
SEHEMU YA 97
ILIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA SITA: Hakika umbea siyo kazi, licha ya kuingia pale mida ya saa mbili na nusu za usiku, lakini uwezi amini kilicho tokea, Kadara alikodi pikipiki mpaka mjini namtumbo, ambako alisubiri magari toka tunduru, ambapo aliyapata magari ya mizigo, na kufika sngea mjini saa saba za usiku, lengo likiwa ni kukutana na Sada akamwona anahali gani juu ya ugonjwa wake na ana hali gani juu ya taarifa za harusi. ……..Endelea…
Usiku ule Kadara akuweza kukwenda hospital, lakini alipanga kesho mapema ajihimu hospital, kumwona Sada kabla ya kwenda kanisani, kushuhudia harusi ya Peter, na huyo mwanamke alie acha gumzo nchi mzima, pasipo kujuwa kuwa yeye ndie atakuwa mtu wa kwanza kwenda kumjulisha Sada juu ya harusi hiyo ya kihistoria.****
Naam saa kumi na mbili kamili siku iliyo fwata, ilimkuta Kadara akiwa kwenye lango la kuingilia pale hospital ya mkoa wa Ruvuma, akiwa miongoni mwa watu waliowai kuja kuwatazama wagonjwa, lakini utofauti ni kwamba, Kadara alikuwa amevaia mavazi yake mazuri, usingejiuliza kuwa akitoka hapa kuna sehemu anatarajia kwenda, tena ni sehemu ambayo inaitaji apendeze kama hivi alivyo sasa.
Moja kwa moja Kachiki alielekea kwenye ward ya mifupa, na alipofika hapo, akaingia na kuanza kukagua kitanda kimoja baada ya kingine lakini akufanikiwa kumwona Sada, ndipo alipoamua kumwuliza nurse mmoja, ambae alimwelekeza sehemu alipo, kwamba ni ward ya daraja la kwanza kabisa, yani VIP.
Kadara alienda haraka upande ule, wa ward za daraja la kwanza, ambako aliielekezezwa chumba alicho lazwa Sada, nae akaingia ndani, akakutana na mschana mmoja alie kuwa anaandaa uji wa maziwa kwaajili ya mgonjwa, alie kuwa amelala kitandani, “mh! nitakuwa nimekosea” alisema Kadara huku anataka kutoka, maana siyo tu kuto kumtambua Sada, ambae alikuwa ameumuka uso wake kwa vimbe mbali mbali na mipasuko ya majelaha makubwa, pia akuzania kuwa Sada anaweza kuhudumiwa na na mschana mzuri alie valia mavazi nadhifu, ya kihudumu, mana ata Sada mwenyewe akuwai kufikia hatua ya unadhifu kama huo, sasa itakuwaje kwa mhudumu wake, “hakikisha sukari inakolea vizuri” ilikuwa ni sauti flani ya tabu kidogo, iliyotoka katika rafudhi ya kirugha chao, ndiyo iliyomfanya Kadara asite kutka nje, “ndio mama” alijibu yule mhudumu, kwa sauti iliyojaa nidhamu, “we Da Queen, kumbe ni wewe yani hapa sikukutambua kabisa” alisema Kadara, huku anaingia ndani na kufunga mlango.
Hapo ata Sada aliekuwa amelala kitandani, ambae akumwona Kadara hapo mwanzo, akageuza shingo yake, ambayo sasa alikuwa na uwezo wakugeuza kidogo, na kutazama upande wa mlangoni, akamwona Kadara akimtazama kwa mshangao, na kabla Sada ajasema chochote, yule mhudumu nae akaacha kila anacho kifanya akamgeukia Kadara, “salaam mgeni wetu mwema” alisalimia mhudumu huku akiinamisha kichwa chake na mkono mmoja wakulia, ameuweka kifuani na mwingine wa kushoto ameuweka mgongoni, Kachiki alitoa macho kwa mshangao akishindwa kujuwa aitikie vipi ile salam, “karibu Kadara, umejuwaje kama nipo hapa” aliuliza Sada huku anajiinua kwa shida na kukaa kitandani.
Ukweli Kadara alikuwa katika mshangao mkubwa, na maswai yasiyo na majibu lathmi, “nime toka kijijini jana, ndio nikaambiwa aya yote yanayoendelea” alisema Kadara, huku akiamini kuwa mpaka Sada ame letewa wahudumu, kama awa, basi tayari amesha patina na Peter, na amekubariana na kila kitu kinachoendelea, “kumbe kijijini wanajuwa kuwa nimelazwa, sasa mbona awaji kunitazama?” aliuliza Sada kwa sauti ya kawaida kamavile akuwa anajari kwakuto kujakwao kumwona hospital, maana tayari aliona mafanikio yapo karibu yake asa baada ya Peter kujileta tena karibu yake, kitu ambacho kilimwaminisha kuwa, Peter bado alikuwa anmpenda, “kuja huku labda harusi ikipita, maana kila mmoja yupo busy na harusi” alisema Kadara ambae sasa alikuwa anaamini kuwa Sada alikuwa anafahamu juu ya harusi ya mzazi mwenzie, na amaekubariana na matokeo, “he! nani uyo anaolewa?” aliuliza Sada kwa sauti iliyojaa shauku, akionyesha wazi kuwa akuwa anafahamu lolote juu ya ndoa inayoenda kufungwa leo.
Hapo Kadara akamtazama yule mwanamke mhudumu aliekuwa anampatia Sada kikombe cha uji wa maziwa, kwa hesima na taadhima, nae akapokea kwa mkono mzima, yani ukiacha ule ambao ulikuwa umefungwa na bandage ngumu, “samahani mama, kuna chochote naweza kukufanyia kabla sijaenda kuandalia baadhi ya maitaji yako muhimu” alisema mhudumu, kwa sauti iliyojaa nidhamu, “hakuna we nenda tu, mimi nipo na rafiki yangu” alisema Sada ambae alijiona mwenye fahari kubwa kwa Farida kushuhudia kile ambacho anatendewa na mschana yule, ambae aliondoka mle ndani mala tu baada ya kuluhusiwa na Sada.
“Umesema kuna harusi, ni yanani hiyo anajiingiza kwenye ndoa” aliuliza Sada, huku ambae alianza kunywa uji na ule mdomo wake uliovimba, “kuna harusi nyingine zaidi yah ii ya Peter na huyo mke wake?” aliuliza Kadara, ambae sasa alitazama saa yake ya kwenye simu.
Kama kuna siku Sada aliwai kushtuka kwa mshangao, basi ni siku ya leo, maana alitoa macho kwa mshangao, usio nakifani, “eti nini Peter anafunga ndoa?” aliuliza Sada kwa mshangao mkubwa, “we Sada inamaana ulikuwa ujuwi kama leo Peter anaowa, mbona mimi mwenzio ndio naelekea kanisani kwenda kushuhudia ndoa” alisema Kadara huku akionyesha kushangaa kutokujuwa kwa Sada, “hapana…..hapana… hapanaaaaa, Peter awezi kunifanyia hivi” alipigakelele Sada, zilikuwa ni kelele za uchungu.
Hapo licha ya umbea wake, lakini ukweli Kadara alishangaa Sada, “lakini Sada si ulishaachana nae, na ulisema aumtaki tena?” aliuliza Kadara, kwa sauti ya mshangao, “hapana Kadara, kumbuka Peter ni mume wangu, na tumezaa mtoto mmoja, awezi kunitelekeza hivi” alisema kwa sauti ya kulalamika, “mh! lakini Sada, ubazani ata hivyo Peter ange kuelewa na kurudiana na wewe kwa yote uliyomfanyia?” aliuliza Kadara kwa sauti ya kusimanga, “Kadara najuwa Peter ananipenda sana, huyo mwanamke ametumia ela zake kumlaghai” alisema Sada kwa sauti ya kulalamika, ungesema kuwa yeye ndie akaonewa kwa kuibiwa mume, “hivi yule polisi ajasikia kama wanaowana?” aliuliza Sada kwa sauti ile ile ya kulalamika, akimaanisha polisi Shanie, yule wa dawati la jinsia.
Hapo kikapita kimya kifupi, kama vile kila mmoja anawaza la kwake, wakati Kadara anawaza namna ya kuaga ili awai kwenye ibada ya misa ya ndoa, huku Sada mwenyewe anawaza namna ha kuzuwia ndoa isifungwe, na wakanza kupata jibu alikuwa ni Sada, “Kadara naomba unisaidie kitu, siwezi kuluhusu hii ndia ifungwe, yule ni mume wangu kabisa” alisema Sada, kwa sauti iliyomaanisha kile anacho kisema.
Hapo bila kuwaza Sada ata izuwiaje ndoa ile isifungwe, asa kutokana na hali yake, yeye akatabasamu moyoni, “wala usikonde, kama uwezo ninao, nitakusaidia dada yangu” alisema Kadara ambae alitamani kuona kitaachofanywa na Sada.****
Yaaap! Ilikuwa ni jumapili iliyochangamka, kama ambavyo ungeweza kuona nje ya eneo la kanisa katoliki, la mtakatifu Telesia lilivyofulika watu, walio gubikwa na nyuso za furaha, wamependeza kwamavazi nadhifu, na masafi, atakama ilikuwa ni nguo ya zamani, lakini siku hiyo ilikuwa imefuliwa, na kupigwa pasi, huku kando kando ya eneo lile kubwa la kanisa, ungeona magari ya kila aina, yani yakifahari ya kawaida na ya bei ya chini yaliyochakaa, kama lile la mbogo Edgar.
Huku kanisa nalo likiwa limepambwa kwa mapambo mbali mbali, kwenye madirisha na milango yote ya kanisa, pia magari sita ya kifahari, yenye kupambwa mauwa na Maputo ya rangi mbali mbali, yalionekana yakiwa yamepambwa vizuri sana, na kujitenga nay ale mengine ya wageni mbali mbali, waliokuja kushuhudia harusi hii ya kihistoria.
Ebu sasa tuingie ndani ya kanisa ili, ambako sasa vilisikika vinanda vizuri vyepesi, huku watu waliokuwepo mle ndani, ya kanisa, wakiwa katika hali ya utulivu, wanatazama mbele ambako walionekana maharusi wawili waliopendeza katika mavazi yao ya harusi, huku bwana harusi mwenye kuvalia suit nyeusi, akifanana kimavazi na mtoto mdogo wa kiume mwenye umri wa miaka zaidi ya miwili, alie simama jirani na mtoto mdogo wa kike mwenye umri unao lingana nae, walioshikilia maua mazuri.
Mala vinanda vikakoma, na utulivu ukatawala, hapo Padre akasogea mbele ya maharusi, “ikiwa matangazo matatu ya ndoa hii yalisha tangazwa na hakutokea mtu yoyote mwenye pingamizi, na sasa kabla ya kukamilisha agano ili landoa, nafasi kwa mala ya mwisho, kama kuna yeyote ambae anapingamizi kuhusu ndoa hii, ajitokeze, maana ikipita agano ili, hakuna atakae weza kuitengenisha ndoa hii, ipokuwa mungu pekee” alisema Padre, na hapo ukafwata ukimya mfupi, huku watu wakiwa na nyuso za tabasamu, niwazi hawakujuwa kinachofwata.
Hapo Careen amtazama Peter, ambae alikuwa anatazama pale walipo kaa wazazi wa pamde zote mbili, yani mzee Jacob na mke wake waliopendeza kweli kweli, usinge juwa kama wametoka kijijini, sikuchache zilizopita, pia walikuwepo wazazi wa Careen, ambao siwezi kuzungumzia kupendeza kwao, sababu ni jadi yao, nyuma yao pia walikuwepo watu kadhaa toka jijini Mwanamonga na wae waliotoka Mbogo land, macho ya Peter yana mwona mzee nyoni, ambae kiukweli alisisitiza sana kualikwa katika sherehe hii, na yeye Peter kuhakikisha kuwa mzee Nyoni na mke wake wanapata mavazi mazuri na kukuja mjini pamoja na wageni wengine wawakilishi toka kijijini, mzee Jacob anatabasamu kidogo, Peter nae anatabasamu, wakati huo Careen anaminya kidogo mkono wa Peter, nae anamtazama mke wake, macho yao yanakutana, wote wanatabasamuliaa kwa raha zao.***
Mhudumu wakiwa na matunda machache kwenye mfuko, aliingia kwenye kile chumba cha ward ya daraja la kwanza, nakukuta chumba kitupu, yani siyo Sada wala yule rafiki yake, wote awakuwepo, akatoka nje kumtazama, nako hakuwepo, akazunguka kwenye majengo kadhaa, lakini akumwona Sada wala Rafiki yake, hapo akatoa simu yake na kupiga kwa Jasmin, ambae bila shaka aliwasiliana na uongozi wa hospital, ambao ulitoa taarifa polisi, kwenye kitengo kilichokuwa kina simamia swala la Sada, kitengo ambacho kinaongozwa na SP Shanie Mohamed, ili waweze kutafuta na kufahamu Sada yupo wapi, na kwanini ametoroka.****
Huku kanisani nako, mambo yalikuwa yana endelea, na baada ya kutangaza tangazo la mwisho la pinga mizi, na kuona kimya, kwamba akuna mtu alie toa pingamizi, Padre akawageukia maharusi, kwaajili ya kuendelea na kipengele kinacho fwata.
Lakini kabla ajasema chochote, ghafla ukasikika ukulele toka kwenye mlango wa kuingilia ndani ya kanisa, “pingamizi!! Jamani pingamizi!!! naomba msaidie” ilikuwa ni sauti kali yakike…….…..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU