme wa mbogo land.

Tayari shamla shamla zilishaanza kuonekana baadhi ya sehemu, mfano Mwanamonga, tayari mikesha ya ngoma za hasiri na music wa kisasa ilishaanza, watu wakinywa bia na pombe za hasiri, vyakula vyakila aina vilipatika kuanzia asubuhi mpaka jioni, hakika ilitumika gharama kubwa sana.

ni week ya tatu toka Sada lazwe hospital pasipo kumwona SP Shanie, wala mpenzi wake Emma, ambae ndie alie msababishia kulazwa hapa hospital, na wala hakupata habari za mpenzi wake huyo au rakiki yake anae mfahamu kwa jina la Janja, ambae kiukweli alikuwa anamuwaza muda wote, kuna wakati alihisi pengine Emma bado amechukizwa, na kitendo cha kumfumania siku ile, “yani ataki ata kujuwa nipo wapi” alijilalamisha Sada, pasipo kujuwa mwezie yupo ward ya wagonjwa wa mifupa, na amaehaanza kukuhudhuria mahakamani, kusikiliza kesi inayo mkabiri, “we mwache tu, akiniona nimepata ela, ata nitamani mwenyewe” aliwaza Sada, ambae sasa ndiyo alimkumbuka Peter.

“Mh! alafu huyu anajifanya yupo busy na huyo mke wake siyo, yani anashindwa ata kuja kunitazama, we ngoja nipone, ndio ata juwa kuwa mimi siyo wa kunichezea” aliwaza Sada, ambae kiukweli licha ya kuhudumiwa na watu ambao anajuwa fika kuwa, wametumwa na Peter, lakini bado alijihisi kupatwa na hasira juu ya mzazi mwenzie huyo, “yani mimi ninapata tabu hapa, alafu yeye anakula raha kwenye gorofa, kama ni uzuri ata mimi ninao, ajanizi chochote, sema tu yeye anaela nyingi” aliwaza Sada, pasipo kujuwa mwenzie, ana jiandaa kwaajili ya kufunga ndoa.

Maendeleo ya Sada yalikuwa ya kuridhisha, sasa alisha funguliwa bandage karibu na sehemu zote za mwili, na kubakia ile ya kichwani, na zile mkononi na miguuni, pia na eneo dogo la tumboni na kifuani, uso wake ulionekana wazi ulivyo vimba, na kupondeka pondeka.

sasa Sada aliweza kujikongoja, kwa kutumia gongo la kutembelea, aliweza kwenda chooni mwenyewe na kutoka nje kupunga upepo.**

Naam siku zilizidi kusogea, ilibakia siku moja, tu kufikia siku ya harusi ya kiistoria, harusi ambayo siyo tu kwamba ilikuwa inaunganisha nchi mbili, ila pia, ilikuwa ina mhusisha mschana mrembo, mfanya biashara, na tajiri mwenye umri mdogo, mtoto wa waziri wa afya jinsia wanawake na watoto, wa Mbogo Land, na rafiki wa utotoni wa mfalme wa #Mbogo_Land.

Hiyo ndiyo siku ambayo, Kadara ambae licha ya kusikia taarifa za harusi hiyo, na kuto kufahamu kuwa Peter anae zungumziwa kufunga ndoa na Careen ni huyu Peter wa Sada, sasa leo ndiyo siku ambayo alipata habari kamili, ni baada ya kufika kijijini Mwanamonga, alikoenda kuwatembelea wazazi wake, na kukuta kuna shamla shamla kubwa ya sherehe za harusi.

Kadara alipewa habari kamili juu ya sherehe zile, na pia alipewa habari juu ya Sada, kuwa yupo hospital amelazwa.

Hakika umbea siyo kazi, licha ya kuingia pale mida ya saa mbili na nusu za usiku, lakini uwezi amini kilicho tokea, Kadara alikodi pikipiki mpaka mjini namtumbo, ambako alisubiri magari toka tunduru, ambapo aliyapata magari ya mizigo, na kufika songea mjini saa saba za usiku, lengo likiwa ni kukutana na Sada akamwona anahali gani juu ya ugonjwa wake na ana hali gani juu ya taarifa za harusi. …….. itaendelea….

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!